Wednesday, April 30, 2014

HISTORIA YA KANISA LA EFATHA.


Photo: APOSTLE N PROPHET MWINGIRA
Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira.
Huduma ya EFATHA yenye msingi wa Kitume na Kinabii, ilianzishwa mwaka 1996 na kuandikishwa kisheria hapa Tanzania mwaka 1997
Huduma hii imeinuliwa kwa majukumu makuu matatu;

1.   Kuponya watu kutokana na mateso ya magonjwa na madhaifu mbalimbali.  2.   Kuwafungua watu kutoka kwenye vifungo mbalimbali vya mwili, nafsi na roho. 
 3.  Kuliandaa kanisa la mwisho tayari kwa ajili ya unyakuo. 

Kanisa la Efatha wamedhamilia  kuwafikia wote waliokusudiwa na Mungu kwa njia mbalimbali kama vile TV, Radio, Mitandao ya Kijamii kama Facebook, Twitter, Blog na Youtube. Pia kupitia Ibada, makongamano na warsha mbalimbali. Huduma ya Efatha chini ya mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat E. Mwingira, ambaye ndiye Mkurugenzi wa huduma hii, ambayo inaendelea kukua kwa kasi hapa Tanzania na nje ya Tanzania ikiwa na makanisa zaidi ya 200 na makanisa zaidi ya 15 nje ya nchi.
Ni hakika kuwa Huduma hii imekuwa makimbilio ya wengi hasa wanyonge waliodharauliwa MUNGU amewainua na kuwathibitisha. 
Makao makuu ya Huduma ya Efatha yapo Kibaha Precious Centre, na kanisa kubwa lilipo Mwenge katika jiji la Dar es salaam, Tanzania. 
Mnakaribishwa watu wote katika ibada za kanisa la Efatha  zinazofanyika katika vituo mbambali vya Efatha ndani na nje ya Tanzania. 
Mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat  Mwingira
Huduma ya Efatha imeanzia Tanzania na kuenea sehemu mbalimbali Afrika na nje ya Afrika. Hadi sasa Efatha ina vituo vya ibada Kenya, Zambia, Malawi, Rwanda, Afrika ya Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Marekani, Ulaya.
YESU ameniponya.
MUNGU akubariki sana.
BWANA YESU akiwa kazini Efatha baada ya kumponya mama.

Kibaha Precious Centre

Saturday, April 26, 2014

KILA KITABU KATIKA BIBLIA KINAMZUNGUMZIA YESU KRISTO.

BWANA YESU asifiwe.
Ubarikiwe sana ndugu popote ulipo na ubariki sana kwa kufatilia habari na mafundisho kupitia Maisha ya ushindi blog na page yetu katika facebook.


Karibu tujifunze mambo haya muhimu kwa kila mtu.

Hapa leo nazungumzia VITABU VYA BIBLIA TAKATIFU NA MAANA ZAKE na JINSI KILA KITABU KINAVYOMZUNGUMZIA BWANA YESU.



1:  MWANZO- Ni kitabu kinachozungumzia uumbaji wa KRISTO. Mwanzo sura nzima ya kwanza inazungumzia uumbaji alioufanya BWANA YESU na kwa kuthibitisha hilo angalia Yohana 1:1-3( Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa MUNGU, naye Neno alikuwa MUNGU.  Huyo mwanzo alikuwako kwa MUNGU. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. ). 
 Bila ya uumbaji wa KRISTO hakuna ambacho kingeumbwa. YESU KRISTO ni MUNGU muumbaji, tusome tena Waebrania 1:2 (mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. ).

Kitabu cha Mwanzo kinazungumzia uumbaji wa KRISTO ambaye vitu vyote aliviumba yeye.

-Tunafahamu kwamba vitu vyote viliumbwa kwa Neno na Neno ni YESU KRISTO. Hivyo YESU KRISTO ni MUNGU muumbaji wetu.



2: KUTOKA-Ni kitabu kinachomwelezea BWANA YESU kama mwanakondoo wa Pasaka. Kumbuka pasipo kumwaga damu hakuna ukombozi.


-Bila sadaka ya mwanakondoo wana wa Israeli wasingetoka utumwani Misri, na ukisoma Biblia tukio la mwisho kabla hawajatoka Misri walichinja kondoo na kupaka damu ya kondoo hao katika miimo ya milango ya nyumba zao, likatokea pigo kwa wazaliwa wa kwanza wa wamisri wote hivyo waisrael wakatoka (Kutoka 12:21-36) na hata sisi bila BWANA YESU kujitoa sadaka msalabani tusingepata wokovu.Waebrania 11:23-29



3: MAMBO YA WALAWI-Kitabu hiki kinamzungumzia YESU KRISTO kama sadaka yetu kwa ajili ya dhambi zetu. Walawi 16:30-34.( Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za BWANA. Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele. Na kuhani atakayetiwa mafuta na kuwekwa wakfu badala ya baba yake, ataufanya huo upatanisho, naye atayavaa mavazi ya kitani, yaani, yale mavazi matakatifu.
Naye atafanya upatanisho kwa ajili ya patakatifu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya hema ya kukutania, na kwa ajili ya madhabahu; naye atafanya upatanisho kwa ajili ya makuhani, na kwa ajili ya watu wote wa kusanyiko. Na amri hii itakuwa amri ya milele kwenu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kila mwaka. Naye akafanya vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa. ).


-Kumbuka kwamba yale ambayo yalitokea katika agano jipya kumhusu BWANA YESU ni yale yale ambayo yeye mwenywe alikishwa yasema katika agano la kale kupitia watumishi wake.



4:HESABU-Kitabu hiki kinamwelezea BWANA YESU kama Mwokozi aliyeinuliwa juu ili kutukomboa Hesabu 33:1-4( Hizi ndizo safari za wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa jeshi zao chini ya mkono wa Musa na Haruni.  Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya BWANA; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa.  Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa mkono wa nguvu mbele ya macho ya Wamisri wote, hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, BWANA aliokuwa amewapiga kati yao; BWANA akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo. ).

YESU ni Pasaka yetu.



5:KUMBUKUMBU LA TORATI-Kitabu hiki kinamwelezea BWANA YESU kuwa nabii wetu mkuu wa kweli Kumbukumbu 18:18( Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. )



6:YOSHUA-Kitabu hiki kinamwelezea BWANA YESU kama Jemedari wetu wa Wokovu wetu.

-Yoshua mwenyewe ni mfano wa KRISTO aliye jemedari wetu wa wokovu.Yoshua 1:1-11.

-Na hata maana ya Yoshua ni Mwokozi, na MWOKOZI wa kweli ni BWANA YESU KRISTO pekee.



7: WAAMUZI-Ni kitabu kinachomwelezea BWANA YESU kama mwamuzi wetu, Ndugu na mwamuzi wetu.

-Katika kitabu cha waamuzi, kulikuwa na waamuzi 15 na 1 wa 16 ambaye yeye alijipa uamuzi yaani Abimeleki.


Waamuzi hao 15 ni Othnieli,Ehudi,Shamgari,Debora,Baraka, Gideoni,Tola,Yairi,Yeftha,Ibzani,Eloni,Abdoni,Samsoni,Eli na Samweli.

-Waamuzi walikuwa katika makundi matatu.



A. Waamuzi wa kivita mfano Samson na Gideoni.


B. Kundi la makuhani. Mfano Eli.


C. Kundi la manabii. Mfano Samweli.


-Makundi haya matatu  ya waamuzi yako ndani ya kila aliyeokoka.

-Sisi sasa ni askari wa BWANA kwa ajili ya vita, sisi sasa ni manabii wa BWANA YESU na sasa sisi ni makuhani wa MUNGU.



8: RUTHI-ni sawasawa na waamuzi kinazungumzia habari moja , pamoja na agano ambalo BWANA YESU atalifanya. Na agano la BWANA YESU ni kweli daima.



9: SAMWELI WA 1 – Kinamwelezea BWANA YESU kama mfalme wetu, aliyetawala na atakayetawala milele.



10: SAMWELI WA 2 –Kinamwelezea YESU kama mtawala  na anaendelea kutawala , mfano licha ya Sauli kutawala lakini BWANA YESU aliendelea kutawala kupitia Daudi.

11: WAFALME NA MAMBO YA NYAKATI- Vitabu hivi pia vinaendelea kumzungumzia BWANA YESU kama mfalme anayetawala.



11: EZRA NA NEHEMIA-Vitabu hivi vinamwonyesha BWANA YESU kama mrudushaji wetu, ametukusanya tena  na pia amerudisha yaliyokuwa yamechukuliwa na adui.

Vitabu hivi mwanzo vilikuwa kitabu kimoja na vinamzungumzia BWANA katika hali sawa.



MUNGU akubariki sana.

Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

                       MUNGU akubariki sana .

                        Ni mimi ndugu yako

                          Peter M Mabula

                    Maisha ya Ushindi Ministry.

                         0714252292

Saturday, April 19, 2014

Je unamfahamu mwenyekiti wa waislamu waliookoka, Afrika Mashariki na Kati!


Mtume Peter Rashid Abubakar

Alitokea kwenye familia ya kichawi, mama yake alijiita ni mungu na kufanya miujiza mbalimbali ikiwemo ya kunyesha mvua. Sheikh Alhaji Rashid Tatashajara Abubakar, aliwahi kufanya shughuli za kisheikh katika msikiti wa Ilala mtaa wa Mwanza ambapo pia alikua mwanafunzi wa sheikh Yahaya Hussein ambaye ni marehemu kwa sasa.

Alianza kujifunza madrasa, akapanda vyeo na kusomea vyuo vya kichawi baada ya kuhitimu majaribio mbalimbali ikiwemo kufukua makaburi, kunywa damu za watu, kuhamisha nyota za watu, na kumeza majini 360 na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mkuu wa wachawi Afrika mashariki na kati!

Anasema katika mambo hayo yote, alikua akitumwa kushambulia watumishi wa Mungu mbalimbali, aliwahi kujaribu kwa Moses Kulola, Emmanuel Lazaro na Askofu Mwanisongole. Lakini alishindwa na kupata mieleka iliyompelekea kuumwa sana.

Akielezea ushuhuda wake kwa ufupi, Jinsi alivyompokea Bwana Yesu, ilikuwa sababu ya mke wake wa pili kupita kwenye mkutano wa Injili na kuponywa tumbo lililomsumbua kwa muda mrefu bila mafanikio ya kupona “mke wangu alikuwa akirudi nyumbani na kuimba nyimbo za makafiri, baadaye anaenda kanisani, sasa adhabu ya mtu anayekiuka sheria ni viboko 40, nilipotaka kumchapa mkono ukaganda, ndio mke wangu akasema piga magoti chini, akaniombea na mkono ukarudi mahala pake, baada ya hapo mengi yalitokea kukatisha story Mungu alianza kunifundisha na kunitumia”

“Siku Moja mtaa wa Salender Bridge kama mliwahi kusikia kisa cha dada aliyeota manyoya, alifikishwa kwangu nikamuombea kwa Jina la Yesu naye akapokea uponyaji. Kwa sasa yuko Marekani! nimemuona Mungu kwa jinsi ya tofauti kule nilikotoka nilikua namtumikia shetani, kwa sasa namtumikia Bwana Yesu, na kila ulimi utakiri kwamba Yesu ndiye Mungu”

Alhaji Rashid Abubakary kwa sasa ni mwenyekiti wa waislamu waliookoka Afrika mashariki na kati. Mungu amekua akimtumia kwa jinsi ya tofauti na amealikwa makanisa mbalimbali na kueleza shuhuda nyingi ambazo Bwana Yesu amefanya na kufanya kwenye maisha ya watu wengine. 

Mtume Peter Rashid Abubakar
Kanisani kwake.

Huu ni ushuhuda kwa ufupi tu kumhusu Mtumishi wa MUNGU Peter Rashid Abubakar pia kumbuka kuwa
YESU akiwa kazini kuwafungua watu kanisani kwa Mtume Peter Rashid Abubakar

Mtume Peter Rashid Abubakar ndiye mwanzilishi wa huduma ya Glory to God Miracle Center(House of Prayer For All Nations) Tanzania jijini Dar es Salaam

Thursday, April 17, 2014

UNABII JUU YA TANZANIA KUHUSU MAMBO YA KATIBA NA MUUNGANO:



Mwana wa Nabii Mchungaji Mtalemwa Dionis wa kanisa la Enlightened Christian Gathering ( ECG ) CHURCH ARUSHA BRANCH TANZANIA amekuwa akitoa unabii mbalimbali kwa watu binafsi na jamii kwa nyakati mbalimbali, Mungu amekuwa akimtumia kutoa unabii wa mabomu Arusha kabla hayajotokea kwa kutaja siku na tarehe na maeneo, majanga ya moto Arusha, mafuriko Dar es salaam na maeneo mengine.Mara zote huwataka watu kuomba na kuchukua tahadhari mapema ili kuepuka madhara, katika mojawapo ya mafundisho yake katika ibada alisema madhara yanayotabiriwa yanatokea kwasababu watu hawaombi kikamilifu baada ya kupewa unabii, wengine wanaomba ila hawachukui tahadhari, wengine wanadharau unabii na kukejeri lakini kundi jingine haliamini kabisa, kwasababu hiyo madhara huwapata watu, akifafanua alisema lengo la Mungu kutujulisha mapema ni ili tuchukue hatua ili madhara yasitupate kama walivyochukua hatua watu wa Ninawi (Yona 3:4-10).Jumapili tarehe 13/04/2014 Mwana wa Nabii akiwa anaongoza ibada ya kinabii kanisani kwake ECG eneo la Sanawari Manchester Arusha aliwahimiza waumini kuomba juu ya malumbano yanayoendelea Bungeni juu ya katiba na Muungano na haya ndiyo yalikuwa maneno yake "Mungu anatutaka tuombe zaidi maana naona kuanzia sasa hadi tarehe 26 Aprili kundi la wanasiasa watakaodai kuchoshwa na mambo ya mjadala wa katiba juu ya Muungano wataamua kupinga kwa vitendo na kuendelea kuwashawishi wengine ili wasiikubali hata siku ya kitaifa ya muungano yaani tarehe 26 april" Aliendelea kusema kwamba tarehe 26 kuna watu wamepanga kwenda barabarani na mabango wakidai pawepo na serikali tatu" Siku zote Mwana wa Nabii huwa anasisitiza kwamba hayuko upande wowote wa chama cha siasa ila huwa anaeleza lile Mungu analosema juu ya watu na kuwaelekeza la kufanya, aliendelea kutoa unabii akisema "watakaokusanyana na kupinga naona wakisambazwa na polisi na wengine kuumizwa vibaya" Tunawashauri watu kuomba ili Mungu atuongoze la kufanya juu ya muundo wa serikali na siyo kurumbana. Kwa waombaji wote andika "Mungu tupe suluhisho la katiba"
BreakingNews:
UKAWA waondoka Bungeni! Lipumba adai wao wanawaachia Intarahamwe ukumbi waendelee watakavyo!
Fuatilia yaliyojiri Bungeni hapa - http://bit.ly/1ipbVBc

KATIBA MPYA

KATIBA MPYA NA INJILI FOREVER


Haleluya wapendwa katika bwana wetu Yesu kristo,

         Nianze kwa kukutoa fikra za uwepo wa udini katika mada hii kwasababu sitazungumzia dini ya Kikristo au yoyote bali nitazungumzia wokovu ambao sio dini. Kuokoka sio dini na kama kuna mtu ameokoka na anamawazo ya kuwa hio ni dini basi hajaelewa. Ukiulizwa katika taasisi yoyote kuwa dini yako ni ipi jibu Mkristo sio Mlokole utakuwa umekosa swali.

       Haya acha tuendelee na mada tajwa hapo juu, Napenda kuzungumzia uhusiano wa katiba na Injili ila sitataja maandiko wala vifungu vya maandiko ila nitaandika kirahisi sana ili kila mtu aelewe. Binafsi naona watu walio okoka (sio kila Mkristo) wakiitumia vyema nafasi yao kunauwezekano mkubwa wa kupata katiba nzuri na yenye manufaa kwa taifa miaka mingi ijayo kwa sababu zifuatazo.

       Chochote unachokiona katika hali ya macho ya nyama kilianza kutokea katika hali ya Roho, namaanisha kabla ya Yesu kuyaona mateso atakayo yapata msalabani aliyaona kwenye maombi getsemane. Ngoja niweke msisitizo hapo, kabla hauja anguka kiroho katika hali ya watu kukuona ulisha anguka rohoni. Kwa maana hio kabla haijatokea machafuko katika nchi sababu ya uwepo wa vifungu vibaya vya kikatiba basi vurugu hizo lazima mtu alieokoka na mwanamaombi aliona katika hali ya Roho.

      Nini maana yake, Nchi yoyote ile hatma yake imewekwa chini ya wanamaombi, nafikili ningekuwa mimi Rais ningekuwa na kikosi cha wanamaombi ambao wataona yajayo kabla hayajatokea. Hebu pata picha wanamaombi wanaingia katika maombi wanapata habari ya hatari ya uwepo wa vifungu vitakavyo iangamiza nchi nadhani licha ya kumshukuru Mungu pia wataenda kutoa maoni yao ili katiba iweje ili isije kupatwa na yale walio yaona.

     Cha ajabu wanamaombi wamekuwa wakijisahau kama tunaishi katika hali ya Roho na Mwili kwa wakati mmoja kitu ambacho huwafanya waishie kufanya maombi bila kutoa maoni katiba mpya iweje, au kutokupiga kura kwa kusingizia siku ya kura ni jumapili.

LENGO LANGU

    Najua muda wa kutoa maoni umeisha naomba watu walio okoka wafatilie Bunge maalum la Katiba ili kujua ni mambo gani muhimu yapo na yapi hapo kwahio ukatae au ukubali utakapofika mchakato wa kupiga kura katika kuikubali ama kuikataa katiba kuliko kungoja wanasiasa wakushawishi ambapo kunauwezekano mkubwa kukubali mawazo ya chama fulani sababu unakipenda.

    Katiba ni makubaliano kati ya watawala na watawaliwa namna ya kuishi na inapotokea umeenda kinyume na hayo inakuwa ni kosa kubwa. Kwa mfano likatoka wazo la kufutwa mikutano yote ya injili Tanzania najua wanamaombi watajifungia kwenye vyumba nakuanza kukemea huku wamesahau kuwa wao hawakutoa mawazo yao katika ukusanyaji wa maoni. Najua maombi hayaepukiki ila tuwe wazuri katika kuzitumia akili zetu pia ili isije kutimia TUNA ANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.

IMEANDIKWA NA ROBERT MAZIKU 0653340950

Saturday, April 12, 2014

ALEX MSAMA WA MSAMA PROMOTION APATA AJALI DODOMA


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amepata ajali baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka wakati akielekea mkoani Dodoma.Chazo cha ajali
kilitokana na yeye kumgonga kijana aliyekua akiendesha basikeli na matokeo yake gari aliyokua akiendesha kupinduka mara 3.Kwa sasa Msama anapatiwa matibabu katika hospitali moja mjini Dodoma.
Picha zote kutoka kwenye Istagram ya mchekeshaji Steve Nyerere
                            Alex msama akiwa hospitalini baada ya ajali.Kulia ni mwenyekiti wa bongo movie Steve Nyerere 

Friday, April 4, 2014

DANIEL KULOLA KUFANYA MKUTANO MKUBWA KAHAMA, SHINYANGA


AKIANDIKA KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK, MTUMISHI WA MUNGU DANIEL KULOLA AMETOA TAARIFA YA UWEPO WA MKUTANO MKUBWA MJINI KAHAMA KATIKA KANISA LA EAGT YERUSALEM. AMESEMA ANATARAJIA KWENDA NA TIMU YA WATU 6 AKIWEMO MAMA YAKE KWA MAANA YA MAMA KULOLA.

 ANASEMA..
WAPENDWA MARAFIKI ZANGU WANA INJILI SALAAM KATIKA JINA LA YESU. NINAOMBA SAPOTI YENU NAANZA MKUTANO MKUBWA WA INJILI KAHAMA MJINI EAGT YERUSALEM. NAONDOKA NA TIMU YA WATU SITA NA MAMA KULOLA NAYE NI MIONGONI MWAO SHIRIKI NAMI NA UTABARIKIWA. NATEGEMEA KUMWONA MUNGU AKITENDA KWA NAMNA YA AJABU.

BLOG YA INJILI FOREVER INAMTAKIA MKUTANO MWEMA WENYE MATUNDA.

BINTI AFUFUKA BAADA YA KUFANYIWA MAOMBI. ALIKUFA GHAFLA SHULENI

MAITI YA BINTI IKILETWA KANISANI

Ni jambo la ajabu masikioni na machoni mwa watu kusikia kuwa mtu aliyekufa aweza kufufuka tena lakini Biblia inasema, Pozeni wagonjwa, TAKASENI WENYE UKOMA, FUFUENI WAFU, TOENI PEPO MMPETA BURE TOENI BURE. Haya ni maneno ya Yesu anayowaambia wanafunzi wake. Andiko lile lile linaloagiza kutoa pepo ndilo linaloagiza kufufua wafu, kumbe wafu wanatakiwa wafufuliwe kwa kiasi kilekile ambacho pepo wanatolewa.

Sawasawa na neno lake, ndilo lililojiri katika kanisa la Ufufuo na Uzima, tawi la Mwanza linaloongozwa na Mch. Kiongozi Samson Gwajima baada ya binti aliyekufa ghafla akiwa shuleni kuletwa kanisani hapo







Buhongwa Mwanza na kufufuka baada ya maombezi.
Mungu amekuwa mwaminifu katika kutimiza neno lake maana wiki chache zilizopita aliletwa mtoto mdogo kanisani hapo na kufufuka mara baada ya maombezi. Pichani kulia ni watu waliombeba binti huyo baada ya kufa shuleni wakimleta kanisani na kushoto ni mahojiahano kati ya Mch. Samson na binti aliyefufuka.

Mungu kwetu ni Mungu wa kuokoa na njia za kutoka mautini zina yeye!!!
Binti aliyefufuka akihojiwa baada ya kufufuka.