SOMO#3. KAINI, HABILI NA SETHI
Andiko Kuu-Mwanzo sura yote ya 4
11. KAINI,
HABILI NA SETHI (Kabla ya Yesu)
1.
Adam na Hawa
·
Adam na Hawa walifukuzwa Bustanini (Maskani)
kwasababu ya Dhambi, lakini Mungu aliwafanyia Upatanisho ingawa haukuwa
mkamilifu kwasababu UTHAMANI WA MWANADAMU SIO SAWA NAWA MNYAMA, ndio maana
mahusiano yao yaliendelea NJE ya Bustani (Maskani).
·
Adamu na kizazi chake chote kilishaingiwa na
Kasoro, walikuwa na Sura ambili – Ya Mungu na Shetani, kwahiyo kila anaezaliwa
kwa asili ni lazima afanye maamuzi ya KUCHAGUA,
ama Mungu au Shetani.
2.
Kaini na Habili – Mwanzo 4:1-7
·
Adam na Hawa walipata watoto-Kaini na Habili
wakiwa na Asili ya wazazi wao
·
Kaini alikuwa mtoto wa kwanza, mkulima, Mungu
alimkataa yeye na Sadaka yake. Lakini Mungu alimtakabali Habili na Sadaka yake,
alikuwa mtoto wa pili, mchunga kondoo. Swali-
Kwanini Mungu amtakabali Habili na asimtakabali Kaini?
·
Sadaka waliyotakiwa kutoa ilikuwa ni sadaka ya
UPATANISHO/KUFUNIKA DHAMBI/KUSITIRI DHAMBI, sasa sadaka yenye hii sifa ni
sadaka yenye DAMU. Kaini alitoa sadaka nzuri lakini haikuwa na Damu
kwani kinachofanya upatanisho ni Damu
·
Kaini alijibunia njia yake ya kufanya upatanisho
kama Baba yake na Mama yake hii inaonyesha hakumuamini Mungu, lakini Habili
alifuata njia ya Mungu ya KUUA KONDOO ili kufanya upatanisho, hii inaonyesha
alimuamini Mungu na akahesaiwa HAKI
kwa hii IMANI yake.
·
Mwanzo
4:8-18. Kaini muasi akamuua mwenye Haki Habili, akalaaniwa TENA kama wazazi
wake na AKAFUKUZWA kwenye uwepo wa Bwana akaenda kuendeleza kizazi KIASI, na
wakati huo hakukua NA kizazi cha haki kwani Habili alishakufa.
3.
Sethi
– Mwanzo 4:25-26
·
Vizazi viwili toka kwa Adam- cha haki
kilishauawa lakini cha UASI kilizidi kuchanua, Dunia nzima ilijawa na kizazi
hiki cha Kaini cha Uasi, hakukua na aliyekuwa AKIMCHA Mungu mpaka MTOTO WA
KIUME alipozaliwa – SETHI.
·
Baada ya Adam kumpata Sethi akasema “ Mungu ameniwekea uzao…..’ Maneno haya
yanaonyesha huyu mtoto wa kiume ni utimilizo mdogo wa ahadi aliyoitoa Mungu
wakati anamlaani Hawa-Mwanzo 3:15.
·
Huyu mtoto wa kiume Sethi akaanza kutengeneza
kizazi cha haki kwani walikuwa wakiliitia jina la Bwana. Adam alidhani kizazi
hiki cha haki kingedumu milele, baada ya vizazi kumi vya haki, haki ikaanza
kupotea kwani wengi walivutwa na kizazi cha uasi cha Kaini.
·
Unabii wa kuzaliwa mtoto wa kiume,
mkombozi-Hakua Sulemani - 1Nyakati 22:9-10, bali ni Imanueli - Isaya 7:14,9:6
. 2. AGANO JIPYA (Wakati
wa Yesu)
1.
Unabii wa kuja Mtoto Yesu
·
Mungu aliwa ahidi Adam na Hawa kuhusu UZAO wa
Mwanamke – kwamba Bikra angepata mtoto wa kiume ambaye ndie angelikuwa
mkombozi. Hawa alipomzaa Sethi alidhani kuwa Sethi alikuwa ndio Utimilizo
kamili wa ahadi ya Mungu.
·
Nabii Isaya anaona uhitaji wa mtoto wa kiume
mwingine ambaye sio Sethi – Isaya 7:14-16.
Sethi hakufaa kwa sababu alikuwa na asili ya uasi ndani yake ingawa kwa nje
alifanya vizuri ukilinganisha na kaka yake Habili. Isaya 9:6-7.
·
Luka 2:10-14. Huu ndio utimilizo wa Ahadi
aliyomuahidi Hawa, ingawa wao walidhani ni Sethi. Mtoto huyu wa Kiume Yesu
ndiye MWOKOZI, mbingu zilifurahi, malaika walishuka , mji ulitaharuki lakini
wakati wa Sethi hakukua na chochote.
2. YESU
·
Kuna laana iliyotakiwa kuwapata Waisraeli kwa
kumwaga Damu za Haki, lakini ili mtu AEPE
hiyo laana alitakiwa kumuamini Yesu asitiriwe- Mathayo 23:34-36.
·
Yohana 3:16- Mungu alimtoa mwanawe ili aanze
upya uzao wa Haki, waliokuwa wakimwamini yesu walipewa uwezo wa kuwa uzao
mteule, watoto wa Mungu kwa njia ya Imani juu ya Yesu – Yohana 1:12-13,
·
1Yohana
2:22-23,3:1-2
3. NYAKATI
ZETU (Baada ya Yesu)
1.
Damu ya
Yesu Yanena Mema- Ebrania 12:24-Tuliona
Damu ya Habili ilikuwa ikinena mbele za Mungu, lakini haikuwa inanena mema bali
mabaya, ingawa Habili alikuwa mwenye haki lakini alipouawa bila hatia alidai
kisasi lakini Yesu hakufanya hivyo, alisema “Baba uwasamehe…’ Luka 23:34. Baadae tutaona mambo 7 ambayo Damu ya
Yesu inayanena.
2.
Vizazi
viwili – uzao mteule na Wana wa Uasi- 1Yohana
3:10-12, Yuda 1:11- wana wa
ibilisi, lakini 1Petro 2:8-10 ni wana
wa mungu. Wale watoto wawili wa Adamu ni Unabii mpaka nyakati hizi, kwamba kuna
watu wa aina mbili tu haijalishi tunajidanganyaje – aidha ni wa Kaini au Habili
ama wa Shetani au wa yesu, hakuna katikati.
3.
Imani juu
ya Yesu – Galatia 3:26- Leo hii
mimi na wewe twaweza kuwa Wana kwa kumuamini Yesu tu. Mungu atakuhesabia Haki
kama Habili alivyohesabiwa haki kwa njia ya Imani tu- Waebrania 11:4
4. HITIMISHO
CHUKUA HATUA- Leo hii unaweza kuwa
mwenye Haki kama Habili kwa njia ya Upatanisho ambayo Mungu aliianzisha kwa
njia ya Damu ya Yesu, Mungu anakupenda hivyo ameamua akusitiri kwasababu
anakupenda – 1Petro 4:8. Lakini pia
Leo hii unaweza UKACHAGUA kuwa
MUASI kama Kaini kwa kujibunia njia zako za kumpendeza Mungu bila Damu-Waebrania 9:22
BY
APOSTLE ELIYA
THE EPANGELIA CHURCH
MAKULU-DODOMA
0753 011 774
No comments:
Post a Comment