Friday, March 21, 2014

MWIGIZAJI WA HOLLYWOOD AMPATIA RIHANNA UJUMBE KUTOKA KWA ROHO MTAKATIFU

Rihanna akijipiga picha ya mchoro(tattoo) wa msalaba aliyojichora hivi karibuni.
Mwigizaji nyota wa nchini Marekani Stephen Baldwin amemtumia ujumbe maalumu kutoka kwa Roho mtakatifu mwimbaji maarufu wa muziki wa nje ya kanisa Rihanna kutokana na wimbo wake uitwao "What Now" ambao unapatikana katika album yake iitwayo 'Unapologetic' aliyoitoa mwaka juzi.

Kupitia anuani yake ya twitter jumanne hii mwigizaji huyo aliandika kwamba huwa hana kawaida ya kufanya kile ambacho anakifanya(kuandika ujumbe) huo, lakini ameiona video ya wimbo wa 'what now' ya mwimbaji Rihanna ambayo mwishoni kuna mwanga umepita ukionyesha msalaba, huku
Stephen Baldwin.
mwimbaji huyo akimalizia kwakusema …hajui aende wapi" na kwamba Roho mtakatifu anajibu kwamba "ni kweli unajua, umenifahamu mimi kitambo sasa toka ulipokuwa mtoto, unakumbuka jina la Yesu, ni nuru ya uso wako, ni furaha ya moyo wako, rudi kwa Yesu" ndivyo alivyoandika mwigizaji huyo huku chanzo cha habari hii kikisema hapana shaka ujumbe huu ulikuwa mahususi kwa mwanadada huyo ambaye jina lake la kuzaliwa ni Robyn Rihanna Fenty.

Baldwin ameongeza kwamba "pia kama ukipata nafasi ikiwa ni dakika ya 3:29 katika video iliyopo YouTube, najisikia Roho mtakatifu ananiambia kitabu cha Yohana 3:29……

Mwigizaji huyo ambaye alimkabidhi Yesu maisha yake baada ya tukio la kigaidi la septemba 11 mwaka 2001 huko nchini Marekani, alitoa ujumbe huu kwa wafuasi wake 35,000 katika anuani yake ya twitter akiwataka kuusoma ujumbe huo huku pia ikiwa haijulikani kama moja ya lengo la mwigizaji huyo ni kukutana na Rihanna kisiri ili kumuhubiria injili ya Yesu. Rihanna ambaye amekulia katika mazingira ya Kikristo katika visiwa vya Barbados inasemekana hataki kuweka bayana imani yake mbele za watu kwakuogopa kupoteza mashabiki ambao wamejigawa katika makundi mbalimbali yakiwepo ya wasiomwamini Mungu, wanaomwamini na wale wa imani nyingine.

Ujumbe wa Stephen kutoka katika anuani yake ya twitter.

Wednesday, March 19, 2014

Gospel Hip Hop wamwita Msama



WAIMBAJI wa miondoko ya muziki wa Injili wa kufokafoka ‘Gospel Hip Hop’ wametoa wito kwa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, kuelekeza nguvu zake katika miondoko hiyo.
Kwa mujibu wa mwimbaji wa nyimbo hizo, Faraja Kampambe ‘Hurukweli’, Msama ni mfano wa kuigwa katika muziki wa Injili ambao unafikisha ujumbe wa Neno la Mungu kwa Jamii.
Hurukweli alisema, Msama anatakiwa kugeukia miondoko hiyo ili kupata ladha tofauti ya ufikishaji wa huduma ya Neno la Mungu kupitia waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje.
Aidha, Hurukweli alisema wakati akimuomba Msama aelekeze nguvu kwenye miondoko hiyo, hivi sasa amekamilisha albamu ya nyimbo nane alizorekodi katika Studio ya K Production ya Tabata na Pantu iliyoko Sinza jijini Dar es Salaam.
Hurukweli anaitaja albamu hiyo kuwa ni ‘Kila Mwenye Pumzi’, ikiwa na nyimbo kama ‘Saa ya Wokovu’, ‘Upendo wa Yesu’, ‘Nitarap Tu’, ‘Sauti Hii’, ‘My Life’, ‘Let it Go’ na ‘Zinduka’.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Tuesday, March 18, 2014

Tanganyika ni nchi iliyonenwa katika unabii – Mchungaji Mtikila

MTIKILA (1)
HOJA MAALUM
MCHAKATO WA KATIBA MPYA USITISHWE
(ILI UANZE UPYA KWA USAHIHI)

Waheshimiwa Wajumbe, huu ni ushauri wa kizalendo kwa wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kwamba mchakato mzima wa Katiba mpya ubatilishwe pamoja na Rasimu ya Katiba, kwa misingi ifuatayo: KIGEZO CHA KWANZA Mchakato wa Katiba halali ya wananchi lazima uanze na uelimishaji wa wananchi wote, kwa sababu wananchi walio wengi hawajui kabisa suala la Katiba, kiasi cha wengine kudhani katiba ni aina fulani ya mboga, wakati ni jambo la msingi wa Taifa lolote duniani linalomhitaji kila mwananchi ashiriki, kama inavyoagiza Ibara ya 21(2) ya Katiba yetu iliyopo, kwamba ni haki ya kila raia kushiriki kwa ukamilifu. Katiba ya Nchi ni lazima itokane na makubaliano ya raia wote, tena kutokana na uelewa sahihi wa kila mmoja wao. Ndiyo maana hatua ya kwanza na muhimu kuliko zote ya kutengeneza Katiba ya Nchi ni uelimishaji makini wa familia yote, zoezi ambalo linaweza kuchukua miaka, kama wenzetu wa Kenya walivyotumia takriban miaka mitatu kuelimisha umma wao ingawa uliokuwa na ufahamu kuliko umma wetu. Ni dhahiri kwamba hata ukusanyaji wa maoni uliofanyika hauna uhalali, kwa sababu yalichukuliwa maoni ya katabaka ka wananchi wachache sana wenye uelewa. Haijalishi hata kama hao waelewa wachache walitoa maoni mazuri yakatengenezewa Rasimu hii, Katiba inamtaka kila raia aeleweshwe vizuri ili ashiriki kwa ukamilifu. Ni usanii kusema wanakusanya maoni ya watu, wakati watoaji wa maoni wametegewa sheria kandamizi kama za “Uchochezi’’ ili wasizungumzie machafu ya watawala yaliyowatesa kwa miaka 53 ya uhuru, kusudi waweze kuyadhibiti vizuri katika Katiba yao. Ndiyo maana tulisema kwanza yafutwe yale masheria kandamizi, ili raia wakishaelimishwa kuhusu Katiba yao waweze kutoa maoni yao bila woga. Hakuna mjadala hapa, kinachotakiwa ni utekelezaji wa matakwa ya Katiba, siyo matakwa ya Rais au CCM. Katiba inataka itumike HAKI sawa kuunda chombo cha haki sawa na wajibu sawa kwa nchi yetu kwetu sisi sote na vizazi vyetu vyote vijavyo. Mchakato wa Katiba unaoendeshwa bila uelewa na uhuru kamili wa wananchi, moja kwa moja unakuwa hauna uhalali, haijalishi hata kama mapesa mengi kiasi gani yametumika katika haramu hiyo. Haramu haiwezi kuzaa halali. Bunge maalum la Katiba linapaswa kuukataa. Katiba inayotokana na kugoma kuwapa ufahamu sawa wananchi wote, na kutumia maoni ya kakundi kadogo tu ka wananchi kwa kuwapuuza raia zaidi ya milioni 46 si halali, tena ni ubaguzi wa kikatili na ukiukaji wa Ibara ya 12 na ya 13 ya Katiba ya Jamhuri. Haramu haiwezi kuzaa halali. Ni wajibu wa Bunge maalum la Katiba kuukataa mchakato mzima wa Katiba mpya, kwa uaminifu kwa Mungu, kwa Wana wa Tanganyika na wananchi wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar. KIGEZO CHA PILIKusimamiwa na watawala utengenezaji wa Katiba ya wananchi, tena viongozi wa CCM isiyoficha azma yake ya kutawala juu ya wenzao milele licha ya kuchukiwa vibaya sana na wananchi, kunafuta kabisa uhalali wa mchakato mzima wa Katiba. Serikali ni kiungo kilicho ndani ya Katiba ambayo ni ya Wananchi, kama isemavyo Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri kwamba mamlaka yote ya utawala wa nchi yamo mikononi mwa wananchi wenyewe, yaani hata mamlaka ya utengenezaji wa Katiba yao wanayo wao, si ya Rais au serikali yenye kuajiriwa tu na wananchi! Kitendo cha Rais cha kuteua yeye Tume ya kukusanya Maoni bila kuwaelewesha kwanza wananchi, na kuipa yeye maelekezo, na kuilipa mapesa lukuki kama rushwa, na kuwanyangánya raia haki yao ya kuhoji juu ya uhalali wa muungano, kinapoteza uhalali wa mchakato mzima wa Katiba, Ndugu Wajumbe, kitendo cha Rais cha kuteua yeye wajumbe wa Bunge la Katiba kwa kuzingatia maslahi yake binafsi na ya chama ckake, badala ya kuwaelewesha wananchi wote vyakutosha, ili wachague wao wenyewe wajumbe wao katika Bunge maalum la Katiba yao, kutokana na kuwaamini jinsi walivyo na mzigo juu ya hatima ya nchi yao na hatima yao na watoto wao, kimelikosesha Bunge hili uhalali Bunge maalum la Katiba limekoseshwa uhalali na Rais Kikwete, kwa kupendelea wanasiasa kwa asilimia 90% na hasa wa chama chake, aliowapenyeza kwa wingi kwa kutumia taasisi za kiraia, majority ya wabunge wao katika Bunge la Muungano, Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar iliyojitoa katika muungano (kitendo ambacho ni matusi kwa Watanganyika), ilimradi CCM wajipatie theluthi mbili za kujipitishia maslahi yao. Katika Watanganyika milioni 48 wanasiasa wako takriban milioni 5, hivyo kwamba wananchi milioni 43 wamepuuzwa katika mchakato wa Katiba. Kwahiyo Katiba itakayoundwa haitakuwa ya Wananchi au Taifa bali ya katabaka kadogo tu. Miongoni mwa wananchi milioni 43 waliopuuzwa ni Jumuiya ya Wapentecoste (PCT) yenye walokole takriban milioni 10, ambao Rais Kikwete amekataa kuwapa uwakilishi katika Bunge maalum la Katiba! Ndugu wajumbe, kuwanyima wananchi wengi namna hii uwakilishi katika Bunge la Katiba ya wananchi wote, kwa kisingizsio chochote kile, kumefuta kabisa uhalali wa Bunge hili. Katika mchakato halali wa Katiba utakaoanza upya, Wawakilishi wa wananchi watachaguliwa na wananchi wenyewe. Ndugu Wajumbe, hata Libya kulikomwagika mito ya kutisha ya damu, tumeshuhudia juzi wananchi wake wakipiga kura kuwachagua wawakilishi wao katika Bunge lao la Katiba. Bunge letu limekosa uhalali kwa kuteuliwa na mtu mmoja tu badala ya kuchaguliwa na wenye nchi. Rais amekiuka Katiba ya Nchi yetu Ibara ya 8, na Ibara ya 21 (2), na Ibara ya 26 (1). Kwahiyo imetupasa sisi Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kutoa Tamko kwa uaminifu na heshima kwa Taifa letu kwamba: 1. Bunge maalum la Katiba lenyewe halina uhalali. 2. Mchakato wa Katiba mpya uanze upya kwa usahihi, kwa kuanza na kufuta sharia kandamizi na kuuelewesha umma kwa makini. Kuitishwa Kongamano la Kitaifa la Katiba hakuwezi kukwepeka katika utengenezaji wa Katiba halali ya wananchi, ambao lazima ufuatie ueleweshaji makini wa wananchi wote, kusudi wote watoe maoni yao kwa uelewa na uzalendo. Ni hilo Kongamano ambalo litateua serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa, ambayo itasimamia mchakato mzima wa Katiba kizalendo na bila upendeleo. Baada ya kukamilisha utengenezaji wa Katiba, Serikali ya mpito ya umoja wa Kitaifa itaitumia Katiba hiyo kwa uchaguzi, na kukabidhi uongozi kwa Serikali mpya itakayochaguliwa kwa Katiba hiyo mpya. Utaratibu huu wa kupata Katiba halali ya wananchi unawezekana tu ikiwa CCM itakuwa imepona ubinafsi na uchoyo wa madaraka, na ikiwa kweli CCM wanayo dhamiri safi na ustarabu wa kuheshimu usawa wa wananchi wote. CCM walikataa utaratibu huu wa haki na usawa, kwa sababu ya uovu wao wa kutaka wawe watawala tu wengine wote tuwe watawaliwa wasio na haki kama wao, unaowafanya wazidi kuchukiwa nchini kote na kubaki kutawala kwa nguvu za dola badala ya ridhaa ya wananchi. KIGEZO CHA TATU Tamko la kiimla la Rais Kikwete kwamba muungano usijadiliwe katika mchakato wa Katiba mpya ya wananchi, linafuta uhalali wa mchakato wenyewe pia. Kwani muungano ni uhusiano wa nchi mbili unaopaswa kuwa wa hiari ya raia wenyewe na siyo ya watawala! Rais amekiuka Ibara ya nane ya Katiba ya Nchi. Upungufu huu wa Rais unachangiwa na udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na Bunge la Jamhuri, alipolihutubia kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2005, alipotamka kuwa hataitii Katiba kama vile msahafu, bali katika mambo mengine atatumia busara yake! Badala ya kumwondoa katika ajira ya wananchi aliyoiapia kwamba ataitii na kuilinda na kuitetea Katiba ya Nchi, akainua msahafu juu na kumwambia Mwenyezi Mungu amsaidie, Wabunge wetu walimshangilia! Si ajabu leo Rais kujisahau akatumia imla katika suala la muungano, wakati ndio msingi wa mengine yote katika mchakato wa Katiba mpya! Rais anapaswa kufahamu kuwa suala la muungano linahusu Uhuru wa Wazanzibari na Uhuru wa Wana wa Tanganyika! Msingi wa Taifa la Watanganyika ni Uhuru wa Tanganyika, kama na Taifa la Wazanzibari lilivyoanza na Uhuru wa Zanzibar.Muungano wao ni uhusiano tu wa nchi na nchi, ambao malengo pekee huwa ni maslahi, hivyo kwamba muungano ukithibitika kuwa unaathiri Uhuru wetu na uchumi wetu sisi Watanganyikatunapaswa kujitoa mara moja, kama ilivyojitoa rasmi Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Ndiyo maana Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipitisha lile Azimio la kuundwa Serikali ya Tanganyika, mwaka 1994, hivyo kwamba wajibu wa Bunge maalum la Katiba ni kuwawajibisha wale waliokiuka Uamuzi huo wa Bunge, ambao kikatiba una uzito wa Sheria, na kuhakikisha kwamba Azimio hili linatekelezwa. Katika Nchi yenye Utawala wa Sheria hakuna kujadili jambo lililopitishwa na Bunge, bali utekelezaji tu wa hilo lililopitishwa. Usahihi (Constitutionality) wa agizo la Rais Kikwete kwamba muungano usijadiliwe katika mchakato wa Katiba mpya ya wananchi, ungesimama katika uadilifu wake wa kuzingatia kiapo chake cha kuitii na kuilinda na kuitetea Katiba ya Nchi, akitetea Azimio lililopitishwa na Bunge la Jamhuri la kuundwa Serikali ya Tanganyika kwamba ni la kutekelezwa tu na siyo kujadiliwa(Suala hili la “muungano” limeelezwa kwa kina zaidi katika Sehemu ya Pili ya Waraka huu) Mchakato pekee ulio na uhalali ni wa Katiba ya Watanganyika, ambao wanapaswa kuunda Serikali yao. Uhuru wao hauhamishiki wala haubadilishiki kwani ni haki yao ya Msingi ya kujitunza uhai wao na watoto wao ndani ya mipaka ya ardhi yao. Haki ya Watanganyika ya Uhuru wao walipewa na Mungu, kama wanadamu wengine wote katika mipaka ya ardhi yao. Ni matusi makubwa kwa Watanganyikia hata kama hawasemi, kwa Zanzibar iliyojitoa katika muungano kuleta wawakilishi wengi kuzidi Tanganyika yenyewe katika Bunge maalum la Katiba, ambalo kimsingi ni la Watanganyika, tena wakaleta mpaka na baraza lao la Wawakilishi lililouvunja muungano kwa kuitoa Zanzibar, bila hata haya kwa kuwachukulia Watanganyika kuwa ‘mataahira’ tu! Saa ya ukombozi ni sasa! Matusi kwa Watanganyika ni machungu zaidi wakoloni wao waliojitoa katika muungano, ambao wako milioni 1 tu, wanapokuwa na wajumbe wengi kuwazidi Watanganyika milioni 48, kiasi cha Wazanzibari kutulazimisha kwa huo uwingi wao kuwa chini ya Uwenyekiti wa muda wa Kificho wao katika Bunge maalum la Katiba! Kutokana na ule unyani, tende na halua zimewafanya wauzaji wa Uhuru na heshima ya Watanganyika wafanye makusudi kwamba chaguzi zote zikifanyika Watanganyika wawe katika minyororo ya Wazanzibari. Ndugu Wajumbe, kila mwadamu aliumbwa na nationalistic spiritau uhanga kwa ajili ya nchi yake pamoja na ndugu zake wa Taifa lake. Ndiyo maana wazee wetu walipouzana utumwani kwa tamaa ya tende na halua tu, wazungu waliotutangulia kustarabika walitudhania kuwa aina fulani ya nyani. Siyo ajabu kuonekana hata leo Mtanganyika anauza au kutoujali utaifa wake na ardhi yake na utambulisho wake (national identity), kwani bado tunao watumwa wenye “unyani” wa kuuza utaifa wetu kwa tende na halua. Ni matusi kuiita Tanganyika “Tanzania Bara” “Unyani” ule ndio unaowafanya baadhi ya Watanganyika wafurahie kongwa la utumwa wetu kwa Wazanzibari, ambao hata baada ya kujitoa rasmi katika muungano feki, bado wanaendelea kutawala Watanganyika na kuishi kwa damu yao, Manzibari mmoja akiwa amepewa thamani ya Watanganyika 48 katika kuitawala Tanganyika, lakini gharama za nchi zote mbili zinabebwa na Watanganyika! KIGEZO CHA NNE Mchakato wa Katiba ukiwa nje ya misingi ya Katiba na Sheria unakuwa BATILI. Rais, Wajumbe wa Tume ya kuratibu maoni na Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba, wanalazimishwa na Ibara ya 26(1) kutii Katiba na Sheria za nchi. Kwa sababu wakipuuza au kukiuka Katiba au Sheria wanakuwa wamepoteza uhalali wa hiyo Tume au hilo Bunge pamoja na maamuzi yake Mfano wa kwanza ni kitendo cha Rais cha kupokonya haki ya wananchi ya kujichagulia wao wenyewe wawakilishi wao katika Bunge maalum la Katiba, akatuteua yeye sisi wajumbe wa Bunge hilo! Ni kosa kubwa pia Rais kuteua yeye Tume ya kuratibu maoni, ambayo kimsingi ilipasa kuchaguliwa na wananchi wenyewe! Rasimu ya Katiba inayotokana na makosa haya haiwi na uhalali, kwa sababu ni ya watawala na siyo ya wananchi, tena ni ukiukaji wa Ibara ya 8 ya Katiba. Isitoshe, Rais aliipa Tume yake ya kuratibu maoni ya wananchi na kutengeneza Rasimu ya Katiba posho ya shilingi 500,000 kwa siku mbali ya mamilioni ya mshahara mwisho wa mwezi, nyumba yenye kodi ya shilingi milioni kadhaa kwa mwezi, shangingi la zaidi ya shilingi milioni 60 kila mmoja, na madereva akawalipia posho ya shilingi 220,000 kila mmoja kwa siku, lakini akawadhalilisha Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba lenye kuikataa au kuipitisha hiyo Rasimu, yaani liko juu kabisa ya hiyo Tume, kwa kuwapa posho ya dereva wa mjumbe wa Tume ya shilingi 220,000 tu! Kwa busara hata ya mtoto mdogo, Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba anapaswa kupewa mafao ya juu kuliko mjumbe wa Tume ya Warioba. Kama Rais alifanya kosa kuwapendelea wajumbe wa Tume yake ya Maoni, basi hapaswi kusahihisha kosa kwa kosa kubwa zaidi! Kama Rais hawezi kusahihisha kosa lake kwa kuwabana wajumbe wa Tume ya Warioba warudishe mabilioni ya fedha aliyowapa, ili wawe wamelipwa kwa usahihi yaani chini ya kiwango cha Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba, basi usahihi na busara pekee ni kuwalipa Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba juu zaidi kuliko wajumbe wa Tume. Tena ni marufuku kukiuka Ibara ya 13 ya Katiba ya Nchi kwa kuwalipa Wabunge wa Bunge la Muungano mishahara na posho zao juu ya mafao ya Bunge maalum la Katiba. Ikiwa kosa hili limefanyika ni lazima na Wajumbe 201 walioteuliwa wepewe hiyo tofauti, ili kufuta kosa kubwa ladiscrimination lililofanyika. Hili ni suala lisilohitaji mjadala wala kubembeleza mtu, bali ni suala la usahihi na busara. Mfano wa pili nikitendo cha Tume ya Warioba ya kuratibu maoni na mchakato mzima kwa jumla, cha kupuuza kesi muhimu sana iliyo katika Mahakama Kuu ya Zanzibar, ambayo wananchi wanataka uvunjwe muungano unaounganisha Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika! Katiba inayotokana na kutojali Katiba na Sheria na kudharau Mahakama kiasi hiki haiwezi kuwa na uhalali. Mfano wa tatu ni kitendo cha Tume ya kuratibu maoni ya Katiba, inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa zamani Joseph Warioba, cha kuendelea na kukusanya maoni juu ya Haki ya kila raia ya kugombea Urais, Ubunge, udiwani na serikali za mitaa bila kujiunga na chama cha siasa, na kuiingiza haki hii katika Rasimu ya Katiba ili eti itolewe uamuzi na Bunge maalum la Katiba, wakati uamuzi ulikwishatolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania! Hata baada ya kuhujumiwa na Mahakama ya Rufaa, wananchi walirudishiwa Haki hii na Mahakama ya Afrika, ambako Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Wanasheria sita! Mchakato wenye kudharau Mahakama mpaka za kimataifa kiasi hiki hauna uhalali wala hauwezi kuzalisha Katiba yenye uhalali! Ni dhahiri kwamba huu ni mchakato feki, uliokosa kabisa hata maadili mema ya taaluma ya Sheria! Mfano wa nne ni kitendo cha Tume ya maoni cha kupuuza hata Sheria iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Tanzania ya kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika. Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba tunao wajibu wa kubatilisha mchakato huu kwa kuwadhalilisha wananchi na kukiuka Katiba ya Nchi yetu na Utawala wa Sheria, kwa kupuuza Hukumu ya Mahakama ya Afrika iliyotoa Haki ya kila raia wa Nchi yetu ya kugombea Urais, Ubunge na Udiwani bila kulazimika kujiunga na chama cha siasa. Kwa uovu wao bado waliendelea na ukusanyaji wa maoni kuhusu Mgombea binafsi hata baada ya Mahakama ya Afrika kumpa kila raia wa Nchi yetu haki hii. Isitoshe wameiingiza HAKI hii hata katika Rasimu ya Katiba, kwamba eti Bunge maalum la Katiba liijadili bila kujali Hukumu ya Mahakama ya Afrika, badala ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhakikisha kwamba inaingizwa ipasavyo katika Katiba hata hiyo mpya ikiwa tayari, na katika Sheria husika za Nchi! Wajibu wa Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba mpya ni kuibatilisha Rasimu hii ya Katiba, na kuagiza kwamba Mchakato wa uundaji wa Katiba uanze upya kwa usahihi, uzalendo, na kwa uzingatiaji wa Katiba na Sheria kwa makini. Hoja hii imewasilishwa na Mjumbe wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila. Mungu ibariki Tanganyika

Sehemu ya Pili
ULAZIMA WA KUVUNJA KINACHOITWA ‘MUUNGANO’
(Kwa ajili ya Uhuru wa Wana wa Tanganyika)

Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba, Moja ya maajabu ya dunia ni sisi Watanganyika kulikubali kongwa la utumwa kwa Wazanzibari kama mataahira, tukakubali hata kudhalilika kama koloni lao, wakati ni Watanganyika wale wale waliomwaga damu yao kwa ajili ya uhuru wa watu wengine! Hii si ile laana tuliyotabiriwa katika Torati tu, bali tu waathirika pia wa ushirikina kama wa “mwenge” na political anesthesia iliyotupofusha kifikra, ikatupandikiza roho ya woga, na kutuhasi maumbile ya binadamu wote ya uhanga kwa ajili ya uhuru wao na utu wao. Ndivyo wahusika walivyofanikiwa kutufanya sisi Watanganyika tusione vibaya kudhalilika kama watumwa au mifugo ya watu wengine!Wajumbe tukumbuke kwamba Uhuru wa kila nchi hautokani na itikadi ya mtu wala ya chama, bali ni mpango wa Mungu kama ilivyoandikwa Kwa maana Mwenyezi Mungu ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote, na ndiye aliyefanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao, ili wamtafute Yeye Mungu ingawa ni kwa kumpapasa papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wao. Ndiyo maana kila taifa lina ibada na wimbo wake wa kumtafuta Mungu aibariki nchi yake, na kuidumishia uhuru na umoja wake kama familia moja kubwa. Kuhusu mipaka ya Utaifa wa kila Nchi, Mungu alipiga marufuku watawala wasithubutu kubadili alama za mipaka watakayoona aliiweka kwa kuwatumia waliokuwa kabla yao, na amesisitiza kwamba yule atakayethubutu kufanya hivyo na alaaniwe, na wote waseme Amina. Tena tumewekewa masharti katika Torati kwamba kila nchi itawaze mtu mwenye sifa zipi ili aweze kuongoza taifa lake kama inavyompendeza Yeye Mwenyezi Mungu, atawalaye juu ya falme zote za wanadamu. Laana ya Tanganyika ilianzia hapo, ilipomtawaza mtawala aliyegeuza sifa na utukufu wa Mungu apewe yeye, kama alivyofanya Lucifer hata akatupwa chini.

UHURU WA TANGANYIKA

Ndugu Wajumbe, Tanganyika ni nchi iliyonenwa katika unabii, ikiambiwa “Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa”, yaani isiyotulia kujijenga kimaendeleo ili watoto wake wamwishie Mungu katika furaha aliyowakusudia, bali inayojitoa kafara kwa ajili ya maslahi ya nchi zingine kama Zanzibar, kama mshumaa unavyowaangaza wengine kwa kujiyeyusha wenyewe, jambo ambalo limeonywa katika Torati kwamba ni laana. Tanganyika inavyodhalilika na kunajisika na kuliwa na Zanzibar ndiyo hali inayoitwa “muungano”! Mwenyezi Mungu aliubariki Uhuru wa Tanganyika (Kanani ya Afrika) tarehe 9 Desemba 1961, kwa kushusha nchini kote viumbe vilivyokuwa na bendera ya Tangantika, vikiwa ni pamoja na nzige, aina ya viwavi juu ya miti, senene, maua na upinde kama wa mvua. Wanaothubutu kuchezea Uhuru wa Tanganyika wana ujasiri gani kuliko Ibilisi, kama imeandikwa katika mambo yanayogusa utukufu wa Mungu hata mashewtani waamini na kutetemeka? Historia ya kweli ya Tanganyika na uhuru wetu ilichakachuliwa, ili kumvika yule dikteta uungu wa taifa letu, lakini ukweli unatayarishwa kwa ajili ya watoto wetu na vizazi vyetu vijavyo. Kwa ufupi Uhuru wetu tulipewa na UNO mwaka 1961 kupitia kwa Mwingereza, aliyekuwa na dhamana ya kutuandaa ili tupate kujitawala wenyewe. UHURU ni haki ya msingi ya Binadamu wote ulimwenguni ya Self determination. ikiwa sehemu muhimu ya utu wao (essential and basic ingredient of their humanity). Ndiyo maana kama kiitwacho ‘muungano’ kinaathiri uhuru na heshima ya Tanganyika ni lazima kitokomezwe! Swali: UHURU ni nini? Kwanini damu nyingi imemwagika duniani kwa ajili ya Uhuru, mpaka na ya Watanganyika ikapotea kwa ajili ya Uhuru wa watu wengine? Kwanini kongwa la ‘muungano’ linalazimishwa kwa Watanganyika wakati linaathiri Uhuru na utu wa Watanganyika, hata tukawa mithili ya koloni la Wazanzibari? Jibu: Uhuru ni HAKI ya msingi ya watu wa kila nchi ya kujitunza wao wenyewe na watoto wao ndani ya mipaka ya ardhi yao, kwa utaratibu waliojiwekea wenyewe (Katiba) na kuutumia kujiundia chombo chao wenyewe (Serikali) cha kutunzia vizuri iwezekanavyo uhai wao ndani ya mipaka ya ardhi yao, ili wapate kuishi kwa furaha kwa siku zote alizowapa Mwenyezi Mungu kuwepo duniani, wakiwa na utambulisho wao (national identity) kama familia kubwa inayojiamulia mambo yake yenyewe kwa ajili ya hatima yake. Hii ni Haki ya Watanganyika pia, na UNO ilitupatia rasmi Uhuru wetu kwa sababu ni Haki ya Msingi ya Binadamu wote(The right to self determination), haki ambayo ni kiungo cha mwanadamu sawa na mguu au kichwa chake, niHaki isiyoweza kuhamishika wala kubadilishika (a Basic Right which is an ingredient of humanity, which is non transferable and non exchangeable. It is the basic right to our territorial integrity, self governance, sovereignty and national identity as sons and daughters of the soil, our Mother Tanganyika). Kuiita Tanganyika ‘Tanzania Bara’ ni matusi kwa Mungu na Watanganyika

KUVUNJA KONGWA LA UTUMWA KWA WATANGANYIKA LIITWALO “MUUNGANO”

MUUNGANO NI NINI? ULIUNDWA NA NANI? KWA LENGO GANI? Ndugu Wajumbe, Bilashaka inaeleweka kwamba muungano ni uhusiano tu wa nchi moja na nyingine, kwa ajili ya maslahi, na hasa ya kiuchumi. Kwani kinachoitwa “Muungano wa Tanzania” kisingeweza kuumba upya nchi zetu, au kuondoa bahari inayotutenganisha, bali ni muungano wa huduma kuu za kiutawala zinazoendesha maisha ya kila siku ya hizi nchi mbili. Yaani muungano halali ni uchangiaji nusu kwa nusu wa gharama ya uendeshaji wa maisha ya nchi washirika, kwa ajili ya faida sawa zilizokusudiwa kwa pande zote za huo uhusiano. Ukweli ni kwamba walichohitaji Watanganyika baada ya uhuru wao ni kuijenga nchi yao na kuboresha maisha yao, kwa kutowesha umasikini, ujinga na maradhi, kwa kutumia kizalendo raslimali zao lukuki. Wala Tanganyika haikuhitaji chochote kutoka Zanzibar. Kiitwacho muungano kilitokana na vita baridi kati ya mataifa mababe ya Magharibi na ya Mashariki yaani Wakomunisti, baada ya mapinduzi ya Zanzibar, ambapo Wakomunisti waliwawahi Wamarekani kukamatana na utawala mpya wa Zanzibar, kama walivyokuwa wamewawahi Cuba hata wakaweka huko makombora yao yaliyohatarisha usalama wa Marekani. Marekani ilipozisitukia siri za mahasimu wao za kutaka kuweka makombora yao Zanzibar, walimkimbilia Mzee Kenyatta kumbembeleza afanye muungano hata wa bandia na Zanzibar, ili uwasaidie kuwadhibiti kabisa Wakomunisti wasijichimbie Zanzibar na kuweka makombora yao kama walivyokuwa wamefanya Cuba, kwa sera ya kutofungamana na upande wowote wa hiyo vita baridi. Ujumbe wa CIA ulipotimuliwa na Kenyatta kwamba marufuku kuchezea Uhuru wa Kenya walioupata kwa damu, ndipo ulipotumika usaliti na ukibaraka wa Julius Nyerere! Karume akadanywa kwamba setalaiti zao eti zimeona manowari za kivita zikielekea kupokonya nchi aliyoikomboa, sharti la kumsaidia likawa aungane na Nyerere ili msaada upitie kwake.Katika kutekeleza matakwa ya CIA ni kweli kwamba baada ya «muungano» Nyerere aligeuka kipaza sauti kikuu cha kaulimbiu yaKutofungamana na upande wowote, na ni kweli kwamba kwa mbinu hizi Wamarekani walifanikiwa kuwahujumu Wakomunisti wasitegemissiles zao Zanzibar. Kwa jinsi Nyerere alivyoutoa kafara Uhuru wa Tanganyika kwa ajili ya maslahi ya Marekani, na bado akaweza kuwapofusha Watanganyika kifikra wasitetee uhuru wao hata kwa damu, na kuwadhibiti wasifahamu siri yake badala yake wamwone yeye kama mungu wao wakati ndiye adui mkuu wa uhuru wao, Kenyatta alighadhabika sana na kusema, Hakika Nyerere anatawala maiti! Katika kuficha doa la ukibaraka wa Nyerere kwa Marekani na usaliti wake kwa Watanganyika, ili kumwezesha asifiwe na kuadhimishwa milele, zilitungwa sababu FEKI za kijinga mno za huu muungano : 1. Eti ‘usalama’, kwamba adui wa Zanzibar angeweza kujificha kwetu na adui zetu wakajificha Zanzibar. Huu ni upuzi mtupu kwavile visiwa vingi ni majirani wa nchi za mabara, lakini hawana miungano wala kuhujumiana, wala hatari ya vita hailetwi na visiwa, kama ambavyo vita yetu na Uganda haikutokana na visiwa. 2. Eti kwa sababu Zanzibar kuna makabila yanayotoka Tanganyika! Basi tungeungana na Kenya waliko Wajaluo, Wamasai, Wakurya, Wapare na Wachaga wengi zaidi ya mara tatu ya Wanzibari wote, au Msumbiji waliko Wayao, Wanyasa na Wamakonde wengi kuliko Wazanzibari, au Zambia waliko Wanyamwanga wengi pia. Hiki ni kigezo cha kufilisika kifikra, kilicholenga kumfichia Nyerere uuzaji wake wa uhuru wa Tanganyika kwa maslahi ya Marekani. Muungano wenyewe ulikuwa uangaliwe upya baada ya miaka 10, kama bado ungehitajika tuendelee nao au la. Na Karume akiwa shujaa wa kuweka hatima ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar mikononi mwa Wazanzibari wenyewe, alitarajiwa kurudisha heshima ya Utaifa wa Wazanzibari, kwani alikwishaanza hata kupinga sera nyingine za Nyerere zisivuke kisiwa cha Chumbe, ziishie huko huko Tanganyika. Karume aliuawa baada ya miaka nane ya muungano, katika mazingira ya kutatanisha. Baada ya kugundua juhudi na mikakati ya Nyerere ya kuficha kabisa kiini cha muungano, yaani siri ya kutumiwa na Marekani akauza uhuru wa Tanganyika, Zanzibar ilikataa kabisa kuchangia gharama za huo muungano, ikijua kuwa Nyerere lazima angebeba mzigo wote kwa ajili ya kutoruhusu muungano wake uvunjike, kwavile ukivunjika lazima siri ya uhujumu wake wa Uhuru wa Watanganyika itafunuka, na kumfanya achukiwe na kulaaniwa milele. Nyerere alifaulu kujiweka mahali pa mungu katika mioyo ya watu, na genge la kimafia la CCM linalodumisha ibada yake kama vile ndiyo hirizi yao ya kutawala nchi milele, ndilo linalolazimisha kongwa la utumwa la muungano pamoja na makafara yake ya kutawalia akili za watu, kama vile mbio za mwenge, bila kujali jinsi kongwa hili linavyoimaliza Tanganyika kiuchumi na kuifanya koloni la Wazanzibari. Ndugu wajumbe, kwavile muungano unaathiri uhuru wa wana wa Tanganyika na hatima yao, Bunge maalum la Katiba linalazimika kujiridhisha kwanza kabisa na uhalali wake, kwa kuzingatia majeraha ya kiuchumi na Uhuru wa Tanganyika. Ukweli ni kwamba Tanganyika ni kafara inayoliwa bure na Zanzibar ambayo tangu mwaka 1964 hadi leo imeishi kwa zaidi ya shilingi trilioni 120 za damu ya Watanganyika, ambazo ni lazima ieleweke zitalipwaje. Saa ya ukombozi ni sasa! Ukupe na ukoloni wa Zanzibar kwa Tanganyika unaoitwa muungano ndio uliopelekea kufutwa matibabu ya bure ya wana wa Tanganyika, bila kujali wanavyokufa ovyo leo kwa magonjwa ambayo yanatibila! Ukupe huu ndio uliolazimisha kufutwa elimu nzuri ya bure ya wana wa Tanganyika, ukapelekea wengi wa watoto wa Tanganyika sasa kuishia uzururaji, umachinga, na kubwia unga na kuelekea kuwa taifa la uhalifu na upunguani! Kulazimisha maisha ya raha na utajirisho kwa Wazanzibari kwa jasho la Watanganyika na raslimali za Watanganyika ni maandalizi ya mmwagiko wa damu, ambao unaepukika leo kwa kuvunja muungano!

ARDHI YA TANGANYIKA KAMWE SI YA MUUNGANO

Ndugu wajumbe, muungano umewapa bure Wazanzibari ardhi ya Watanganyika, na siyo siri kwamba Wazanzibari wanajimilikisha kwa kasi kuliko Watanganyika wenyewe, wanaogeuzwa na muungano kuwa wakimbizi katika nchi yao wenyewe. Watanganyika wamepofushwa akili wasiione hatari kwamba walikuwa milioni 8.5 tu walipokabidhiwa nchi yao tarehe 9 Desemba 1961, lakini leo wako milioni 48 wakati ardhi yao haijaongezeka hata inchi moja! Wazanzibari wanashauriwa waanze kuwauzia Watanganyika ardhi yao waliyokuwa wamewatapeli kwa kigezo cha «muungano» sasa watapata pesa nzuri, kuliko watakapoamka Wana wa Tanganyika kuitwaa ardhi yao. Ndugu wajumbe, mbali ya Tanganyika kuangamizwa na muungano kiuchumi, tangu mwaka 1964 ilipoteza Uhuru wake kwa kupokonywa haki yake ya kuwa na Katiba yake na serikali yake yenyewe ndani ya mipaka ya ardhi yake! Tusingoje Watanganyika wamwage damu kwa ajili ya Uhuru wao, bali Bunge hili litumike kuwapa haki yao kwa kuvunja kongwa hili la ‘muungano’ kwa amani. Saa ya ukombozi ni sasa!

KUUNDWA SERIKALI YA TANGANYIKA

Ndiyo maana mwaka 1994 Bunge la huo ‘muungano’ lenyewe lilipitisha Azimio la Kuundwa Serikali ya Tanganyika, ambalo bado liko hai.Kama kweli utawala wetu ni wa Kikatiba na Kisheria, basi ni wajibu wa Bunge hili la Katiba kuhakikisha kwamba Serikali ya Tanganyika inaundwa, bila mjadala wowote kwa sababu ni Sheria, yaani uamuzi uliopitishwa na Bunge la Jamhuri. Ni muhimu kwa kila Mjumbe wa Bunge la Katiba kupitia Hansard ya Azimio hili Takatifu. DP ilimwandikia Rais Kikwete na waziri wake wa Fedha hayati William Mgimwa, waziri wa masuala ya muungano katika ofisi ya Makamu wa Rais na Waziri wa Sheria, kwamba watuambie ni kiasi gani cha fedha ya Watanganyika iliyotunza maisha ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar tangu mwaka 1964 (ambayo inakisiwa kuwa zaidi ya shilingi trilioni 120), lakini hatukujibiwa!Lakini Mahakamani watatueleza tena kwa adabu. Ndugu Wajumbe, mmeelewa kwamba Muungano ni unyang’anyi wa Haki ya Msingi ya Uhuru wa Tanganyika, ambao nchi nyingi zimeupata kwa kumwagika damu, hata yetu sisi Watanganyika. Ukoloni ni nchi yoyote kuwa na viongozi wa ngazi za urais, uwaziri, ukatibu mkuu, ukurugenzi wa taasisi za kiserikali, ukuu wa mikoa na wilaya n.k kutoka nchi nyingine, kama Tanganyika inavyokaliwa na watawala kutoka Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Saa ya ukombozi ni sasa! Huu ni ukoloni halisi, hakuna mjadala, siyo muungano kwa sababu ni Tanganyika tu kuliwa na kutawaliwa na Wazanzibari, lakini ni marufuku kabisa Mtanganyika kuthubutu kwenda kuitawala Zanzubar. Ni sawa kabisa na Waingereza walivyokuja kuitawala Tanganyika, lakini ni marufuku kabisa Mtanganyika kwenda Ulaya akaitawale Uingereza! Saa ya ukombozi ni sasa! Ndugu Wajumbe, utumwa na udhalili wa Watanganyikakwa watu wa Zanzibari ni pamoja na Wazanzibari milioni moja kuja kukamata nusu ya Bunge la Watanganyika milioni 48, tena kwa mabilioni ya mapesa ya Watanganyika wenyewe. Ni tusi la thamani ya Mzanzibari mmoja kuwa sawa na Watanganyika 48! Isitoshe Wazanzibari wanakuja kutunga sheria ziwabane Watanganyika, wao wakiwa na Bunge lao wenyewe kule kwao, ambalo ni marufuku watumwa wao wa Tanganyika kuingiza pua zao humo! Hili ni kongwa la ukoloni linaloitesa Tanganyika. Muungano unavunja Ibara ya 12 na ya 13 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano, zinazotaka Watanganyika nao wawe na Katiba na Serikali yao wenyewe kama Wazanzibari walivyo nazo, na kuishi kwa damu yao pia kama wao wanavyoishi kwa damu yetu ingawa wenzetu hawanayo, wanategemea ukupe kwa Tanganyika. Muungano hata umefika kulaaniwa na Watanganyika hadharani kwa uchungu, kwamba Mzanzibari anakuja na msuli katika Bunge lao asilolichangia hata senti moja, na kuondoka na Prado la mataahira wa Tanganyika! Muungano huu ni ubeberu dhidi ya Wana wa Tanganyika, ambao ni lazima utokomezwe kwa amani. Ndugu Wajumbe, utwana huu wa wana wa Tanganyika unaonekana hata katika ‘mabwana’ wa Zanzibar kuwa wengi zaidi katika Bunge hili la Katiba, lakini gharama zote wanaumia Watanganyika! Tusi la ‘utaahira’ wa Watanganyika limezidishwa kwa kulileta katika Bunge maalum la KatibaBaraza la Wawakilishi, lililoitoa Zanzibar katika muungano kwa mabadiliko lililofanya katika Katiba yao! Wazanzibari wamejitoa kabisa katika muungano. Wamebaki kutumia neno muungano kwa ajili ya kuendeleza ukupe wao kwa Watanganyika (parasitic advantages). Katika mabadiliko hayo Wazanzibari wamefuta kipengele kilichowaingiza katika huo Muungano kwa Tamko kwamba Zanzibar ni sehemu ya Muungano, kwa Tamko kwamba sasa Zanzibar ni Nchi iliyo huru, au Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Ni dhahiri kwamba watu wa Jamhuri ya Zanzibar wameletwa katika Bunge hili la Katiba ambalo haliwahusu baada ya kujitoa rasmi katika muungano, ili watumiwe kwa maslahi ya kikundi cha ki-Mafia cha CCM kinachotaka kutawala milele, hata kwa kuhonga Uhuru wa Tanganyika! Waheshimiwa Wajumbe, haya ni mambo yanayobatilisha kabisa uhalali wa Rasimu ya Katiba, pamoja na mchakato wenyewe ulioitengeneza! Bunge hili la Katiba linapaswa kuvunja kongwa la utumwa kwa Watanganyika. Ni kongwa la kutokomezwa hata kwa kumwaga damu nyingi kuliko tulivyoimwaga kwa ajili ya Uhuru wa watu wengine! Bunge maalum la Katiba linafahamu kwamba kiitwacho “Muungano” kiliwarudisha Watanganyika katika utumwa na ukoloni, kama lilivyothibitisha Bunge la huo Muungano mwaka 1994 (Ni muhimu kila mjumbe wa Bunge maalum la Katiba apewe nakala ya Hansard hiyo ili aweze kuwajibika impasavyo), Bunge likapitisha Azimio la kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika, ambalo kisheria bado liko HAI likisubiri kutekelezwa tu. Azimio la Bunge la kuundwa Serikali ya Tanganyika liko hai kwa sababu Bunge halijawahi kupitisha Azimio mbadala la kubatilisha Azimio lake hilo, na sababu za kuundwa Serikali ya Tanganyika ni nzito zaidi leo kuliko hata wakati ule. Kilichotokea ni kwamba Nyerere aliwafokea Wabunge kwamba wao eti ni kamati ya siasa ya chama chake CCM, ambacho sera yake ni muungano wa serikali mbili tu, hivyo akawashambulia wale wanaotaka Serikali ya Tanganyika kwamba watoke CCM waende DP. Wabunge walinywea kwa sababu wangejitoa CCM wangekuwa wamejivua Ubunge, kwani Wabunge walikuwa bado ni kutoka CCM peke yake. Lakini Azimio hili liko hai, na ni Sheria ambayo Bunge maalum la Katiba ni lazima liitii. Wala Nyerere hakuwa mkweli kwa sababu Bunge lile halikuwa la CCM bali la Taifa, na lilichaguliwa na wananchi wote. Rasimu hii imepoteza kabisa uhalali mbele ya Bunge maalum la Katiba, kwa kutozingatia Azimio hili! Kwahiyo Rasimu ya Katiba ni batili. Ni wajibu wa Bunge maalum la Katiba kuhoji kwanini Serikali ya Tanganyika haijaundwa hadi leo, na kusitisha zoezi la Katiba ya muunganompaka Watanganyika waunde kwanza Katiba yao na kuwa na Serikali yao.

Imewasilishwa na Mchungaji C. Mtikila wa Democratic Party (DP)

Fanya kibali chako kiwe kibali binafsi.


Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira

 

"Katika Agano la MUNGU kwetu Mwaka huu amesema ni mwaka wa KIBALI, utaenda kuuona ukuu wa MUNGU, Mwanzo: 12:1-3 (BWANA Akamwambia Abramu …) MUNGU Anaongea na mtu wake “Toka”, na sio watu ila wewe. Ili uweze kuelewa ujumbe wa Kibali fanya KIBALI chako kiwe cha binafsi, Usifanye cha harambee, Kibali chako ni cha kipekee.

Kumbuka kuna mtu anashuhudia matendo makuu ya MUNGU aliyomtendea kila iitwapo leo maana yake amemfanya MUNGU kuwa ni wa kwake lakini wewe tangu ushuhudie mwaka juzi hujashuhudia tena, MFANYE MUNGU WA Kwako.

TOKA;
- Toka wewe katika Nchi yako - kuna tabia za kitaifa/ tabia za nchi zisizofaa, Toka katika hizo.
- Toka wewe katika jamaa zako - kuna tabia za jamii/ unawafahamu huko toka, TOKA katika tabia mbaya za jamaa zako unaowafahamu, wanaokuzunguka.
- Toka wewe katika nyumba ya baba yako – toka katika tabia za nyumba ya baba yako.

Kwa hiyo sisi hatuna haja ya kutoka nchini kwetu na kwenda ulaya kutumikishwa hiyo siyo akili nzuri. Walokole wengi wameokoka lakini “Kutoka” katika tabia za baba zao, nchi yako, jamaa yako bado hawajatoka, hilo ni tatizo, Bibilia inasema katika kitabu cha Amosi ‘Niondoleeni kelele zenu’ ni kweli unaweza kufunga kwalezima/ ramadhani, Bibilia inauliza ‘hiyo ndiyo saumu niliyokueleza’? Siku UTAKAPOTOKA katika TABIA za nchi yako, jamaa zako, Uzao wa baba yako nakuhakikishia MUNGU Atakuonyesha NJIA ya kwenda. Unapoamua KUACHANA na Tabia za nyumba ya baba yako, Jamaa zako, Nchi yako UTUKUFU WA MUNGU Utakuzunguka.

Mnasikia sana Mafundisho, Mahubiri lakini kuchukua hatua ya kutenda inakuwa kazi, nakumbuka mimi nilipoamua kutoka katika tabia za nchi yangu, jamaa zangu, na katika tabia za nyumba ya baba yangu, nilibaki peke yangu hata wale niliokuwa nasali nao walisema usifuatane na sisi wenye dhambi. Unapoamua kuachana na dhambi UTUKUFU WA MUNGU Unakufunika, hata nilipokuwa nasali KKKT nikisimama kuhubiri kweli ya MUNGU wazee wa kanisa wananitoa nje, maana walikuwa hawataki kunisikiliza niwaambie kile NINACHOELEKEZWA na MUNGU.

IBADA maana yake nini?, Ibada maana yake ni watu kupeleka MAHITAJI yao kwa MUNGU na MUNGU kuwajibu, Ibada sio Utakatifu, MUNGU hufanya mambo yake kwa sekunde chache inategemea ulivyojiandaa. Kutoka kuna gharama, MUNGU alimuambia “Toka” katika nyumba ya baba yako, Ibrahimu alipotoka akakosea akatoka na baba yake, lakini baba yake alifia njiani maana MUNGU haitaji mizigo!

TOKA; Ukishatoka ndio Anakuonyesha, ni kweli “Amekuokoa, Amekufungua, Amekuweka HURU”, lakini Anataka UTOKE."
MUNGU akubariki.

Wednesday, March 12, 2014

AGANO NA MUNGU(3)













Na Joseph Goliama
HATUA YA SITA YA USHUHUDA HUU NI HII HAPA
Kila mwanadamu anapaswa kujua kuwa Mungu ni msingi wa kila kitu kinachoonekana na kisichoonekana, Ninaposema Mungu ni Msingi wa kiila kitu namaanisha kuwa Mungu ni chanzo cha kila kitu yeye ni asili ya kila kitu na yeye ni mwanzo wa kila kitu yaani Mungu ni kiini cha kila kitu hapa nataka ujue wazi kuwa ninaposema Mungu ni msingi, kiini, asili, mwanzo na chanzo cha kila kitu namaanisha kwamba Uzima, upendo na haki ndio msingi, asili, kiini,mwanzo na chanzo cha uumbaji wote wa Mungu, ninapata matumaini sana pale ninapojua kwa hakika kuwa Mungu niye chanzo cha maisha yangu ya hapa duniani ufahamu huu umenifanya nifanye kila niwezalo kurudi kwenye msingi wangu, kurudi kwenye kiini changu, kurudi kwenye asili yangu, kurudi kwenye mwanzo wangu, kurudi kwenye chanzo changu kwa hakika kurudi kwenye chanzo,asili,kiini,mwanzo na msingi wangu ni kurudi katika maisha ya Uzima maisha ya upendo maisha ya haki na kwa hakika mtu yule ambaye amerudi katika chanzo chake milele Uzima, upendo na haki havitakuwa adimu katika maisha yake kwakuwa ameunganishwa na majibu ya uhitaji wake
Nataka wanadamu wenzangu ambao wanatafuta Uzima wanaotafuta Upendo na wanaotafuta haki wajue wazi kuwa wanamtafuta Mungu na yakwamba naweza kwa neema ya Mungu kuwasaidia kukutana naye kwasababu amenituma kumtambulisha kwa wanadamu ili yeye mwenyewe Mungu akutane nao nakujhitimisha uhitaji wao katika maisha yao


HATUA YA SABA YA USHUHUDA HUU NI HII HAPA
Baada ya kueleza jinsi Mungu alivyojifunua kwangu sasa nataka wanadamu wenzangu muelewe kuwa Mungu alisema nami kuhusu miili yenu aliniambia watu wangu wanakufa kabla ya wakati wao kwa sababu Uzima , nguvu za Uzima na mamlaka ya Uzima imeadimika katika maisha yao, kiukweli maneno ya Mungu yalinichoma sana hasa ukizingatia kuwa Mungu tayari alishaniambia kuwa yeye ni Uzima yeye ni nguvu za Uzima(UPENDO) na yeye ni mamlaka ya Uzima(HAKI), hivyo aliponiambia kuwa wanadamu wanakufa kabla ya wakati wao moja kwa moja niliangalia nakujua wazi kuwa ni kweli hapa duniani wanadamu wengi wanahangaika sana kwa sababu miili yao inahitaji Uzima, nguvu na mamlaka yakufanya kazi ipasavyo, miili au viungo vya wanadamu mara nyingi vinapata magonjwa na magonjwa hayo yamekuwa sababisho la roho za wanadamu kutoka ndani ya miili hiyo
Ukiienda mahospitalini utajua nini naongea hapa hospitali utawakuta wagonjwa wengi sanA na wote wanahitaji Uzima, wanahitaji uzima wa kiungo chao kimoja baadhi kwa mujibu wa maelezo hapo nyuma nataka uelewe wazi kuwa mwanadamu anapohitaji uzima humuitaji Mungu kwakuwa Mungu ni Uzima hapa nataka kukuuliza wewe mwenye pumu wewe mwenye vidonda vya tumbo, wewe mwenye kisukari, wewe mwenye ngiri, wewe mwenye kansa, wewe ,mwenye ugonjwa wa moyo ,wewe mwenye ugonjwa wa mifupa wewe mwenye leukemia, wewe mwenye uonjwa wa kichwa, wewe mwenye ugonjwa wa kifua, wewemwenye ugonjwa wa kiungo chochote cha mwili wako jeeeee unajua kuwa unahitaji Uzima? najeee unajua Uzima ni Mungu?

HATUA YA NANE YA USHUHUDA HUU HII HAPA ISOME
Baada ya kukujulisha kuwa Mungu ni Uzima ni Upendo nani Haki, na baada ya kukujulisha kuwa Mungu hana umbo ndio maana hata Uzima hauna umbo hata upendo hauna umbo hata haki haina umbo na baada ya kukujulisha kuwa duniani kote wanadamu wanahitaji Uzima, Upendo na haki nayakwamba wanadamu tunamtafuta Mungu bila kujua kuwa tunamtafuta pale tunapotafuta Uzima, upendo na haki , na baada ya kukusaidia kujua wazi kuwa hata Yesu mwenyewe aliishi na Mungu kwakuwa aliishi na Uzima na Upendo na haki, na kwakuwa Yesu aliishi na Mungu ndio maana maisha yake yote aliishi maisha ya kumfunua Mungu baba yake kwakufunua Uzima, upendo na haki kwa wale wote waliokuwa wanatafuta Uzima, upendo na haki na kwakuwa Yesu aliishi na kutembea na Mungu baba yake ndio maana alifunua asili ya Mungu ya wokovu, utakatifu na ushindi. kwa ukweli huo huo nataka ujue kwa hakika kuwa Mungu wetu yeye ni Uzima yeye ni Upendo yeye ni haki, Mungu huyu ninayemzungumzia anataka kujifunua kwako yeye mwenyewe anataka kujifunua kwako ili wewe ujue wazi kuwa yeye ndiye Uzima wako yeye ndiye Upendo wako yeye ndiye haki yako, kwa hakika ili Mungu ajifunue kwako unapaswa wewe kwanza kumjua yeye, kumjua Mungu ni kujua mawazo yake ni kujua mtazamo wake ni kujua maneno ya kinywa chake ni kujua matendo yake ni kujua mwonekano wake ni kujua mahusiano yake ni kujua maamuzi yake ni kujua misimamo yake, kuyajua haya ni kujua maisha ya Mungu, maisha ya Mungu ni maisha ya Uzima ni maisha ya upendo nani maisha ya haki, maisha ya Mungu ndio yanayomfanya tumuite Mwokozi, mtakatifu na Mshindi, maisha ya Mungu ndio yanayotufanya wanadamu tumjuao, tuweze kuishi maisha ya kumtegemea, kumpenda na kumuamini, maisha ya Mungu yenye sehemu hizo nane nilizozitaja yanamfanya Mungu kuwa adui mkubwa wa shetani, Mungu ni adui wa shetani maana yake adui wa mauti adui wa uovu ni adui wa yasiyo ya haki. Mwanadamu anayetaka kukutana na Mungu yaani kukutana na Uzima kukutana na Upendo na kukutana na haki lazima akubali kuyatoa maisha yake ili ndani yake Mungu(Uzima, upendo,haki)aishi na pia akubali Mungu kuutumia mwili wake kujifunua kwake na kwa wanadamu wengine
Jiulize maswali haya
1. Uko tayari Mungu aishi nawewe? yaana uko tayari Uzima, upendo na haki viwe maisha yako ya kila siku kila wakati?
2. Uko tayari Mungu atumie mwili wako kujifunua kwako na pia autumie mwili wako kujifunua kwa wengine? kwanini Mungu anataka aafikiane (akubaliane nawewe,aweke agano nawewe, apatane nawewe) nawewe kuishi nawewe mwanadamu na kutembea nawewe mwanadamu hapa duniani? jibu ni rahisi yeye Mungu hana Umbo yeye hana mwili kama sisi wanadamu , hivyo ili aishi na kutembea hapa duniani ni lazima akubaliane apatane,aweke agano afikie mapatano nawewe mwanadamu anayetaka kuishi nawewe na kutembea nawewe, ndio maana tunasema Mungu wetu ni Mungu wa maagano
Jee! uko tayari kukubaliana na Mungu aishi ndani yako kama alivyoishi ndani ya Yesu Kristo? na jee! uko tayari kutembea na Mungu hapa duniani kama alivyotembea na Yesu Kristo? kama Utakubali kuishi na kutembea na Mungu nakuhakikishia Uzima, upendo na haki havitakuwa adimu siku zote za maisha yako
Kumbuka katika MUNGU NI MMOJA PART HII YA 8 , tumejifunza maisha ya Mungu wetu yale maeneo nane na yakwamba Mungu anataka kuishi na kila mwanadamu na kutembea na kila mwanadamu ili Uzima, upendo nahaki visiwe adimu hapa duniani.

HATUA YA TISA YA USHUHUDA HUU HII HAPA ISOME
Baada ya kujifunza katika hatua za awali za kumjua Mungu wetu kisha kuyajua maisha anayoishi Mungu wetu sasa tujifunze ni kwa namna gani mwanadamu bila kujali dini yake, kabila lake, rangi yake, Taifa lake, jinsia yake ,rika lake, asili yake, ukoo wake au bila kujali chochote awezavyo kuweka makubaliano na Mungu, mapatano na Mungu,maafikiano na Mungu,agano na Mungu la kuishi na Mungu na Kutembea na Mungu hapa duniani na milele mbinguni
Tukumbuke kuwa Mungu hana umbo wala mwili, yeye ni Mungu wa wote wenye mwili, yeye ni Uzima yeye ni Upendo yeye ni haki, Mungu hana mwili ndio maana akikaribishwa na mwenye mwili kwake ni rahisi kuingia ndani ya mwenye mwili na kufanya makao ndani yake, hufanya makao kwa kuishi ndani ya mwenye mwili na kwa kawaida akiishi ndani ya mwanadamu humsaidia mwanadamu huyo kila anapohitaji Uzima, upendo na haki kwakuwa yeye mwenyewe ndiye jibu la uhitaji wa mwanadamu, huwezi ukaishi na Mungu uzima ukawa adimu au upendo ukawa adimu au haki ikawa adimu kwako, ukiishi na Mungu unaishi na utoshelevu wako, yeye anakuwa maji kwa kiu yako anakuwa chakula kwa njaa yako, utajiona huitaji kitu kwakuwa yeye ni kila kitu kwako. kuishi na Mungu ni sawa na mwanamke anayeishi na mwanaume wake mwenye kila kitu anachokihitaji hakika mwanamke huyo huishi na utoshelevu wake wote na hujiona kila anachokihitaji ni mume wake tuu na hatahitaji mwingine zaidi ya mume wake, hali hiyo ndio inayompata mwanadamu anayeishi na Mungu na kutembea na Mungu hapa duniani hatahitaji chochote zaidi ya Mungu, maisha yangu yamebadilika sana baada ya kukutana na Mungu wangu hivi sassa moyo wangu unahitaji kuishi na Mungu na kutembea na Mungu tuu kwani najua kama ntaishi naye na kutembea naye basi atanisaidia mimi na wanadamu wenzangu kupitia mimi
Kuingia agano na Mungu ndio njia pekee yakuingia katika maisha ya Uzima ya upendo na ya haki yaani maisha ya Mungu ndani yetu, agano na Mungu unapaswa kuliweka kwa kukubali yafuatayo
1. Kumkubali Mungu maishani mwako kwa kukubali Uzima, upendo na haki kuwa maisha yako ya hapa duniani na milele mbinguni
2. Kukubali maisha ya Mungu kuwa maisha yako ya hapa duniani na milele mbinguni
3. Kukubali kuyajenga maisha yako ya hapa duniani kwa kumtumikia Mungu yaani kutumikia Uzima,upendo na haki kwa kuyafuata maisha ya Mungu yaani kwakufuata mawazo yake,mtazamo wake,maneno ya kinywa chake,matendo yake,mwonekani wake,mahusiano yake,maamuzi yake na misimamo yake
Kama utaamua kukubaliana na Mungu maisha hayo kuyaishi ndipo utakuwa umefanyika kiumbe kipya na kimsingi ndio kuzaliwa mara ya pili, ndio kuanza maisha mapya na Mungu ndio kuingia katika ufalme wa Mungu ndipo kuanzia hapo Mungu atakuwa mfalme wako atakuwa Mungu wako yaani atakuwa uzima wako atakuwa Upendo wako atakuwa haki yako. nasisitiza kabisa kuingia katika agano na Mungu kunakupa sauti ya Mungu na mwelekeo wa Mungu maishani mwako, kama hauisiki sauti ya Mungu wala hauoni mwelekeo wa MUNGU MAISHANI MWAKO USIJIULIZE,sababu ni hii hauna makubaliana yoyote na Mungu, hauna mapatano yoyote na Mungu hauna maafikiano yoyote na Mungu, kama utaweka mapatano na Mungu,kama utaafikiana na Mungu maisha yako yatapata sauti ya kuisikiliza na yatapata mwelekeo wa kuufuata nawe utakuwa na amani na Mungu. unajua kwanini wanadamu wengi wanaogopa kifo ?wanaogopa kifo kwasababu hawana agano na Mungu,hawana maafikiano yoyote na Mungu na maisha yao wanaishi kama wamekuja duniani kwa bahati mbaya. lakini nakushauri wewe mfanye Mungu kuwa maisha yako ya hapa duniani ili ukienda mbinguni uishi naye na kutembea naye milele
Mungu ni Mungu wa agano sisi ni warithi wa agano jipya tunapaswa kuishi katika agano letu ambalo linatutaka tuishi na Mungu na kutembea na Mungu hapa duniani na milele mbinguni. weka agano na Mungu sasa,kubali kuishi naye na kutembea naye hapa duniani na milele mbinguni. ukiweka agano na Mungu unakuwa umejikabidhi maisha yako kwa Mungu naye atawajibika kukutunza,kukulinda na kukutetea siku zote za maisha yako wewe na yeye hapa duniani mpaka atakapoamua urudi nyumbani ukakae nae milele

HATUA YA KUMI YA USHUHUDA HUU HII HAPA ISOME
Ikiwa utaamua kuweka agano na Mungu ikiwa utapatana naye kuishi naye na kutembea naye hapa duniani na milele mbinguni baada ya kifo chako cha mwili, basi unakuwa tayari umeanza maisha mapya, maisha haya nayafananisha na maisha ya wawili waliooana na sasa wanaanza maisha ya ndoa yao, cha kwanza kinachopaswa kufanyika baada ya kuingia Agano na Mungu ni kujua kwa upande wako unapaswa kuishije katika agano lako na Mungu, hapa jiulize unapaswa utumikiaje mawazo ya Mungu?unapaswa utumikiaje mtazamo wa Mungu?unapaswa utumikiaje maneno ya kinywa cha Mungu?unapaswa utumikiaje matendo ya Mungu?unapaswa utumikiaje mwonekano wa Mungu?unapaswa utumikiaje mahusiano ya Mungu?unapaswa utumikiaje maamuzi ya Mungu?unapsawa utumikiaje misimamo ya Mungu......hapa nataka ujue wazi kuwa unakuwa wakati umewadia wa wewe kufa ili Mungu aishi ndani ya mwili wako kupitia wewe, hapa unapaswa kufa yaani mawazo yako yanapaswa kufa,mtazamo wako unapaswa kufa, maneno ya kinywa chako yanapaswa kufa, matendo yako yanapaswa kufa, mwonekano wako unapaswa kufa,mahusiano yako yanapaswa kufa,maamuzi yako yanapaswa kufa na misimamo yako inapaswa kufa na kama maisha yako hayo yakifa yanafufuka maisha ya Mungu ndani yako, maisah ya Mungu maana yake mawazo ya Mungu,mtazamo wa Mungu,maneno ya kinywa cha Mungu,matendo ya Mungu,mwonekano wa Mungu,maamuzi ya Mungu na misimamo ya Mungu kwa misingi hiyo nataka ifike wazi wewe usiiishi bali Mungu aishi ndani yako ndani ya mwili wako.
Kumruhusu Mungu aishi ndani yako ni hatua ya kwanza kabisa ya ukombozi wa mwili wako mwanadamu, Mungu anapoishi ndani ya mwili wako anaua nafsi yako anaua self yako anaua uwewe(your self)anaua yale maeneo yako nane niliyoyataja hapo juu, anapoua self yako wakati huo huo yeye anachipua ndani yako,yaani maeneo yake yale nane yanaanzan kuchipua ndani ya moyo wako

Kuishi na Mungu ni kufanya nini? kuishi na Mungu ni kwa namna gani? kuishi na Mungu ni kwakumtafakari yeye Mungu,,kama unataka kuishi na Mungu lazima,lazima,lazima,lazima,lazima,lazima,lazima uishi naye katika mawazo yako kwa kumuwaza yeye wakati wote,unapomtafakari Mungu most of your time unamruhusu aumbike ndani ya moyo wako, Mungu huumbika ndani ya moyo wa mwanadamu pale mwanadamu anapochukua muda wake masaa yake kumtafakari, kumtafakari Mungu ni kufanya nini? Nikuchukua muda kutafakari,kuwaza kufikiria sana 1. mawazo yake, 2. mtazamo wake, 3. maneno ya kinywa chake,4. matendo yake,5. mwonekano wake,6. mahusiano yake,7. maamuzi yake na 8. misimamo yake kama utachukua muda kwanza kuyajua maisha hayo ya Mungu kisha ukaamua kuchukua muda wako mwingi kama sio wote wakukaa hapa duniani kuwaza hayo,matokeo yake utaanza kuyasahau maisha yako ya kibinadamu na kujikuta unabadilika na watu watakaokuwa jirani nawe wataanza kuona mabadiliko ya maisha yako sana tena sana.
Kuishi na Mungu ni ukombozi wa mwili wako unakuwa umempata wa kukusaidia dhidi ya mauti ,nguvu zake na mamlaka zake, unakuwa umejitenga na wanadamu wanaokufa bila Mungu kutaka, inaniuma sana kujua wazi kuwa wapo wanadamu maisha ya miili yao yamekatiliwa na ajari, silaha,magonjwa,sumu,wanyama wakali,wanadamu wenzao,hali za hewa,mabadiliko ya maumbile ya dunia nk inaniuma sana kuona hayo yanatokea huku Mungu akitangazwa bila mabadiliko yoyote.
Kuishi na Mungu kunamnyima nafasi shetani kuteka nyara mawazo yako nakuishi ndani yako, shetani ambae ndiye matatizo yetu wanadamu anapigana vita vikubwa na Mungu wakigombea mawazo ya wanadamu , Mungu na Shetani wote wanagombea kumiliki mawazo ya wanadamu na kuyatumia kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu. SHETANI NA MUNGU WANAPIGANIA KILA MMOJA KUMILIKI MAWAZO YA MWANADAMU, MWANADAMU ANAYEKUBALI MAWAZO YAKE KUTEKWA NYARA NA KUTUMIWA NA SHETANI DAIMA HATMA YA MAISHA YAKE INAKUWA MIKONONI MWA SHETANI NA UUMBAJI WA MUNGU.

..................................................MWISHO........................................

Monday, March 10, 2014

KUWEKA AGANO NA MUNGU (2)







Na Joseph Goliama
 HATUA YA TATU YA USHUHUDA HUU SOMA HAPA
Wakati nawaza sana kuhusu Mungu ni Upendo nilijiona gafla nipo maeneo ya chuo kikuu cha Dar es salaam baadae nikapelekwa katika vyuo vingine na nikatembezwa shule za sekondari Dar na mwisho nikajiona nipo mahakama ya kisutu na mahakama ya mwanzo kariakoo nikiwa katika hali hiyo huku kwa wakati mmoja najihisi ninaona kuwa nipo katika maeneohayo yote nikasikia swali kutoka kwa Mungu akiniuliza Mwanangu kote duniani katika maeneo kama haya watu huenda kutafuta nini? ndipo nikawa nawaza chakujibu wakati nataka kutamka cha kujibu ghafla nikasikia nanong'onezwa niseme kwamba watu huenda katika maeneo hayo yote kutafuta Haki, nami nikamwambia Mungu nikasema katika maeneo kama hayo duniani kote watu huenda kutafuta haki, nikamwambia kule chuo kikuu, mashuleni na vyuoni watu huenda kutafuta haki yakuwa na elimu ili wawe na maisha bora, nakule mahakamani nikamwabia Mungu kuwa watu huenda kutafuta haki zao za aina mbalimbali, ndipo Mungu akaniambia Mwanangu kumbuka siku zote za maisha yako mimi Mungu ni Haki, aliponiambia kuwa yeye Mungu ni haki niliingia katika mawazo mengi sana nikawaza kumbe wanadamu tunapotafuta haki ndani ya maisha yetu ndani ya ndoa ndani ya familia ndani ya ukoo ndani ya kabila ndani ya chama ndani ya Taifa ndani ya huduma ndani ya shirika ndani ya taasisi ndani ya bara ndani ya EAC ndani ya Umoja wa mataifa na katika kila eneo la maisha kumbe tunamtafuta Mungu pasipokujua ,kwakweli niliwaza sana tena sana kwa jinsi Mungu alivyojifunua kwangu siku ile hata hivyo wakati nawaza hayo Mungu akaniambia Mwanangu pamoja nakwamba Mimi Mungu ni uzima ni upendo nani haki lakini sina umbo ,akaniambia sina umbo ndio maana niliwaambia wana wa Israel wasinifananishe na kitu chochote kilicho juu mbinguni kilicho chini ya dunia au kilicho majini chini ya dunia kwakuwa mimi sifanani na chochote. Mungu akaniambia kwakuwa sifanani nachochote ndio maana hata uzima huwezi ukaufanananisha na chochote kwakuwa hauonekani pia akaniambia kuwa kwakuwa hafanani na chochote ndio maana hata upendo haufanani na chochote japo upo na pia akaniambia kuwa kwakuwa hafanani na chochote ndio maaana hata haki huwezi kuifananisha na chochote. Ndipo Mungu akaendelea kuniambia kuwa kwakuwa hana Umbo ndio maana aliishi ndani ya Kristo Yesu na kumtumia Kristo Yesu kujifunua hapa duniani, akaniambia watu wote waliomfuata Yesu hawakumfuata kwasababu ya sura yake au kwasababu ya umbo lake au kwasababu ya taifa lake au kwasababu ya mavazi yake au kwasababu ya rangi yake au kwasababu ya chochote alichokuwa nacho au alivyoonekana , Mungu akaniambia wazi Kuwa waliomfuata Yesu walimfuata kwasababu alikuwa na yeye Mungu yaani Yesu alikuwa na Uzima alikuwa na Upendo alikuwa na Haki yaani Yesu hapa duniani alikuwa na Mungu Baba yake wa Mbinguni
Ndipo kwa mara ya kwanza nilijua wazi kuwa Uzima,upendo na haki aliishi ndani ya Yesu Kristo naye Uzima ,upendo na haki ndiye Mungu wetu wa milele.
Baada ya Mungu kuniambia maneno hayo ndipo akasema..................

HATUA YA NNE YA USHUHUDA HUU HII HAPA ISOME
Baada ya Mungu kujifunua kwangu nakunithibitishia kwamba yeye ni Uzima ni Upendo nani Haki ndipo akaniambia kama nilivyoishi na Yesu Kristo na kutembea na Yesu Kristo hapa duniani Pia nimekuchagua wewe nataka kuishi nawewe na kutembea nawewe hapa duniani kama nilivyoishi na kutembea na Yesu Kristo, maneno haya hayakuwa rahisi kwangu kwani nilikuwa kijana mdogo kwa umri nasikuwa najitambua kama ninavyojitambua hivi leo, na kwakweli maisha yangu yalikuwa njia panda kwa mambo mengi wakati huo , nikiwa pale chini hofu ilikuwa kubwa sana moyoni mwangu lakini amani ilikuwa kubwa zaidi hivyo niliendelea kumsikiliza Mwisho Mungu akasema namimi akaniambia ninakutuma kwenda duniani katika kizazi chako kwenda kunitambulisha ili wanadamu wanijue mimi Mungu wa pekee wa kweli niliyemtuma Yesu Kristo na manabii na mitume wengine
Kwakweli
Kwakweli utukufu wa Mungu niliokutana nao siku ile sijawahi kukutana nao maisha yangu yote hakika Mungu ana nguvu na mamlaka yake ni ya milele, baada ya utukufu wa Mungu yaani uwepo wa Mungu kuniachia nilirudi katika akilia yangu ya kawaida nakujikuta nipo pale pale sebuleni nilipokuwa awali kabla sijaingia katika kukutana na uwepo wa Mungu na utukufu wa ajabua. nilijifunza nini kwa Mungu kujitambulisha kwangu? ninini nilifanya baada ya tukio hilo? Mungu amenituma kufanya nini duniani kuanzia Tanzania

HATUA YA TANO YA USHUHUDA HUU HII HAPA ISOME
Baada ya Mungu kunitokea na kujifunua kwangu ndipo kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilimjua Mungu wa pekee wa kweli nilimjua Mungu kwamba kumbe hana umbo kama wengine wanavyofikiria nilijua Mungu anaweza kuingia ndani ya mwanadamu yeyote amtakaye na kumtumia kukutana na shida za wanadamu wengine, nilijua wazi kuwa Matatizo ya wanadamu ndio ibilisi na majibu ya matatizo ya wanadamu ndio Mungu mwenyewe yani hapa nilijua kwa hakika kuwa wanadamu tunasumbuliwa na shetani yaani shetani ni Mauti, Uovu na yasiyo ya haki na ndipo nilijua wazi jibu la matatizo yaani jibu la shetani duniani ni Mungu yaaani Uzima, upendo na haki kwa hakika nimejua wazi kuwa wanadamu wakimjua Mungu watajua namna ya kumsinda shetani ambaye ni adui wa MUNGU NAni adui yao , kwa hakika mimi binafsi nimejua wazi wanadamu wote wa dini zote makabila yote na mataifa yote sote tunamuhitaji Mungu yaani tunaitaji uzima, upendo na haki na daima tunaishi maisha ya kumtafuta bila kujua kuwa tunamtafuta Mungu. kwa hakika maisha yangu tangu nimjue MUNGU yamebadilika sana hivi sasa ninaishi na Mungu na ninatembea na Mungu kumfunua kwa wanadamu wengine wote wanaomuhitaji katika maisha yao
Katika maisha yangu nimegundua kwa hakika kuwa miili ya wanadamu,ndoa zao, familia zao,ko zao, makabila yao, vyama vyao, mataifa yao, huduma zao, taasisi zao, mashirika yao, vikundi vyao, madhehhebu yao, dini zao, mabara yao na umoja wa mataifa vyote vinahitaji Uzima , upendo na haki, na ndivyo ambavyo wanadamu katika maeneo hayo ya maisha wanavipigania na kuvitafuta daima, pia niligundua kitu kimoja nacho ni kwamba popote palipo na uzima pana amani, hivyo twaweza kusema wakati mwingine kuwa Mungu ni amani ni upendo nani haki kwakusema hivi nataka ujue wazi kuwa Amani , upendo na haki ndio msingi wa maisha ya mwanadamu katika ndoa ,familia, ukoo nk... ITAENDELEA

Sunday, March 9, 2014

KUWEKA AGANO NA MUNGU









 JOSEPH GOLIAMA

AGANO NA MUNGU
Agano na Mungu ni maafikiano na Mungu, ni makubaliano baina yako na Mungu, ni mapatano na Mungu wako, kufikia agano na Mungu au kuweka agano na Mungu ni lazima kwa kila mwanadamu anayetaka kuingia mbinguni, agano na Mungu ni makubaliana ambayo unapaswa wewe binafsi mwanadamu uyaingie na Mungu wako makubaliano ya kuamua kuyatoa maisha yako kuishi na Mungu na kutembewa na Mungu siku zote za maisha yako ya hapa duniani
Kuweka agano na Mungu kunawezekana endapo tu utamjua Mungu na endapo utayajua maisha anayoyaishi Mungu wako, kuweka agano na Mungu ni sawa na kuweka agano la ndoa na mume wako au mke wako mnayetaka kuoana, kwanza kabla ya kuingia agano la ndoa ni lazima kila mmoja amjue mwenzi wake kumjua mwenzi wako kunakupa fulsa ya kujua kama atakuwa msaada kwako katika maisha ya ndoa pili unapaswa kujua maisha ambayo mwenzi wako anayaishi hii itakupa kujua kama maisha yake yanaendana nawewe au maisha yake yatakua sababu ya ndoa yenu kuwa na matatizo na kuvunjika...ndivyo ilivyo katika maisha kama unataka kuweka agano na Mungu kwanza unapaswa kujua Mungu ninani pili utapaswa kuyajua maisha ya Mungu anayoyaishi, baada ya kuyajua mambo hayo mawili ndipo sasa waweza kuweka makubaliana na Mungu ya kuishi nayeye na kutembea naye hapa duniani kwasababu mnakua mmejuana
SOMA USHUDA HUU JINSI MUNGU ALIVYONITOKEA MIMI NAKUJITAMBULISHA KWANGU NAMIMI NIKAMJUA
Ndugu wanadamu wenzangu napenda kuwashuhudia jinsi nilivyokutana na Mungu na maisha yangu kubadilika ilikuwa mwaka 2007 mwezi wa saba nikiwa naishi tegeta siku hiyo ilikuwa yapata kama saa saba mchana, nikiwa chumbani ghafla nilijisikia kama moyoni nimetenda dhambi ambayo ilikuwa ikinisuta nikaanza kuomba rehema za Mungu niliomba kwakuwa nilijisikia hatia sana, wakati ninaomba nilianza kutembea huku na huku mpaka nikafika sebuleni, nikiwa sebuleni huku nikiomba nikahisi kama moshi unatokea na kujaa pale sebuleni, hali ile ilinishangaza sana nikahisi kama kuna mtu pengine amekoka moto ndio maana dirishani moshi unapenya, hivyo nikaamua kukatiza maombi na kutoka nje ,nilizunguka nyumba yote niliyokuwepo kuona kama kuna mtu amewasha moto katika ile nyumba, hata hivyo sikuona moto wala dalili za moto nikaamua kurudi ndani nilipofungua mlango huku nikiendela kuomba nikaona ule moshi ndio kwanza unazidi nakuongezeka sana, kwakweli niliingiwa na uwoga sana, wakati natafakari hali hiyo gafla nikakumbuka mafundisho aliyonifundisha mchungaji mmoja jina nalihifadhi aliyeniambia habari za alama zinazoonyesha uwepo wa Mungu naye alinitajia kuwa Wingu, Moto,Njiwa, Malaika, Moshi na alama nyingi nimezisahau kuwa ni alama zinazoonyesha uwepo wa Mungu na yakwamba Mungu ameonekana akijifunua kupitia alama hizo mara kwa mara alipokuwa anawatokea wanadamu kwa kwakuwa yeye hana umbo. Mara baada ya kukumbuka jambo hilo nilipiga magoti chini na kusujudu ,nilipokuwa nasujudu gafla nilisikia sauti ikiniambia usiogope mara Nne iliongea maneno hayo, usiogope...usiogope...usiogope...usiogope nimimi Mungu nimekuja kujifunua kwako ili unijue nataka unitambulishe katika kizazi chako ilisema sauti ile
Nikiwa nimesujudu pale chini hofu ilinitawala nisijue lakusema nikiwa sielewi niseme nini ile sauti ikaniambia tena nimekuja kujitambulisha kwako kama nilivyokuahidi ndipo sasa nilijua kuwa Mungu anaongea nami akaniambia yafuatayo
Mwanangu mimi Mungu ndiye yule ambaye ninyi wanadamu kote duniani katika mataifa yote mnanitafuta kwasababu mnanihitaji, akarudia tena mara ya pili akaniambia Mwanangu mimi Mungu ndiye yule ambaye ninyi wanadamu kote duniani katika mataifa mbalimbali mnanitafuta kwasababu mnanihitaji aliponiambia kwa mara ya pili nikajiuliza hivi hapa duniani katika mataifa yote sisi wanadamu tunatafuta nini? wakati najiuliza swali hilo akaniambia tena akasema mwanangu mimi Mungu ndiye yule ambaye ninyi wanadamu kote duniani katika mataifa mbalimbali mnanitafuta sana kwasababu mnanihitaji sana mnanitafuta kwa kuzunguka huko na huko duniani kunitafuta,mnanitafuta kwa kupanda ndege, kwakupanda meli kwakupanda magari kwakupanda treni kwakupanda wanyama kwakutembea kwa miguu na kwa njia nyingine nyingi kwasababu mnanihitaji sana. Baada ya Mungu kuniambia maneno hayo nilijiuliza sana juu ya maneno hayo nikawa najiuliza hivi sisi wanadamu tunatumia vyombo vya usafiri na miguui tunazunguka huku na huko tunatafuta nini kote duniani? wakati najiuliza maswali hayo gafla nilijikuta nipo hospitali ya muhimbile kisha nikajiona nipo hospitali ya mwananyamala na kisha nikajiona nipo hospitali ya mikocheni mbele yangu niliwaona wagonjwa wakila kiungo wamelazwa mawodini na wengine wako nje ya hospitali, hali ilikuwa mbaya sana kwasababu hospitali karibu zote niliona zimefulika wagonjwa niliwatambua wagonjwa wa kansa wa matumbo wa ngozi wa nywele wa masikio, wa macho karibu kila mgonjwa alisumbiliwa na kiungo kimoja ua kadhaa, nikiwa kwa huzuni na fadhaa nikiwaona wale wagonjwa kafla nilisikia sauti ya Mungu ikiniuliza maneo yafuatayo 'bila shaka watu hao wametoka sehemu mbalimbali za dunia hii na wamekuja kwa kutumia njia mbalimbali wanatafuta nini mahali hapo? ni swali ambalo kwakweli lilinipa kuwaza sana wakati najiandaa kulijibu nikasikia sauti ya ndani kama inaniong'oneza ikiniambia sema wamekuja kutafuta Uzima wa viungo vya miili yao name bila ajizi nikasema MUNGU WATU HAWA wanahitaji uzima katika miili yao ndio maana wapo hospitali nikaonyesha nikasema mtazame yule anatafuta uzima wa jicho yule uzima wa miguu yule uzima wa tumbo yule uzima wa damu yule uzima wa mifupa yake yule uzima wa kiuno yule uzima wa matiti yule uzima wa shingo yule uzima wa meno yule uzima wa goti yule uzima wa ..........nilitaja kila kiungo kilichokuwa kinahitaji uzima baada yakumaliza kumuambia Mungu hitaji la watu niliokuwa nawaona ndipo Mungu akasema name akaniambia Mwanangu usisahau siku zote za maisha yako kwamba Mimi Mungu wako ni Uzima
Neno hilo lilinipa mshangao sana nikajiuliza moyoni inamaana wanadamu wanapotafuta uzima kumbe wanamtafuta Mungu bila kujua?kumbe Mungu ni Uzima ufunuo huu mara ya kwanza ulinipa kujua wazi kuwa Mungu ni Uzima unapohitaji Uzima katika mwili wako kumbe unamuhitaji Uzima yaani unamuhitaji Mungu
HATUA YA PILI YA USHUHUDA HUU NI HII ISOME
Nikiwa katika dimbwi zito la kutafakari kuhusu Mungu ni Uzima na jinsi wanadamu tunavyotumia ghalama kubwa kutafuta uzima ,kumbe hatujui kuwa tunamtafuta Mungu ndipo nikajiona nipo mbele za umati wa watu wengi sana, watu wale niliowaona walikuwa wengi na idadi yao sikuweza kabisa kuijua na walikuwa katika makundi matatu, kundi la kulia kwangu walikuwa ni watoto niliowatambua kuwa ni yatima na katikati niliwaona wakina mama ambao niliwatambua kuwa ni wajane na kushoto niliwaona wadada ambao kimsingi nilijua kuwa ni makahaba, huku nikiwaangalia watu hawa wote kwa makini nilisikia sauti ya Mungu ikisema name na kuniuliza ikisema, 'bila shaka watu hawa wapo kote duniani katika maisha yao wanatafuta nini? swali hili lilikuwa gumu kwangu kulijibu mara moja wakati nawaza nijibu nini nikasikia sauti ndani ya moyo wangu ikininong'oneza tena ikisema sema wanatafuta Upendo maishani mwao, nami bila ajizi nikasema Mungu wangu hawa watu katika maisha yao wanatafuta upendo nikamwambia waangalie wale watoto yatima wazazi wao wamefariki wanatafuta mtu atakayewahudumia kama wazazi wao walivyokuwa wanafanya, wanahitaji mtu anayeweza kuwajali na kuwathamini ili waendelee kushi kama watoto wengine, tena nikamwambia wale kina mama wajane nao wamefiwa na waume zao wanahitaji mtu wakuweza kuwahudumia kuwaonyesha upendo kama waume zao walivyokuwa wanawahudumia kwa kuwaonyesha upendo na nikamwambia na wale wanadada makahaba nao pia wanahitaji upendo maishani mwao wanahitaji kuendesha maisha yao wanahitaji kuishi hivyo wanahitaji kuhudumiwa ili waache maisha yao machafu kimsingi nilimwambia Mungu kuwa makundi yote matatu yanahitaji upendo, kujaliwa ,kuthaminiwa .ndipo Mungu akasema namimi nakuniambia 'mwanangu kumbuka siku zote za maisha yako kuwa mimi Mungu ni UPENDO, aliponiambia kuwa yeye Mungu ni Upendo ghafla niliingia katika dimbwi zito sana la mawazo nikawa nawaza kumbe wanadamu tunapotafuta upendo kumbe tunamtafuta Mungu pasipokujua kuwa tunamtafuta Mungu kuanzia pale nikawa nawaza mambo mengi sana tena nikawa nawaza maisha yangu nilipotoka na pale nilipo, wakati nawaza haya gafla nikajiona nipo... ITAENDELEA KESHO USIKOSE MWENDELEZO HUU WA MAKALA ITAKAYO BADILISHA MAISHA YAKO.

Wednesday, March 5, 2014

IDUMU INJILI MTAANI, DODOMA KITAELEWEKA TU


Sanamu ya kumuenzo baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwenye eneo la Nyerere Square ikionekana kwa mbali, ambapo Oscar Mwanyanje akipita mbele yake kwa nje na megaphone yake akihubiri injili mitaani.
Mara zote inaia moyo kuona kwamba bado kuna hudma ya Injili mtaani, na kwamba wako wenye kuitwa kwa namna hiyo wapate kupanda mbegu na kisha kusubiria mavuno. Hali ndivyo ilivyo kwa Bwana Oscar Mwanyanje, mhitimu wa shahada ya uhasibu kutoka chuo cha biashara (CBE) Dodoma.

GK ilipomtia machoni, ilipata shauku ya kujua kunani, ili basi nawe upate kujuzwa mwanzo wa jambo hili ukoje. Kwa maelezo ya Bwana Mwanyanje, anasema kuwa ameitiwa kwa hili jambo, na punde tu alipohitimu masomo mwaka jana, basi sauti ya kuhubiri Injili mtaani ilimjia.

Hakuna kulala hadi kieleweke, wiki ya pili ya injili inasonga.
Licha ya kwamba alijua kwamba ndani yake jambo hili limekuwepo kwa muda mrefu, aliufanya moyo kuwa mgumu kutii, jambo ambalo anasema lilimletea matatizo makubwa hata kiasi cha kukaribia kufa.
Muuzaji wa Biblia pamoja na wapita njia wengine wakimshangaa Oscar Mwanyanje wakati akihubiri maeneo ya uhindini, Dodoma.

Kwa elimu yake, na kwa baadhi ya kazi ambazo aliwahi kuomba, anaeleza kwamba zingine zilikuwa rahisi, na hata 'interview' kuwa rahisi, lakini kuna siku alipotoka kwenye 'interview', sauti ikamjia ikimwambia kuwa hatopata kazi hadi afanye kwanza kile ambacho Mungu amemuagiza.

Halikadhalika, Bwana Mwanyanje ametoa rai kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba kumtafuta Mungu kwanza, kwani kutokana na ukinzani wa mawazo kutoka makundi mbalimbali ya wajumbe hao bungeni, hawatoweza kufikia muafaka kwa maslahi ya taifa, basi ni vema wakatambua kwamba Bunge linamhitaji Mungu.

CHANZO: GOSPEL KITAA BLOG