Thursday, December 5, 2013

UTUME, UNABII NA MIUJIZA UNAVYO LIPASUA KANISA.










Na Robert E. Maziku 0653340950

1wakorintho 12:4~6
Efeso 4:11~13

Bwana Yesu asifiwe,
Nimekuwa nikifurahishwa sana na ninapo sikia Mtumishi fulani anatumiwa na Mungu katika upande fulan ikiwa yote ni kuujenga mwili wa Kristo. Kwa mfano ni nadra kumpata mtumishi aliyekilimiwa huduma zote tano kwa maana ya Mtume, Mchungaji, Nabii, Mwinjilisti na Mwalimu.
Kumekuwa na huduma tatu ambazo mtu akisikiwa anayo wala watu hawashtuki nadhani hii inatokana na fikra kuwa hizo ni kawaida mtu kuwanayo ambazo ni UCHUNGAJI, UINJILISTI na UWALIMU. Utata huwa unaanza pale mtu anapojitambulisha ni NABII au MTUME, hii inatokana na watu au wapendwa kuzipa uadimu ndani ya kanisa.
Kabla sijaendelea hebu niweke kamsingi kadogo hapa, DHEHEBU sio WOKOVU. Dhehebu huweka mipango mbalimbali ili kumfikia Mungu yaani Mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu, wakati tunapozungumza wokovu, ni mpango wa Mungu kumtafuta Mwanadamu.
Kwa msingi huo, kanisa au dhehebu ili angalau litimize lengo la kumtafuta Mungu basi yapaswa kanisa/Dhehebu kuwa na huduma zote tano kwa wakati mmoja kwani hivi vitu vinasaidiana katika utenda kazi.


CHANZO CHA MPASUKO.
Kumekuwa na hofu ya kuibiwa washirika kutokana na uwepo wa watumishi wajiitao manabii ambao wamekuwa na mvuto kwa watu kutokana UPAKO na MIUJIZA. Mtumishi ambae si Nabii ila ni Mwalimu au Mchungaji tu wamejikuta wakianzisha siasa za dini yaani kupanga mipango ya kuwachafua hao wenye upako ili kurejesha washirika.
Nimejaribu kujiuliza hivi, kuna Mtumishi gani hapa Tanzania au nje ya Tanzania mwenye neema ya kutumiwa katika ishara na miujiza hajawahi kuchafuliwa kutokana na Huduma yake?? Jibu ni hakuna hebu angalia hii list halafu ujiulize nani hana kashfa, NABII GB MALISA, ASKOFU ZACHARY KAKOBE, MH. GEODAVY, ASKOFU DUNSTAN MABOYA, MCH. GWAJIMA, NABII TB. JOSHUA, NABII UEBERT ANGEL, MCH BULDOZER MWAMPOSA ASKOFU MWINGIRA na wengine uwajuao wewe wenye neema hiyo wote hawa wana kashfa ya uchawi sasa tatizo ni upako au uchawi?.
Kumekuwa na kamsemo cha kawaida sana siku hizi mtu asikiapo habari za matendo makuu ya Mungu utasikia ZICHUNGUZENI HIZO ROHO!!, sawa hata mimi nakubaliana na hilo neno ila tatzo huwa hawazichunguzi hizo Roho zaidi yakuishia kuhubiri ubaya wa Mtumishi. Kunasiku rafiki yangu mmoja alikuwa anajaribu kunionesha ni namna gani Mama Rwakatale na Mzee wa Upako wanatumia uchawi kwa kutoa pointi ya kitoto kabisa, anasema kwenye TV matangazo yao huwa yana EFFECT(mionzi flani ambayo huonekana mikononi ikimaanisha nguvu). Akadai utatoaje hizo nguvu Mtumishi wa Mungu kama mchawi, nikagundua hizo ndizo siasa za kanisa.


UTUME, UNABII NA MIUJIZA UNAVYO LIPASUA KANISA.
Mtazamo wa Manabii na Mitume kwa sasa hakuna na kama wapo ni wachache ndio unao sababisha haya yote. Shetani amekuwa akifurahia sana hivi vikumbo. Katika hao nilio wataja hapo juu na wale ambao sijawataja ila wapo katika njia hio ni ngumu sana kuwasikia kwenye vyombo vya habari wakiwaponda watumishi wengine zaidi sana hao walio kinyume nao kuwasikia wakiwaponda. Hivi inakuwaje mtu yuko radhi kuamini mchawi anauwezo wa kumrudisha mtu mzukule ila haamini kama Gwajima anaweza akatumiwa na Mungu kuwarudisha mizukule??, Mtu kuombewa akiwa mbali bila kuguswa akapona watu wanashangaa wanasahau kama kuna mitume waliponya kwa VIVULI vyao!! Sasa hivi kanisa limegawanyika, wapo wanao chukulia kama MIUJIZA ni mpango wa shetani kukamata watu na wapo wanao amini MIUJIZA ni mpango wa Mungu kuwa hudumia watu.


PONGEZI
Pongezi za pekee ziende kwa Mchungaji Swai wa T.A.G Mwanza kwakuwa Mtumishi asiye kuwa na udini wa Udhehebu ndani yake. Amekuwa baba wa Kiroho mzuri wa Mchungaji Gwajima pamoja na kuwa tofauti kihuduma kwa sasa ila amekuwa akimtia moyo wakati huo kuna walokole wako kidini zaidi hawawezi kumtia moyo au kumkubali mtumishi asiye katika Dhehebu lake.
 Mchungaji Gwajima na Mchungaji Swai wakisaidiana kumchakaza Shetani Tanga
PONGEZI YA PILI
Nawashukuru waimbaji wainjili wamekuwa wakikwepa sana Dhambi ya ubaguzi na kutoa hukumu zisizo na uhakika kiroho. Siajabu kumuona Flora Mbasha akihudumu katika mkutano usio wa EAGT, Sio yeye bali waimbaji wengi wako hivyo najua yawezekana sababu ya ikawa ni masilahi lakini hata kama mimi huwa nasema IWE KWA HAKI AMA KWA HILA INJILI ITAHUBIRIWA(INJILI FOREVER).
 Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha wakifatilia mkutano Tanga
 John Lisu kama kawaida akiongoza sifa katika mkutano wa Injili chini ya kanisa la UFUFUO NA UZIMA
WITO WANGU
Naomba watu tukubali kuwa Mungu anauwezo wakufanya zaidi ya fikra zetu, Pia tuchunge sana maneno yetu kwani muda mwingi yamekuwa yakimsifia shetani badala ya Mungu. Kwa mfano unapo kubali kuwa shetani anaweza kufanya jambo fulani halafu hilohilo unakataa Mungu hawezi hapo shetani unamfurahisha sana. TUZICHUNGUZE HIZO ROHO, Hakikisha unazichunguza sio unaishia kusema halafu huchunguzi, hata mimi najua shetani anambinu nyingi za kukamata ikiwemo hizo za kutumia manabii wa wauongo kwahio tuwe makini tusimkatae Mtumishi kisa hatumiwi kama Mchungaji wako.


HII NDIO INJILI FOREVER


No comments:

Post a Comment