Katika siku ya pili ya Mkutano Mkubwa wa kutokea katika mkoa wa Tanga kumekuwa na matendo makuu na maajbu ambayo Mungu ameyatenda kupitia kwa Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, wa Kanisa la Glory of Christ (T) Church- Ufufuo na Uzima.
Mchungaji Gwajima akiwabariki na kuwawekea ulinzi maelfu ya watu ili wasichukuliwe au kudhuriwa tena na shetani kwa Jina la Yesu |
HALIMA ALLY
Anatoa ushuhuda wake na kuelezea kuwa alikuwa amechukuliwa msukule na Bibi mmoja aitwaye Nyatanga ambaye ni mchawi, na alikuwa amemuweka kwenye shimo kubwa jeusi.
Halima aliendelea kuelezea akiwa na machungu sana huku akilia kutokana na mateso makali na mambo ya kikatili aliyoyaona huko msukuleni, aliuelezea uamti kuwa chakula alichokuwa anakula ni Pumba za mahindi na za mtama...na shughuli yake kubwa ilikuwa ni kutumikishwa mambo ya kichawi na kuwadhuru wanadamu.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa na HALIMA ALLY akiwa anatoa ushuhuda wake kwa machungu sana huku akibubujikwa na machozi ya kwikwi. |
Mama yake mzazi aliweza kuitwa na kujitokeza na akaelezea kuwa mtoto wake alikuwa hana maendeleo mazuri shuleni wala nyumbani na alikuwa hajui hasa chanzo ni nini. |
HUSSEIN OMARY
Ni kijana ambaye anaishi Tanga mjini alifika siku ya Pili ya mkutano, maisha yake yalikuwa na mikosi isiyoisha.
Lakini baada ya maombezi ya Mchungaji Josephat Gwajima ikaja kugundulika kuwa nafsi ya Hussein ilikuwa imechukuliwa msukule kwa njia za kichawi na alikuwa anatumikishwa kulima mashambani huko Bumbuli.
Mchungaji Josephat Gwajima akiwa na Hussein Omari mbele ya maelfu ya watu akiwa anatoa ushuhuda wake. |
Mama yake Hussein akilia kwa uchungu huku akielezea furaha yake moyoni kwa kummpata tena mwanae wa mwisho Hussein,Pia Hussein akiwa analia kwa furaha kwa kuweza tena kumuona mama yake Mzazi |
Hussein akimshukuru Mungu na kuahidi kumkabidhi bwana Yesu maisha yake milele. |
Mama yake mzazi Hussein (mwenye nyekundu) na Mama mdogo katikati wakimlaki mtoto wao baada ya kurudishwa kutoka msukuleni. |
Dada huyu alipokea uponyaji wake baada ya kuombewa na mchungaji Josephat Gwajima kwa Jina la Yesu, ni msichana ambaye kwa muda mwingi ameishi na mama yake wa kambo.
Lakini ikafikia wakati akachukuliwa msukule na huyo huyo mama wa kambo na kuplekwa kutumikishwa katika mashamba, ambapo, yeye mwenyewe anaelezea huku akiwa analia sana kiasi cha kuishiwa nguvu, kuwa alikuwa analimishwa sana kwa njia za kichawi mashamba ambayo ni makubwa sana..
Lakini Baada ya maombezi alianza kusikia sauti ya Mungu inamuita njoo..na ndipo alipoambiwa na huyo mchawi aliyekuwa anamtumikisha kuwa hafai na aondoke mara moja na hatimaye akajishtukia yuko uwanja wa Tangamano.
Mwanaidi Julias akimshukuru Mungu kwa kumuokoa kutoka katika kifungo cha shetani. |
Baada ya maombezi Khadija alikiri kuchukizwa sana na mambo ya kutumikishwa na shetani na alikiri kumkabidhi Yesu Kristo maisha yake.
Alimshukuru sana Mungu kwa kumuokoa.
Khadija Kassian akihojiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima na akikiri mbele za watu kazi alizokuwa anaifanya ya kumufanyia ushirikina mme wake, ila amekiri kuacha na kumpokea Yesu. |
Jojina akiwa anamshukuru Mchungaji Kiongozi kwa kumuombea kwa Jina la Yesu na amerudishwa kutoka msukuleni. |
HILDA JOHN
Ni mwanamke aliyekuwa anaishi mjini Tanga lakini kumbe alikuwa amechukuliwa msukule na bibi yake huko barabara ya 19 ambako alikuwa anatumikishwa mabo mengi ya kichawi
Hilda akiombewa na Mchungaji Kiongozi Josphat Gwajiama. |
SIKUZANI MSIAKA
Huyu ni mtoto wa kike mwenye umri wa Miaka 19 anaishi Tanga Barabara ya 16, baada ya kuombewa na Mchungaji Josephat Gwajima katika uwanja wa Tangamano, alianza kutoa ushuhuda wake.
Alisema alikuwa anaishi chini ya Bahari ya Hindi, na huko alikuwa analishwa nyama za watu, alianza kuelezea ilikuwaje hadi akawa huko chini ya bahari na ndipo akasema katika siku ambayo haifahamu vizuri mwaka 2009 alianza kuota ndoto mbaya mbaya sana, na zikaendelea kwa kipindi kirefu sana hadi siku moja akawa anaota ameshikiwa upanga na mkuki akiongozwa aelekee baharini na ndipo alipokuwa hadi anarudishwa uwanjani hapo.
Msichana aitwaye Sikuzani akimuelezea Mchungaji Josphat Gwajima kuhusu maisha yake ya kulishwa nyama za watu chini ya bahari ambako amekuwa huko Tangu mwaka 2009. |
Sikuzani alimshukuru Mungu kwa Kumukomboa kutoka katika vifungo vya shetani na aliahidi kumpokea Yesu kuwa Bwana na Muokozi wa Maisha yake. |
Yeye mwenyewe alishuhudia akisema kuwa alikuwa analimishwa mashamba makubwa sana, na anamfahamu aliyekuwa amamchukua kwa njia za kichawi na kumtumikisha , na akadai kuwa na Mama wa nyumba ya Jirani..
Pia akasema kuna vipindi anapelekwa kishirikina katika msitu mkubwa sana kufanya mambo ya uchawi pia.
Fadhili Chamshama akilia kwa uchungu akiwa anaelezea mateso makalia aliyokuwa anatendewa huko msukuleni |
RODGERS FREDERICK
Ni kijana mdogo ambaye na yeye alifanikiwa kuachiwa shetani baada ya maombezi na Mchungaji Josephat Gwajima, Rodgers alipoulizwa aelezee alikuwa wapi akasema alikuwa msikitini alipokuwa amekewa jini maimuna.
Na aliyekuwa amemmpeleka msikitini ni shekh aliyemtambulisha kwa Jina moja la Hassan ambaye ni sheikh kwenye msikiti uliopo mjini Tanga katika barabara ya 15
Rodgers anaelezea jinsi sheikh Hassan alipokuwa anamtumia kupandisha mashetani na kuongea kiarabu, na kumtumia kwenye mambo ya kishirikina |
Kijana Rodgers Frederick alimshukuru Mungu kwa Kumuokoa na akaahidi kummpokea Yesu kuwa Bwana na muokozi binafsi wa Maisha yake. |
ZAWADI
Anaelezea kuwa alikuwa amechukuliwa msukule na Bibi upande wa Baba yake mzazi, anaendlea kusema kuwa bibi huyo alikuwa anamtuma usiku wa manane akawamwagie watu madawa ambayo yeye anaelezea kuwa zile dawa ni kwa ajili ya kuwapumbaza watu akili, na kuwavurugia maisha.
Zawadi alipoulizwa kuwa ametoka wapi kwa sasa akasema alikuwa chini ya meza kwenye nyumba ya huyo bibi, ghafla akaanza kusikia sauti inamwita na bibi yakee akaiskia pia akshtuka sana, bibi yake akaanza kumfukuza kwa kumpigia kelele "ondoka! ondoka! usiniletee balaa""!! na yeye akaanza kusikia kwa jina la Yesu Njooo"" na ndipo akazidi kukimbia na akajishtukia yuko katika uwanja wa Tangamano
Zawadi anamshukuru sana Mungu kwa kumkomboa aliahidi kummpokea Yesu na kuanza kumtumikia Mungu. |
ANNA RAPHAELI
Kisa cha Anna kinasikitisha na kinafanya kila mtu mwenye akili amlaani shetani, Anna alirudishwa baada ya kuombewa na Mchungaji Josephat Gwajima, Aisema huku akiwa analia kwa uchungu sana na kudai kuwa alikuwa amewekwa kwenye chupa, ambako alikuwa amewekwa kwa ajili ya kuwalea watoto, kwenye hiyo hiyo chupa.
Anna Raphaeli alimshukuru Mungu kwa kumkomboa kutoka kwenye kifungo cha shetani na ameahidi kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Muokozi wa Maisha yake. |
Mungu amembariki sana Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima kwa kumfikisha katika mikoa ya Arusha, Moshi na sasa ni Tanga na kote huko kumekuwa na miujiza na matendo makuu ya Mungu ambayo yamewafanya watu waokolewe kutoka katika mikono ya shetani.
No comments:
Post a Comment