Thursday, January 23, 2014
Mfahamu Mwimbaji na Mchungaji John Shabani
John S. Shabani ni mzaliwa wa kijiji cha Kirando katika kitongoji cha Nyankima, kata ya sunuka, Wilaya ya Kigoma Vijijini, Nchini Tanzania. Ukoo wake ni waumini wazuri wa dini ya kiislam (Islamic Religion).
Baada ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi kirando, alijiunga na elimu ya sekondari, lakini kutokana na itikadi za kidini, alijikuta akiwa katika wakati mgumu wa kupigwa vita na wazazi, ni baada ya uamuzi wake wa kujiunga na Dini ya kikristo. Hivyo John ameishi miaka mingi akiwa mbali na wazazi wake, lakini hata hivyo hakukata tamaa.
| John Shabani:Safari ya kuelekea Sudan |
Mwaka 1992, John akiwa kijana mdogo, alipata ufadhili wa kwenda nchni Kongo (Zamani Zaire), ambako huko alijifunza muziki na kusoma Chuo cha Biblia (Bible knowledge), na huko kipaji chake cha kutunga nyimbo na kuimba kilijitokeza kwa kasi, hata akatokea kupendwa sana.
John hakutaka kuona mtu yeyote akiwa katika hali ya kukata tamaa, maana alifahamu madhara yake. Kwasababu hiyo, alianzisha vikundi mbalimbali vya vijana akiwa na lengo la kuwaelimisha ili kujikwamua katika hali ya kukata tamaa na kutokujihusisha na vitendo viovu kama madawa ya kulevya, Ukahaba na anasa za kila aina, mambo ambavyo aliyapiga vita sana.
![]() |
| JOHN SHABANI AKIWA NA RAIS JK KIKWETE |
John ameishi miaka mingi kama yatima, lakini hali hiyo imemsaidia kujifunza mengi na kuwa na tabia njema, kumheshimu na kumthamini kila mtu, mambo yaliyompelekea kupata kibali machoni pa wengi hata kuwa mfano wa kuigwa. Amekuwa msaada kwa Vijana wengi (Ndani na nnje ya nchi) na kuwakwamua wengi waliokuwa wamekata tamaa na kujihusisha na vitendo viovu. Pia kutokana na ujuzi wa muziki alioupata na pia kipaji kikubwa alichonacho cha kutunga, kuandika nyimbo na kuimba, John amekuwa msaada kwa waimbaji mbalimbali binafsi na vikundi ndani na nje ya nchi, hasa nyimbo za Injili. Ni mwalimu bora na mshauri kwa waimbaji. Wengi waliopitia kwake sasa ni waimbaji wazuri na maarufu.
Mwaka 2001 John alifunga pingu za maisha na binti aitwaye Debora Shabani na mwaka 2002 walipata mtoto wa kike. Alimwita mwanaye Joyce, akiwa na maana ya kuyasahau maisha ya huzuni na shida na kujitabiria maisha ya furaha.
Mwaka 2004, John aliajiriwa katika kampuni ya Msama promotions ya jijini Dare es salaam, kampuni inayojihusisha na kuinua vipaji na pia kuwainua vijana na watu wa rika na jinsia zote waliokata tamaa ya maisha n.k, na hasa wale walioko vijiweni wakijihusisha na madawa ya kulevya, ukahaba n.k. Kampuni hiyo imewasaidia Vijana wengi na Jamii kwa ujumla, na wengi wamejikomboa kimaisha![]() |
| John Shabani akiwa na Rose Muhando na Bahati Bukuku |
Tarehe 19/03/04, John alirekodi Album yake aliyoiita “Marufuku kukata tamaa”
Album ambayo imewasaidia wengi waliokata tamaa na kuwapa matumaini mapya. Album hiyo na nyingine alioirekodi mwaka 2009 inayoitwa “Huu ni wakati wangu”, zimekuwa msaada mkubwa kwa kila aliye au anayezinunua, zimegusa na kuinua mioyo ya watu wengi. Kwani amepokea shuhuda nyingi ndani na nnje, hata za wale waliodiriki kujiua, lakini baada ya kusikiliza nyimbo hizo waliahirisha. “Nakusii nunua kanda hizo, naamini zitakusaidia”. Pia utakuwa mchango wako kwa kutimiza ndoto na malengo ya John.
John ametembelea nchi mbalimbali, akijifunza maisha ya watu. Amegundua kwamba karibu asilimia kubwa ya wanadamu, awe maskini, tajiri, msomi au asiye na elimu, wenye vyeo au waajiriwa, watoto kwa wakubwa, wanaume kwa wanawake, awe mzungu au mweusi n.k, wote kwa njia moja au nyingine wamepitia katika hali ya kukata tamaa au kukatishwa tamaa na jambo fulani, mtu, watu, hali au mazingira fulani. Ndipo mwaka 2006, alipata maono na msukumo mkubwa wa kuandika Kitabu ambacho kitakuwa msaada kwa njia moja au nyingine kwa kila atakayekipata.
Tarehe 26.04. 2009, John alitunukiwa tuzo ya heshima pamoja na cheti (certicate of appreciation) kwa kutambua mchango wake kwa ajili ya kuinua vipaji na pia kuchangia kuinua muziki wa Injili Afrika mashariki na kati. Pamoja na hayo amekua akianzisha makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu maisha ya kujitegemea, kujishughulisha na kuhepukana na vitendo viovu kama wizi, ujambazi, utumiaji madaswa ya kulevya, ukahaba n.k. Tuzo hiyo ilitolewa na kampuni moja maarufu Tanzania yenye makao makuu jijini Dar es salaam (Christian promoters Ltd).
John ameanzisha huduma inayoitwa Never give up “Usikate tamaa” Ambayo anategemea kuisajili wakati wowote. Huduma hii, inalenga kuinua vipaji, mipango na mbinu za kuwakwamua vijana au watu kujihusisha na madawa ya kulevya, ukahaba, utapeli wizi, ujambazi nk, mambo yanayosabisha magonjwa kama vile ukimwi, kufungwa jela au kufa kabla ya wakati, matokeo yake kuacha wototo wengi yatima na wajane nk. Pia kutafuta ufadhili kwa ajili ya kuaendeleza vijana ki-elimu pamoja na kuwawezesha pale inapobidi. Kwa sasa anayo program inayoitwa Touching voice program (Darasa la uhimbaji)
Ni kwa ajili ya kwaya, Band/vikundi na waimbaji binafsi.
-Mwisho-
CHANZO: MAISHA YA USHINDI BLOG
Tuesday, January 21, 2014
USIJIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA ??????
YALIYOMO
1. UTANGULIZI 2. JIFUNZE
KWA WALIOFANIKIWA
3. USIJIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA 4. HITIMISHO
ANDIKO KUU: Ezekieli 28:1-7,11-13
1.UTANGULIZI
- Andiko kuu linazungumzia watawala wawili, kuna mkuu wa
Tiro-Ezek 28:1-7, huyu ni mwanadamu, na Mfalme wa Tiro-Ezek 28:11-13, huyu ni
mkuu wa anga(shetani). Hawa wawili walikuwa na mahusiano, mwanadamu akiwa kama kawaida yake KIBARAKA, hakuna mtu atakaye kuambia
mahusiano yake na mapepo, mpaka siri zifichuliwe.
-Kila tajiri mkubwa hapa Duniani, anayo siri moyoni mwake ya
huo utajiri, na ukishasikia SIRI, ujue ni Siri kweli. Kwakifupi hakuna
aliyezaliwa masikini, kila mmoja wetu amezaliwa kuwa tajiri mkubwa, tatizo ni
namna ya kufanya huo utajiri uwe halisi..
-Mafanikio na utajiri ni AIDIA, ni WAZO. Wewe
msomaji unahitaji kitu kimoja tu uwe tajiri wa kutupwa, otea nini !! AIDIA.
Swali linakuja, nitapata wapi Aidia ili niisimamie hiyo Aidia niwe tajiri?.
Apostle Eliya atakusaidia kufichua hii SIRI ya AIDIA ya matajiri na
waliofanikiwa. Twende pamoja……………..
2. JIFUNZE
KWA WALIOFANIKIWA
-Mafanikio ni hali ya kutokuwa muhitaji, utajiri ni hali ya
kuwa huru ki-fedha. Kwa hizi maana za mafanikio na utajiri utagundua kuwa
mafanikio ni muhimu kuliko utajiri kwasababu utajiri ni sehemu mojawapo ya
mafanikio. Vyote viwili vinahitaji AIDIA.
- Huu msemo umekuwa maarufu, na wengi wameunukuu kwa nyimbo
au misemo,kwamba “jifunze kwa waliofanikiwa, usijifunze kwa walioshindwa”.
Sijajua kama wanajua huu msemo umebuniwa na nani, mimi ninashauri usijifunze
kwa waliofanikiwa.
-Njia rahisi ya kujifunza kuhusu Mafanikio na utajiri ni;
(a) kuwatambua waliofanikiwa (b) kujifunza kwao na (c)
Kufanya maamuzi.
-Kabla sijaelezea hivyo vipengele vitatu, naomba utambue
kuwa Mwanadamu ana asili mbili, yakwanza ambayo ina nguvu ni asili ya rohoni,
na yapili ni asili ya mwilini. Roho ya mtu ndio inayochukua mambo ya rohoni na
kuipatia nafsi, na nafsi inaungoza mwili. Ninapokwenda kueleza vipengele vitatu
utambue kuwa yanayooneka mwilini ni matokeo.
- WATAMBUE WALIOFANIKIWA
-Ili kuwatambua
waliofanikiwa, nitatumia uzoefu wa mwanadamu wa kujifanikisha, historia huwa
inajirudia, Aidia za mafanikio za watu wa zamani ni sawa kabisa na Aidia za
ulimwengu huu isipokuwa tofauti ni namna ya kuendesha na kusimamia hizo Aidia.
-Nitataja watu 5 ambao walifanikiwa sana,
na mafanikio yao
yaliweza kubadirii tamaduni na maisha ya ulimwengu wote. Kwa kupitia hawa
matajiri 5, utagundua asili ya mwanadamu na vyanzo vya Aidia ya mafanikio yao.
-Watambue Waliofanikiwa kupitiliza:
1. NEBUKADREZA, 2. DARIO NA KORESHI
3. SULEMANI, 4. ALEKZANDA, 5. AGASTUS
- JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA
- Hebu tuone hawa watu 5 walivyofanikiwa, naomba utambue
kwamba mwanadamu hajabadirika, asili ya hawa 5 ndio uliyonayo wewe na kila
unayemjua kuwa kafanikiwa.
1.
NEBUKADREZA
-Alikuwa Mfalme wa Babeli, utajiri na mafanikio yake kila
mtu Duniani aliyatambua, aliweza kuishi anavyotaka, kila aliyempinga aliweza
kumuangamiza kwa uweza wa nguvu za mafanikio yake.
-Chanzo cha Mafanikio yake – Soma DANIELI 3:1-7. Kama mafanikio ya Nebukadreza yangekuwa ya kawaida
asingetengeneza sanamu, hapa utagundua kwamba Mfalme alikuwa na mahusiano na
ulimwengu wa kiroho wa shetani. Baadae akatawala mtoto wa Mfalme, tazama nayeye
alichokifanya,DANIELI 5:3-4. Hii ndio asili ya Mwanadamu na haijabadirika .
2.
DARIO NA KORESHI
- Dario alikuwa mfalme wa Umedi. Koreshi alikuwa mfalme wa
Uajemi, Hawa wafalme walifanya ushirika Kung’oa mafanikio ya Babeli, mafanikio yao yalitambulika kila kona
ya Duniani .
-Chanzo cha Mafanikio yao- (Dario) DANIELI 6:7- Alikuwa na
miungu yake ambayo ilimdanganya kuwa yeye mfalme angeweza kuwa mungu, (Koreshi)
DANIELI 10:13 huyu jamaa alikuwa na mahusiano na mkuu wa anga lake, yeye
alikuwa ni kibaraka tu.
3.
SULEMANI
-Alikuwa Mfalme wa Israeli, kama
kawaida, mafanikio yake yalipita viambaza vya Dunia yote.
-Chanzo cha Mafanikio yake- 2 NYAKATI 1:7-12, Umejifunza
nini? Umeona chanzo cha AIDIA ya mafanikio ya Sulemani?. Hapa tumeona chanzo
kingine cha mafanikio,ni JEHOVA
4.
ALEKZANDA
-Alikuwa Mfalme wa Ugiriki, mafanikio yake yalitawala Dunia
yote
-Chanzo cha mafanikio yake- Gaya ndiye mungu wa wagiriki, wanaamini kuwa
ndiye aliyeumba na ndiye mwenye milki ya kila kitu. Aidia za mafanikio zilitoka
kwa huyu mungu Gaya
wa wagiriki.
5.
AGASTUS
-Alikuwa Mfalme wa Rumi, Mafanikio yake yalienea Duniani
kote, mpaka leo tunaweza tukaona mabaki ya mafanikio ya Rumi(ROMA).
- Chanzo cha Mafanikio yake; alikuwa na miungu mingi, lakini
mungu aliyekuwa maarufu ni MALIKIA WA ULIMWENGU, ambaye miaka hii wanamuita
MAMA WA MUNGU(mama maria), lakini huyu mungu siyo yule Mungu wa Sulemani.
- FANYA MAAMUZI
- Wataalamu walisema usifanye maamuzi kama
huna habari(informations) kamili, nimejaribu kukuonyesha hapo juu vyanzo vikuu
vya waliofanikiwa, kumbuka asili ya mwanadamu ya kutafuta msaada wa mafanikio
haijabadirika.
- Hebu nivigawe vyanzo vya mafanikio kabla hujafanya
maamuzi, nimevigawa vyanzo katika makundi matatu;
1. Mtu
Binafsi 2.Shetani na 3.Mungu(Yesu)
-Kama tukiwakusanya waliofanikiwa na kuwagawanya katika
makundi, bila shaka tunapata makundi matatu, mgawanyo huu ni kutegemea vyanzo
vya mafanikio yao:
1. Mtu Binafsi
-Chanzo cha mafanikio hapa mtu BINAFSI. Hapa mtu anatumia
Elimu,uzoefu,mipango kabambe,juhudi,kuwekeza,mikopo, nk. Watu wanaotumia hii
njia ki-ukweli huwa hawana mafanikio sana,
wakijitahidi sana
wataweza kula vizuri na kupata ka-usafiri na ki-nyumba cha kuishi.Hawana uwezo
wa kuikopesha serikali,siku zote wao hukopa.
2. Shetani
-Chanzo cha mafanikio hapa ni SHETANI, Hili kundi wanapata
muongozo na mipango kutoka kwa Shetani, juhudi binafsi zinakuwa ni za pili.
Kundi hili limefanikiwa sana
kuliko la kwanza kwasababu wanaye msaidizi wa kuwapa ramani.
3. YESU
- Chanzo cha Mafanikio hapa ni Mungu(Yesu), Mipango na aidia
inatoka kwa Yesu, nikimaanisha Yesu ndiye anayempa wazo mtu afanye nini, lakini
usimamizi wote anakuwanao mwanadamu. Kundi hili ndio lilipaswa lifanikiwe kuliko
makundi yote mawili ya hapo juu, kwasababu Yesu ananguvu kuliko Shetani.
►Kwa ujumla tumejifunza kuwa AIDIA za utajiri mkubwa upo
ulimwengu wa roho, na ulimwengu wa roho ni Mungu au Shetani tu,hakuna katikati,
naomba niseme kwamba mwanadamu ni dhaifu mno, hana lolote wala si chochote,
tumezuiliwa na MUDA(time) na NAFASI(space).
- Pamoja na kwamba Mungu ana nguvu kuliko Shetani lakini
watu wanaomwamini Yesu ndio walio masikini wazuri,tatizo ni nini? Hili swali
linamajibu mawili, labda tatizo lipo kwa hawa wanaomwamini au mtazamo wa Mungu
kuhusu mafanikio upo tofauti.
►Kati ya hao waliofanikiwa watano, tumeona mmoja kati yao ndiye aliyekuwa na chanzo sahihi cha Aidia, kwahiyo kama ukienda kujifunza kwa hao wane maana yake
watakuingiaza chaka. Usijifunze kwa waliofanikiwa tu kwasababu watakupoteza.
3. USIJIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA
Kwanini watoto wa Mungu wengi ni masikini???????
- Nimesema hapo juu kuwa kuna majibu mawili:
(a)Tatizo la watoto wa Mungu, au (b) Mtazamo wa Mungu wa
Mafanikio ni tofauti na tunavyodhani.
A.WATOTO WA
MUNGU
-Nimegundua wakristo wengi tumeshindwa kuifichua hii siri ya
kupata Aidia ya mafanikio. Baada ya kufanya utafiti wa mafanikio, nimegundua
kitu nyeti sana,
kwamba AIDIA ya mafanikio anayo Mungu ambayo yupo rohoni, na mwanadamu
anaihitaji hiyo AIDIA lakini yupo mwilini, kwahiyo mwanadamu anahitaji MAWASIRIANO
kati yake na Mungu.
-Mawasiriano ni KUSIKIA, KUONA. Kusikia nini? Sauti
ya Mungu. Kuona nini? Maono na kuota ndoto. Hapa tu ndio tatizo. Wakristo wengi
hawajui kuwa Mungu anaongea mpaka sasa na hivyo hawakotayari kusikia Mungu
anachowaambia, hawataki kuingia rohoni, wanapenda mambo ya mwilini na
kujitahidi.
- 2 NYAKATI 1:7-12. Hapa utagundua Mungu anaongea na
Sulemani katika ndoto/maono na Sulemani ANAMSIKIA Mungu, kisha ANATII
alichokisikia. Baada ya kupata AIDIA toka kwa Mungu kwa kusikia ndipo unapoweza
kuanza juhudi binafsi.
B.MTAZAMO WA
MUNGU
-Mtazamo wa Mungu kuhusu mafanikio ukoje? Ili
kujibu swali hili utapaswa uangalie ni yupi ambaye Mungu alimfurahia.
Tukishampata mtu ambaye Mungu anamfurahia ndipo tutakapoangalia maisha yake kisha
tutajua mtazamo wa Mungu kuhusu mafanikio. Hapa nitachukua watu watatu :1. SULEMANI,
2.NEBUKADREZA, 3. YESU.
SULEMANI- 1FALME
11:9- Mungu anamghadhibikia Suleimani, aliyekuwa tajiri sana, na utajiri wake Mungu ndiye aliyempa,
2NYAKATI 9:22-24.
NEBUKADREZA- soma
DANIELI 4:22, 25.Mafanikio ya Nebukadreza yangefutiliwa mbali na Mungu
kwasababu alishindwa kumtambua Mungu.
YESU- Mathayo
17:5. Mungu anasema “ …NINAYEPENDEZWA NAYE…” Kwenye Biblia kuna watu wawili
ambao Mungu alizungumza nao maneno kama haya,
ni Musa-HESABU 12:6-8, na Daudi-1SAMWELI 13:14, lakini hawa wote hawafui dafu
kwa Yesu.
►Umejifunza nini? Kumbe utajiri sio kipimo kizuri cha
mafanikio, tulipochukua wale wafalme 5,tuliona sulemani ndiye aliyestahili
lakini baada ya kumchukua Sulemani na kumlinganisha na Yesu tumeona hafai
kabisa. Hivyo mtu ambaye tungepaswa kujifunza kwake ni…….YESU, kwanini?
Kwasababu Mungu amependezwa naye.
YESU
-Msomaji, unataka kufanikiwa? Jifunze kwa Yesu, yeye alikuwa
amefanikiwa, akapoteza mafanikio yote kisha akayapata yote. Ndio maana mwanzo
nikasema usijifunze kwa waliofanikiwa bali jifunze kwa waliofanikiwa kwanza,
harafu wakaishiwa kisha wakafanikiwa tena.
=Ngoja nikupe siri, Yesu hakuwa tajiri lakini hakuwa
mhitaji, nahii ndiyo kanuni ya mkristo sahihi, kumbuka utajiri ni zawadi ya
Mungu kwakuwa umempendeza, angalia hapa anavyomwambia Ibrahimu, baba wa Imani –MWANZO
15:1. Naomba uelewe kwamba kuna mtoa utajiri na utajiri, wakristo wengi wanahangaikia
utajiri, lakini hawana haja ya mtoa utajiri- Mathayo 6:25
-Kilichomfanikisha Ibrahimu, Musa, Daudi na Yesu ni kuipenda
sheria ya kwanza, unajua ni ipi?-MATHAYO 22:37. Usisahau kuwa Mungu ana wivu,
hapendi kuona mtu anampenda kwasababu yeye ana mali
au mtu anapenda mali
kuliko mtoaji.
4.HITIMISHO
-Tafuta kitabu kilichoandikwa na tajiri yeyote kuhusu
utajiri, kuna maneno yafuatayo hutayakosa: DESIRE, PLAN, PERSISTANCE, DECISION,
INVEST, DETERMINATION, ACHIEVE, GOAL, MANAGE, COOPERATION, na maneno kibao
watakupa, unajua siri ni nini? Hawakwambii, wengi wao wanamahusiano ya moja kwa
moja na shetani, kama huamini fanya kila
wanachoshauri uone, ukishashindwa fuata njia yangu, mimi ndo nimeshaanza,
kwasababu nimegundua siri.
Maneno yote hapo juu ni juhudi binafsi, yanatakiwa yafuate
ukishapata AIDIA toka ulimwengu wa roho
yaani Mungu au shetani, nakushauri chagua Mungu, na ukishagua Mungu kubali
kuendanan na mtazamo wa Mungu sio wako wewe.SIKIA sauti ya Mungu, pia ona Maono
MWANZO 12:6, nnje ya hapo utaniwia radhi jamani.
…….Remembe…………THE BEST HAS COMES…0717 267676
Monday, January 20, 2014
JE WAJUA KUWA LUGHA SIO KIELELEZO CHA IMANI?,
Imeandikwa na Robert E. Maziku
اَلْمَزْمُورُُ الْمِئَةُ
وَالْخَمْسُونَ
USHUHUDA WA MUISLAMU ALIYEOKOKA ALIKUWA NA MAJINI YA CHUMA ULETE SASA NI MWINJILISTI, COSMAS JUMA HAMIS
Mimi Mwinjilisti Cosmas Juma Hamis nimezaliwa mwaka 1975 Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora nikiwa ni mtoto wa kwanza wa mama Mwamini Said Ntembela na Baba Shekh Juma Hamis Mdaki, Baba akiwa msumbwa na mkazi wa Wilaya mpya ya Kaliua na Mama mwenyeji wa tarafa ya Usoke wilaya Urambo akiwa ni wa kabila la watusi wazawa wa mkoa Tabora. Mwaka 1985 nikiwa na umri wa miaka 10 nilianza elimu ya msingi katika shule ya msingi mapinduzi iliyoko tarafa ya Usoke wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora pamoja na kuanza elimu ya msingi pia nilijiunga na shule ya kiislamu (yaani nilijiunga na shule ya kiislamu (madrasat) kusoma elimu ya kiislamu na hii ilitokana na Baba yangu na Mama yangu kuwa ni waislamu hivyo nilipelekwa katika madrtasa hiyo ili nisome uislam ambao ndio dini ya wazazi wangu na ndugu zangu wote.
Nikiwa ni mzaliwa wa kwanza kati ya watoto 12 katika tumbo la mama yangu Mwamini Said Ntembela ambapo mimi kwa Baba tumezaliwa watoto 2 mimi na dada yangu Johari Juma Hamis na mimi nikiitwa wakati ule kwa jina la Hamisi Juma Mdaki mama yangu aliachana na Baba yangu shekh Juma Hamisi Mdaki tukiwa tumezaliwa watoto wawili na baada ya kuachana Mama na Baba ambapo ilikuwa mwaka 1979 mimi nikiwa na umri wa miaka minne na dada yangu akiwa na miaka miwili tukaenda kuishi kwao na Mama ambapo ni tarafa ya Usoke wilaya ya Urambo kwani hapo mwanzo tulikuwa tukiishi mwanza na kaliua baada ya kuishi pale usoke mama yangu aliolewa nma mume mwingine ambae anaitwa Shabani bakari amri moja. Waliishi na mume huyo ambapo kisheria alikuwa mume halali kutokana na mafundisho ya dini ya kiislamu kwa kuwa alishapewa taraka, hivyo waliendelea kuzaa watoto ambapo jumla walifika watoto kumi na hivyo kufanya idadi ya watoto wa Mama huyo kufikia 12 na mimi nikiwa mkubwa wa wote.
Baada ya kuanza Elimu ya dini ya kiislamu sambamba na elimu ya msingi niliitimu elimu ya msingi mwaka 1991 na baada ya kutokuchaguliwa na elimu ya secondary mwaka 1992 nilichukuliwa na Baba yangu Shekh Juma Hamis Mdaki na kunipeleka alipokuwa akiishi yeye ambapo ni kijiji cha Igagala No 3 na kuniandikisha katika shule ya msingi kamusekwa iliyopo kijiji cha Igagala No 2 ili niludie masomo ya elimu ya msingi ambapo yeye kwa wakati huo alikuwa ni shekh wa msikiti wa Igagala No 3 pamoja na mwalimu wa madrasat ya pale msikitini hivyo na mimi niliendelea na masomo ya elimu ya dini yeye Baba yangu akiwa mwalimu wetu nilisoma kwa mwaka mmoja na kuhamia mjini, wakati huo ikiwa bado ni tarafa hivyo nikiwa kaliua nilijiunga na madrasat ya kiislamu pale kaliua kwa mwalimu mwingine ambae aliitwa shehe Omari mimi na wenzangu tuliendelea na masomo pale mpaka mwaka 1993. Mwaka 1994 niliondoka kwa shekh huyo ambae kwa sasa ni marehemu na kurudi Usoke baada ya kushindikana kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari. baada ya kufika Usoke iliyoko wilaya ya Urambo niliendelea na masomo ya dini ya kiislamu kwa shekh aitwaye Juma Almas mpaka mwaka 1995 nikaondoka kwenda mwanza nikiwa nimeshakuwa mwelewa katika dini yangu ya kiislamu nikaendelea na masomo kwa mashekh mbalimbali akiwemo shekh Juma Hamis Sungusungu ambae alikuwa akitoa darasa na masomo katika msikiti wa Mabatini uliopo katika kota za mapolisi pale Mabatini Mwaza. Mwaka 1999 nilihama Mwanza na kuhamia mkoani Shinyanga wakati huo nilikuwa na miaka 24 nilipofika Shinyanga niliingia katika chuo cha kiislamu kiitwacho MADRASAT NURANIA chini ya mwalimu Masoud na walimu wengine nikaendelea na Uislam nikiwa Muumini mzuri wa imani ya dini ya kiislamu.
Niliendelea na masomo hapo ambapo chuo hicho kilikuwa katika msikiti wa Ngokolo matope chini ya Imamu alieitwa Maalimu Selfu. Mwaka 2000 niliondoka shinyanga wakati huo nikiwa tayari na uelewa wa kutosha juu ya dini yangu na tayari ninao uwezo wa kufundisha na wengine nilielekea jijini Dar es Salaam na nikiwa Dar nilifikia kurasini kwa Shekh Juma Kassim Ngupepe yeye akiwa mwenye asili ya Rufiji na Mafia nikiwa pale nilijifunza Elimu nya unajimu au Tiba za Kiarabu nikiwa naendelea kuishi hapo na wakati huo nilikuwa na majini ya Uganga ambayo yaliniongoza katika mambo yangu ya kimaisha nilifanya kazi pale kwa shekh huyo kwa muda wa mwaka mmoja nasikuchelewa kuanza kufanya kazi zangu binafsi za uganga wa majini kwani tayari nilishapata baraka toka kwa shekh wangu na ndipo nikafungua na mimi ofisi yangu ya uganga maeneo hayohayo ya kurasini, tiba ya majini na mimi binafsi nilikuwa namiliki majini.
Mwaka 2002 niliendelea na kazi hiyo huku nikienda kwa mashehe mbalimbali kujiongezea elimu zaidi juu ya majini na tabia zao(yaani elimudunia) watu wengi walikuja kwangu wakati huo nilikuwa nimekwishaoa na kuishi na mwanamke ambaye yeye asili yake alikuwa mkristo maana majini yangu yalinitaka nioe mwanamke ambaye ni mkristo kwa maana kwamba ipo siku na yeye huyo mwanamke atabadili dini na kuwa muislam kama mimi na hayo majini. Baada ya kufanya kazi hiyo ikiwa pamoja na kuwafundisha wengine mwaka 2003 majini yalinitaka niende kwa mganga ili nikajiongezee karama ya kipato wakati huo nikiwa nina mtoto mmoja niliyezaa na mwanamke huyo niliyekuwa ninaishi naye.
Niliondoka na kuelekea Mwanza na pale nilikutana na rafiki yangu na kunipeleka kwa mganga mkoani Shinyanga maeneo ya Bariadi kijiji cha Bunamalambugani nikakaa kwa mganga kwa miezi mitatu(3) nikapewa majini ya chuma ulete nikarudi Dar, nikiwa Dar ndani ya muda mfupi mambo yalianza kwenda vizuri sana kwani nilitumia chuma ulete kwa kujiongezea kipato nikaweza kununua gari mwaka huo na kupanga nyumba nzuri na ya kisasa nikaachana na kazi ya uganga, chuma ulete niliitumia kwa watu wasio mkubali Yesu pamoja na kuwa walikuwa wakristo (yaani wasiookoka) hivyo ndani ya mwaka mwingine niliweza kujenga nyumba kwetu Tabora na kuishi maisha ya uhakika sikuwa na shida, ila chuma ulete nilipewa sharti nitumie kwa watu walio wakristo tu tena kwa wale ambao hawajaokoka kwani niliambiwa nikitumia kwa wale waliyookoka haitafanya kazi itazidiwa nguvu na walokole maana wao wanauwezo zaidi ya chuma ulete, basi nilisafiri mikoa mingi hapa nchini na hiyo chuma ulete nikiwachukulia watu fedha bila kunigundua.
Baada ya mafanikio mganga aliniagiza niende kule kwake, Bariadi ili akanielekeze mambo muhimu wakati ule maisha yangu yalikuwa mazuri sana! kwani niliweza kuwasaidia ndugu zangu, nikiwa kwa mganga mwaka huo wa 2004 mganga akanitaka nimtoe mwanangu wa kwanza afe (yaani nimtoe sadaka mali iweze kukaa na kutulia) baada ya kusema hivyo mganga mimi nilikataa akanifukuza na baada ya kuondoka kwa mganga huyo mali ziliteketea ikiwa pamoja na magari nyumba na mwisho nikakubali, ila wakati na mpeleka yule mtoto kwa mganga kumtoa sadaka nikakuta mganga amekufa mwaka huo ulikua mwaka 2005, mwishoni mwaka 2006 nikiwa nimeshafilisika na wakati huo nikiwa na watoto watatu nikalukwa akili ndugu zangu wamenipeleka kwa waganga wengi bila mafanikio mwishowe ndugu wakanitelekeza bila msaada, mke wangu akaenda kwao na mali chache ndugu waliziuza ili kunitibisha kwa waganga bila mafanikio niliendelea kuteseka na nilipokutana na YESU KRISTO kwa kufanyiwa maombi hiyo ilikuwa mwaka 2008 Magomeni kanisa Anglikana,a mbapo siku ya jumanne nilifika pale nikakutana na mtumishi wa Mungu haitwae Henry Ramadhani ambaye alinifanyia maombi nikapona kabisa majini yote yakaondoka, mwaka huo huo 2008 nikabatizwa hapo magomeni Angalikana na chini ya mchungaji Elisha Tendwa ambapo ilikuwa tarehe 11- 5 -2008 nilibatizwa mimi Hamis Juma Hamisi nakupewa jina la Cosmas Juma Hamis nilisimamiwa ubatizo na huyo mzee Henry Ramadhani ambaye aliniombea nakupona nilibatizwa mimi na wanangu siku hiyo hiyo ambao mmoja anaitwa Suzana Cosmas Juma mwingine Martin Cosmas Juma na yule ambaye alitaka mganga amchukue kichawi ili niendelee kumiliki mali alibatizwa Zanzibar kwa jina la Marrygoreth Cosmas Juma.
Baada ya ubatizo niliendelea na mafundisho juu ya imani mpya ya kristo nikapata kipaimara kanisa la Angalikani mbezi lous chini ya mchumngaji Paul Mtweve na baada ya kipa imara mzee Ramadhani aliongea na wachungaji ambapo nilipelekwa kwenda kusomea kozi ya utumishi wakanisani chuo cha Anglikana morogoro kiitwacho kwa jina la MOROGORO BIBLE COLLEGE nilisoma mpaka mwaka 2010 baaada ya kumaliza masomo nikaludi Dar, nikiwa Dar nilipangiwa kituo cha kazi kama mwijilisti kanisani, kanisa la Anglikana na Roho Mtakatifu chini ya mchungaji Johnson Lameck ambapo mwaka mmoja nilipata pigo kubwa sana kifamilia la kufiwa nikarudi Tabora, nikiwa Tabora niliendelea kumtumikia mungu ambapo pamoja na ndugu kuwa waislam na, mimi ni Mkristo nimeona njia ya mimi kwenda mbinguni nikimfuata Yesu Kristo yeye ndiye njia, kwa sasa napatikana katika kanisa la Anglikana Kakola Kahama dayosisi ya Tabora nikiwa ndie Mwinjilisti wa kanisa hilo lakini pia ni mwenyekiti wa Kamati ya uinjilisti chini ya mchungaji Israel Baada, lengo langu ni kuendelea na masomo zaidi kwani namshukuru mungu kwa kuisoma elimu ya kiislam kwa miaka 25 hivyo naelewa dini hiyo vilivyo kwanza nikiwa nimeisoma na pia kukulia katika familia ya kisomi ya dini hiyo na wenye kufuata maadili yote kiislam, kiu yangu kwa sasa pamoja nakutumika kwenye makanisa mengi nikifundisha semina mbalimbali, endapo na nitapata mfadhili wa kuniendeleza kimasomo zaidi kwa upande Ukristo nitafurahi zaidi na muda huu ambao niko Kahama Shinyanga nimeendelea kutumika nikiwa na mwinjilisti wa kanisa la Angalikana katika parishi ya Kakola, natumika katika kutoa ushuhuda namna nilivyo zama katika uchawi wa kimajini baada ya kukaa nayo na jinsi ambavyo Babu yangu alivyonilisisha uchawi na namna nilivyo achana na hayo yote na kumupokea yesu kristo, endapo mtu au kanisa au kikundi chochote cha kikristo kikinihitaji kwa ajili ya ushuhuda wa nguvu za Yesu zilizo niokoa mimi na wanangu napatikana kwa
No:- 0789 351 590 ,0714 351 590
au Barua pepe
amostelesphory@gmail.com
Asante Mungu Awabariki sana
Mimi Ev Cosmas Juma
Mwislam niliyeokoka.
CHANZO: MAISHA YA USHINDI BLOG
Saturday, January 18, 2014
HUYO NDIYE MUIGIZAJI BRIAN DEACON ALIYEIGIZA KAMA "YESU" NA ANACHOKIFANYA KWA SASA KATIKA MAISHA..!!

Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji
huyo ambaye ni
mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko
Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia
yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni
nesi. Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo
alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa
yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo
mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS'' Aliigiza filamu ya
Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama
akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa
waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano
huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba
wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael
walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo
New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za
majukwaani na uigizaji. Brian Deacon miaka iliyofuatia baada
ya kuigiza kama Yesu.Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani
wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake
aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama
yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema
alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka
kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza
jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo
mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na
maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla
hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka
mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa
kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake
kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na
kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina
gani.watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian
Deacon ni mwigizaji mkuu.Katika miezi saba waliyochukua
kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa
masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa
siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake
kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba
angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa
anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na
kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa
mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu
mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati
anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja
alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea
na mapepo yalimtoka mwanamama huyo. Siku nyingine
waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12
wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma
kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian
anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze
nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni
Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36
walikubali kurudi kuendelea na kaziAmesema mtihani
mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18
usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya
mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau
kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri
hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda
mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema
usiku.Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom
Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa
umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa
muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo
lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio
maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu
hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya
kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa
kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya
kwanza akaona ni
kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo
ya watu. Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza
majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya
30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na
watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za
mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha
maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo
ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao
kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo
chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari
imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200
zikiwa njiani kutafsiriwa. Brian anawaambia watu kwamba
yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na
kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema
ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na
kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu
hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya
filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao
Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo
imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya
watu. kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed &
Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya
mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa
mwaka 1978.
Subscribe to:
Posts (Atom)





