Saturday, December 28, 2013

Ufufuo wa Theo Nez

Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu 

Nafasi ya Pili 
www.DivineRevelations.info/Swahili 
Theo Nez alikulia katika taifa wa Wanavajo karibu na pembe 4 za USA. 
Bado anaishi katika eneo hilo. Mwaka 1995 alinunua kitabu cha Mary 
Baxter “Ufunuo wa kuhusu Kuzimu” akifikiri ataishi tena miaka 30 ijayo 
hivyo angeweza kuwa na muda mzuri kurekebisha na Mungu. Akakiweka 
kandolakini, miezi sita baadae alipokuwa akifanya Meth nyumbani kwake 
alikufa kwa sababu ya kutumia nyingi (over dose). Yesu Kristo mwenyewe akamchukua Theo 
kwa mkono wake na akampeleka katika shimo lake la Kuzimu. Kwa masaa mawili alimsihi Yesu 
asimpeleke pale….. Lakini Yesu hakuweza kubadili kitu. Mpaka pale aliposikia mke wake, 
muamini, akimuombea….Yesu akamueleza kuwa atakwenda kujibu maombi yake kwa sababu 
alisimama katika neon na hakurudi nyuma… Yesu akampeleka Mbinguni na kwa masaa mawili 
alimuonyesha mambo yajayo na akamuamuru awaambie wengine kwamba tunaishi katika 
nyakati za mwisho naya kwamba Bwana amekaribia kurudi. Ujumbe wake ni kuwa hatuwezi 
kuwatumikia mabwana wawili. 
Hello Kaka na dada zangu wapendwa. Jina langu ni Theo nez na ninnaishi Farmington New 
Mexico. Leo ningependa kushiriki nanyi ushuhuda wangu, Jinsi Mungu alivyofanya kitu cha 
ajabu sana, Kwangu mimi na kwa familia yangu. Alileta Wokovu wake katika nyumba yetu. 
Mwaka 1995, Nilikuwa ni mtu wa asili. Nilikunywa na kutumia madawa, sikujali kitu 
chochote.Siku moja, Nilitumia zaidi kupindukia kwa haraka na moyo wangu ukasimama. Nikafa 
kwa masaa. Kile nachotaka kuwaeleza, kitawafanya mfikiri mara mbili kwa habari ya maisha na 
kifo. Moyo wangu uliposimama, kelele za ulimwengu zikatoweka kabisa na giza kuu likaja 
kwangu. Nikaona mapepo matatu yakitoka kwenye moyo wangu, yakienda nje ya dirisha huku 
yakicheka. Nilipotoka kwenye Mwili wangu, Niligeuka nyuma nikamuona Yesu alikuwa 
amesimama nyuma yangu. Nywele zake zilikuwa ni dhahabu yenye weupe; Alikuwa amevalia 
vazi jeupe lenye mshipi wa dhahabu. Viatu vyake vilikuwa ni sandosi za dhahabu, na alisogea na 
akaongea kwa sauti ya upole.Viatu sandosi za dhahabu. Viatu vyake vilikuwa ni sandosi za 
dhahabu, na alisogea na akaongea kwa sauti tulivu. Kulikuwa na mwanga uliomzunguka na 
Roho yangu ikawa imekwisha mtambua. Nilitembea mpaka kwake na kumuuliza; Yesu ulikuwa 
wapi, nilikuwa nikikutafuta. na akaongea kwa upole na kusema; sikuwahi kukuacha, nimekuwa 
pembeni yako siku zote. Nilikuwa nikisubiri wewe utubu na kufanya kusudi la Baba. 
Unafahamu, nilikuwa nimeitwa kuhubiri miaka michache iliyopita. Nikasema, Nitakwenda,lakini 
nilikimbia. Nikasema siwezi kufanya, Bado ni kijana sana. Mungu anapokuita na kuingilia 
maisha yako huna uchaguzi mwingine lakini inakupasa useme ndiyo Bwana. Kisha 
nikamwambia Yesu, nilifikiri ningeishi miaka mingine thelathini. Njoo, imekupasa kuona mengi. 
Alinishika mkono wangu na tukaanza kutembea kuelekea chini kwenye njia. Ilikuwa ni giza na Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu 

Yesu mwenyewe ndiye alikuwa mwanga. Mara nikaanza kuona pepo wametuzunguka. 
Walikuwa wakijaribu kunirarua, lakini nikamshikilia Yesu mkononi kama mtoto mdogo. 
Alikuwa ni kinga yangu na akaanza kuongea nami. Akasema, unajua Baba anahasira nawe. Ni 
kwa sababu nilikuwa na cheza na kanisa na kukimbia kama Yona. Biblia inasema Yona aliitwa 
kuhubiri lakini alimkimbia Mungu. Nimefanya hivi kwa muda wa miaka mingi. Sasa imenishika 
mimi pia. Nilifahamu kuwa nilikuwa nimekufa katika dhambi zangu, na nilikuwa nimekwisha 
chelewa. Tulipoendelea mbele, Yesu akaongea mambo mengi na nikamuuliza maswali mengi. 
Tukasima mahali fulani na yesu akaniambia, angalia mbele. Niliweza kuona aina fulani ya 
mwanga kwa mbali. Yesu akaniuliza; Unafikiri hiyo ni nini? Nikasema, Bwana hiyo inaonekana 
kama kuzimu, Labda ni miali ya moto wa kuzimu. Hakika, tuliposogelea karibu, tukafika juu ya 
bonde. Bonde lilikuwa kama maili mbili kwa kina na maili tatu kwa upana 
Chini niliweza kuona miali ya moto, kila kitu kilikuwa ni orenji nyekundu, Nikaanza 
kutetemeka, Nikaanza kuogopa. Nilifahamu kuwa nitawenda kuishia mahali pale.Yesu 
akaniambia niangalie chini. Sikuweza hata kuangalia chini, nilianza kulia huku nikimkimbilia 
Yesu nyuma. Nikaanza kutubu, na kuliakwa Bwana ili anisamehe. Nitahubiri sasa, nipe nafasi 
moja ya mwisho. Nililia kama mtoto mdogo. 
Tuliendelea mpaka tukafika chini kabisa kwenye shimo la kuzimu. Nilona vitu vingi ambavyo 
maneno hayawezi kusimulia. Sehemu ile ilijaa roho za watu, na mapepo yalikuwa kila eneo. 
Biblia inasema Isaya 5:14 Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake 
bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, 
hushuka na kuingia humo. 
Kulikuwa na Roho za watu zikiwaka katika miali ya moto. Vilio na 
kelele zilikuwa kila sehemu. Hakukuwa na tumaini, hakukuwa na 
tumaini kwa roho zilizopotea. Kwa nini ? Kwa sababu walimkataa 
Yesu. Wengine walisubiri muda mrefu. Wengi walifanya mdhaa na 
wakamkimbia Mungu. Kumkimbia Mungu kutakufanya uingie 
Kuzimu. Ukishaingia mule huwezi kutoka. Tafadhali, ningependa 
uinue mikono yako na kumwambia Bwana; Usiruhusu hili kutokea 
kwangu. Tulipoendelea kutembea, Niliona mamia ya elfu ya mashimo. 
Nilikuwa nikilia na kuomboleza tulipokuja kwenye shimo moja 
ambalo ni tupu. lilikuwa na moto uliokuwa ukitoka ndani yake. Yesu 
akaniambia; Hili ndilo shimo ambalo shetani amekuchimbia. Kisha nikaanza kupiga mayowe, 
nikilia, Bwana sitaki kwenda pale. Nililia na kutubu, NikimuombaYesu anipe nafasi moja 
nyingine tena. Nililia kama Yona alipokuwa kwenye tumbo la Kuzimu. 
Katika Kitabu cha Luka 16, tunasoma kwa habari ya Lazaro na Tajiri mmoja. Tajiri alikuwa na 
kila kitu. 20 Kulikuwa pia na maskini mmoja jina lake Lazaro, aliyekuwa amejaa vidonda na 
alikuwa analazwa mlangoni pa nyumba ya huyo tajiri. 21 Lazaro alitamani kula makombo 
yaliyoanguka kutoka meza ya tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kulamba 
vidonda vyake! 22 Ikatokea kwamba huyo maskini akafa, malaika wakamchukua, wakamweka Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu 

karibu na Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa. 23 Huyo tajiri, alikuwa na mateso 
makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu 
naye. 24 Basi, akaita kwa sauti: Baba Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau 
achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno 
katika moto huu. 25 Lakini Abrahamu akamjibu: Kumbuka mwanangu, kwamba ulipokea mema 
yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini, yeye anatulizwa, nawe 
unateswa. 26 Licha ya hayo, kati yetu na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wanaotaka kuja 
kwenu kutoka huku wasiweze, wala wanaotaka kutoka kwenu kuja kwetu wasiweze. 27 Huyo 
aliyekuwa tajiri akasema: Basi baba, nakuomba umtume aende nyumbani kwa baba yangu, 
28 maana ninao ndugu watano, ili awaonye wasije wakaja huku kwenye mateso. 29 Lakini 
Abrahamu akamwambia: Ndugu zako wanao Mose na manabii; waache wawasikilize hao. 
30 Lakini yeye akasema: Sivyo baba Abrahamu, ila kama mtu atafufuka kutoka wafu na 
kuwaendea, watatubu. 31 Naye Abrahamu akasema: Kama hawawasikilizi Mose na manabii, 
hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka wafu." 
Oh Watu , tafadhali mnisikilize,hii ni halisi,weka mambo yako sawa na Mungu vile uwezavyo 
.Tulipotoka nje, tulisimama katika eneo lenye ukiwa. Yesu akasema;sikia. Na nikaanza kusikia 
mwanamke akisali niliweza kusikia sauti yake vizuri wakati akiomba alisema; Bwana mrudishe 
tena! Mpe tena nafasi nyingine. Bwana ana watoto wawili wa kiume wa kuwalea. Yeye ndiye 
pekee niliyenaye. Usimchukue Bwana! 
Unaamini maombi ya imani yanaweza kuamisha chochote? Biblia inasema, chochote 
mnachohitaji mkiomba , amini umekwisha pokea,na hakika mtapokea. Mwanamke huyu 
akaendelea kuomba. Yesu akaniuliza, Unafikiri huyo ni nani? Nikamwambia huyo ni mke 
wangu. Bwana akasema, unasikia hicho,nina watoto wawili wa kuwalea. Nikaanza kumshika 
Bwana kwenye mabega, siwezi kufa sasa, familia yangubado inanihitaji. Nikaanza kutoa sababu 
mbalimbali, lakini hakukuwa na jibu. Nikaanza kulia tena. 

Mke wangu aliendelea kuomba. Kulikuwa na kipindi cha kusubiri ambacho kilikuwa kama 
masaa na mwisho Mungu Baba akajibu hili, Akaongea na sauti yake ilikuwa kama Maji mengi. 
Akasema Mwanangu; nakwenda kukupa tena nafasi nyingine kwa sababu ya maombi na imani 
ya mke wako,nitakuhifadhi. Nikikurudisha, nitakwenda kukutumia. 
Hapo nikaanza kusema kwa viapo,Bwana nitahubiri. Nitafanya chochote, Nitawaeleza watu 
kuhusu sehemu hii, Nikasema Bwana ,Nitakusaidia kuokoa roho . 
Kisha tukatembea kuelekea kwenye chumba chenye kioo kikubwa kama Televisheni. 
Nilionyeshwa wakati wangu uliopita,wa sasa na utakaokuja. Nikaweza kuona ,maisha yangu 
kuanzia mtoto mpaka nilipokuwa mkubwa. Yesu alinipa ufunuo, maono. Alinionyesha mambo 
mengi sana ambayo ni lazima yatokee. Akasema, kweli tunaishi katika nyakati za mwisho. 
Nenda na uwaeleze watu. waambie watembee katika njia sahihi na watubu. Waeleze waache 
kucheza na mimi na waanze kushika amri zangu. 
 Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu 

Akanionyesha jinsi watu wanavyojificha nyuma ya Biblia, wanayaficha matendo yao,na 
wanaishi katika dhambi. Mungu anasikia na kuona kila kitu. Akasema watu hawa 
wanamuheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nae. Oh jinsi wanavyopenda 
kufundisha amri kwa watu, lakini wanaziacha amri za Mungu. 

Akasema , usogope,Mimi ni alpha na omega, wa kwanza na wa mwisho, Unachokisikia ni haki. 
Akasema; yeye aliye na sikio, na sikie kile Roho anasema kwa kanisa. Akanipa mistari mitatu,Ta
hadhari. Wa kwanza ni Kumbukumbu la torati 6:15. (15 kwani Bwana, Mungu wako, aliye 
katikati yako ni Mungu mwenye wivu;) isije ikawaka juu yako hasira ya Bwana, Mungu wako, 
akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi. 

Mstari wa pili katika Luka 16:13. Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili; 
kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au ataambatana na mmoja na 
kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. 

Msitari wa tatu katika kitabu cha Ufunuo 3:3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi 
ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua 
saa nitakayokuja kwako. 
Kaka na dada, Hatujui ni siku gani tutaonndoka katika ulimwengu huu, hatujui kesho imebeba 
nini ,kwa hivyo ninaomba kwamba uweke mambo yako sawa na Mungu wakati bado unaweza. 

Baada ya hili Yesu akanichukua mpaka mbinguni 
na tukatembea katika malango haya ya dhahabu 
katika mtaa wa dhahabu. Nikaona watu wengi wa 
kila taifa na walikuwa wamesimama mbele ya kiti 
kile cha enzi, wamevalia mavazi meupe, Baadhi 
yao ni watu niliowafahamu, wachungaji na 
manabii wa kwenye biblia. kila kitu kilikuwa ni 
kizuri,kila mtu alikuwa ni mwenye 
furaha;ungeweza kuona upendo wao kwenye sura 
zao. Nilianza kuhisi furaha na amani.Nilipokuwa 
nikitembeatembea, sikutaka tena kurudi. Yesu 
akanifunulia saa kubwa. Mkono wa saa ulikuwa 
umekaribia kufikia kamili kwenye 12,wakati 
unakimbia haraka,wakati wa kwenda sasa. 
Nikasema Bwana, sitapenda kwenda, nataka 
nibaki. Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu 

Lakini ilinipasa kurudi. Tulipokuwa tukirudi niliona dunia kama kampira kadogo kama ule wa 
golf. Alinileta tena kwenye chumba changumwili wangu ulipokuwa umelala. Alisogelea mahali 
ambapo moyo wangu ulikuwepo. Nyama iliyozungukza moyo wanguilifunguka. Yesu 
akachukua moyo wangu wa kale nje, na akautupa katika ziwa la moto, Kisha akanipa moyo 
mpya, na mwanga ukaja juu yake. Nilisimama pale nikiagalia na kutafakari,wow; hata ngozi na 
mifupa inasikia Yesu. 


Baadae nilitafuta katika biblia yangu na nikakuta Ezekieil sura 36 :26-27, Nililia kama mtoto 
mdogo kwa sababu ilikuwa imeandikwa, Pale Biblia inasema hivi: 26 Nami nitawapa ninyi 
moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya 
mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na 
kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. 

Baada ya Yesu kurejesha roho yangu kwenye mwili wangu, lakini moyo wangu mpya haukuwa 
unafanya kazi bado.Nilimuona mke wangu ameshika mikono yangu anaomba. Muda nikaona 
chumba changu kimezungukwa na maelfu ya malaika, walikuwa wakisifu na kuimba kwa 
nyimbo nzuri ambazo sikuwahi kuzisikia. Muziki tu wenyewe ulikuwa ni waajabu sana,Malaika 
mmoja akatokeza kwa nje na akatamka, akisema; Damu ya Yesu inakuja. Na malaika wote 
wakaanza kusifu na kuabudu. Kisha Damu ya Yesu ikaja tulipo,na kunisafisha mimi kuanzia 
kichwani mpaka kwenye vidole vyangu vya miguu ikasafisha dhambi zangu zote. Pombe na 
madawa vikatoka nje ya mwili. Nikahisi kama maji ya moto. Nilipojiangalia, ule weusi wote wa 
mwili wangu ukaondoka. Nilikuwa mweupe na msafi. 
Baadae malaika Yule Yule akatoka nje tena na akasema; Roho Mtakatifu anakuja.Malaika 
wakaanza kuimba na kuabudu tena. Holy spirit akaja kwetu tulipo na kutujaza. Roho yangu 
ikaanza kuruka tena juu na chini. Kisha nikampata Roho Mtakatifu. Roho ya Bwana ilikuwa na 
moto kama umeme; ilikuwa kama moto unaowaka kwenye mifupa yangu. 

Malaika walikuwa bado wakiimba na kusifu Yesu aliposema; Mwanangu, nenda kawaambie 
watu nilicho kushuhudia wewe. Akaugusa moyo wangu mpya kwa vidole vyake na ukaanza 
kufanya kazi. Ndipo kidogo kidogo macho yangu yakaanza kufunguka. Nikagundua mwili 
wangu umekuwa wa baridi, ilikuwa ni vigumu kidogo kuongea. Nikamuuliza mke wangu 
kilichotokea. Akaniangalia na kuniambia; Uko sawa? Kisha akaanza kulia. 

Kulikuwa bado kuna maumivu kwenye kifua changu chote, nikaona kama ninaopresheni. 
Nilikuwa mdhaifu na kiu; Kitu cha kwanza kuuliza ilikuwa ni maji. Kisha fahamu zangu Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu 

zikaanza kunirudia na nikakumbuka kilichonitokea. Kisha nikaanguka kwa Magoti na kuomba 
kwa muda wa masaa matatu mpaka jua likachomoka. 
Kutoka siku hiyo maisha yangu yamekuwa tofauti. Nilikuwa muasi, Lakini Mungu akanishusha 
kwa magoti , nikaanza kulia kama mtoto mdogo, nikiomba rehema. Nilikuwa nikifikiri, nikienda 
kuzimu, haitajalisha. Lakini sikuwa najua ni kiasi gani kuzimu ni chungu mpaka pale Bwana 
aliponifunulia. Sasa namshukuru Bwana kila siku kwa maisha ambayo amenirejeshea, familia, na 
huduma aliyonipa. 
Kaka na dada ,Ninaomba kwamba msichezee kanisa na kuwa na mabwana wawili, Kwa sababu 
huwezi ukacheza na Mungu. Ni kitu cha kutisha kama nini kuangukia katika mikono ya Mungu 
aliyehai. Hivyo usidanganyike,Mungu hadhiakiwi. Biblia inasema;Apandacho mtu, ndicho 
atakachovuna, Yeye apandaye uovu, atavuna huo. Ndiyo Mungu ni Mungu wa upendo; amejaa 
huruma na rehema. ni Mungu wa nafasi ya pili, lakini ni Mungu wa hukumu .Biblia inasema 
Yeye ni moto ulao.hivyo imetupasa tujiandae, kwa sababu hujui ni lini utakwenda kufa, Bilblia 
inasema katika waebrania 9:27, kama inavyoamriwa kwa wanadamu kufa mara moja, lakini 
baada ya hili ni Hukumu. 

Siku inakuja ambayo sote tutasimama mbele zake Mungu, na vitabu vyetu vitafunguliwa. Utakw
enda kuwa pale. Kila Mtu ambaye anasikiliza ushuhuda huu atakwenda kuwa pale. Hiyo itakuwa 
ni mwito ambao huwezi kukosa. Hii inaweza kuwa ni mwito wako wa mwisho, usiasi mbele zak
e Mungu. Tafakari kwa makini kuhusu hili, Itaenda kuwa peponi au kuzimu. Unaweza usipate na
fasi nyingine kama mimi; Ni kwa neema ya Mungu tu. 
Niko hapa leo ilikushiriki nanyi ushuhuda huu, ningependa unyanyue mikono yako na uongee na
Bwana, Mshukuru Yeye kwa kuwatahadharisha, Mshukuru Yeye kwa maisha haya ya thamani. 
Kama ungependa kuokoka, unahitaji sala hii, Ngoja niombe sala hii pamoja nawe hivi sasa. 

Bwana Yesu ,nisamehe. Ninakupokea wewe kama Bwana Mwokozi wangu. Njoo moyoni mwan
gu na maishani mwangu. Nipe Uzima wa milele, ili niweze kuishi nawe milele. Nipe maisha ya a
mani na furaha. Aksante Bwana. Katika Jina la Yesu, Amen. 




 Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu 

Kama ukipenda kuniandikia anuani yangu ni: 

Last living days Ministries 
P.O. Box 3701 
Farmington, NM 87499 
USA 
Unachokisikia kwenye ushuhuda huu ni simulizi ya kweli. Mimi ni
 Mtu wa India Mnavajo.Ninaishi Four Corners. Nina rasimisha kan
da hii kwa Wamarekani wenyeji wote Marekani nzima. 
Ninatoa Ruhusa kunakili ushuhuda huu. 




Ndugu aliyefasiri ufunuo huu ni Peter Kahale ni kijana aliyeokoka na anampenda Yesu na 
mwenye shauku ya kuhubiri injili ya Yesu Kristo. 
Simu ya Mkononi: +255-769-610460, +255-653-610460. 
Barua Pepe: kahalepeter@gmail.com 

BENNY HINN Reconciliation And Restoration Continues


Pastor Benny HinnIt all began at Christmas when we were together at Suzanne's house in Orlando, Florida. Suzanne and I and all of our children and grandchildren were there. It was a beautiful day I will never forget, and that is when the Lord began to do His mighty work.
Suzanne and I want to thank you, from the bottom of our hearts, for praying for us and our family. The Lord has surely answered your prayers! Suzanne and I are more in love with each other than ever before.
The covenant we made with God more than 30 years ago was never broken in His sight. Both of us believe our greatest days are ahead and the best is yet to come.
The last three years have been very painful for Suzanne and me and for the children—more painful than we can ever explain or describe. Suzanne and I will share much more with you in a future letter and soon on This Is Your Day. Please be watching next Thursday and Friday, June 7–8.
Our marriage died for two reasons. One, I, Benny Hinn, was married to the ministry, not realizing it was killing my marriage. And two, Suzanne started taking certain prescription medications to help her cope with some of her personal struggles. She became dependent on those for nearly 15 years, and those medications made her behave erratically at times. As her husband, I did not know what kinds of medicine she was taking or realize what they were doing to her.
 After the divorce, Suzanne, on her own accord, decided that she needed professional help to gain freedom from her chemical dependence and checked herself into the Betty Ford clinic in early 2010. And for three and a half months she underwent exhaustive treatment. Today she is totally set free from the need for these medications—she is completely whole—and for that I give the Lord Jesus the praise.
The truth of the matter is that Suzanne filed for divorce because she was crying out for help. The divorce most certainly woke me up, and the Lord used it to show me—as a man of God and as a man—that I cannot function properly without my wife and family.
Not only did our family suffer as a result, but the ministry also suffered greatly. Many partners walked away, not realizing or knowing what took place and why. But I believe that the Lord is restoring not just my family but also the ministry.
I need you as my partner today more than ever. And I promise you I will continue to preach the Gospel with all my heart and with Suzanne at my side. She and I will travel the world together, ministering the Gospel and the power of God. And we both believe that God will not only save lives and heal bodies but will also heal families. God is no respecter of persons, and if He did it for us, He will do it for others.
Because of our experience, God will do more with us in the future.
I need to hear from you today. Again thank you, from the depths of our hearts, for your prayers and financial support. And I'm asking you again today to help Suzanne and me to continue serving the Lord as we must. We have many crusades planned oversees and in the U.S., and we must keep the ministry strong through television, crusades, and helping the needy around the world.
I await your response today and pray the Lord will bless you and keep you as the apple of His eye, hiding you under the shadow of His wings, meeting all your needs—spiritually, emotionally, physically, and financially—and blessing your family and home, bringing glory to His name,

Benny Hinn

Friday, December 27, 2013

Ushuhuda wa Rodolfo Acevedo Juu ya Mbinguni, Kuzimu na Hali ya Kanisa la Leo

Ufuatao ni ushuhuda wa Mwinjilisti Rodolfo kutoka Jamuhuri ya Domonika, ambao Bwana alimwonyesha kuhusiana na kuzimu, mbinguni pamoja na mambo yanayoendelea katika Kanisa la siku za leo.



Utangulizi
Mimi ni Mwinjilisti Rodolfo Acevedo Hernandez kutoka Jamuhuri ya Dominika. Koo langu limeathirika kutokana na usimuliaji wa ushuhuda huu lakini bado nitafanya hivyo tena leo hata kama kuna upinzani. Utukufu ni kwa Mungu! Tupo hapa kuhubiri Neno la Bwana Yesu Kristo na ninaenda kutoa ushuhuda ambao ulibadili maisha yangu na maisha ya maelfu kwa maelfu ya watu wengine!!


Hebu tuende kwenye Ufunuo 1:14-15: “Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto; na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.”

Kwa kuwa sikuridhika kuwa kwenye hali ileile ya kiroho niliyokuwa nayo, nilijifungia kanisani kwangu kwa siku nane; siku nane za kufunga na kuomba, nikiwa nimejifungia na Bwana Yesu. Kabla ya kuanza zile siku nane, Bwana, aliniambia hivi kupitia maono, “Rodolfo, ni wakati sasa ujiweke wakfu kwa ajili yangu,” na nilipewa vazi jeupe ambalo liliandikwa maneno:  “Utakatifu kwa Yehova.” Baaya ya maono yale, mama mmoja mmisionari kutoka kwenye kanisa langu aliniambia, “Rodolfo, niliota kuwa Bwana ananiambia nikueleze kwamba: “jitenge na madhabahu (maana nilikuwa mhubiri); ninaenda kukuonyesha jambo kubwa ambalo litabadili maisha ya mataifa duniani.” Kwa hiyo, ndipo nikaanza mfungo wangu wa siku nane kwa Bwana.

Nilipata changamoto
Kwenye siku ya nne ya mfungo na maombi, nilikuwa nikiomba madhabahuni na ghafla, mbele yangu yalitokea mapepo mawili, ambayo niliyaona kama unavyoweza kumwona mtu uso kwa uso. Mapepo haya yaliniambia, “Rodolfo, hatutakubali wewe uvuke kizuizi chetu”, kisha mara moja yalitoweka. Nilianza kuwa na hofu kubwa maana unapoona viumbe wa rohoni kimwili, inaogopesha sana! Viumbe hawa walikuwa warefu na walikuwa na harufu ya salfa kama vile ndio wametoka moja kwa moja kwenye shimo la jehanamu. Walitumwa kuja kuniambia kuwa hawako tayari kuruhusu mimi nivuke kizingiti walichoweka. Lakini shetani ndiye pekee mwenye ukomo; Bwana Yesu Kristo alimshinda kwenye msalaba wa Kalvari. Utukufu kwa Mungu, haleluya! 

Zilipopita siku saba, nilimwambia Bwana, “Bwana, siwezi kuendelea zaidi. Mwili wangu ni dhaifu. Sina nguvu za kutosha. Bwana, tafadhali nisaidie. Siwezi kutimiza jambo hili. Tafadhali, nisamehe; nipe nguvu.”

Ghafla, nilihisi mtu anatembea nyuma kuelekea kwangu, na akasema sikioni mwangu, “Rodolfo, usiache kuendelea na jambo hili hadi tukuonyeshe mambo ambayo uko karibu kuyaona.”  Nilitiwa moyo na kujisikia ni mwenye nguvu zaidi. Siku iliyofuata, ilikuwa ni Jumapili. Nilijisikia dhaifu kidogo asubuhi. Jioni wakati wa ibada, kulikuwa na ujumbe wenye nguvu kutoka kwa Mwinjilisti  Ruben Bells. Alipomaliza, nilikuwa nawasalimu ndugu zangu wote katika Kristo. Nilianza kuhisi kama pumzi zinaniishia. Nikawa nashindwa hata kupumua.

Ndugu wa kanisani wakanizunguka na kuanza kuomba. Ghafla, nilihisi kana kwamba kupitia kucha na vidole vyangu, kulikuwa na sindano zinapenya mwilini mwangu. Ubaridi wa zile sindano ulipenya mwilini kama hewa ya baridi na nikahisi pumzi yangu ya mwisho imeondoka na kwamba moyo wangu umesimama. Nilidondoka sakafuni na ndugu zangu wakaanza kujaribu kuniamsha. Walikuwa kama ndugu 12 hivi. Ghafla, nilihisi roho yangu ikitoka kwenye mwili na nikawa nautazama mwili wangu nikiwa nje, ukiwa umelala sakafuni. Hao wapendwa hawakujua kilichokuwa kikiendelea kuhusiana na mimi. Dada mmoja ambaye alikuwa ni nesi aliwaambia, “Amepata mshtuko wa moyo.” Nilikuwa natamani kwenda kwao na kurudi kwenye mwili wangu lakini nikawa nashindwa.

Kuzimu
Ghafla, nilihisi mwanga umepotea na nikaanza kupaa juu. Kule juu kuna mtu
alinisimamisha na nikaanza kushuka chini hadi nikafika mahali ambako nilihisi joto kali mno! Kisha, nikaona milango miwili myeusi inayonuka sana. Hapo ilikuwa ni kuzimu na kulikuwa kunatisha sana! 

Nilipokuwa ndio niingie ndani ya ile milango, joka kubwa, ambalo kichwa chake kilijaa miiba na mwili wake ulifunikwa kwa nyembe badala ya magamba ya kawaida, lilitangulia kuingia kwenye gereza hilo. Nilipokuwa naingia kwenye milango ile, niliona macho ya kila aina ukutani, yakiwa yananiangalia. Lakini macho yale yalikuwa yamechorwa ukutani. Mara niliona macho mawili yananijia na kumbe lilikuwa ni pepo ambalo kifuani lilikuwa na bamba lililoandikwa: ‘Mimi ni Kisasi.’ 

Hukumu ya watumishi wasio waaminifu
Wakati huohuo, mapepo zaidi yalianza kutoka ukutani. Lile pepo linaloitwa Kisasi lilisema kwa sauti, “Mfalme Belzebub, tumempata mmojawapo aliye mkubwa ambaye aliendesha vita dhidi ya sisi, ufalme wa giza …” Biblia inasema: “Maana ingalikuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.” (2 Petro 2:21). Kanisa linalomjua Bwana ni lazima liendelee kuwa thabiti na kutambua kuwa Yesu ndiye tumaini PEKEE kwa ajili ya wokovu wa roho zao.

Nikiwa ningali pale, lile pepo Kisasi lilikuja karibu yangu na kuniambia, “Rodolfo, nataka unitoe kama ambavyo ulifanya kule duniani.” Lilipokuwa likisema haya tena na tena, lilikuwa linaendelea kunitesa. Na nikaona mapepo mengi yamejipanga tayari kwa ajili ya kunitesa!


Mateso ya kuzimu kwa ajili ya wachungaji, wahubiri, na wainjilisti wanaoacha nguvu na upako wa Mungu ni makali zaidi kuliko yale ya roho zingine kule kuzimu! Uwe thabiti katika mwendo wako na Mungu! Hii ni saa ya Kanisa kuwa imara. Wakati ni sasa. Muda wa kuchezacheza kanisani umeshapita. Ni lazima tuwe na ujasiri na kuzishinda nguvu za kuzimu kwa jina la Yesu – Yeye peke yake ndiye nuru.

Mara kulitokea pepo lililoruka na kutupa mkuki kwangu ambao ulipita kwenye moyo wangu. Nilihisi maumivu yasiyoweza kuelezeka. Pia nilihisi kama vile kulikuwa kunanyesha salfa kule kuzimu. Nilihisi nyama ya mwili wangu inatoka kwenye mifupa na minyoo ikaanza kupekecha mifupa yangu.


Biblia inasema,“ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.” (Marko 9:48); na pia kwenye inasema, “Funza wametandazwa chini yako, na vidudu vinakufunika” (Isaya 14:11). Kuzimu ni mahali halisi. Yesu na Agano la Kale wanazungumzia kuhusu kuzimu.  
  
Mara niliona kundi la mapepo wanaleta jeneza, lakini lilikuwa ni jeneza tofauti na haya tunayoyafahamu hapa duniani. Lile pepo Kisasi lilinishika sehemu ya chini ya mdomo wangu na kuniambia kwa dhihaka,  “Rodolfo, nataka unitoe!  Nguvu zako ziko wapi? Upako wako uko wapi? Uko wapi utukufu wako uliokuwa nao?”

Ujumbe ninaotaka uupate hapa ni kuwa, wakati mwingine kwa sababu tunahubiri, tunadhani kuwa upako ule ni wetu, na kwamba zile nguvu ni zetu, na kwamba uponyaji ni wetu. Biblia inasema kuwa utukufu unatoka kwa Mungu na utukufu ni wake pekee. Kwa sababu hiihii, ibilisi alitupwa nje ya Mbingu maana alitaka kutwaa utukufu wa Mungu. Kwa hiyo, wengi wanadhani kuwa wagonjwa wanaponywa kutokana na nguvu zao; na wenye mapepo wanafunguliwa kutokana na nguvu zao! Acha nikuambie kuwa, kile ambacho Bwana amekupa ni zawadi kutoka mbinguni. Ni rehema za Mungu kwa lengo la kuwafungua wanaoteswa, na pia ili roho ziweze kuokolewa.  

Mimi ni ‘Niko’
Mapepo yalipokuwa yananiingiza kwenye lile jeneza, nilihisi upepo na kama kuna kitu kimedondoka sakafuni. Pepo Kisasi na mapepo mengine yalikimbia haraka na kujificha mbali na uwepo wake. Nilikuwa niko sakafuni kutokana na kuteswa na yale mapepo; na jambo la kwanza nililoona ambalo sitakaa nilisahau … Oh, Utukufu kwa Mungu! Niliona ‘mtu’ akiyejaa nuru … Haleluya! 

Niliona makovu kwenye miguu yake. Nilipoinua kichwa changu, nilimwona huyu mtu wa ajabu, akiwa na mkanda kifuani mwake ulioandikwa: “Mimi ni MFALME WA WAFALME, na BWANA WA MABWANA.” Alikuwa amevaa taji kubwa sana la dhahabu kichwani mwake.  Alinyoosha mkono wake kwangu na kusema, “Rodolfo, MIMI NI YESU na ninaenda kukuonyesha mambo mengi humu kuzimu, mbinguni pamoja na hali ya Kanisa langu duniani.” Alinishika mkono na kusema, “Twende sasa, Rodolfo.”

Ukahaba
Niliona amefungua chumba kikubwa ambamo kulikuwamo mwanamke. Akasema, “Naenda kukuonyesha adhabu ambayo shetani huwapa wale ambao walikuwa wakifanya ukahaba duniani. Kahaba anapokufa, anakuja kwenye sehemu hii. Angalia kwa makini, Rodolfo.” Niliangalia na kuona ndani ya chumba kile, mwanamke ambaye alikuwa amekaa mkao wa hatari sana, na nikaliona joka lilelile ambalo nililiona hapo mwanzo. Joka hili liliingia kwenye chumba kile kisha likajiingiza kwenye sehemu zake za siri. Kumbuka nilikuambia kwamba ngozi ya joka hili haina magamba ya kawaida bali ni nyembe. 


Joka hilo lilipoingia, lilimharibu kabisa viungo vyake vya ndani, kisha likatokea mdomoni. Pepo linalosimamia ukahaba duniani linaitwa, “Metresa” au “Martha”, au “The Domineur”.  Wakatoliki wengi wana “mtakatifu” huyu akiwa kama mwanamke ambaye mwili wake umeviringwa na nyoka; na pepo hili ndilo ambalo linawatesa makahaba kuzimu.

Bwana aliniambia kwamba ulikuwa ni wakati wa kuondoka hapo na tukamwacha mwanamke yule akilia kutokana na mateso na maumivu. Alikuwa akisema, “Nahitaji mtu wa kunisaidia!” Bwana akaniambia, “Rodolfo, hukumu imeshawekwa kwa ajili yao! Sasa Rodolfo, nitaenda kukuonyesha sehemu ambako shetani anawatesa wanawake ambao walitoa mimba za watoto wao duniani!” 

Utoaji mimba
Ghafla, nilimwona mwanamke akiwa katika mkao wa kujifungua na nikaona pepo baya sana ambalo mikono na miguu yake ilikuwa kama ya farasi na mwonekano wake kama wa mnyama na alikuwa na keekee (drill) mikononi mwake. Keekee hii ilikuwa imejaa minyoo. Minyoo hii ilikuwa ni mikubwa sana na meno yao yalikuwa makali na miili yao ilijaa miiba iliyochongoka. Pepo lile liliingiza ile keekee kwenye sehemu zake za siri hadi akaonekana kama mwenye mimba.
              
Pepo lile likaanza kumpigia kelele, likimwambia kuwa azae huko kuzimu kwa kuwa alikataa kuzaa duniani. Kisha likasema, “Utukuzwe, utukuzwe shetani! Huu ni ufalme wako!”

Nilipomwuliza Bwana kwa nini adhabu ilikuwa kali kiasi kile kwa mwanamke yule, Bwana akasema, “Rodolfo, adhabu imeshawekwa kwa ajili ya mwanamke huyu!” Biblia inasema kwamba wauaji hawataingia kwenye Ufalme wa mbinguni.  Watu wanatoa mimba au kuwaua watoto huku wakiamini kuwa huko ni kama kuua tu mnyama lakini kile hasa wanachofanya ni kuua mwanadamu mwenye roho na mwili.

Pepo lile liliendelea kumpazia sauti, likimwambia amtukuze shetani maana ule ulikuwa ni ufalme wake. Wale minyoo walianza kutoka kupitia tumboni mwa yule mwanamke huku wakiharibu kabisa sehemu za ndani ya mwili na kutoka wakiwa na vipande vya nyama midomoni mwao. Ungeweza kuona maumivu makali aliyokuwa akiyahisi. Bwana akaniambia,  “Tuondoke kwenye sehemu hii.”

Shetani anashambulia watoto na familia
Tulienda kwenye sehemu iliyoonekana kama kuna fito nyeusi. Nikaanza kuona watoto wengi kule kuzimu. Nikamwuliza Bwana, “Kwa nini kuna watoto huku kuzimu?” Lakini Bwana akaniambia kuwa wale hawakuwa watoto; na kwamba ufalme wa mbinguni ni wa watoto na inabidi uzaliwe upya ili kuingia kwenye ufalme wa mbinguni.
“Sasa, Bwana vipi kuhusu watoto hawa?” niliuliza.


Bwana akaniambia tena, “Rodolfo, hawa si watoto”, kisha akaniambia nisikilize maagizo ambayo shetani alikuwa anawapatia.

Nilipogeuka, nikaona kuwa kumbe hawakuwa watoto bali ni mapepo na walikuwa wanacheza mchezo unaoitwaNintendo. Nikaanza kuona kila aina ya ‘programming’ na michezo ya kishetani, huku wakitoa alama na mijongeo kwa kutumia mikono yao, vyote vikiwa na makusudi ya kishetani.

Bwana alipowaamuru wageuke, ndipo nikaona jinsi sura zao zilivyo mbaya, za kutisha na zinazotia kinyaa. Shetani aliwapa maagizo akisema, “Wanangu, nendeni mkaue, mkaibe, na kuharibu.”  Alikuwa yuko sahihi kwa sababu Biblia inasema kuwa shetani haji ila kuiba, kuchinja na kuharibu lakini Yesu alikuja ili kuleta uzima na uzima tele. (Yohana 10:10).

Wakati huo, hivi vipepo vidogo viliingia duniani na Bwana akaniambia kuwa hii ndiyo sababu watoto wa duniani wanajiua. Hivi sasa, wanasayansi na wanasaikolojia ya watoto hawaelewi ni kwa nini watoto wanajiua. Miezi michache iliyopita, mtoto wa kiume wa miaka 12 alimuua mama yake kwa kisu; mwingine alijinyonga hapa Marekani; na mtoto wa miaka 7 alimwua mama yake, wadogo zake na yeye mwenyewe kwa bastola ambayo aliipata. Mtoto mwingine alijitupa kutoka ghorofa ya pili na kufa. Barua wanazoacha hawa watoto zinasema kuwa maisha hayana maana pamoja na mambo mengine mengi.

Haya yanatokea kwa sababu mapepo yanaingia kwenye miili yao na kutawala fahamu zao na kuwafanya wachukue uamuzi wa kujiua. Iweni makini enyi wazazi na kile ambacho watoto wenu wanaangalia kwenye televisheni. Kile ambacho watoto wenu wanaangalia kwenye intaneti au wanachosikiliza kwenye redio kina athari kubwa. Mapepo yanaingia kupitia televisheni, redio, muziki na michezo ya vichekesho ya kishetani. Utukufu ni kwa Mungu, haleluya, kwa kutuamsha!!

Kisha Bwana akaniambia, ni kwa sababu hii ndoa nyingi zinaharibiwa, maana baadhi ya wazazi wanalaumu watoto wakidhani kuwa kwa sababu ya mtoto fulani, basi ni lazima wapeane talaka. Lakini mtoto si tatizo. Tatizo ni mashambulizi ya kipepo dhidi ya umoja wa ndoa na familia. Mwiteni Yesu Kristo! Liite Kanisa! Omba ufanyiwe maombi ili kuwa na nyumba isiyo na mashambulizi ya kipepo!   “Sasa, Rodolfo,”Bwana akasema, “ni wakati wa kutoka wenye sehemu hii.”

Ibada ya sanamu
Tulipotoka kwenye sehemu ile, nilimwona mwanamke ambaye alikuwa amemezwa kabisa ndani ya moto. Mwanamke huyu alikuwa akilia sana akisema, “Kufa, kufa, kufa! Nitoe humu!”

Kile nilichoona ni kwamba, mwanamke huyu alishika mikononi mwake picha ya ‘Moyo mtakatifu wa Yesu’ kulingana na taratibu na mapokeo ya Kikatoliki.
                     
Nikauliza, “Bwana, huyo ni mwanamke gani?”
Bwana akasema, “Rodolfo, mwanamke huyo ni bibi yako.”  Biblia inasema kuwa waabudu sanamu hawataingia kwenye ufalme wa mbinguni (Gal. 5:20, Efe. 5:5).  Bwana alinionyesha maisha ya bibi yangu yalivyokuwa duniani na nikaona kwamba kweli alikuwa ni mwabudu sanamu. Nikasema, “Bwana, tafadhali msaidie.”
Bwana akaniambia, “Rodolfo, sina cha kufanya! Hukumu imeshawekwa kwa ajili yake!”  Kisha akaniambia, “Naenda kukuonyesha kile ambacho  kitakuletea mateso duniani. Wengi hawataamini kile ambacho unaenda kukiona. Lakini usiwe na wasiwasi, nitakuwa pamoja na wewe.”

Celia Cruz (Malkia wa Salsa) yuko kuzimu
Mara nilimwona mwanamke ambaye miguu yake ilikuwa inapondwapondwa kwa visu ambavyo vilifika hata kwenye magoti yake kwa wakati uleule. Mwanamke huyu alikuwa akiteswa na mapepo mengi. 

                         
Bwana alinionyesha video ya Celia Cruz akifanya mikataba ya kishetani kule Hollywood kwa kutumia damu; na nikamwona akifanya mambo mengi ya kishetani. Bwana akasema,“Alikuwa ni mwabudu shetani. Alikuwa ni mfanya ibada ya sanamu. Alikuwa ni mchawi akiwa na maagano mengi ya damu. Kwa hiyo, muziki wake ulikuwa ukishika sana chati za juu. Ilikuwa ni vivyo hivyo kwa kundi lake la wanamuziki.” Na Bwana akanisikizisha muziki wake mmoja unaoitwa ‘Yemaya’, ambao ni maarufu sana kwenye ulimwengu wa Kihispania. Lakini unapoimba wimbo ule na kurudiarudia, maana yake hasa ni: ‘Mfalme shetani, njoo utawale ndani yangu!’ Na Bwana akaniambia, “Hukumu imeshapangwa kwa ajili ya Celia Cruz.”

Mwasisi wa Mashahidi wa Yehova yuko kuzimu
Tuliendelea kutembea na Bwana akanionyesha mwanamume mmoja mweupe ambaye mikono yake ilikuwa imetanuliwa. Na kitu cha ajabu kuhusiana na mtu huyu ni kuwa alikuwa na upanga mzuri sana ndani ya ulimi wake na upanga huu ulipenya hadi kichwani na kutokeza nje. Miguu yake ilikuwa imefungwa kwa minyororo na mgongo wake ulikuwa umejaa nyembe sehemu mbalimbali kwa namna kwamba, vyovyote ambavyo angejisogeza, ni lazima zinamkata. Nilipomwona mtu huyu katika hali hii, nikamwambia Yesu,  “Bwana, tafadhali msaidie. Fanya kitu, Bwana Yesu. Hebu ona jinsi anavyoteseka kwa maumivu.” Bwana akaniambia, “Je, unajua huyu ni nani?”


“Hapana, Bwana,” nilisema. Niliona jinsi visu vilivyopenya kwenye ngozi yake na kisha kwenye mifupa na jinsi vilivyotokeza upande mwingine. Mtu huyo alipiga tu kelele kwa maumivu.

Bwana akaniambia, “Hukumu juu ya mtu huyu imeshatolewa. Sasa nitakuambia huyu ni nani.”

Kutokana na unabii huu, Bwana akasema,“Itakubidi kukimbia kutoka mji mmoja hadi mwingine maana jambo hili litakuletea mateso makubwa, lakini nitakuwa pamoja na wewe.” Akaendelea kusema, “Rodolfo, huyu mtu ni Charles T. Russell.” Nikasema, “Bwana, yeye ni nani?” Bwana akaniambia kwamba mwanamume yule alikuwa ni mwanzilishi wa kanisa la Mashahidi wa Yehova. Nikaomba, “Bwana, tafadhali msaidie,” na Bwana akasema, “Hapana, Rodolfo.”Kisha Bwana alifanya ishara kwa mkono, na mara moja nikaona roho nyingi zikiangukia kwenye shimo la kuzimu kwa kila namna. Walikuwa wakiangukia humo kichwa kwanza, miguu kwanza, tumbo kwanza, n.k.
“Rodolfo, kutokana na huyo mtu aliyelaaniwa, roho hizi zote zinaangukia kuzimu. Mtu huyu alifundisha kwamba Mungu ni Mungu wa upendo tu. Biblia inasema kwamba Mungu ni moto ulao. Mtu huyu, Charles Russell, aliondoa maneno ‘hell’  kutoka kwenye Biblia na akaondoa maneno yote ‘sheol’ na ‘Abaddon’. Pia, alikana uungu wa Yesu Kristo na pia alikana uungu wa Roho Mtakatifu, halafu akaweka tu neno Yehova kwenye Biblia. Aliondoa maneno Yesu na Roho Mtakatifu. Kutokana na mtu huyu aliyelaaniwa, roho hizi zote zinaangukia kuzimu.” (Ufu. 22:18-19). Kisha Bwana akasema: “Namlaani mtu huyu.”

Tafadhali enyi Mashahidi wa Yehova mnaonisikiliza wakati huu, si lengo langu kuwakwaza. Tokeni ndani ya kundi hilo na mje kwa Yesu haraka. Mimi siwachukii na wala sichukii dini yenu lakini mko ndani ya mahali pabaya. Njooni kwa Yesu. Anawangoja kwa mikono iliyo wazi kabisa. Charles Russell yuko kuzimu kwa sababu alifundisha uongo!! Msifuate uongo wake.

Tulipoondoka sehemu hii, milango hii ya gereza ilijifunga na moto ukawaka na mwanamume huyu, Charles Taze Russell, alipiga kelele na kumlaani Yesu tena na tena kwa sababu Yesu alisema, “Hukumu imeshaamuliwa kwa ajili ya mtu huyu.”

Kisha Bwana akasema, “Rodolfo, sasa nitakuonyesha magereza meusi ya kuzimu. Hii ni adhabu ya kupita kiasi ya shetani kwa roho zilizoko kuzimu.”

“Hapana, Bwana, tafadhali! Tayari nimeshaona mambo ya kutisha. Niondoe hapa, tafadhali …”

Bwana akasema, “Haya, Rodolfo, sitafanya kingine chochote kama hauniruhusu. Nitakupeleka mbinguni sasa.”

Mbinguni
Tuliondoka kwa kasi sana na tukafika mahali hapa. Malaika wawili walinisimamisha mbele ya milango hii iliyokuwa mizuri sana. Walikuwa wazuri
sana. Hawa malaika wawili waliniambia, “Rodolfo, ukiwa na mavazi hayo ya dhambi, huwezi kuingia kwenye ufalme wa Mungu.” Kwa hiyo, walinipatia mavazi mapya ambayo yameandikwa: Utakatifu.  
  
Ujumbe sahihi
Wachungaji, wainjilisti, wahubiri na wamisionari, tafadhali samahanini na mnisikilize. Mungu hajawaita kuhubiri kuhusu utajiri au unabii juu ya hilo. Mungu amewaita kuhubiri kuhusu utakatifu na utakaso, maana bila utakatifu, hakuna atakayemwona Bwana. Pelekeni neno la utakatifu na kulihubiri!!! 

Malaika waliniruhusu kuingia na Yesu alikuwa ananingoja na akaniambia, “Rodolfo mwanangu, karibu kwenye Ufalme wa Mungu wako.” Tulianza kutembea. Niliona kuwa barabara zilikuwa za dhahabu tupu, na nikaona mto uliokuwa kama kioo; ni maji halisi! Niliona pia almasi na mapambo kwenye mitaa, kitu ambacho watu wa duniani wanaweza kuuana kwa ajili yake! Kisha Bwana alinishika mkono na kuniambia,  “Sasa nitaenda kukuonyesha hekalu.” Hekalu lilikuwa zuri sana! Niliona bilauri za dhahabu, vyombo vya dhahabu na nikasikia wimbo mzuri ambao ulikuwa unaimbwa na watoto. Bwana akaniambia kuwa waliokuwa wanaimba ni watoto ambao duniani watu waliwakataa lakini wana uzima kwenye ufalme wa mbinguni. Utukufu kwa Mungu, haleluya! 

Mavazi ya harusi, chakula cha harusi, mataji
Tuliendelea kutembea mbinguni na nikaona mavazi meupe mazuri, yaliyopambwa kwa dhahabu pamoja na mataji juu yake. Bwana akaniambia lilikuwa ni Kanisa lake. Kwamba linatakiwa kuwa takatifu na lililotakaswa. Taji ni taji ya uzima na kwamba Bwana atakwenda kulipatia Kanisa.

Tulipotoka pale, niliona msururu mrefu wa watu waliovaa mavazi meupe. Niliona malaika wawili wakubwa, wenye sura nzuri ukiwatazama machoni. Niliona amani na upendo. Malaika mmoja akasema, “Karibu kwenye ufalme wa Mungu wako.” Malaika mwingine alipiga makofi. Niliona jinsi watu walivyo na furaha kuwa pale na sasa naelewa kile ambacho mtume Paulo alichosema kwamba, mateso ya dunia hii yanayopita si lolote ukilinganisha na utukufu unaotungojea kule mbinguni. 

Bwana alinipeleka mahali ambako niliona meza ndefu sana isiyo na mwisho. Meza ilikuwa ya dhahabu. Kitambaa kilichoifunika kilikuwa cha dhahabu, bilauri za dhahabu, visu na nyuma za dhahabu, viti vya dhahabu, n.k. Kisha nikaona mataji makubwa kwa madogo na Bwana akaniambia kuwa yale mataji makubwa ni ya watumishi wake, pale watakapokuja kwenye harusi ya Mwanakondoo.  Akasema, “Kwa vile harusi ya Mwanakondoo iko karibu kuanza, niko karibu kuja kuchukua Kanisa langu. Waambie kuwa ninakuja kulichukua Kanisa langu.”
Nikamwuliza Bwana, “Je, na haya mataji madogo ni ya nani?”
Akasema, “Hayo mataji madogo ni ya watu walio ndani ya Kanisa ambao wanaishi katika utakatifu lakini hawafanyi chochote kwa ajili ya Ufalme. Lakini nakwambia, usiridhike kupokea taji dogo bali fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya taji kubwa. Fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Mungu ili aje kukupa thawabu ya uzima.”

Jambo la ajabu lilikuwa kwamba, kila kiti kina jina nyuma yake na hakuna mtu mwingine yeyote ambaye atakikalia zaidi ya mwenye jina hilo!

Hali ya Kanisa la leo
Bwana aliniambia, “Sasa Rodolfo, naenda kukuonyesha hali halisi ya Kanisa ilivyo hivi sasa.” Nilimwona samaki mdogo akimsifu na kumwabudu Yesu kwa sababu Biblia inasema: Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana! (Zab 150:6).

Kwa hiyo, Bwana alinionyesha dunia ambako ningerudi kwenda kuhubiri kile nilichokiona. Lakini nikawa na picha kwamba sikuwa na kumbukumbu kuhusiana na dunia na Bwana akanipa ufahamu kwamba, mtu anayeingia mbinguni, anasahau kila kitu kilichotokea duniani! Lakini sivyo ilivyo kuzimu. Kila anayeingia kuzimu, anakuwa na kumbukumbu za kila kitu alichotenda alipokuwa duniani, familia zao, na kwamba wasingependa waende kuzimu! Hayo nayo ni mateso mengine yanayoongezwa juu yao. Lakini yule anayeingia mbinguni, akili yake inabadilishwa ili ifanane na ufahamu wa kimbingu. 

Bwana asifiwe! Kwa sababu hiyo, si Petro, wala Mariamu, wala Stephano, wala Elisha au Yohana mwenye kumbukumbu ya kile alichofanya alipokuwa duniani. Baada ya maisha yao ya duniani, wala hawana tena habari kamwe na kile kinachoendelea hapa. Petro wala hawezi hata kuwaza kuwa Kanisa Katoliki wanamwomba yeye au mtakatifu mwingine yeyote. Na Yesu akasema,  “Hakuna jina jingine chini ya mbingu litupasalo kuokolewa kwalo.” Huyo ni Yesu Kristo, Mwana wa Mungu Aliye Hai. Na Mariamu alisema kule kwenye harusi ya Kana, “Lolote atakalowaambia, fanyeni.” Na … waabudu shetani wako Vatican. Wanaficha njia zote za dhambi za makasisi kutembea na watawa; makasisi kutuhumiwa kunajisi watoto na hata hapa kwenye Jamuhuri ya Dominika. Na Wakatoliki wanaendelea kuamini uongo huo.   (Tafadhali ona pia ushuhuda mwingine wa ajabu: “Prepareto meet your God – Angelica Zambrano” Sehemu ya 1&2 ambao unaongelea zaidi kuhusiana na masuala ya Ukatoliki).

Watumishi wanaolenga fedha na wasio waaminifu
Sasa Bwana alianza kulia pale alipoanza kunionyesha mimi hali ya Kanisa. Ghafla, nilimwona mchungaji duniani amebeba begi kubwa lililojaa fedha. Bwana akaniambia, “Hawa ni wahubiri na wainjilisti wanaojitajirisha kutokana na matoleo kwa sababu wanafundisha uongo kwa watu wangu na kuwafanya watu wangu wapotee.”

Nawaambia enyi wahubiri na wainjilisti, mhubirini Yesu hata kama hakuna zaka au sadaka mnazopokea. Litakaseni Kanisa!

Mara niliona fedha za kwenye lile sanduku zimetoweka. Nilimwuliza Bwana naye akaniambia,  “Kama ambavyo fedha zake zimetoweka, ndivyo na yeye atakayotoweka pamoja na mpinga Kristo. Lakini bado ninayo masalia ya watu wangu ambao hawajanajisika.”

Naona siku hizi jinsi wahubiri wengi, wachungaji, wainjilisti, n.k. walivyo matajiri na mamilionea. Hata hivyo, waumini wa makanisa yao wanaogelea kwenye umaskini, uhitaji wa chakula, huku mchungaji akiwa katika utajiri na wala hawasaidii! Wainjilisti wengi ni mamilionea wakubwa na hata mabilionea wakiwa na magari ya kifahari kupita kiasi. Je, Msamaria mwema yuko wapi?

Pia niliona wachungaji wengi wakihudumu kwenye madhabahu lakini nikamwona huyu mmoja akimalizia kuhudumu siku ile, akaondoka nyumbani alikokuwa mke wake, na kwenda kukutana na hawara yake ambaye anaishi naye pia; huku akiwa naye ni mshirika wa kanisa lake! 

Nilimwona pia mwinjilisti akiondoka kanisani kwake na baada nyumba chache tu kutoka kwenye kanisa, akaenda kukutana na kahaba. Ni mwinjilisti yuleyule aliyekuwa akihudumu kwenye madhabahu! Bwana, tafadhali uturehemu!

Matendo yasiyo matakatifu – kujichua
Baada ya hapo, Bwana alinionyesha kundi la vijana wa Kanisa, kwamba wanapoondoka kanisani wanaenda kwenye sehemu ya giza maana wanadhani kuwa Bwana hawaoni. Wanapoenda huko wanaanza kujichua (kupiga punyeto) na kuzini dhidi ya miili yao wenyewe. Baada ya hapo, wanarudi na kuhudumu madhabahuni! Viongozi wa vijana, viongozi wa Kanisa! (Kama unahitaji msaada wa kushinda dhambi hii, angalia  video hii).

Muziki usio na utakatifu kanisani
Sasa Bwana alinionyesha disko na Kanisa na akaniambia, “Angalia kwa makini.” Na mimi nikaangalia na kuona kwamba Kanisa lilikuwa ni sawasawa tu
na lile disko! Hakukuwa na tofauti yoyote! Walikuwa na mfumo uleule wa sauti, muziki uleule! Vifaa vilevile kutoka duniani vinaingia kanisani!

Dunia inatakiwa kubadilika iingie kwenye Ukristo lakini si Ukristo kuingia duniani! Tunaileta dunia kanisani! Pia niwaambie hili: Hatuwezi kumsifu na kumwabudu Mungu kwa kutumia Reggaeton, kwa Bachaton au Rock. Hata leo zipo nyimbo za Kikristo anazoimbiwa Mungu na pia zinaimbwa duniani kwa kutumia maneno yaleyale! Hazimtaji Mungu bali zinataja tu neno ‘upendo.’

Niliona pia muziki wa Rap na Perreo kanisani na hilo halikubaliki. Biblia inasema kuwa tunatakiwa kumwabudu Bwana katika uzuri na utakatifu (kwa ajili ya kuabudu kwa kweli, tazama Kol. 3:16 na Yoh. 4:23-24). Muziki wa Rock ni wa kishetani na ulibuniwa kuzimu.Wachungaji na wainjilisti, tafadhali, ondoeni makanisani muziki huo uliolaaniwa!!!

Bwana alinionyesha wanamuziki ambao wameshapotoka. Kwa upande mmoja wanaimba kanisani, na kwa upande wa pili wanaingia mikataba ya kuimba hata kwenye mahoteli kama waimbaji wa kujitegemea. Wanaenda kanisani kumsifu Bwana!

Ngoja niwaambie: muziki kama huo Bwana wala haukubali na tafadhali, samahani, ni lazima niwaambie ukweli - kile kinachotoka kwa Mungu ni kitakatifu na kimetengwa kwa ajili ya Mungu peke yake. Na kile ambacho wanamuziki wa leo wanakifanya, wanaenda kuimba kanisani, kisha wanapotea kutoka kwenye huduma, maana wanaonekana kama vile wanamwimbia Mungu kwa mkataba. Kwa hiyo, wanadhani hawana ulazima wa kuwapo pale muda wote wa huduma; wanaondoka mapema. Bwana aliniambia, “Kwa bahati mbaya, kanisa la aina hiyo halitaingia kwenye ufalme wa mbinguni.”

Masalia walio watakatifu
Baada ya hapo, Bwana alinionyesha kundi la watu – maelfu kwa melfu ya watu wanaojilinda katika utakatifu. Kwa mfano, nilimwona dada akimwambia mwingine, “Umekula leo? Nina kipande cha mkate nyumbani.” Nilimwona mwingine akiwa amebeba jozi ya viatu akimpelekea mwingine ambaye hana. Nikamwona mwingine akiwatia moyo wale wasio na nguvu. Wengine, kutokana na kujua matatizo ya wenzao, walikuwa wakiwasaidia na kuwaombea katika mahitaji yao bila mtu mwingine kujua.

Lakini leo, katika makanisa mengi, kuna masengenyo mengi kwa sababu watu hawajui kukaa kimya kuhusiana na watu wengine. Tubu leo! Yesu Kristo anataka kukupatia ukombozi na wokovu. Anaweza kukupatia zawadi ya toba.

Utukufu kwa Mungu!
Msifuni na kumwabudu Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana!
Rehema zake zadumu milele.

Mwinjilisti Rodolfo Acevedo

Chanzo: YESU NI NJIA BLOG