Thursday, October 24, 2013

DINI MPYA YA SHETANI IMEIBUKA MBEYA INAITWA DIMAYO



SHALOM:
 Dini inayoamini katika MUNGU lakini ikiruhusu yale ambayo dini zingine zinapinga imeanzishwa eneo la mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya,
 Dini hiyo haiamini katika kutoa sadaka bali inasema tunamtolea nani sadaka wakati Vitu vyote tulivyonavyo ni mali ya MUNGU,kwa nini tunampa MUNGU mali zake Mwnyewe.!
Dini hiyo inaruhusu ulevi,uchawi na uzinzi kwa sababu vimeumbwa na MUNGU,Vile vile inaamini hakuna dhambi duniani,Dini hiyo inaitwa DIMAYO, sasa imeanza kuenezwa Mbeya.


Habari hii mwanzo ilinishtua sana mwanzo nilipoipata kutoka katika mtandao wa kijamii ujulikanao kwa jina la Jamii Forum. Ila nikakumbuka kuwa kila sehemu penye neema kubwa ya wokovu pia ndipo shetani hupapigania sana. Kama unaelewa neema ya wokovu iliyopo Nigeria ambako kuna watumishi wakubwa wenye upako wa kila aina kama TB. JOSHUA na wengine ila usisahau Nigeria inasifika pia kwa uchawi.

Wakati Mbeya ikiwa na neema kubwa ya wokovu kwa kutoa wainjilisti, Waimbaji, Wachungaji wengi nchi hii pia ni Mkoa unaosifika kwa matukio ya ajabu ajabu ikiwemo mauaji. Ukiulizwa ni mkoa gani unamakanisa mengi Tanzania huwezi kuacha kuanza na Mbeya.

LENGO LANGU.

TUONAPO MAMBO YA KUMDHIHILISHA SHETANI WAZI WAZI KAMA DINI YA DIMAYO BASI UJUE NEEMA YA WOKOVU NAYO INAZIDI. Hakuna haja ya kushtuka zaidi sana ni kumshukuru Mungu maana anaenda kudhihilika. Tusisahau kuwa endapo Mungu angemlainisha Farao awaruhusu wana wa Israeli kirahisi rahisi basi Tusingejua nguvu zake na maajabu ikiwemo kuitenganisha Bahari kisha kuirudisha. Ni lazima dini kama hizi zije ili watu wazione nguvu na maajabu ya Mungu wa kweli ukitofautisha na DIMAYO.

IMEANDIKWA NA ROBERT MAZIKU 0653340950

No comments:

Post a Comment