SOMO #2. ADAMU NA HAWA
Andiko Kuu- Mwanzo sura ya 3 yote.
1. ANGUKO (Kabla ya
Yesu)
1. Kila
kilichoumbwa kilikuwa kikamilifu-Mwanzo
1:3
·
Anga - Jua, mwezi, nyota, sayari, mawingu nk
·
Dunia – Mimea, wanyama,miamba, madini nk
·
Bahari – Samaki wakubwa kwa Wadogo nk
2. Mungu
akaumba Mtu (Adam na Hawa)-Mwanzo 1:26
·
Walimuumba kwa MFANO wao na SURA yao
·
Ili Mtu awe - Mwenye HAKI, MTAKATIFU na MTUKUFU
3. Dhumuni Kuu
la Mungu kumuumba Mtu
·
Wawe na MAHUSIANO
·
Kwamba “Mungu awe Mungu wao na Watu wawe Watu wake”
4. Adam na
Hawa
·
Wanafanya DHAMBI kwani WALIMUAMINI na KUMTII Shetani kuliko Mungu
·
Matokeo ya Dhambi ni :- Kuvunjika kwa Mahusiano, Mtu
alipoteza (Haki, Utakatifu na Utukufu), mwishowe AKAFUKUZWA-Mwanzo 3:24
·
Mtu akawa MTUMWA wa Dhambi,
akawa (Anaona AIBU, UCHI,
ANAJIFICHA)
5. Njia ya
Adam ya KUJISITIRI NA KUJIPATANISHA
·
Walidhani wangejisitiri kwenye vichaka
·
Walidhani wangeendeleza Mahusiano kwa upatanisho wa
majani (Eproni)
·
Mungu anawakataa wao na njia zao zote walizobuni kwa
laana-Mwanzo 3:1-3,16-19
6. Njia ya
Mungu ya KUSITIRI NA KUPATANA
·
Kondoo asiye na Hatia ANAUAWA – Ili Damu yake ifanye
UPATANISHO na ngozi yake IWASITIRI na achukue adhabu ya Mtu. Alikuwa kama
MWOKOZI- Mwanzo 3:20
·
Kwa kufa kwa Kondoo, Dhambi ILIFUNIKWA na HAIKUFUTWA,
hivyo UREJESHO haukuwa kamili na Mahusiano yaliendelea NJE ya Bustani ya EDENI
(MASKANI ya Mungu na Mtu)
7. Mungu
anatoa AHADI
·
Mungu alimpenda sana Adam ingawa alikuwa ameshaingiwa
na dosari, sasa alikuwa na asili mbili (Asili ya Mungu na Shetani), na Mungu
alijua Kondoo hawezi KUFUTA dhambi,
na hizi Asili mbili zimeingia kwenye vizazi vyote vya Adam-50% kwa 50%
·
Mungu akatoa AHADI
kwamba angelikuja MKOMBOZI afe badala yao ili Dhambi zao ZIFUTWE-Isaya 7:14,9:6-7, Imanueli maana
yake ni Mungu pamoja nasi.
·
Lakini Kabla hajaja KRISTO ilitakiwa KAFARA iendelee
kutolewa kila mwaka ili Dhambi ziendelee KUFUNIKWA na sio KUFUTWA mpaka
itakapotolewa Kafara KAMILIFU, isiyo
na WAA, wala ILA, au KUNYANZI – Kutoka 30:10
2. AGANO JIPYA (Wakati wa
Yesu)
1. Yesu KONDOO wa Mungu amekuja-Yohana 1:29,36
·
Kama Mungu alivyotoa Kondoo wakati wa Adam, ndivyo
alivyotoa tena kwa ajili y a vizazi vyote vya Adam, tofauti ya kondoo huyu ni
KUFUTA Dhambi zote.
·
Yesu ni Kondoo mkamilifu aliyeahidiwa. Fidia yake INATOSHEREZA malipo yote kwani UHAI wake
unathamani kuliko chochote-Marko 14:24
·
Yesu ni Mwokozi HALISI sio kama Kondoo aliyefunika
Dhambi- Luka 2:11
2. Mungu
Anamkataa Yesu
·
Kama Mungu alivyo MFUKUZA Adamu-Mwanzo 3:24, ndivyo alivyo MUACHA Yesu kwa sababu alikuja
afe Badala ya Uzao wa Adam-Marko 15:34,
Yohana 19:28.
·
Hivyo Yesu alikataliwa, na akaenda kuzimu ambapo
angetakiwa kwenda Mwanadamu aliyeasi, lakini akaenda badala yake.
3. NYAKATI ZETU-mwaka 2017
(Baada ya Yesu )
1. ASILI ya
Adam na Yesu-1Wakorintho 15:21-22
·
Tunachukua Asili, sura na Chapa za Adam kwasababu
tulizaliwa toka viunoni mwake, Adamu ni wa Chini na sisi ni wa Chini, Adam wa
Udongo na sisi ni wa Udongo.
·
Habari njema ni kwamba Tukimwamini Mungu alichokifanya
kwa ajili yetu kupitia Yesu, tunapokea ASILI mpya ya Yesu. Yesu alitoka juu, Yesu
ni Roho inayohuisha, ndivyo tutakavyokuwa –
1 Wakorintho 15:45-49
2. DAMU ya
Yesu
·
Inasitiri (Covering), hivyo hutaona Aibu wala
hutajificha tena-Warumi 4:7-8
·
Inatufanyia UPATANISHO kati ya Sisi na Mungu- Efeso 2:16
·
Kama hujui Damu ya Yesu inachofanya mpaka usamehewe,
ndio inaitwa Imani. Unaamini vidonge vitakusaidia ingawa hujui vinafanyaje,
ndio inaitwa Imani. Muamini Mungu kuwa anasamehe watu kupitiaa Damu ya Mtoto
wake Yesu.
4 HITIMISHO
CHUKUA HATUA-Warumi
10:9-10
LEO HII, MUDA HUU - 2Wakorintho
2:2-Ukimwamini Mungu alichokifanya kwa ajili yetu kupitia Yesu;-
utasamehewa Dhambi, Utarejeshwa,Utasitiriwa, utapatanishwa, utarudishiwa (Haki,
utakatifu na Utukufu), hutakuwa mtumwa tena wa Dhambi,na utakuwa na MAHUSIANO
na Mungu tena.
By
APOSTLE ELIYA SIMON
THE EPANGELIA
CHURCH
MAKULU-DODOMA
MJINI
0753 011 774
No comments:
Post a Comment