Tuesday, February 25, 2014

Misri na Historia ya Biblia

Farao wa Misri



Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 1

Biblia iliandikwa katika kipindi cha miaka 1,600 hivi. Historia na unabii unaopatikana ndani yake unahusiana na serikali saba kuu za ulimwengu: Misri, Ashuru, Babiloni, Umedi na Uajemi, Ugiriki, Roma, na Muungano wa Uingereza na Marekani. Serikali hizo saba zitazungumziwa katika mfululizo wa makala saba. Kusudi la makala hizo ni nini? Kuonyesha kwamba Biblia inategemeka na imeongozwa na roho ya Mungu na kwamba ujumbe wake unatoa tumaini—tumaini la kwamba matatizo yanayosababishwa na utawala mbaya wa wanadamu yatakwisha.
MISRI, inayojulikana sana kwa piramidi zake na Mto Nile, ilikuwa serikali kuu ya kwanza katika historia ya Biblia. Taifa la Israeli lilitokezwa chini ya ulinzi wake. Musa aliyeandika vitabu vitano vya kwanza vya Biblia, alizaliwa na kuelimishwa huko Misri. Je, historia na vitu vya kale vilivyochimbuliwa vinapatana na mambo ambayo Musa aliandika kuhusu nchi hiyo ya kale? Chunguza mifano michache.

Historia Inayotegemeka

Majina ya cheo.

Mara nyingi historia sahihi huonekana kupitia habari zinazotajwa—utamaduni, njia ya kufanya mambo, majina ya maofisa na majina yao ya cheo, na kadhalika. Je, habari inayopatikana katika vile vitabu viwili vya kwanza vya Biblia, Mwanzo na Kutoka, ni sahihi? J. Garrow Duncan anatoa maelezo haya katika kitabu chake New Light on Hebrew Origins kuhusu simulizi la Yosefu mwana wa mzee wa ukoo Yakobo, linalopatikana katika kitabu cha Mwanzo, na pia kuhusu kitabu cha Biblia cha Kutoka: “[Mwandikaji huyo wa Biblia] alifahamu vizuri lugha, utamaduni, imani, maisha katika makao ya mfalme, njia ya kufanya mambo, na jinsi maofisa walivyofanya kazi huko Misri.” Anaongezea hivi: “[Mwandikaji] anatumia majina sahihi ya cheo kama yalivyotumiwa katika kipindi anachozungumzia. . . . Kwa kweli, hakuna kitu kingine kinachothibitisha kwamba waandikaji wa Agano la Kale wana ujuzi wenye kina wa mambo ya Misri na wanategemeka, kuliko utumizi wa neno Farao katika vipindi mbalimbali.” Duncan anaendelea kusema: “Wakati [mwandikaji] anapowaonyesha wahusika wake wakiwa mbele ya Farao, anawaonyesha wakifanya mambo kwa njia inayofaa na wakizungumza kwa njia inayostahili.”


Matofali yaliyotengenezwa kwa nyasi na kukaushwa juani


Bado matofali yaliyotengenezwa kwa nyasi na kukaushwa juani yanatumiwa Misri leo

Kutengeneza matofali.

Wakati wa utumwa wao huko Misri, Waisraeli walitengeneza matofali yaliyochanganywa na nyasi, iliyotumiwa kama kiunganishi. (Kutoka 1:14; 5:6-18) * Miaka fulani iliyopita, kitabu Ancient Egyptian Materials and Industries kilisema hivi: “Ni katika maeneo machache tu ambapo [utengenezaji wa matofali] umefanywa kuliko unavyofanywa huko Misri, ambako tangu zamani matofali yaliyokaushwa kwenye jua ndiyo  yanayotumiwa zaidi katika ujenzi nchini kote.” Kitabu hicho pia kinataja “zoea la Wamisri la kutumia nyasi kutengeneza matofali,” na hivyo kuthibitisha jambo hilo la ziada linalotajwa katika Biblia.


Baadhi ya vifaa vya kunyoa vya Misri


Baadhi ya vifaa vya kunyoa vya Misri—wembe na kioo

Kunyoa ndevu.

Wanaume Waebrania wa nyakati za kale walikuwa na ndevu. Hata hivyo, Biblia inatuambia kwamba Yosefu alinyoa ndevu kabla ya kusimama mbele ya Farao. (Mwanzo 41:14) Kwa nini alizinyoa? Ili atende kulingana na utamaduni wa Misri kwani walimwona mtu aliye na nywele usoni kuwa mchafu. “[Wamisri] walijisifu kwa kunyoa ndevu zote,” kinasema kitabu Everyday Life in Ancient Egypt. Kwa kweli, vikasha vya kujipodoa vimepatikana katika makaburi vikiwa na nyembe, vibano, na vioo. Kwa wazi, Musa aliandika mambo kwa usahihi kabisa. Jambo hilohilo linaweza kusemwa kuwahusu waandikaji wengine wa Biblia walioandika matukio kuhusu Misri ya kale.

Biashara.

Yeremia, aliyeandika vitabu viwili vya Wafalme, alitoa habari hususa kuhusu biashara ya farasi na ya magari kati ya Mfalme Sulemani na Wamisri na Wahiti. Gari liligharimu “vipande 600 vya fedha, na farasi . . . vipande 150,” au robo ya gharama ya gari, inasema Biblia.—1 Wafalme 10:29.
Kulingana na kitabu Archaeology and the Religion of Israel, uthibitisho uliotolewa na mwanahistoria Mgiriki Herodoto na uliopatikana katika vitu vilivyochimbuliwa unathibitisha kwamba biashara kubwa ya farasi na magari iliendelezwa wakati wa utawala wa Sulemani. Kwa kweli, “ilikuwa kawaida kubadilisha farasi wanne . . . kwa gari moja la Misri,” kitabu hicho kinasema, na hilo linathibitisha tarakimu zinazoonyeshwa katika Biblia.

Vita.

Yeremia na Ezra wanataja pia kuhusu Farao Shishaki aliyeivamia Yuda, wakitaja kihususa kwamba uvamizi huo ulitukia “katika mwaka wa tano wa Mfalme Rehoboamu [wa Yuda],” au 993 K.W.K. (1 Wafalme 14:25-28; 2 Mambo ya Nyakati 12:1-12) Kwa muda mrefu sana, habari pekee iliyopatikana kuhusu uvamizi huo ilikuwa ile ya Biblia. Kisha mchoro ukapatikana katika ukuta wa hekalu la Karnak (Thebesi ya kale) huko Misri.
Mchoro huo unamwonyesha Shishaki akiwa amesimama mbele ya mungu Amoni, mkono wa Shishaki ukiwa umeinuliwa akiwachinja mateka. Pia majina ya miji ya Israeli iliyoshindwa imeandikwa katika mchoro huo, na mengi ya miji hiyo inahusianishwa na maeneo yanayotajwa katika  Biblia. Zaidi ya hilo, maandishi hayo yanataja “Shamba la Abramu”—na hayo ndiyo maandishi ya kale zaidi ya Misri kumtaja mzee wa ukoo Abrahamu anayetajwa katika Biblia.—Mwanzo 25:7-10.
Ni wazi kwamba waandikaji wa Biblia hawakuandika mambo ya kuwaziwa. Wakitambua kwamba wanawajibika mbele za Mungu wao waliandika ukweli, hata wakati ambapo kufanya hivyo hakukupendeza—kama ilivyokuwa na ushindi wa Shishaki dhidi ya Yuda. Unyoofu huo unatofautiana sana na maandishi ya waandishi wa kale Wamisri ambao walikataa kuandika chochote ambacho kingewashushia heshima watawala au watu wa Misri.

Unabii Unaotegemeka

Ni Yehova Mungu peke yake, Mtungaji wa Biblia, anayeweza kutabiri wakati ujao kwa usahihi. Kwa mfano, ona kile ambacho alimwongoza Yeremia kutabiri kuhusu majiji mawili ya Misri—Memfisi na Thebesi. Wakati mmoja Memfisi, au Nofu lilikuwa kituo maarufu cha kibiashara, kisiasa, na kidini. Lakini Mungu alisema hivi: “Nofu litakuwa kitu cha kushangaza na kwa kweli litawashwa moto, hivi kwamba lisiwe na mkaaji.” (Yeremia 46:19) Na hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa. Kitabu In the Steps of Moses the Lawgiver kinasema kwamba “magofu makubwa sana ya Memfisi” yaliporwa na washindi Waarabu, ambao walitumia mawe ya jiji hilo kwa ajili ya ujenzi. Kitabu hicho kinaongezea kwamba leo “hakuna jiwe linaloonekana juu ya udongo mweusi wa jiji hilo la kale na eneo linalozunguka.”


A statue from ancient Egypt


Sanamu hii kubwa iliyopatikana karibu na Memfisi ikiwa imeanguka ilikuwa na kimo cha mita 12 hivi
Thebesi, ambalo zamani lilijulikana kama No-amoni au No, lilipatwa na msiba kama huo, pamoja na miungu yake isiyojiweza. Yehova alisema hivi kuhusu mji huo ambao wakati mmoja ulikuwa mji mkuu wa Misri na kituo cha ibada ya mungu Amoni: “Tazama, ninakaza fikira zangu juu ya Amoni . . . na juu ya Farao na juu ya Misri na juu ya miungu yake . . . Nami nitawatia . . . mkononi mwa Nebukadreza mfalme wa Babiloni.” (Yeremia 46:25, 26) Kama ilivyotabiriwa, mtawala wa Babiloni alishinda Misri na jiji hilo maarufu lililoitwa No-amoni. Kisha, baada ya mtawala wa Uajemi Cambyses wa Pili kulishinda jiji hilo kwa mara nyingine katika mwaka wa 525 K.W.K., lilipoteza umaarufu wake upesi na mwishowe likaharibiwa kabisa na Waroma. Naam, unabii sahihi unafanya Biblia iwe kitabu kisichoweza kulinganishwa na kitabu kingine, na hivyo kufanya tuwe na uhakika kuhusu mambo inayosema juu ya wakati wetu ujao.

Tumaini Lenye Kutegemeka

Unabii wa kwanza katika Biblia uliandikwa na Musa wakati wa utawala wa serikali kuu ya  ulimwengu ya Misri. * Unabii huo unaopatikana katika Mwanzo 3:15, unasema kwamba Mungu angetokeza “uzao,” ambao ungemponda Shetani na “uzao” wake, yaani, wale wanaotenda kulingana na njia za Shetani zenye uovu. (Yohana 8:44; 1 Yohana 3:8) Sehemu ya msingi ya “uzao” wa Mungu ilikuja kuwa Masihi, Yesu Kristo.—Luka 2:9-14.
Kristo ataitawala dunia yote naye ataondoa uovu na ukandamizaji wote unaoletwa na serikali za wanadamu. Mwanadamu hataendelea ‘kumtawala mwanadamu kwa kumuumiza.’ (Mhubiri 8:9) Zaidi ya hilo, kama Yoshua wa kale ambaye aliwaongoza Waisraeli kwenye Nchi ya Ahadi, Yesu ataongoza “umati mkubwa” wa wanadamu wanaomwogopa Mungu waingie katika ‘Nchi kubwa zaidi ya Ahadi’—dunia iliyosafishwa na kufanywa kuwa paradiso.—Ufunuo 7:9, 10, 14, 17; Luka 23:43.
Tumaini hilo lenye thamani linatukumbusha unabii mwingine ulioandikwa katika nyakati za Misri ya kale. Katika Ayubu 33:24, 25, unabii huo unasema kwamba Mungu atawakomboa wanadamu kutoka “shimoni,” au kaburini, kupitia ufufuo. Naam, mbali na wale watakaookoka uharibifu unaokuja wa waovu, mamilioni ya wengine waliokufa watafufuliwa wawe hai wakiwa na taraja la kuishi milele katika Paradiso duniani. (Matendo 24:15) “Hema la Mungu liko pamoja na wanadamu,” inasema Ufunuo 21:3, 4. “Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena.”
Historia na unabii wenye kutegemeka—mambo hayo yataendelea kuzungumziwa katika makala ifuatayo ya mfululizo huu, ambayo itakazia fikira Ashuru ya kale, serikali kuu ya ulimwengu iliyofuata baada ya Misri.

Kanisa lavamiwa Jijini Dar

Vitendo vya kuvamiwa kwa makanisa nchini, vimekosa mwarobaini hivyo kuvutia maadui wa ukristo kuendelea kuharibu nyumba za ibada bila hofu. Tukio la hivi karibuni, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mbezi Kati, kuvamiwa usiku tena wakati ambao vijana walikuwa wakiendela na mkesha ni ushahidi kuwa hali inazidi kuwa mbaya badala ya suluhisho kupatikana.
   

 Mchungaji Samson Swai wa kanisa hilo, akizungumza na chazo cha habari alisema kuwa, Ijumaa flani majira ya saa saba usiku, alipigiwa simu na vijana waliokuwa katika mkesha kanisani hapo na kumjulisha kuwa palikuwa na mtu aliyefahamika (jina tunalihifadhi kwa sasa) ameliharibu kanisa kwa kubomoa milango yote.
  
Aliongeza kuwa mara baada ya taarifa hiyo alipiga simu kituo cha Polisi Kawe, na kuwajulisha kuhusu tukio na walipofika eneo la tukio,mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa maeneo hayo alikwisha kimbilia nyumbani kwake.

  Alisema, uharibifu uliofanywa na mtu huyo majira hayo ya usiku mnene bila sababu ya msingi ni kuing'oa milango vibaya.Kwa mujibu wa Mchungaji Swai, Polisi walionyeshwa nyumba anamoishi mtuhumiwa huyo na walipofika nyumbani kwake kwa lengo la kujua sababu ya kufanya uharifu huo, hakuwafungulia mlango licha ya kumgongea  kwa muda mrefu lakini  jitihada hizo ziligonga mwamba, hivyo Polisi kuahidi kumfuatilia.
 Mchungaji Swai aliweka wazi kuwa, ikiwa Serikali haitaiangalia kati suala la uvamizi wa makanisa na kulishughulikia kwa jicho pevu; huenda vikatokea vita vya kidini, wakristo watakapochoka na matukio hayo kila kona.

 Mtumishi huyo alisema baada ya kushindwa kumpata mtu huyo, Polisi waliondoka eneo hilo, na kesho yake mtu huyo aliendelea kujigamba kuwa, Jeshi la Polisi limeshindwa kumtia hatiani ili aeleze nani anamtuma kufanya uhalifu katika nyumba ya Bwana.

Mtu huyo anayehisiwa kuwa, pengine alikuwa na silaha ya moto, anadaiwa kuendelea kutamba mitaani kuwa hakuna wa kumfanyajambo lolote na ataendelea na mashambulizi yake.

Pengine Serikali isipokuwa makini na kung'oa mizizi hii, hali ya vurugu inaweza kuchukua nafasi mpya na kusababisha kutoweka kwa amani na kuifanya Tanzania yenye sifa ya kuwa 'kisiwa cha amani' kupoteza sifa hiyo ya kipekee na kuingia kwenye sintofahamu.

Chanzo chetu kilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, ambaye alisema kuwa, taarifa ya kuvamiwa kwa kanisa haijafika mezani kwake na kuahidi kulifuatilia, na kubainisha kibarua hicho amemwachia OCD kulifuatilia kwa karibu ili apate taarifa. 
 
                                             Chanzo:Jesus vision
 

Sunday, February 23, 2014

Monday, February 17, 2014

Mchungaji Jennifer Cormack asimikwa kuwa Mchungaji kiongozi wa C.A.G Arusha, Sombetini.



Kanisa la Sombetini Arusha(Calvary Assemblies of God) jana limepata Mchungaji kiongozi ambaye ni Jennifer Cormack, Hapo awali kanisa hilo lilikuwa likiongozwa na Askofu Mkuu wa C.A.G ambae pia ni Mtume huku Jennifer Cormack akiwa Mchungaji msaidizi.

Ibada hio ilihudhuliwa na watu mbali mbali ikiwemo katibu mkuu wa C.A.G Mchungaji Zefania Ryoba ambae aliongozana na Mkewe. Katika ibada hio pia alikuwepo Askofu Mkuu wa C.A.G Mtume Dunstan Maboya.

Katibu Mkuu wa C.A.G Mchungaji Zefania Ryoba akifundisha
Askofu Mkuu wa C.A.G Dunstan Maboya, Mama Mchungaji Ryoba na Mchungaji Jennifer Cormack wakifatilia kwa umakini Neno la Mungu.
 Mchungaji Jennifer Cormack akipongezwa na kutiwa moyo kwa kazi ya Mungu anayoianza kwa Cheo tofauti ndani ya kanisa.


 Washirika wakifuatilia Ibada hio maalum ya kusimikwa kwa Mchungaji kiongozi







 Mchungaji Jennifer Cormack akiwa tayari kwa ajili ya kusimikwa kuwa Mchungaji kiongozi

Injili Forever inatoa pongezi maalumu kwa Mchungaji Jenifer Cormac kwa kusimikwa kwake ni ishara alikuwa mwaminifu katika nafasi yake ya Uchungaji msaidizi. 

Sunday, February 16, 2014

UKUMBI WA PTA WARINDIMA KWA MAOMBEZI YALIYOFANYWA NA WAPENTEKOSTE KWA TAIFA

Siku ya jana ndani ya ukumbi wa PTA uliopo ndani ya viwanja vya maonyesho vya mwalimu JK Nyerere almaarufu kama Sabasaba kulifanyika maombi maalumu kwa Taifa yakiongozwa na umoja wa makanisa ya Kipentekoste nchini. Katika maombi hayo yaliyohudhuriwa na waumini lukuki sambamba na wachungaji wao ilishuhudia askofu Zachary Kakobe pamoja na Josephat Gwajima wakiongoza maelfu ya waumini waliofika ukumbini hapo katika kuhubiri neno la Mungu kwa ufupi kisha kuingia katika maombi ambayo yaliandaliwa vyema na umoja huo.






PICHA YA SIKU


Saturday, February 15, 2014

it is well with my soul" / "Salama rohoni mwangu


Horatio Gates Spafford na Anna Spafford

Katika miaka ya 1860 Horatio aliishi na mke wake

 Anna Chicago,Marekani. Spafford alikuwa

 mwanasheria mkubwa aliyewekeza zaidi kwenye 

majengo (real estates). Maisha yalianza kubadilika

 mwaka 1870 ambapo mtoto wao pekee wa kiume

 alifariki kwa ugonjwa wa nimonia, Mda mfupi baadae

 janga la moto mkubwa wa Chicago uliteketeza 

sehemu kubwa sana ya mali zake.

Wakiwa na matumaini ya kupunguza maumivu

 waliyopata kutokana na matatizo yote,


Mwaka 1873 Spafford na mkewe walikubaliana

 kwenda Uingereza ambapo rafiki yake alikuwa ana

 hubiri injili.

Katika maandalizi ya mwisho kazi zilimbana Horatio, 

Akawaambia mke wake na watoto wake wakike 

wanne watangulie akiahidi kuwafuata haraka.

Ndipo jambo lisiloweza kufikirika likatokea, Boti 

aliyopanda mke wake na watoto wake ikapata ajali 

na watoto wake wote wanne walizama na kupoteza

 maisha, Mke wake pekee alipona nae baada ya

 kufika ufukweni akamuandikia note spaffors ikisema 

"Saved Alone, What shall I do?" yaani "Nimeokolewa

 peke yangu, Nitafanya nini?"


Horatio akiwa njiani kwenda kumfariji mke wake,

 akipita eneo ambalo watoto wake walizama na

 kupoteza maisha ndipo aliandika mashairi ya wimbo

 uliopata umaarufu sana mpaka miaka hii,

Wimbo unaitwa "it is well with my soul" / "Salama

 rohoni mwangu"

Haya hapa mashairi yake


When peace, like a river, attendeth my way,

When sorrows like sea billows roll;

Whatever my lot, Thou hast taught me to say,

It is well, it is well with my soul.

(Refrain:) It is well (it is well),

with my soul (with my soul),

It is well, it is well with my soul.

Though Satan should buffet, though trials should

 come,

Let this blest assurance control,

That Christ hath regarded my helpless estate,

And hath shed His own blood for my soul.

(Refrain)

My sin, oh the bliss of this glorious thought!

My sin, not in part but the whole,

Is nailed to His cross, and I bear it no more,

Praise the Lord, praise the Lord, O my soul!

(Refrain)

For me, be it Christ, be it Christ hence to live:

If Jordan above me shall roll,

No pain shall be mine, for in death as in life

Thou wilt whisper Thy peace to my soul.

(Refrain)

And Lord haste the day, when my faith shall be sight,

The clouds be rolled back as a scroll;

The trump shall resound, and the Lord shall descend,

Even so, it is well with my soul.

(Refrain)

Baadae Anna alibarikiwa na watoto watatu, Mmoja

 wa kiume ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka

 minne, na wakike wawili. Na baada ya mda walienda

 kuishi Israel na familia yake wakaanzisha kundi la

 kusaidia masikini huko Israel. 




Binafsi Siku ya leo wimbo huu umekua ukijirudia

 ndani yangu kila ninapotafakari matendo makuu

 ambayo Mungu amenifanyia hasa kwa kipindi hiki

 ambacho nimezungukwa na mambo mengi, siwezi

 kuwaza lolote Mungu ni muweza wa yote.

Chanzo: Injili Tanzania Blog

Friday, February 14, 2014

HITIMISHO LA MFUNGO WA SIKU 40 KWA WAPENTEKOSTE TAREHE 15 PTA


Siku 40 za mfungo wa makanisa ya Kipentekoste hatimaye unatarjiwa kumalizika tarehe 15, ambapo hitimisho lake litakuwa kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba, ambapo ratiba itaanza kuanzia saa tatu asubuhi na kuendelea.

Kufuatia hilo, mwenyekiti wa baraza la makanisa ya Kipentekoste kwa mkoa wa Dar es Salaam, Askofu Bruno Mwakibolwa anawaalika wachungaji, waalimu, wainjilisiti, mitume, na manabii wote wa pentekoste kwenye hitimisho la maombi hayo ambayo yalianza tarehe 6 Januari 2014.

Hitimisho la mfungo huu wa siku 40 linakuja ikiwa ni siku chache ambapo baraza la makanisa ya kipentekoste taifa (PCT) walitoa tamko kuhusiana na kutoridhishwa na namna Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wa wajumbe wa bunge maalumu la katiba, huku akiacha kuteua mjumbe angalau mmoja kutoka  PCT, na hivyo kutokuwa sehemu ya utungaji wa katiba hiyo mpya katika hatua iliyofikia.

Maaskofu wa PCT wakati wakitoa tamko kuhusu uteuzi wa wabunge wa bunge malumu la katiba jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne. ©fb/ufufuo crew


Katika tamko la maaskofu hao, mwenyektiti wa PCT taifa, Askofu David Batenzi alisema kuwa baraza hilo linaundwa na makanisa takriban 75, huku wakiwa na mamilioni ya waamini, jambo ambalo kutengwa kwao na kuchukua wajumbe kutoka TEC, CCT na Baraza la Waislamu tu ni kutotendewa haki.

Baraza la makanisa ya Kipentekoste nchini linaundwa na makanisa 75, ambapoi kwa uchache wao ni Tanzania Assemblies of God (TAG), Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT), Glory of Christ Church Tanzania (GCCT - Ufufuo na Uzima), Naioth Gospel Assembly (NGA), Kanisa la Pentekoste Tanzania (KLPT), Efatha, Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT), Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) na kadha wa kadha.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusiana na siku ya hitimisho ya kufunga na kuomba, unaweza kuwasiliana na Askofu Bruno Mwakibolwa kwa simu namba 0713418660.

Source: Gospel Kitaa Blog

Sunday, February 2, 2014

ATAKUOKOA NA MATESO SITA


Wimbo wa Injili mpya uliotungwa na Robert Maziku umepokelewa vyema na wapenzi wa nyimbo hizo hasa ni mpangilio wa ujumbe uliomo ambao sehemu kubwa umetoka kitabu cha Ayubu 5:19 (Yeye atakuokoa na mateso sita: Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.), Ayubu 14:8-9 Inasema Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani, Na shina lake kufa katika udongo, 9. Lakini kwa Harufu ya maji utachipuka, Na kutoa matawi kama mche.

Robert Maziku anawimbo mmoja tu ambao ameimba kama Single artist Ingawa ni mtunzi na mwalimu mzoefu wa kwaya. Kwaya ambazo alishawahi kuzifundisha ni PRS CHOIR ya Dodoma, Kahama Revival ya Wilayani Kahama, Kwaya ya Casfeta Jamhuri Sekondari (Dodoma), Kwaya ya TAFES Hombolo Dodoma, Amani kwaya ya Heaven of Peace Christian Church (Morogoro) na kwa sasa anafundisha kwaya ya Nazareth katika huduma ya Bethel Jijini Dar-es-salaam.

Wimbo wake huo umerekodiwa katika Studio ijulikanayo ALFA ONE LOVE PRODUCTION chini ya Producer kijana Baraka Nathan huku video ikifanywa na BRG ENTERTANMENT chini ya Director Steve Manrizo.

Kwa mwaliko au kutaka kujua chochote kuhusu kazi hii piga 0653340950