Monday, October 28, 2013

WITO NA UTUMISHI




WITO NA UTUMISHI
By Apostle Eliya

YALIYOMO;
  1. Utangulizi, 2. Wito, 3. Utumishi, 4. Hitimisho

DHUMUNI
-         Kuonyesha njia sahihi ya kuwa Mtumishi
-         Kusaidia mtu ajue Wito wake

ANDIKO KUU;- MATENDO 13:2-3 “…..nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia

1. UTANGULIZI
- Maisha ya Binadamu hayatakuwa na matokeo makamilifu mpaka siku atayogundua Wito wake. Kwanini Mungu alikuumba ? Kwanini upo Duniani ?.

-Kuna aina nyingi za wito, lakini nataka nizungumzie Wito wa Utumishi. Wito hautegemei elimu, fedha, muonekano ,umasikini. Wito ni wewe.

2. WITO
Maana Ya Wito
-Wito ni kitendo cha KUMSIKIA Mungu akitoa majukumu ya utumishi wako.
YEREMIA 1:5, ISAYA 42:6-7
Dhumuni la Wito
- Dhumuni la kuitwa ni Mungu anataka jambo litendeke kwa kupitia wewe, kwahiyo wewe unakuwa ni chombo, kazi yako ni kutii na kutenda.
YEREMIA 51:20-23
a) Naanzanje safari yangu ?
- Mambo mawili ya msingi katika mwanzo wa mchakato;-
     (1) Amini injili (2) Pokea zawadi( Roho Mt)
INJILI- Ni habari njema za Yesu kuhusu msamaha kamili wa dhambi zote, injili ina habari nne kuu;- Maji, Damu, Mwili na Msalaba.-RUMI 1:16, Unaiamini Injili kwa kuliamini JINA LA YESUMdo 4:12, 16:31

ROHO MTAKATIFU Ni zawadi pekee, ni ahadi pekee ya Mungu kwa anaeiamini injili. Huwa anatoa hii zawadi kwa kupitia watumishi aliowatia muhuri. Hakikisha unakuwa na Roho Mt, sio hisia-hisia.
MATENDO 2:38-39,5:32, YOEL 2:32, ISAYA 44:3, YEREMIA 36:27.

b) Mungu anamuitaje mtu ?
- Ingawa Mungu huwa anaita watu kwa namna tofauti lakini anatumia njia moja ya mawasiliano kwa kila muitwaji. Mungu huwasiliana na mwanadamu kwa njia ya sita ya ufahamu ya mtu(fourth dimension), namaanisha Mungu hutumia MAONO, NDOTO, MASIKIO YA NDANI, MACHO YA NDANI.

- Mungu ni Roho, huwa anapenda kuongea na roho aliyompa mwanadamu kwa njia ya Yesu na kupita Roho Mt.WAEBRANIA 1:1-2, YOHANA 10:4,16,27. Naomba nikwambie kwamba Mungu anataka kila mtu aweze kumsikia.

c) Utajuaje Wito wako ?
- Wito wako ni lazima uanzie ndani, Mungu atakuambia wito wako kwa kupitia MAONO(MDO 18:9), NDOTO(1Falme 3:5), KUSIKIA(1 Falme 19:13) NA KUONA KWA UTU WA NDANI(Ufu 1:12), hizi njia nne za mawasilia ninaziita kwa jina moja KUSIKIA au KUWA ROHONI(Ufu 1:10). Kwahiyo ili ujue wito wako utatakiwa USIKIE KWA BIDII. TORATI 28:1, YEREMIA 1:7,9-10. 

- Baada ya kuwa UMESIKIA KWA BIDII wito wako, usikulupuke, subiri uthibitisho, Mungu atamtumia Mtumishi wake ( aliyeamini injili na kupokea Roho Mt)aje akuthibitishie huo wito wako, au ataongea na wewe kwa mara ya pili, mpaka mara ya tatu. MATENDO 9:17-18, 1 SAM 3:8-9

d) Nianze Utumishi?
- Kutokana na ulivyosikia, Mungu atatimiza kile alichokwambia, huwa analiangalia Neno lake, we anza huduma usiogope. ISAYA 55:11.Mungu atatuma watumishi kwa ajili yako, -- Mdo 18:26.

e) Sina Pesa,nitaanzaje huduma ? WALAWI 10:13
- Makuhani walikula matoleo yaliyosongezwa kwa moto, Moto ni Roho Mt, kwahiyo utakapoanza kufanya huduma kwa Moto(Roho Mt), Mungu atakupa matunzo kwa huo moto, Roho Mt. hutatumia nguvu kupata pesa, yeye Mungu atawaamulu watu walete - MITHALI 8:18-21,sababu ni moja --- umefanya kazi kwa Roho Mt MDO 28:8-10, wala hukutumia Moto wa kigeni     WALAWI 10:1

3. UTUMISHI

Wito ni tofauti kwa watumishi lakini misingi ya utumishi ni sawa.
a)Misingi Miwili ya Utumishi sahihi;-- MDO 2:38
- Misingi hii ni (1) Injili na (2) Kutoa vipawa.WAEBRANIA 8:3
Kila mtumishi wa kweli lazima awe nahii misingi, hii misingi ndiyo itakayokupa uelekeo wa wito wako ambao ni tofauti na mwingine.

b) Makuhani na misingi yao.
-Makuhani Agano la kale walikuwa na kazi kuu mbili, kufanya upatanisho na kutoa vipawa WAEBRANIA 8:3. Mtumishi wa Agano jipya anatakiwa kuhubiri ondoleo la dhambi kwa njia ya Yesu(Injili) MARKO 16:15, na kuwezesha watu kupokea Roho Mt YOHANA 20:22

c) Tofauti za Utumishi 

-  Kama uliamini Injili kwa usahihi, ukapokea zawadi kwa usahihi, Mungu hana ujanja, lazima akwambie kwa kupitia Simu yake Roho Mt eneo alilokuitia. Hapa sitaweza kueleza sana kwasababu hii ni siri kati yako na Roho wa Mungu. 1 KORINTHO 12:4-6, WAKOLOSAI 1:26-27

d) Kipi Cha Kuzingatia

- Kama utumishi wako ulianza kwa KUSIKIA Roho Mt, utatakiwa kuendelea kusikia na kutii 100% unachoelekezwa na Roho Mt, hii ndio inaitwa Sabato. Mungu hataki wanaojitolea kumtumikia 1 SAMWEL 16:1, TORATI 18:5, anataka wanaoisikia sauti yake siku zote YEREMIA 18:1-2, Kama Baba yako alikuteua au Jopo la maaskofu waliona unafaa badili mtazamo.

e) Nitamjuaje Mtumishi wa Kweli na Mshirika wa kweli? ,Rahisi sana;

 MTUMISHI --- (1) Anahubiri Injili (2) Anatoa vipawa
MSHIRIKA --- (1)Anaamini Injili  (2) Anapokea Vipawa

Kigezo cha INJILI kinasaidia kuvumbua wanaotumia nguvu za giza na Mawakala wa shetani,ukweli ni kwamba hakuna shetani hata mmoja anaeweza kuhubiri injili, hakuna. -- WAGALATIA 1:8, 2 KORINTHO 11:4,Mdo 4:18

Kigezo cha VIPAWA kinasaidia kuvumbua wale waliojiita, wanaosema watatumia elimu zao, kuna walioona maisha magumu wakaona utumishi unalipa. Mtu ambaye Mungu hajamuita hata afanyaje hawezi kuwapa watu zawadi au vipawa ( Roho Mt). -- MATENDO 19:6, 10:44,

f) Kuna Watumishi feki ?
- Ndiyo. 
Ufeki wa watumishi upo wa aina mbili;
(1) Mawakala wa shetani siku zote wanaipinga Injili wanapinga maji ya Yesu,damu ya Yesu,mwili wa Yesu na msalaba wa Yesu.
(2) Watafuta pesa Wanaikubali injili na wanaiamini, tatizo hawajaitwa, matokeo yake wanashindwa kutoa vipawa, mafundisho yao ni pesa, zaka ni amri, wanataka sana heshima, waitwe majina makubwa- baba askofu, watafanya juu chini waonekane njema, wao huwa hawatoi vipawa ni kupokea tu zaka na sadaka.- MATENDO 19:1-3, watumishi hawa mara nyingi wanatumia moto wa kigeni sijui siku ya hukumu itakuwaje !!!!

4. HITIMISHO

- Kuna watu wengi walioanza utumishi bila kujua hizi kanuni, usijali, anza upya kwa kufuata utaratibu hapa chini ;

          a) Tamani/omba Mungu akupe NENO-Isa 44:3, Math 7:11
     b) Tarajia KUSIKIA —Danieli 2:17-19, Habakuki 2:1-2
     c) Amini(believe) utakayo YASIKIA —Mwanzo 15:6
     d) Fanya(Faith)uliyo YASIKIA —Yohana 14:12
     e) Kiri/tamka Imani yako —Warumi 10:10b
     f) Mungu atakutumia —Yeremia 1:12, Isaya 55:11

…………….THE BEST HAS COME…………………

2 comments:

  1. aisee imekaa vizuri mtumishi............huu moto wa kigeni ndo upi hasa???

    ReplyDelete
    Replies
    1. NINAJIBU SWALI LAKO KWA KUANDIKA SOMO LA MOTO WA KIGENI,PITIA TENA BLOG NIMERUSHA SOMO LA MOTO WA KIGENI

      Delete