Thursday, January 4, 2018

SIRI YA DAMU YA YESU(THE JESUS BLOOD MYSTERY)

Na Asafu Robert Maziku


Shalom
Kwa mtu mwenye akili timamu naelewa alishawahi kujiuliza kwanini ukitamka jina la YESU kunatokea mrejesho usio wa kawaida.

Hapo kuna mambo mawili kwa pamoja.
A) Jina
B) Damu

Kila jina ulijualo huwa lina nguvu nyuma yake. Nguvu hio inabebwa na asili ya jina, mfano jina Asafu/ Emmanuel, Shida, Eliya au lolote huwa lina nguvu kutokana na asili. Ninapo sema asili namaanisha NANI AMELIITA na KWANINI AMEKUITA. Hii ndipo inaweza kutofautisha nguvu ya jina la watu wawili tofauti lakini jina Moja. Mfano kuna mtu anaweza kuitwa Emmanuel na Babu yake kwasababu kuna Rafiki yake anayempenda sana anaitwa hivyo, Pia mwingine anaweza kumuita Emmanuel sababu ya Kufunuliwa na Roho mtakatifu. Watu hao wataitwa wote Emmanuel lakini kilamtu na Nguvu yake.

DAMU
Damu yoyote uijuavyo huwa imebeba uhai, Pia hunena. Damu ya YESU ni tofauti kidogo na damu uzijuazo kwa sababu zifiatazo, kwanza ni Damu ya Mungu mwenyewe.

Ili binadamu au mnyama yeyote awe anaishi ni lazima awe anaishi na mchanganyiko wa damu kutoka kwa mama na Baba. Ili damu hizo zimkamilishe binadamu ni lazima liwepo tendo la ndoa.

Damu ya Yesu haina mchanganyiko kati ya Baba na Mama kwani hakuna uwepo wa Tendo la ndoa Bali Uwepo kwa Uwezo wa Mungu mwenyewe.

IKIWA KILA DAMU UIJUAVYO INA UHAI NA INANENA VIPI DAMU YA MUNGU MWENYEWE. Kwakupitia damu ya Yesu inenayo mema kwa mwanadamu mapepo yanatetemeka.

HIVYO BASI,
JINA + DAMU YA YESU inapatikana nguvu ya ajabu iwezayo kutikisa ufalme wa giza......

MWAKA 2018 TUTASHINDA KWA DAMU YA YESU                                               0653340950

Tuesday, July 11, 2017

RATIBA YA MAFUNDISHO YA apostle eliya

YESU NI KRISTO

MASOMO YA MWAKA MMOJA (2017-2018)
Somo moja kila wiki, masomo 4 kila mwezi



A.TORATI
B. WAAMUZI/MANABII
C. ZABURI
I
MWANZO-KUTOKA
WAAMUZI – ESTA
AYUBU – WIMBO BORA


MWEZI WA 7
        1.    Hapo Mwanzo (ZIADA)                      
        2.        Adam na Hawa
        3.        Kaini, Habili na Sethi
        4.        Kitabu cha Vizazi
        5.        Safina na Dhabihu ya Nuhu


MWEZI WA 8
1.        Ibrahim na Isaka
2.        Yakobo (Makabila 12)
3.        Kutoka/Pasaka
4.        Kuvuka Maji
5.        Sabato (ZIADA)



MWEZI WA 1
       1.         Miji 3 ya Makimbilio
       2.        kwa Bwana,na Gideoni
       3.        Samsoni Mnadhiri
       4.        Boazi
       5.        Yabesi (ZIADA)


MWEZI WA 2
       1.        Mfalme Daudi
       2.        Sulemani
       3.        Yehoshafati
       4.        Yosia
       5.        Toba (ZIADA)

MWEZI WA 5
       1.        Hekima,Ufahamu,Maarifa
       2.        Dhambi,Hatia na Uasi
       3.        Mungu,mbona umeniacha?
       4.        Neno Lako (Bwana)
       5.        Wamchao Bwana (ZIADA)


MWEZI WA 6
       1.        Jina Jema
       2.        Mwanamke na Mwanamume
       3.        Ubatili Mtupu
       4.        Mpenzi Wangu
       5.        Neema na Kibari (ZIADA)
II
WALAWI-HESABU
ISAYA – MALAKI



MWEZI WA 9
       1.        Hema la kukutania
       2.        Madhabahu/Matoleo
       3.        Sanduku la Agano
       4.        Mpakwa mafuta
       5.        Damu ya Agano (ZIADA)

MWEZI WA 10
       1.        Mzaliwa wa kwanza
       2.        Nyoka wa Shaba
       3.        Tamaduni na Sikukuu
       4.        Pembe ya Wokovu
       5.        Mbuzi wa Azazeli (ZIADA)




MWEZI WA 3
       1.        Mtoto wa Bikra
       2.        Chipukizi/Shina la Haki
       3.        Watumishi Wanne(4)
       4.        Masihi
       5.        Siku za Mwisho (ZIADA)

MWEZI WA 4
       1.        Ruhama/Ishi
       2.        Mji wa Ninawi
       3.        Mwenye Haki/Imani
       4.        Mchungaji
       5.        Siku ya  Bwana (ZIADA)

III
KUMBU.TOR-JOSHUA




MWEZI WA 11
       1.        Musa
       2.        Agano
       3.        Adui Safarini/Majitu
       4.        Kiongozi Bora
       5.        Moyo na Kinywa (ZIADA)

MWEZI WA 12
       1.        Amri, Hukumu, Sheria
       2.        Ufalme wa Makuhani
       3.        Chagua-Baraka au Laana         4.        Pumziko la Joshua                5.        Kapteni (ZIADA)





JUMLA YA MASOMO=30
JUMLA YA MASOMO=20
JUMLA YA MASOMO=10


SOMO #1. HAPO MWANZO

SOMO #1. HAPO MWANZO
Andiko Kuu:- Mwanzo Sura ya 1 yote


1.      MAHUSIANO
Neno “Mungu” katika kitabu cha Mwanzo 1:1 ni ELOHIM, ni neno lenye uwingi katika umoja. Neno ELOHIM linabeba nafsi tatu katika umoja, hizi nafsi tatu bila shaka ni – Mungu Baba, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu au Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, kuwapanga huku hakumaanishi mmoja ni mkubwa kuliko mwingine ila kwa namna walivyo jitokeza kwetu.

·         UUMBAJI-           Mungu alitaka awe na MAHUSIANO NA MWANADAMU, ila asingeweza kuendesha mahusiano bila kuwa na MASKANI,kwahiyo andiko linaanza na kutuonyesha Mungu anavyoshughulika na maandalizi ya Maskani. Kuanzia  Mwanzo 1:1 mpaka Mwanzo 1:25-Mungu alikua akiandaa maskani ili aanze mahusiano na mwanadamu.

·         MWANADAMU             Kilele cha uumbaji wa Mungu ni mwanadamu, baada ya Mungu kua amemaliza kuandaa maskani  na siku ya kukutania (SABATO), ndipo alipomuumba na Mtu ili aanze Mahusiano nae. Kama tunavyojua mwanadamu ana asili mbili – Utu wa Ndani-Mwanzo 1:26-31 na Utu wa Nje-Mwanzo 2:7,15. Baada ya haya yote Mungu alikua akimtembelea Adamu muda wa Jua kupunga ili awe na mahusiano nae  “awe Mungu wake na Mtu awe Mtu wake”.

2.      DHAMBI
·         Mungu alimuumba Mwanadamu akiwa na Asili ya Mungu, alikua Mwenye Haki, Mtakatifu amejaa Utukufu na HIYARI.Mungu alimpa mwanadamu uhuru wa hiyari kwasababu alimuumba kwa mfano wake.Mwanadamu sio roboti au mwanasesele, haendeshwi na mitambo bali ni lazima achague kwa hiyari yake. Kwasababu mwanadamu ana uhuru ni lazima achague kutii na kuamini atakacho.

·         JARIBIO LA UTII –     Mungu alipenda kujua kama Adamu atamtii na Kumuamini anachosema au laa, wakati huo Shetani ambaye ni Baba wa Uongo nae yupo kazini kuhakikisha Mwanadamu hamtii Mungu na hivyo kuvunja  mahusiano. Mungu alitoa katazo-Mwanzo 2:17, Adamu alitii hii kauli siku zote mpaka siku Shetani aliyofanikiwa kumuingia Mwanamke-  Mwanzo 3:1-9. Hivyo Mwanadamu alifanya Dhambi kwa kumtii na kumuamini Shetani kuliko Mungu, matokeo yake ni KUFUKUZWA-Mwanzo 3:24, mahusiano YAKAVUNJIKA, mpaka Dhambi na urejesho wa utukufu vishughulikiwe kwanza, ndio maana Mungu akatoa Ahadi ya kuondoa Dhambi na kumrejeshea mwanadamu utukufu.

3.      UREJESHO

a.       MASIHI:-      Mungu alimpenda sana Mwanadamu, hivyo akawa na wivu nae lakini gharama ya kumrejesha ili mahusiano yaendelee ni kubwa mno, ikabidi Mungu awaahidi kwamba angalikuja mtu mwenye thamani atakae wafanyia UREJESHO,mtu huyo angeliitwa MASIHI- Mwanzo 3:15. Mungu alionyesha namna huyo masihi atavyowarejesha, kwa kuchinjwa – Mwanzo 3:21.

Kabla ya huyo masihi kuja, mwanadamu itatakiwa atoe sadaka ya mnyama aliye safi ili Dhambi yake iendelee kufunikwa kila mwaka, na kila asiyeua mnyama alionyesha kumtii na kumuamini Shetani kuliko Mungu kwani njia pekee ya kumkaribia Mungu ni kumwaga Damu isiyo na Hatia.

Mungu alionyesha NJIA YA UPATANISHO kwa mfano kwa kumvika Adamu Koti la Ngozi, wakati huo Damu ya mnyama ilifanya upatanisho, huu mfano ulipaswa uigwe na Wanadamu.Tatizo linakuja – Damu za wanyama hazikufaa KUMFUTIA HATIA MWANADAMU kwani uthamani wa Mwanadamu ni mkubwa kuliko wa mnyama, hivyo Damu ya mnyama ILIFUNIKA TU DHAMBI, na ndio maana Mungu akaahidi MASIHI ili arejeshe Mahusiano kwa KUFUTA DHAMBI – Isaya 59:20.

b.      ROHO MTAKATIFU:- Mwanadamu alipoasi alipungukiwa na utukufu, hivyo Mtu akishasamehewa Dhambi hupewa zawadi ya Roho Mtakatigu (Utukufu).Kama Mungu alivyoahidi kuwapa wanadamu ZAWADI ya MASIHI ndivyo Mungu alivoahidi kuwapa wanadamu ROHO WAKE MTAKATIFU – Isaya 44:3,kwahiyo Masihi na Roho Mtakatifu ni ZAWADI – Luka 24:49 ambazo Mungu aliziahidi ili arejeshe MAHUSIANO yaliyokua yamevunjika kwasababu ya Dhambi – Isaya 59:2.

Mungu alimpulizia PUMZI mwanadamu akawa nafsi hai lakini baada ya Dhambi Mungu hakumuona tena Adamu (alishakufa kiroho), ile pumzi ilikua imetoka, ndio maana Mungu akaahidi- atatia Roho yake na Mtu ataishi tena – Ezekieli 37:14.

c.       MAHUSIANO:- Mungu alianzisha Mahusiano, baada ya Dhambi mahusiano yakavunjika mpaka Dhambi ishughurikiwe na baada ya Dhambi kushughurikiwa mwanadamu anapewa utukufu tena na hatimae MAHUSIANO YALIYOVUNJIKA yanarejeshwa.Mahusiano haya tunaonjeshwa tukiwa hapa Duniani lakini Mahusiano kamili yatakua Mbinguni – Ufunuo 21:3-7, iko hivyo kwasababu Mahusiano ya Mungu na Adamu yaliendeshewa kwenye MASKANI YA EDENI, hapa Duniani hakuna Edeni, ndio maana Yesu akasema anakwenda kuandaa mahali – Yohana 14:2-3.

Licha ya Mungu kuahidi zawadi ya MASIHI na ROHO MT, pia aliahidi MAHUSIANO kurejeshwa, sharti likiwa ni kusamehewa Dhambi kwanza(kwa Yesu) na kupewa nguvu (Kwa ROHO MT), baada ya hapo Mwanadamu anaanza kuonja Mahusiano ya Mbinguni akiwa hapa Duniani – Mathayo 6:10. Mungu aliahidi kurejesha Mahusiano kwa kufanya Maskani yake kuwa katikati ya Wanadamu – Walawi 26:12, Ezekieli 27:37 “Mungu anakua Mungu wao na Watu wanakua watu wake”.

4.       HITIMISHO
·         Kuanzia sura ya 4 ya kitabu cha mwanzo mpaka malaki, kumejaa ahadi za ujio wa Masihi,ujazo wa Roho MT na urejesho wa Mahusiano, vitabu vya Injili vinaonyesha utimilizo wa Ahadi zilivyoahidiwa na Mungu-Yohana 4:25-26, 11:27. Nyaraka za mitume zinathibitisha utimilizo wa Ahadi – Mdo2:39, 13:23 na Efeso 2:22.Hivyo LEO hii tunaweza kudai kile kilichoahidiwa na kutimizwa na Mungu.
·         Kwanini Mungu anafanya haya yote? – Kwasababu ANAMPENDA Mwanadamu sana.

·         Hizi Zawadi zilizoahidiwa ndio zinaitwa EPANGELIA  na ndio mpango mkuu wa Mungu.

by 0753 011 774

SOMO #2. ADAMU NA HAWA

SOMO #2. ADAMU NA HAWA

Andiko Kuu- Mwanzo sura ya 3 yote.
  1.       ANGUKO (Kabla ya Yesu)
1.       Kila kilichoumbwa kilikuwa kikamilifu-Mwanzo 1:3
·         Anga - Jua, mwezi, nyota, sayari, mawingu nk
·         Dunia – Mimea, wanyama,miamba, madini nk
·         Bahari – Samaki wakubwa kwa Wadogo nk
2.       Mungu akaumba Mtu (Adam na Hawa)-Mwanzo 1:26
·         Walimuumba kwa MFANO wao na SURA yao
·         Ili Mtu awe - Mwenye HAKI, MTAKATIFU na MTUKUFU
3.       Dhumuni Kuu la Mungu kumuumba Mtu
·         Wawe na MAHUSIANO
·         Kwamba “Mungu awe Mungu wao na Watu wawe Watu wake”
4.       Adam na Hawa
·         Wanafanya DHAMBI kwani WALIMUAMINI na KUMTII Shetani kuliko Mungu
·         Matokeo ya Dhambi ni :- Kuvunjika kwa Mahusiano, Mtu alipoteza (Haki, Utakatifu na Utukufu), mwishowe AKAFUKUZWA-Mwanzo 3:24
·         Mtu akawa MTUMWA wa Dhambi, akawa (Anaona AIBU, UCHI, ANAJIFICHA)
5.       Njia ya Adam ya KUJISITIRI NA KUJIPATANISHA
·         Walidhani wangejisitiri kwenye vichaka
·         Walidhani wangeendeleza Mahusiano kwa upatanisho wa majani (Eproni)
·         Mungu anawakataa wao na njia zao zote walizobuni kwa laana-Mwanzo 3:1-3,16-19
6.       Njia ya Mungu ya KUSITIRI NA KUPATANA
·         Kondoo asiye na Hatia ANAUAWA – Ili Damu yake ifanye UPATANISHO na ngozi yake IWASITIRI na achukue adhabu ya Mtu. Alikuwa kama MWOKOZI- Mwanzo 3:20
·         Kwa kufa kwa Kondoo, Dhambi ILIFUNIKWA na HAIKUFUTWA, hivyo UREJESHO haukuwa kamili na Mahusiano yaliendelea NJE ya Bustani ya EDENI (MASKANI ya Mungu na Mtu)
7.       Mungu anatoa AHADI
·         Mungu alimpenda sana Adam ingawa alikuwa ameshaingiwa na dosari, sasa alikuwa na asili mbili (Asili ya Mungu na Shetani), na Mungu alijua Kondoo hawezi KUFUTA dhambi, na hizi Asili mbili zimeingia kwenye vizazi vyote vya Adam-50% kwa 50%
·         Mungu akatoa AHADI kwamba angelikuja MKOMBOZI afe badala yao ili Dhambi zao ZIFUTWE-Isaya 7:14,9:6-7, Imanueli maana yake ni Mungu pamoja nasi.
·         Lakini Kabla hajaja KRISTO ilitakiwa KAFARA iendelee kutolewa kila mwaka ili Dhambi ziendelee KUFUNIKWA na sio KUFUTWA mpaka itakapotolewa Kafara KAMILIFU, isiyo na WAA, wala ILA, au KUNYANZI – Kutoka 30:10


   2.       AGANO JIPYA (Wakati wa Yesu)
1.       Yesu KONDOO wa Mungu amekuja-Yohana 1:29,36
·         Kama Mungu alivyotoa Kondoo wakati wa Adam, ndivyo alivyotoa tena kwa ajili y a vizazi vyote vya Adam, tofauti ya kondoo huyu ni KUFUTA Dhambi zote.
·         Yesu ni Kondoo mkamilifu aliyeahidiwa. Fidia yake INATOSHEREZA malipo yote kwani UHAI wake unathamani kuliko chochote-Marko 14:24
·         Yesu ni Mwokozi HALISI sio kama Kondoo aliyefunika Dhambi- Luka 2:11
2.       Mungu Anamkataa Yesu
·         Kama Mungu alivyo MFUKUZA Adamu-Mwanzo 3:24, ndivyo alivyo MUACHA Yesu kwa sababu alikuja afe Badala ya Uzao wa Adam-Marko 15:34, Yohana 19:28.
·         Hivyo Yesu alikataliwa, na akaenda kuzimu ambapo angetakiwa kwenda Mwanadamu aliyeasi, lakini akaenda badala yake.

   3.       NYAKATI ZETU-mwaka 2017 (Baada ya Yesu )
1.       ASILI ya Adam na Yesu-1Wakorintho 15:21-22
·         Tunachukua Asili, sura na Chapa za Adam kwasababu tulizaliwa toka viunoni mwake, Adamu ni wa Chini na sisi ni wa Chini, Adam wa Udongo na sisi ni wa Udongo.
·         Habari njema ni kwamba Tukimwamini Mungu alichokifanya kwa ajili yetu kupitia Yesu, tunapokea ASILI mpya ya Yesu. Yesu alitoka juu, Yesu ni Roho inayohuisha, ndivyo tutakavyokuwa – 1 Wakorintho 15:45-49
2.       DAMU ya Yesu
·         Inasitiri (Covering), hivyo hutaona Aibu wala hutajificha tena-Warumi 4:7-8
·         Inatufanyia UPATANISHO kati ya Sisi na Mungu- Efeso 2:16
·         Kama hujui Damu ya Yesu inachofanya mpaka usamehewe, ndio inaitwa Imani. Unaamini vidonge vitakusaidia ingawa hujui vinafanyaje, ndio inaitwa Imani. Muamini Mungu kuwa anasamehe watu kupitiaa Damu ya Mtoto wake Yesu.


      4    HITIMISHO
CHUKUA HATUA-Warumi 10:9-10
LEO HII, MUDA HUU - 2Wakorintho 2:2-Ukimwamini Mungu alichokifanya kwa ajili yetu kupitia Yesu;- utasamehewa Dhambi, Utarejeshwa,Utasitiriwa, utapatanishwa, utarudishiwa (Haki, utakatifu na Utukufu), hutakuwa mtumwa tena wa Dhambi,na utakuwa na MAHUSIANO na Mungu tena.



By
 APOSTLE  ELIYA SIMON
THE EPANGELIA CHURCH
MAKULU-DODOMA MJINI
0753 011 774