YALIYOMO
1. UTANGULIZI 2. JIFUNZE
KWA WALIOFANIKIWA
3. USIJIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA 4. HITIMISHO
ANDIKO KUU: Ezekieli 28:1-7,11-13
1.UTANGULIZI
- Andiko kuu linazungumzia watawala wawili, kuna mkuu wa
Tiro-Ezek 28:1-7, huyu ni mwanadamu, na Mfalme wa Tiro-Ezek 28:11-13, huyu ni
mkuu wa anga(shetani). Hawa wawili walikuwa na mahusiano, mwanadamu akiwa kama kawaida yake KIBARAKA, hakuna mtu atakaye kuambia
mahusiano yake na mapepo, mpaka siri zifichuliwe.
-Kila tajiri mkubwa hapa Duniani, anayo siri moyoni mwake ya
huo utajiri, na ukishasikia SIRI, ujue ni Siri kweli. Kwakifupi hakuna
aliyezaliwa masikini, kila mmoja wetu amezaliwa kuwa tajiri mkubwa, tatizo ni
namna ya kufanya huo utajiri uwe halisi..
-Mafanikio na utajiri ni AIDIA, ni WAZO. Wewe
msomaji unahitaji kitu kimoja tu uwe tajiri wa kutupwa, otea nini !! AIDIA.
Swali linakuja, nitapata wapi Aidia ili niisimamie hiyo Aidia niwe tajiri?.
Apostle Eliya atakusaidia kufichua hii SIRI ya AIDIA ya matajiri na
waliofanikiwa. Twende pamoja……………..
2. JIFUNZE
KWA WALIOFANIKIWA
-Mafanikio ni hali ya kutokuwa muhitaji, utajiri ni hali ya
kuwa huru ki-fedha. Kwa hizi maana za mafanikio na utajiri utagundua kuwa
mafanikio ni muhimu kuliko utajiri kwasababu utajiri ni sehemu mojawapo ya
mafanikio. Vyote viwili vinahitaji AIDIA.
- Huu msemo umekuwa maarufu, na wengi wameunukuu kwa nyimbo
au misemo,kwamba “jifunze kwa waliofanikiwa, usijifunze kwa walioshindwa”.
Sijajua kama wanajua huu msemo umebuniwa na nani, mimi ninashauri usijifunze
kwa waliofanikiwa.
-Njia rahisi ya kujifunza kuhusu Mafanikio na utajiri ni;
(a) kuwatambua waliofanikiwa (b) kujifunza kwao na (c)
Kufanya maamuzi.
-Kabla sijaelezea hivyo vipengele vitatu, naomba utambue
kuwa Mwanadamu ana asili mbili, yakwanza ambayo ina nguvu ni asili ya rohoni,
na yapili ni asili ya mwilini. Roho ya mtu ndio inayochukua mambo ya rohoni na
kuipatia nafsi, na nafsi inaungoza mwili. Ninapokwenda kueleza vipengele vitatu
utambue kuwa yanayooneka mwilini ni matokeo.
- WATAMBUE WALIOFANIKIWA
-Ili kuwatambua
waliofanikiwa, nitatumia uzoefu wa mwanadamu wa kujifanikisha, historia huwa
inajirudia, Aidia za mafanikio za watu wa zamani ni sawa kabisa na Aidia za
ulimwengu huu isipokuwa tofauti ni namna ya kuendesha na kusimamia hizo Aidia.
-Nitataja watu 5 ambao walifanikiwa sana,
na mafanikio yao
yaliweza kubadirii tamaduni na maisha ya ulimwengu wote. Kwa kupitia hawa
matajiri 5, utagundua asili ya mwanadamu na vyanzo vya Aidia ya mafanikio yao.
-Watambue Waliofanikiwa kupitiliza:
1. NEBUKADREZA, 2. DARIO NA KORESHI
3. SULEMANI, 4. ALEKZANDA, 5. AGASTUS
- JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA
- Hebu tuone hawa watu 5 walivyofanikiwa, naomba utambue
kwamba mwanadamu hajabadirika, asili ya hawa 5 ndio uliyonayo wewe na kila
unayemjua kuwa kafanikiwa.
1.
NEBUKADREZA
-Alikuwa Mfalme wa Babeli, utajiri na mafanikio yake kila
mtu Duniani aliyatambua, aliweza kuishi anavyotaka, kila aliyempinga aliweza
kumuangamiza kwa uweza wa nguvu za mafanikio yake.
-Chanzo cha Mafanikio yake – Soma DANIELI 3:1-7. Kama mafanikio ya Nebukadreza yangekuwa ya kawaida
asingetengeneza sanamu, hapa utagundua kwamba Mfalme alikuwa na mahusiano na
ulimwengu wa kiroho wa shetani. Baadae akatawala mtoto wa Mfalme, tazama nayeye
alichokifanya,DANIELI 5:3-4. Hii ndio asili ya Mwanadamu na haijabadirika .
2.
DARIO NA KORESHI
- Dario alikuwa mfalme wa Umedi. Koreshi alikuwa mfalme wa
Uajemi, Hawa wafalme walifanya ushirika Kung’oa mafanikio ya Babeli, mafanikio yao yalitambulika kila kona
ya Duniani .
-Chanzo cha Mafanikio yao- (Dario) DANIELI 6:7- Alikuwa na
miungu yake ambayo ilimdanganya kuwa yeye mfalme angeweza kuwa mungu, (Koreshi)
DANIELI 10:13 huyu jamaa alikuwa na mahusiano na mkuu wa anga lake, yeye
alikuwa ni kibaraka tu.
3.
SULEMANI
-Alikuwa Mfalme wa Israeli, kama
kawaida, mafanikio yake yalipita viambaza vya Dunia yote.
-Chanzo cha Mafanikio yake- 2 NYAKATI 1:7-12, Umejifunza
nini? Umeona chanzo cha AIDIA ya mafanikio ya Sulemani?. Hapa tumeona chanzo
kingine cha mafanikio,ni JEHOVA
4.
ALEKZANDA
-Alikuwa Mfalme wa Ugiriki, mafanikio yake yalitawala Dunia
yote
-Chanzo cha mafanikio yake- Gaya ndiye mungu wa wagiriki, wanaamini kuwa
ndiye aliyeumba na ndiye mwenye milki ya kila kitu. Aidia za mafanikio zilitoka
kwa huyu mungu Gaya
wa wagiriki.
5.
AGASTUS
-Alikuwa Mfalme wa Rumi, Mafanikio yake yalienea Duniani
kote, mpaka leo tunaweza tukaona mabaki ya mafanikio ya Rumi(ROMA).
- Chanzo cha Mafanikio yake; alikuwa na miungu mingi, lakini
mungu aliyekuwa maarufu ni MALIKIA WA ULIMWENGU, ambaye miaka hii wanamuita
MAMA WA MUNGU(mama maria), lakini huyu mungu siyo yule Mungu wa Sulemani.
- FANYA MAAMUZI
- Wataalamu walisema usifanye maamuzi kama
huna habari(informations) kamili, nimejaribu kukuonyesha hapo juu vyanzo vikuu
vya waliofanikiwa, kumbuka asili ya mwanadamu ya kutafuta msaada wa mafanikio
haijabadirika.
- Hebu nivigawe vyanzo vya mafanikio kabla hujafanya
maamuzi, nimevigawa vyanzo katika makundi matatu;
1. Mtu
Binafsi 2.Shetani na 3.Mungu(Yesu)
-Kama tukiwakusanya waliofanikiwa na kuwagawanya katika
makundi, bila shaka tunapata makundi matatu, mgawanyo huu ni kutegemea vyanzo
vya mafanikio yao:
1. Mtu Binafsi
-Chanzo cha mafanikio hapa mtu BINAFSI. Hapa mtu anatumia
Elimu,uzoefu,mipango kabambe,juhudi,kuwekeza,mikopo, nk. Watu wanaotumia hii
njia ki-ukweli huwa hawana mafanikio sana,
wakijitahidi sana
wataweza kula vizuri na kupata ka-usafiri na ki-nyumba cha kuishi.Hawana uwezo
wa kuikopesha serikali,siku zote wao hukopa.
2. Shetani
-Chanzo cha mafanikio hapa ni SHETANI, Hili kundi wanapata
muongozo na mipango kutoka kwa Shetani, juhudi binafsi zinakuwa ni za pili.
Kundi hili limefanikiwa sana
kuliko la kwanza kwasababu wanaye msaidizi wa kuwapa ramani.
3. YESU
- Chanzo cha Mafanikio hapa ni Mungu(Yesu), Mipango na aidia
inatoka kwa Yesu, nikimaanisha Yesu ndiye anayempa wazo mtu afanye nini, lakini
usimamizi wote anakuwanao mwanadamu. Kundi hili ndio lilipaswa lifanikiwe kuliko
makundi yote mawili ya hapo juu, kwasababu Yesu ananguvu kuliko Shetani.
►Kwa ujumla tumejifunza kuwa AIDIA za utajiri mkubwa upo
ulimwengu wa roho, na ulimwengu wa roho ni Mungu au Shetani tu,hakuna katikati,
naomba niseme kwamba mwanadamu ni dhaifu mno, hana lolote wala si chochote,
tumezuiliwa na MUDA(time) na NAFASI(space).
- Pamoja na kwamba Mungu ana nguvu kuliko Shetani lakini
watu wanaomwamini Yesu ndio walio masikini wazuri,tatizo ni nini? Hili swali
linamajibu mawili, labda tatizo lipo kwa hawa wanaomwamini au mtazamo wa Mungu
kuhusu mafanikio upo tofauti.
►Kati ya hao waliofanikiwa watano, tumeona mmoja kati yao ndiye aliyekuwa na chanzo sahihi cha Aidia, kwahiyo kama ukienda kujifunza kwa hao wane maana yake
watakuingiaza chaka. Usijifunze kwa waliofanikiwa tu kwasababu watakupoteza.
3. USIJIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA
Kwanini watoto wa Mungu wengi ni masikini???????
- Nimesema hapo juu kuwa kuna majibu mawili:
(a)Tatizo la watoto wa Mungu, au (b) Mtazamo wa Mungu wa
Mafanikio ni tofauti na tunavyodhani.
A.WATOTO WA
MUNGU
-Nimegundua wakristo wengi tumeshindwa kuifichua hii siri ya
kupata Aidia ya mafanikio. Baada ya kufanya utafiti wa mafanikio, nimegundua
kitu nyeti sana,
kwamba AIDIA ya mafanikio anayo Mungu ambayo yupo rohoni, na mwanadamu
anaihitaji hiyo AIDIA lakini yupo mwilini, kwahiyo mwanadamu anahitaji MAWASIRIANO
kati yake na Mungu.
-Mawasiriano ni KUSIKIA, KUONA. Kusikia nini? Sauti
ya Mungu. Kuona nini? Maono na kuota ndoto. Hapa tu ndio tatizo. Wakristo wengi
hawajui kuwa Mungu anaongea mpaka sasa na hivyo hawakotayari kusikia Mungu
anachowaambia, hawataki kuingia rohoni, wanapenda mambo ya mwilini na
kujitahidi.
- 2 NYAKATI 1:7-12. Hapa utagundua Mungu anaongea na
Sulemani katika ndoto/maono na Sulemani ANAMSIKIA Mungu, kisha ANATII
alichokisikia. Baada ya kupata AIDIA toka kwa Mungu kwa kusikia ndipo unapoweza
kuanza juhudi binafsi.
B.MTAZAMO WA
MUNGU
-Mtazamo wa Mungu kuhusu mafanikio ukoje? Ili
kujibu swali hili utapaswa uangalie ni yupi ambaye Mungu alimfurahia.
Tukishampata mtu ambaye Mungu anamfurahia ndipo tutakapoangalia maisha yake kisha
tutajua mtazamo wa Mungu kuhusu mafanikio. Hapa nitachukua watu watatu :1. SULEMANI,
2.NEBUKADREZA, 3. YESU.
SULEMANI- 1FALME
11:9- Mungu anamghadhibikia Suleimani, aliyekuwa tajiri sana, na utajiri wake Mungu ndiye aliyempa,
2NYAKATI 9:22-24.
NEBUKADREZA- soma
DANIELI 4:22, 25.Mafanikio ya Nebukadreza yangefutiliwa mbali na Mungu
kwasababu alishindwa kumtambua Mungu.
YESU- Mathayo
17:5. Mungu anasema “ …NINAYEPENDEZWA NAYE…” Kwenye Biblia kuna watu wawili
ambao Mungu alizungumza nao maneno kama haya,
ni Musa-HESABU 12:6-8, na Daudi-1SAMWELI 13:14, lakini hawa wote hawafui dafu
kwa Yesu.
►Umejifunza nini? Kumbe utajiri sio kipimo kizuri cha
mafanikio, tulipochukua wale wafalme 5,tuliona sulemani ndiye aliyestahili
lakini baada ya kumchukua Sulemani na kumlinganisha na Yesu tumeona hafai
kabisa. Hivyo mtu ambaye tungepaswa kujifunza kwake ni…….YESU, kwanini?
Kwasababu Mungu amependezwa naye.
YESU
-Msomaji, unataka kufanikiwa? Jifunze kwa Yesu, yeye alikuwa
amefanikiwa, akapoteza mafanikio yote kisha akayapata yote. Ndio maana mwanzo
nikasema usijifunze kwa waliofanikiwa bali jifunze kwa waliofanikiwa kwanza,
harafu wakaishiwa kisha wakafanikiwa tena.
=Ngoja nikupe siri, Yesu hakuwa tajiri lakini hakuwa
mhitaji, nahii ndiyo kanuni ya mkristo sahihi, kumbuka utajiri ni zawadi ya
Mungu kwakuwa umempendeza, angalia hapa anavyomwambia Ibrahimu, baba wa Imani –MWANZO
15:1. Naomba uelewe kwamba kuna mtoa utajiri na utajiri, wakristo wengi wanahangaikia
utajiri, lakini hawana haja ya mtoa utajiri- Mathayo 6:25
-Kilichomfanikisha Ibrahimu, Musa, Daudi na Yesu ni kuipenda
sheria ya kwanza, unajua ni ipi?-MATHAYO 22:37. Usisahau kuwa Mungu ana wivu,
hapendi kuona mtu anampenda kwasababu yeye ana mali
au mtu anapenda mali
kuliko mtoaji.
4.HITIMISHO
-Tafuta kitabu kilichoandikwa na tajiri yeyote kuhusu
utajiri, kuna maneno yafuatayo hutayakosa: DESIRE, PLAN, PERSISTANCE, DECISION,
INVEST, DETERMINATION, ACHIEVE, GOAL, MANAGE, COOPERATION, na maneno kibao
watakupa, unajua siri ni nini? Hawakwambii, wengi wao wanamahusiano ya moja kwa
moja na shetani, kama huamini fanya kila
wanachoshauri uone, ukishashindwa fuata njia yangu, mimi ndo nimeshaanza,
kwasababu nimegundua siri.
Maneno yote hapo juu ni juhudi binafsi, yanatakiwa yafuate
ukishapata AIDIA toka ulimwengu wa roho
yaani Mungu au shetani, nakushauri chagua Mungu, na ukishagua Mungu kubali
kuendanan na mtazamo wa Mungu sio wako wewe.SIKIA sauti ya Mungu, pia ona Maono
MWANZO 12:6, nnje ya hapo utaniwia radhi jamani.
…….Remembe…………THE BEST HAS COMES…0717 267676
No comments:
Post a Comment