Friday, February 14, 2014

HITIMISHO LA MFUNGO WA SIKU 40 KWA WAPENTEKOSTE TAREHE 15 PTA


Siku 40 za mfungo wa makanisa ya Kipentekoste hatimaye unatarjiwa kumalizika tarehe 15, ambapo hitimisho lake litakuwa kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba, ambapo ratiba itaanza kuanzia saa tatu asubuhi na kuendelea.

Kufuatia hilo, mwenyekiti wa baraza la makanisa ya Kipentekoste kwa mkoa wa Dar es Salaam, Askofu Bruno Mwakibolwa anawaalika wachungaji, waalimu, wainjilisiti, mitume, na manabii wote wa pentekoste kwenye hitimisho la maombi hayo ambayo yalianza tarehe 6 Januari 2014.

Hitimisho la mfungo huu wa siku 40 linakuja ikiwa ni siku chache ambapo baraza la makanisa ya kipentekoste taifa (PCT) walitoa tamko kuhusiana na kutoridhishwa na namna Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wa wajumbe wa bunge maalumu la katiba, huku akiacha kuteua mjumbe angalau mmoja kutoka  PCT, na hivyo kutokuwa sehemu ya utungaji wa katiba hiyo mpya katika hatua iliyofikia.

Maaskofu wa PCT wakati wakitoa tamko kuhusu uteuzi wa wabunge wa bunge malumu la katiba jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne. ©fb/ufufuo crew


Katika tamko la maaskofu hao, mwenyektiti wa PCT taifa, Askofu David Batenzi alisema kuwa baraza hilo linaundwa na makanisa takriban 75, huku wakiwa na mamilioni ya waamini, jambo ambalo kutengwa kwao na kuchukua wajumbe kutoka TEC, CCT na Baraza la Waislamu tu ni kutotendewa haki.

Baraza la makanisa ya Kipentekoste nchini linaundwa na makanisa 75, ambapoi kwa uchache wao ni Tanzania Assemblies of God (TAG), Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT), Glory of Christ Church Tanzania (GCCT - Ufufuo na Uzima), Naioth Gospel Assembly (NGA), Kanisa la Pentekoste Tanzania (KLPT), Efatha, Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT), Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) na kadha wa kadha.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusiana na siku ya hitimisho ya kufunga na kuomba, unaweza kuwasiliana na Askofu Bruno Mwakibolwa kwa simu namba 0713418660.

Source: Gospel Kitaa Blog

No comments:

Post a Comment