Saturday, January 18, 2014
HUYO NDIYE MUIGIZAJI BRIAN DEACON ALIYEIGIZA KAMA "YESU" NA ANACHOKIFANYA KWA SASA KATIKA MAISHA..!!
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji
huyo ambaye ni
mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko
Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia
yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni
nesi. Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo
alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa
yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo
mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS'' Aliigiza filamu ya
Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama
akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa
waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano
huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba
wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael
walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo
New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za
majukwaani na uigizaji. Brian Deacon miaka iliyofuatia baada
ya kuigiza kama Yesu.Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani
wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake
aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama
yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema
alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka
kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza
jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo
mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na
maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla
hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka
mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa
kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake
kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na
kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina
gani.watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian
Deacon ni mwigizaji mkuu.Katika miezi saba waliyochukua
kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa
masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa
siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake
kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba
angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa
anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na
kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa
mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu
mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati
anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja
alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea
na mapepo yalimtoka mwanamama huyo. Siku nyingine
waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12
wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma
kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian
anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze
nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni
Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36
walikubali kurudi kuendelea na kaziAmesema mtihani
mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18
usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya
mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau
kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri
hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda
mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema
usiku.Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom
Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa
umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa
muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo
lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio
maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu
hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya
kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa
kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya
kwanza akaona ni
kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo
ya watu. Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza
majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya
30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na
watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za
mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha
maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo
ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao
kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo
chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari
imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200
zikiwa njiani kutafsiriwa. Brian anawaambia watu kwamba
yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na
kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema
ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na
kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu
hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya
filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao
Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo
imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya
watu. kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed &
Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya
mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa
mwaka 1978.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment