Monday, February 17, 2014

Mchungaji Jennifer Cormack asimikwa kuwa Mchungaji kiongozi wa C.A.G Arusha, Sombetini.



Kanisa la Sombetini Arusha(Calvary Assemblies of God) jana limepata Mchungaji kiongozi ambaye ni Jennifer Cormack, Hapo awali kanisa hilo lilikuwa likiongozwa na Askofu Mkuu wa C.A.G ambae pia ni Mtume huku Jennifer Cormack akiwa Mchungaji msaidizi.

Ibada hio ilihudhuliwa na watu mbali mbali ikiwemo katibu mkuu wa C.A.G Mchungaji Zefania Ryoba ambae aliongozana na Mkewe. Katika ibada hio pia alikuwepo Askofu Mkuu wa C.A.G Mtume Dunstan Maboya.

Katibu Mkuu wa C.A.G Mchungaji Zefania Ryoba akifundisha
Askofu Mkuu wa C.A.G Dunstan Maboya, Mama Mchungaji Ryoba na Mchungaji Jennifer Cormack wakifatilia kwa umakini Neno la Mungu.
 Mchungaji Jennifer Cormack akipongezwa na kutiwa moyo kwa kazi ya Mungu anayoianza kwa Cheo tofauti ndani ya kanisa.


 Washirika wakifuatilia Ibada hio maalum ya kusimikwa kwa Mchungaji kiongozi







 Mchungaji Jennifer Cormack akiwa tayari kwa ajili ya kusimikwa kuwa Mchungaji kiongozi

Injili Forever inatoa pongezi maalumu kwa Mchungaji Jenifer Cormac kwa kusimikwa kwake ni ishara alikuwa mwaminifu katika nafasi yake ya Uchungaji msaidizi. 

Sunday, February 16, 2014

UKUMBI WA PTA WARINDIMA KWA MAOMBEZI YALIYOFANYWA NA WAPENTEKOSTE KWA TAIFA

Siku ya jana ndani ya ukumbi wa PTA uliopo ndani ya viwanja vya maonyesho vya mwalimu JK Nyerere almaarufu kama Sabasaba kulifanyika maombi maalumu kwa Taifa yakiongozwa na umoja wa makanisa ya Kipentekoste nchini. Katika maombi hayo yaliyohudhuriwa na waumini lukuki sambamba na wachungaji wao ilishuhudia askofu Zachary Kakobe pamoja na Josephat Gwajima wakiongoza maelfu ya waumini waliofika ukumbini hapo katika kuhubiri neno la Mungu kwa ufupi kisha kuingia katika maombi ambayo yaliandaliwa vyema na umoja huo.






PICHA YA SIKU


Saturday, February 15, 2014

it is well with my soul" / "Salama rohoni mwangu


Horatio Gates Spafford na Anna Spafford

Katika miaka ya 1860 Horatio aliishi na mke wake

 Anna Chicago,Marekani. Spafford alikuwa

 mwanasheria mkubwa aliyewekeza zaidi kwenye 

majengo (real estates). Maisha yalianza kubadilika

 mwaka 1870 ambapo mtoto wao pekee wa kiume

 alifariki kwa ugonjwa wa nimonia, Mda mfupi baadae

 janga la moto mkubwa wa Chicago uliteketeza 

sehemu kubwa sana ya mali zake.

Wakiwa na matumaini ya kupunguza maumivu

 waliyopata kutokana na matatizo yote,


Mwaka 1873 Spafford na mkewe walikubaliana

 kwenda Uingereza ambapo rafiki yake alikuwa ana

 hubiri injili.

Katika maandalizi ya mwisho kazi zilimbana Horatio, 

Akawaambia mke wake na watoto wake wakike 

wanne watangulie akiahidi kuwafuata haraka.

Ndipo jambo lisiloweza kufikirika likatokea, Boti 

aliyopanda mke wake na watoto wake ikapata ajali 

na watoto wake wote wanne walizama na kupoteza

 maisha, Mke wake pekee alipona nae baada ya

 kufika ufukweni akamuandikia note spaffors ikisema 

"Saved Alone, What shall I do?" yaani "Nimeokolewa

 peke yangu, Nitafanya nini?"


Horatio akiwa njiani kwenda kumfariji mke wake,

 akipita eneo ambalo watoto wake walizama na

 kupoteza maisha ndipo aliandika mashairi ya wimbo

 uliopata umaarufu sana mpaka miaka hii,

Wimbo unaitwa "it is well with my soul" / "Salama

 rohoni mwangu"

Haya hapa mashairi yake


When peace, like a river, attendeth my way,

When sorrows like sea billows roll;

Whatever my lot, Thou hast taught me to say,

It is well, it is well with my soul.

(Refrain:) It is well (it is well),

with my soul (with my soul),

It is well, it is well with my soul.

Though Satan should buffet, though trials should

 come,

Let this blest assurance control,

That Christ hath regarded my helpless estate,

And hath shed His own blood for my soul.

(Refrain)

My sin, oh the bliss of this glorious thought!

My sin, not in part but the whole,

Is nailed to His cross, and I bear it no more,

Praise the Lord, praise the Lord, O my soul!

(Refrain)

For me, be it Christ, be it Christ hence to live:

If Jordan above me shall roll,

No pain shall be mine, for in death as in life

Thou wilt whisper Thy peace to my soul.

(Refrain)

And Lord haste the day, when my faith shall be sight,

The clouds be rolled back as a scroll;

The trump shall resound, and the Lord shall descend,

Even so, it is well with my soul.

(Refrain)

Baadae Anna alibarikiwa na watoto watatu, Mmoja

 wa kiume ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka

 minne, na wakike wawili. Na baada ya mda walienda

 kuishi Israel na familia yake wakaanzisha kundi la

 kusaidia masikini huko Israel. 




Binafsi Siku ya leo wimbo huu umekua ukijirudia

 ndani yangu kila ninapotafakari matendo makuu

 ambayo Mungu amenifanyia hasa kwa kipindi hiki

 ambacho nimezungukwa na mambo mengi, siwezi

 kuwaza lolote Mungu ni muweza wa yote.

Chanzo: Injili Tanzania Blog

Friday, February 14, 2014

HITIMISHO LA MFUNGO WA SIKU 40 KWA WAPENTEKOSTE TAREHE 15 PTA


Siku 40 za mfungo wa makanisa ya Kipentekoste hatimaye unatarjiwa kumalizika tarehe 15, ambapo hitimisho lake litakuwa kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba, ambapo ratiba itaanza kuanzia saa tatu asubuhi na kuendelea.

Kufuatia hilo, mwenyekiti wa baraza la makanisa ya Kipentekoste kwa mkoa wa Dar es Salaam, Askofu Bruno Mwakibolwa anawaalika wachungaji, waalimu, wainjilisiti, mitume, na manabii wote wa pentekoste kwenye hitimisho la maombi hayo ambayo yalianza tarehe 6 Januari 2014.

Hitimisho la mfungo huu wa siku 40 linakuja ikiwa ni siku chache ambapo baraza la makanisa ya kipentekoste taifa (PCT) walitoa tamko kuhusiana na kutoridhishwa na namna Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wa wajumbe wa bunge maalumu la katiba, huku akiacha kuteua mjumbe angalau mmoja kutoka  PCT, na hivyo kutokuwa sehemu ya utungaji wa katiba hiyo mpya katika hatua iliyofikia.

Maaskofu wa PCT wakati wakitoa tamko kuhusu uteuzi wa wabunge wa bunge malumu la katiba jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne. ©fb/ufufuo crew


Katika tamko la maaskofu hao, mwenyektiti wa PCT taifa, Askofu David Batenzi alisema kuwa baraza hilo linaundwa na makanisa takriban 75, huku wakiwa na mamilioni ya waamini, jambo ambalo kutengwa kwao na kuchukua wajumbe kutoka TEC, CCT na Baraza la Waislamu tu ni kutotendewa haki.

Baraza la makanisa ya Kipentekoste nchini linaundwa na makanisa 75, ambapoi kwa uchache wao ni Tanzania Assemblies of God (TAG), Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT), Glory of Christ Church Tanzania (GCCT - Ufufuo na Uzima), Naioth Gospel Assembly (NGA), Kanisa la Pentekoste Tanzania (KLPT), Efatha, Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT), Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) na kadha wa kadha.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusiana na siku ya hitimisho ya kufunga na kuomba, unaweza kuwasiliana na Askofu Bruno Mwakibolwa kwa simu namba 0713418660.

Source: Gospel Kitaa Blog

Sunday, February 2, 2014

ATAKUOKOA NA MATESO SITA


Wimbo wa Injili mpya uliotungwa na Robert Maziku umepokelewa vyema na wapenzi wa nyimbo hizo hasa ni mpangilio wa ujumbe uliomo ambao sehemu kubwa umetoka kitabu cha Ayubu 5:19 (Yeye atakuokoa na mateso sita: Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.), Ayubu 14:8-9 Inasema Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo, 9. Lakini kwa Harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche.

Robert Maziku anawimbo mmoja tu ambao ameimba kama Single artist Ingawa ni mtunzi na mwalimu mzoefu wa kwaya. Kwaya ambazo alishawahi kuzifundisha ni PRS CHOIR ya Dodoma, Kahama Revival ya Wilayani Kahama, Kwaya ya Casfeta Jamhuri Sekondari (Dodoma), Kwaya ya TAFES Hombolo Dodoma, Amani kwaya ya Heaven of Peace Christian Church (Morogoro) na kwa sasa anafundisha kwaya ya Nazareth katika huduma ya Bethel Jijini Dar-es-salaam.

Wimbo wake huo umerekodiwa katika Studio ijulikanayo ALFA ONE LOVE PRODUCTION chini ya Producer kijana Baraka Nathan huku video ikifanywa na BRG ENTERTANMENT chini ya Director Steve Manrizo.

Kwa mwaliko au kutaka kujua chochote kuhusu kazi hii piga 0653340950