Thursday, January 23, 2014

PICHA YA SIKU


Mfahamu Mwimbaji na Mchungaji John Shabani

John S. Shabani ni mzaliwa wa kijiji cha Kirando katika kitongoji cha Nyankima, kata ya sunuka, Wilaya ya Kigoma Vijijini, Nchini Tanzania. Ukoo wake ni waumini wazuri wa dini ya kiislam (Islamic Religion).

Baada ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi kirando, alijiunga na elimu ya sekondari, lakini kutokana na itikadi za kidini, alijikuta akiwa katika wakati mgumu wa kupigwa vita na wazazi, ni baada ya uamuzi wake wa kujiunga na Dini ya kikristo. Hivyo John ameishi miaka mingi akiwa mbali na wazazi wake, lakini hata hivyo hakukata tamaa.
John Shabani:Safari ya kuelekea Sudan

Mwaka 1992, John akiwa kijana mdogo, alipata ufadhili wa kwenda nchni Kongo (Zamani Zaire), ambako huko alijifunza muziki na kusoma Chuo cha Biblia (Bible knowledge), na huko kipaji chake cha kutunga nyimbo na kuimba kilijitokeza kwa kasi, hata akatokea kupendwa sana.

John hakutaka kuona mtu yeyote akiwa katika hali ya kukata tamaa, maana alifahamu madhara yake. Kwasababu hiyo, alianzisha vikundi mbalimbali vya vijana akiwa na lengo la kuwaelimisha ili kujikwamua katika hali ya kukata tamaa na kutokujihusisha na vitendo viovu kama madawa ya kulevya, Ukahaba na anasa za kila aina, mambo ambavyo aliyapiga vita sana.

JOHN SHABANI AKIWA NA RAIS  JK KIKWETE
John ameishi miaka mingi kama yatima, lakini hali hiyo imemsaidia kujifunza mengi na kuwa na tabia njema, kumheshimu na kumthamini kila mtu, mambo yaliyompelekea kupata kibali machoni pa wengi hata kuwa mfano wa kuigwa. Amekuwa msaada kwa Vijana wengi (Ndani na nnje ya nchi) na kuwakwamua wengi waliokuwa wamekata tamaa na kujihusisha na vitendo viovu. Pia kutokana na ujuzi wa muziki alioupata na pia kipaji kikubwa alichonacho cha kutunga, kuandika nyimbo na kuimba, John amekuwa msaada kwa waimbaji mbalimbali binafsi na vikundi ndani na nje ya nchi, hasa nyimbo za Injili. Ni mwalimu bora na mshauri kwa waimbaji. Wengi waliopitia kwake sasa ni waimbaji wazuri na maarufu.

Mwaka 2001 John alifunga pingu za maisha na binti aitwaye Debora Shabani na mwaka 2002 walipata mtoto wa kike. Alimwita mwanaye Joyce, akiwa na maana ya kuyasahau maisha ya huzuni na shida na kujitabiria maisha ya furaha.

Mwaka 2004, John aliajiriwa katika kampuni ya Msama promotions ya jijini Dare es salaam, kampuni inayojihusisha na kuinua vipaji na pia kuwainua vijana na watu wa rika na jinsia zote waliokata tamaa ya maisha n.k, na hasa wale walioko vijiweni wakijihusisha na madawa ya kulevya, ukahaba n.k. Kampuni hiyo imewasaidia Vijana wengi na Jamii kwa ujumla, na wengi wamejikomboa kimaisha
John Shabani akiwa na Rose Muhando na Bahati Bukuku
Tarehe 19/03/04, John alirekodi Album yake aliyoiita “Marufuku kukata tamaa”
Album ambayo imewasaidia wengi waliokata tamaa na kuwapa matumaini mapya. Album hiyo na nyingine alioirekodi mwaka 2009 inayoitwa “Huu ni wakati wangu”, zimekuwa msaada mkubwa kwa kila aliye au anayezinunua, zimegusa na kuinua mioyo ya watu wengi. Kwani amepokea shuhuda nyingi ndani na nnje, hata za wale waliodiriki kujiua, lakini baada ya kusikiliza nyimbo hizo waliahirisha. “Nakusii nunua kanda hizo, naamini zitakusaidia”. Pia utakuwa mchango wako kwa kutimiza ndoto na malengo ya John.

John ametembelea nchi mbalimbali, akijifunza maisha ya watu. Amegundua kwamba karibu asilimia kubwa ya wanadamu, awe maskini, tajiri, msomi au asiye na elimu, wenye vyeo au waajiriwa, watoto kwa wakubwa, wanaume kwa wanawake, awe mzungu au mweusi n.k, wote kwa njia moja au nyingine wamepitia katika hali ya kukata tamaa au kukatishwa tamaa na jambo fulani, mtu, watu, hali au mazingira fulani. Ndipo mwaka 2006, alipata maono na msukumo mkubwa wa kuandika Kitabu ambacho kitakuwa msaada kwa njia moja au nyingine kwa kila atakayekipata.

Tarehehe 11/7/08 ni siku ambayo John hawezi kuisahau. Siku ya huzuni na majonzi, siku ya kilio na kuomboleza. Ni siku alipofariki mke wake mpendwa na mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili, Debora Shabani, mwimbaji aliyegusa mioyo ya watu wengi ndani na nnje ya nchi, mwimbaji ambaye msiba na mazishi yake yalihudhuriwa na maelfu ya watu, wakiwepo Maaskofu, Wachungaji, Waimbaji binafsi, Kwaya pamoja na viongozi mbalimbali wa serekali. Hata hivyo, John hakukata tamaa.

Tarehe 26.04. 2009, John alitunukiwa tuzo ya heshima pamoja na cheti (certicate of appreciation) kwa kutambua mchango wake kwa ajili ya kuinua vipaji na pia kuchangia kuinua muziki wa Injili Afrika mashariki na kati. Pamoja na hayo amekua akianzisha makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu maisha ya kujitegemea, kujishughulisha na kuhepukana na vitendo viovu kama wizi, ujambazi, utumiaji madaswa ya kulevya, ukahaba n.k. Tuzo hiyo ilitolewa na kampuni moja maarufu Tanzania yenye makao makuu jijini Dar es salaam (Christian promoters Ltd).

John ameanzisha huduma inayoitwa Never give up “Usikate tamaa” Ambayo anategemea kuisajili wakati wowote. Huduma hii, inalenga kuinua vipaji, mipango na mbinu za kuwakwamua vijana au watu kujihusisha na madawa ya kulevya, ukahaba, utapeli wizi, ujambazi nk, mambo yanayosabisha magonjwa kama vile ukimwi, kufungwa jela au kufa kabla ya wakati, matokeo yake kuacha wototo wengi yatima na wajane nk. Pia kutafuta ufadhili kwa ajili ya kuaendeleza vijana ki-elimu pamoja na kuwawezesha pale inapobidi. Kwa sasa anayo program inayoitwa Touching voice program (Darasa la uhimbaji)
Ni kwa ajili ya kwaya, Band/vikundi na waimbaji binafsi.
                                -Mwisho-

CHANZO: MAISHA YA USHINDI BLOG
 

Tuesday, January 21, 2014

USIJIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA ??????


NAMNA YA KUWA TAJIRI MKUBWA

YALIYOMO
1. UTANGULIZI    2. JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA
3. USIJIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA   4. HITIMISHO

ANDIKO KUU: Ezekieli 28:1-7,11-13

1.UTANGULIZI
- Andiko kuu linazungumzia watawala wawili, kuna mkuu wa Tiro-Ezek 28:1-7, huyu ni mwanadamu, na Mfalme wa Tiro-Ezek 28:11-13, huyu ni mkuu wa anga(shetani). Hawa wawili walikuwa na mahusiano, mwanadamu akiwa kama kawaida yake KIBARAKA, hakuna mtu atakaye kuambia mahusiano yake na mapepo, mpaka siri zifichuliwe.

-Kila tajiri mkubwa hapa Duniani, anayo siri moyoni mwake ya huo utajiri, na ukishasikia SIRI, ujue ni Siri kweli. Kwakifupi hakuna aliyezaliwa masikini, kila mmoja wetu amezaliwa kuwa tajiri mkubwa, tatizo ni namna ya kufanya huo utajiri uwe halisi..

-Mafanikio na utajiri ni AIDIA, ni WAZO. Wewe msomaji unahitaji kitu kimoja tu uwe tajiri wa kutupwa, otea nini !! AIDIA. Swali linakuja, nitapata wapi Aidia ili niisimamie hiyo Aidia niwe tajiri?. Apostle Eliya atakusaidia kufichua hii SIRI ya AIDIA ya matajiri na waliofanikiwa. Twende pamoja……………..


2. JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA

-Mafanikio ni hali ya kutokuwa muhitaji, utajiri ni hali ya kuwa huru ki-fedha. Kwa hizi maana za mafanikio na utajiri utagundua kuwa mafanikio ni muhimu kuliko utajiri kwasababu utajiri ni sehemu mojawapo ya mafanikio. Vyote viwili vinahitaji AIDIA.

- Huu msemo umekuwa maarufu, na wengi wameunukuu kwa nyimbo au misemo,kwamba “jifunze kwa waliofanikiwa, usijifunze kwa walioshindwa”. Sijajua kama wanajua huu msemo umebuniwa na nani, mimi ninashauri usijifunze kwa waliofanikiwa.

-Njia rahisi ya kujifunza kuhusu Mafanikio na utajiri ni;
(a) kuwatambua waliofanikiwa (b) kujifunza kwao na (c) Kufanya maamuzi.

-Kabla sijaelezea hivyo vipengele vitatu, naomba utambue kuwa Mwanadamu ana asili mbili, yakwanza ambayo ina nguvu ni asili ya rohoni, na yapili ni asili ya mwilini. Roho ya mtu ndio inayochukua mambo ya rohoni na kuipatia nafsi, na nafsi inaungoza mwili. Ninapokwenda kueleza vipengele vitatu utambue kuwa yanayooneka mwilini ni matokeo.

  1. WATAMBUE WALIOFANIKIWA
-Ili kuwatambua waliofanikiwa, nitatumia uzoefu wa mwanadamu wa kujifanikisha, historia huwa inajirudia, Aidia za mafanikio za watu wa zamani ni sawa kabisa na Aidia za ulimwengu huu isipokuwa tofauti ni namna ya kuendesha na kusimamia hizo Aidia.

-Nitataja watu 5 ambao walifanikiwa sana, na mafanikio yao yaliweza kubadirii tamaduni na maisha ya ulimwengu wote. Kwa kupitia hawa matajiri 5, utagundua asili ya mwanadamu na vyanzo vya Aidia ya mafanikio yao.

-Watambue Waliofanikiwa kupitiliza:
1. NEBUKADREZA, 2. DARIO NA KORESHI
3. SULEMANI, 4. ALEKZANDA, 5. AGASTUS

  1. JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA
- Hebu tuone hawa watu 5 walivyofanikiwa, naomba utambue kwamba mwanadamu hajabadirika, asili ya hawa 5 ndio uliyonayo wewe na kila unayemjua kuwa kafanikiwa.

1. NEBUKADREZA
-Alikuwa Mfalme wa Babeli, utajiri na mafanikio yake kila mtu Duniani aliyatambua, aliweza kuishi anavyotaka, kila aliyempinga aliweza kumuangamiza kwa uweza wa nguvu za mafanikio yake.

-Chanzo cha Mafanikio yake – Soma DANIELI 3:1-7. Kama mafanikio ya Nebukadreza yangekuwa ya kawaida asingetengeneza sanamu, hapa utagundua kwamba Mfalme alikuwa na mahusiano na ulimwengu wa kiroho wa shetani. Baadae akatawala mtoto wa Mfalme, tazama nayeye alichokifanya,DANIELI 5:3-4. Hii ndio asili ya Mwanadamu na haijabadirika .

2. DARIO NA KORESHI
- Dario alikuwa mfalme wa Umedi. Koreshi alikuwa mfalme wa Uajemi, Hawa wafalme walifanya ushirika Kung’oa mafanikio ya Babeli, mafanikio yao yalitambulika kila kona ya Duniani .

-Chanzo cha Mafanikio yao- (Dario) DANIELI 6:7- Alikuwa na miungu yake ambayo ilimdanganya kuwa yeye mfalme angeweza kuwa mungu, (Koreshi) DANIELI 10:13 huyu jamaa alikuwa na mahusiano na mkuu wa anga lake, yeye alikuwa ni kibaraka tu.

3. SULEMANI
-Alikuwa Mfalme wa Israeli, kama kawaida, mafanikio yake yalipita viambaza vya Dunia yote.

-Chanzo cha Mafanikio yake- 2 NYAKATI 1:7-12, Umejifunza nini? Umeona chanzo cha AIDIA ya mafanikio ya Sulemani?. Hapa tumeona chanzo kingine cha mafanikio,ni JEHOVA

4. ALEKZANDA
-Alikuwa Mfalme wa Ugiriki, mafanikio yake yalitawala Dunia yote

-Chanzo cha mafanikio yake- Gaya ndiye mungu wa wagiriki, wanaamini kuwa ndiye aliyeumba na ndiye mwenye milki ya kila kitu. Aidia za mafanikio zilitoka kwa huyu mungu Gaya wa wagiriki.

5. AGASTUS
-Alikuwa Mfalme wa Rumi, Mafanikio yake yalienea Duniani kote, mpaka leo tunaweza tukaona mabaki ya mafanikio ya Rumi(ROMA).

- Chanzo cha Mafanikio yake; alikuwa na miungu mingi, lakini mungu aliyekuwa maarufu ni MALIKIA WA ULIMWENGU, ambaye miaka hii wanamuita MAMA WA MUNGU(mama maria), lakini huyu mungu siyo yule Mungu wa Sulemani.

  1. FANYA MAAMUZI
- Wataalamu walisema usifanye maamuzi kama huna habari(informations) kamili, nimejaribu kukuonyesha hapo juu vyanzo vikuu vya waliofanikiwa, kumbuka asili ya mwanadamu ya kutafuta msaada wa mafanikio haijabadirika.

- Hebu nivigawe vyanzo vya mafanikio kabla hujafanya maamuzi, nimevigawa vyanzo katika makundi matatu;
   1. Mtu Binafsi  2.Shetani na 3.Mungu(Yesu)

-Kama tukiwakusanya waliofanikiwa na kuwagawanya katika makundi, bila shaka tunapata makundi matatu, mgawanyo huu ni kutegemea vyanzo vya mafanikio yao:

1. Mtu Binafsi
-Chanzo cha mafanikio hapa mtu BINAFSI. Hapa mtu anatumia Elimu,uzoefu,mipango kabambe,juhudi,kuwekeza,mikopo, nk. Watu wanaotumia hii njia ki-ukweli huwa hawana mafanikio sana, wakijitahidi sana wataweza kula vizuri na kupata ka-usafiri na ki-nyumba cha kuishi.Hawana uwezo wa kuikopesha serikali,siku zote wao hukopa.

2. Shetani
-Chanzo cha mafanikio hapa ni SHETANI, Hili kundi wanapata muongozo na mipango kutoka kwa Shetani, juhudi binafsi zinakuwa ni za pili. Kundi hili limefanikiwa sana kuliko la kwanza kwasababu wanaye msaidizi wa kuwapa ramani.

3. YESU
- Chanzo cha Mafanikio hapa ni Mungu(Yesu), Mipango na aidia inatoka kwa Yesu, nikimaanisha Yesu ndiye anayempa wazo mtu afanye nini, lakini usimamizi wote anakuwanao mwanadamu. Kundi hili ndio lilipaswa lifanikiwe kuliko makundi yote mawili ya hapo juu, kwasababu Yesu ananguvu kuliko Shetani.


►Kwa ujumla tumejifunza kuwa AIDIA za utajiri mkubwa upo ulimwengu wa roho, na ulimwengu wa roho ni Mungu au Shetani tu,hakuna katikati, naomba niseme kwamba mwanadamu ni dhaifu mno, hana lolote wala si chochote, tumezuiliwa na MUDA(time) na NAFASI(space).

- Pamoja na kwamba Mungu ana nguvu kuliko Shetani lakini watu wanaomwamini Yesu ndio walio masikini wazuri,tatizo ni nini? Hili swali linamajibu mawili, labda tatizo lipo kwa hawa wanaomwamini au mtazamo wa Mungu kuhusu mafanikio upo tofauti.

►Kati ya hao waliofanikiwa watano, tumeona mmoja kati yao ndiye aliyekuwa na chanzo sahihi cha Aidia, kwahiyo kama ukienda kujifunza kwa hao wane maana yake watakuingiaza chaka. Usijifunze kwa waliofanikiwa tu kwasababu watakupoteza.

3. USIJIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA

Kwanini watoto wa Mungu wengi ni masikini???????

- Nimesema hapo juu kuwa kuna majibu mawili:
(a)Tatizo la watoto wa Mungu, au (b) Mtazamo wa Mungu wa Mafanikio ni tofauti na tunavyodhani.

A.WATOTO WA MUNGU
-Nimegundua wakristo wengi tumeshindwa kuifichua hii siri ya kupata Aidia ya mafanikio. Baada ya kufanya utafiti wa mafanikio, nimegundua kitu nyeti sana, kwamba AIDIA ya mafanikio anayo Mungu ambayo yupo rohoni, na mwanadamu anaihitaji hiyo AIDIA lakini yupo mwilini, kwahiyo mwanadamu anahitaji MAWASIRIANO kati yake na Mungu.

-Mawasiriano ni KUSIKIA, KUONA. Kusikia nini? Sauti ya Mungu. Kuona nini? Maono na kuota ndoto. Hapa tu ndio tatizo. Wakristo wengi hawajui kuwa Mungu anaongea mpaka sasa na hivyo hawakotayari kusikia Mungu anachowaambia, hawataki kuingia rohoni, wanapenda mambo ya mwilini na kujitahidi.

- 2 NYAKATI 1:7-12. Hapa utagundua Mungu anaongea na Sulemani katika ndoto/maono na Sulemani ANAMSIKIA Mungu, kisha ANATII alichokisikia. Baada ya kupata AIDIA toka kwa Mungu kwa kusikia ndipo unapoweza kuanza juhudi binafsi.

B.MTAZAMO WA MUNGU
-Mtazamo wa Mungu kuhusu mafanikio ukoje? Ili kujibu swali hili utapaswa uangalie ni yupi ambaye Mungu alimfurahia. Tukishampata mtu ambaye Mungu anamfurahia ndipo tutakapoangalia maisha yake kisha tutajua mtazamo wa Mungu kuhusu mafanikio. Hapa nitachukua watu watatu :1. SULEMANI,  2.NEBUKADREZA, 3. YESU.

SULEMANI- 1FALME 11:9- Mungu anamghadhibikia Suleimani, aliyekuwa tajiri sana, na utajiri wake Mungu ndiye aliyempa, 2NYAKATI 9:22-24.

NEBUKADREZA- soma DANIELI 4:22, 25.Mafanikio ya Nebukadreza yangefutiliwa mbali na Mungu kwasababu alishindwa kumtambua Mungu.

YESU- Mathayo 17:5. Mungu anasema “ …NINAYEPENDEZWA NAYE…” Kwenye Biblia kuna watu wawili ambao Mungu alizungumza nao maneno kama haya, ni Musa-HESABU 12:6-8, na Daudi-1SAMWELI 13:14, lakini hawa wote hawafui dafu kwa Yesu.

►Umejifunza nini? Kumbe utajiri sio kipimo kizuri cha mafanikio, tulipochukua wale wafalme 5,tuliona sulemani ndiye aliyestahili lakini baada ya kumchukua Sulemani na kumlinganisha na Yesu tumeona hafai kabisa. Hivyo mtu ambaye tungepaswa kujifunza kwake ni…….YESU, kwanini? Kwasababu Mungu amependezwa naye.

YESU
-Msomaji, unataka kufanikiwa? Jifunze kwa Yesu, yeye alikuwa amefanikiwa, akapoteza mafanikio yote kisha akayapata yote. Ndio maana mwanzo nikasema usijifunze kwa waliofanikiwa bali jifunze kwa waliofanikiwa kwanza, harafu wakaishiwa kisha wakafanikiwa tena.

=Ngoja nikupe siri, Yesu hakuwa tajiri lakini hakuwa mhitaji, nahii ndiyo kanuni ya mkristo sahihi, kumbuka utajiri ni zawadi ya Mungu kwakuwa umempendeza, angalia hapa anavyomwambia Ibrahimu, baba wa Imani –MWANZO 15:1. Naomba uelewe kwamba kuna mtoa utajiri na utajiri, wakristo wengi wanahangaikia utajiri, lakini hawana haja ya mtoa utajiri- Mathayo 6:25

-Kilichomfanikisha Ibrahimu, Musa, Daudi na Yesu ni kuipenda sheria ya kwanza, unajua ni ipi?-MATHAYO 22:37. Usisahau kuwa Mungu ana wivu, hapendi kuona mtu anampenda kwasababu yeye ana mali au mtu anapenda mali kuliko mtoaji.


4.HITIMISHO

-Tafuta kitabu kilichoandikwa na tajiri yeyote kuhusu utajiri, kuna maneno yafuatayo hutayakosa: DESIRE, PLAN, PERSISTANCE, DECISION, INVEST, DETERMINATION, ACHIEVE, GOAL, MANAGE, COOPERATION, na maneno kibao watakupa, unajua siri ni nini? Hawakwambii, wengi wao wanamahusiano ya moja kwa moja na shetani, kama huamini fanya kila wanachoshauri uone, ukishashindwa fuata njia yangu, mimi ndo nimeshaanza, kwasababu nimegundua siri.

Maneno yote hapo juu ni juhudi binafsi, yanatakiwa yafuate ukishapata AIDIA toka ulimwengu wa roho yaani Mungu au shetani, nakushauri chagua Mungu, na ukishagua Mungu kubali kuendanan na mtazamo wa Mungu sio wako wewe.SIKIA sauti ya Mungu, pia ona Maono MWANZO 12:6, nnje ya hapo utaniwia radhi jamani.

…….Remembe…………THE BEST HAS COMES…0717 267676

Monday, January 20, 2014

JE WAJUA KUWA LUGHA SIO KIELELEZO CHA IMANI?,


Imeandikwa na Robert E. Maziku

Watu huchanganya wakati mwingine kwa kufikili kuwa Lugha ni kielelezo cha  Imani, Kwa mfano akiongea kiingereza au kiarabu ni ishara ya Imani fulani. Naomba niwakumbushe sio kweli.

Lugha ni chombo cha mawasiliano baina ya kiumbe flani na kingine chombo hiki kikiwa katika mfumo wa sauti tena wataalamu wanatuambia sauti zenyewe ni za nasibu tu yaani hakukuwa na makubaliano maalumu kuwa tutakuwa tunatoa sauti hii ikimaanisha hivi bali zilitokea tu, na ndio maana kuna Lugha za wanyama na Lugha za watu. Nyuki wanasauti zao zinazo wafanya wao kwa wao kuelewana kama ilivyo binadamu watumiavyo sauti kuelewana. Hizi Lugha hazitoi ishara ya wewe ni dini gani.

Hii ni sura ya 150 kutoka katika kitabu cha Zaburi kinachopatikana katika Biblia takatifu kikiwa kimeandikwa kiarabu atakae weza kusoma asome kwa kuhakiki asiyeweza basi aamini tu kuwa KIARABU NI LUGHA NA SIO UKIKUTA KITABU KIMEANDIKWA KIARABU KINAMAANISHA DINI BALI NI LUGHA YA MAWASILIANO KWA WAARABU NA WANAOTUMIA KIARABU.


اَلْمَزْمُورُُ الْمِئَةُ وَالْخَمْسُونَ

1هَلِّلُويَا. سَبِّحُوا اللهَ فِي قُدْسِهِ. سَبِّحُوهُ فِي فَلَكِ قُوَّتِهِ. 2سَبِّحُوهُ عَلَى قُوَّاتِهِ. سَبِّحُوهُ حَسَبَ كَثْرَةِ عَظَمَتِهِ. 3سَبِّحُوهُ بِصَوْتِ الصُّورِ. سَبِّحُوهُ بِرَبَابٍ وَعُودٍ. 4سَبِّحُوهُ بِدُفّ وَرَقْصٍ. سَبِّحُوهُ بِأَوْتَارٍ وَمِزْمَارٍ. 5سَبِّحُوهُ بِصُنُوجِ التَّصْوِيتِ. سَبِّحُوهُ بِصُنُوجِ الْهُتَافِ. كُلُّ نَسَمَةٍ فَلْتُسَبِّحِ الرَّبَّ. هَلِّلُويَا.

USHUHUDA WA MUISLAMU ALIYEOKOKA ALIKUWA NA MAJINI YA CHUMA ULETE SASA NI MWINJILISTI, COSMAS JUMA HAMIS


 Mimi Mwinjilisti Cosmas Juma Hamis nimezaliwa mwaka 1975 Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora nikiwa ni mtoto wa kwanza wa mama Mwamini Said Ntembela na Baba Shekh Juma Hamis Mdaki, Baba akiwa msumbwa na mkazi wa Wilaya mpya ya Kaliua na Mama mwenyeji wa tarafa ya Usoke wilaya Urambo akiwa ni wa  kabila la watusi wazawa wa mkoa Tabora. Mwaka 1985 nikiwa na umri wa miaka 10 nilianza elimu ya msingi katika shule ya msingi mapinduzi iliyoko tarafa ya Usoke wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora pamoja na kuanza elimu ya msingi pia nilijiunga na shule ya kiislamu (yaani nilijiunga na shule ya kiislamu (madrasat) kusoma elimu ya kiislamu na hii ilitokana na Baba yangu na Mama yangu kuwa ni waislamu hivyo nilipelekwa katika madrtasa hiyo ili nisome uislam ambao ndio dini ya wazazi wangu na ndugu zangu wote.

 Nikiwa ni mzaliwa wa kwanza kati ya watoto 12 katika tumbo la mama yangu Mwamini Said Ntembela ambapo mimi kwa Baba tumezaliwa watoto 2 mimi na dada yangu Johari Juma Hamis na mimi nikiitwa wakati ule kwa jina la Hamisi Juma Mdaki mama yangu aliachana na Baba yangu shekh Juma Hamisi Mdaki tukiwa tumezaliwa watoto wawili na baada ya kuachana Mama na Baba ambapo ilikuwa mwaka 1979 mimi nikiwa na umri wa miaka minne na dada yangu akiwa na miaka miwili tukaenda kuishi kwao na Mama ambapo ni tarafa ya Usoke wilaya ya Urambo kwani hapo mwanzo tulikuwa tukiishi mwanza na kaliua baada ya kuishi pale usoke mama yangu aliolewa nma mume mwingine ambae anaitwa Shabani bakari amri moja. Waliishi na mume huyo ambapo kisheria alikuwa mume halali kutokana na mafundisho ya dini ya kiislamu kwa kuwa alishapewa taraka, hivyo waliendelea kuzaa watoto ambapo jumla walifika watoto kumi na hivyo kufanya idadi ya watoto wa Mama huyo kufikia 12 na mimi nikiwa mkubwa wa wote.
 Baada ya kuanza Elimu ya dini ya kiislamu sambamba na elimu ya msingi niliitimu elimu ya msingi mwaka 1991 na baada ya kutokuchaguliwa na elimu ya secondary mwaka 1992 nilichukuliwa na Baba yangu Shekh Juma Hamis Mdaki na kunipeleka alipokuwa akiishi yeye ambapo ni kijiji cha Igagala No 3 na kuniandikisha katika shule ya msingi kamusekwa iliyopo kijiji cha Igagala No 2 ili niludie masomo ya elimu ya  msingi ambapo yeye kwa wakati huo alikuwa ni shekh wa msikiti wa Igagala No 3 pamoja na mwalimu wa madrasat ya pale msikitini hivyo na mimi niliendelea na masomo ya elimu ya dini yeye Baba yangu akiwa mwalimu wetu nilisoma kwa mwaka mmoja na kuhamia mjini, wakati huo ikiwa bado ni tarafa hivyo nikiwa kaliua nilijiunga na madrasat ya kiislamu pale kaliua kwa mwalimu mwingine ambae aliitwa shehe Omari mimi na wenzangu tuliendelea na masomo pale mpaka mwaka 1993. Mwaka 1994 niliondoka kwa shekh huyo ambae kwa sasa ni marehemu na kurudi Usoke baada ya kushindikana kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari. baada ya kufika Usoke iliyoko wilaya ya Urambo niliendelea na masomo ya dini ya kiislamu kwa shekh aitwaye Juma Almas mpaka mwaka 1995 nikaondoka kwenda mwanza nikiwa nimeshakuwa mwelewa katika dini yangu ya kiislamu nikaendelea na masomo kwa mashekh mbalimbali akiwemo shekh Juma Hamis Sungusungu ambae alikuwa akitoa darasa na masomo katika msikiti wa Mabatini uliopo katika kota za mapolisi pale Mabatini Mwaza. Mwaka 1999 nilihama Mwanza na kuhamia mkoani Shinyanga wakati huo nilikuwa na miaka 24 nilipofika Shinyanga niliingia katika chuo cha kiislamu kiitwacho MADRASAT NURANIA chini ya mwalimu Masoud na walimu wengine nikaendelea na Uislam nikiwa Muumini mzuri wa imani ya dini ya kiislamu. 
Niliendelea na masomo hapo ambapo chuo hicho kilikuwa katika msikiti wa Ngokolo matope chini ya Imamu alieitwa Maalimu Selfu. Mwaka 2000 niliondoka shinyanga wakati huo nikiwa tayari na uelewa wa kutosha juu ya dini yangu na tayari ninao uwezo wa kufundisha na wengine nilielekea jijini Dar es Salaam na nikiwa Dar nilifikia kurasini kwa Shekh Juma Kassim Ngupepe yeye akiwa mwenye asili ya Rufiji na Mafia nikiwa pale nilijifunza Elimu nya unajimu au Tiba za Kiarabu nikiwa naendelea kuishi hapo na wakati huo nilikuwa na majini ya Uganga ambayo yaliniongoza katika mambo yangu ya kimaisha nilifanya kazi pale kwa shekh huyo kwa muda wa mwaka mmoja nasikuchelewa kuanza kufanya kazi zangu binafsi za uganga wa majini kwani tayari nilishapata baraka toka kwa shekh wangu na ndipo nikafungua na mimi ofisi yangu ya uganga maeneo hayohayo ya kurasini, tiba ya majini na mimi binafsi nilikuwa namiliki majini. 
Mwaka 2002 niliendelea na kazi hiyo huku nikienda kwa mashehe mbalimbali kujiongezea elimu zaidi juu ya majini na tabia zao(yaani elimudunia) watu wengi walikuja kwangu wakati huo nilikuwa nimekwishaoa na kuishi na mwanamke ambaye yeye asili yake alikuwa mkristo maana majini yangu yalinitaka nioe mwanamke ambaye ni mkristo kwa maana kwamba ipo siku na yeye huyo mwanamke atabadili dini na kuwa muislam kama mimi na hayo majini. Baada ya kufanya kazi hiyo ikiwa pamoja na kuwafundisha wengine mwaka 2003 majini yalinitaka niende kwa mganga ili nikajiongezee karama ya kipato wakati huo nikiwa nina mtoto mmoja niliyezaa na mwanamke huyo niliyekuwa ninaishi naye. 
Niliondoka na kuelekea Mwanza na pale nilikutana na rafiki yangu na kunipeleka kwa mganga mkoani Shinyanga maeneo ya Bariadi kijiji cha Bunamalambugani nikakaa kwa mganga kwa miezi mitatu(3) nikapewa majini ya chuma ulete nikarudi Dar, nikiwa Dar ndani ya muda mfupi mambo yalianza kwenda vizuri sana kwani nilitumia chuma ulete kwa kujiongezea kipato nikaweza kununua gari mwaka huo na kupanga nyumba nzuri na ya kisasa nikaachana na kazi ya uganga, chuma ulete niliitumia kwa watu wasio mkubali Yesu pamoja na kuwa walikuwa wakristo (yaani wasiookoka) hivyo ndani ya mwaka mwingine niliweza kujenga nyumba kwetu Tabora na kuishi maisha ya uhakika sikuwa na shida, ila chuma ulete nilipewa sharti nitumie kwa watu walio wakristo tu tena kwa wale ambao hawajaokoka kwani niliambiwa nikitumia kwa wale waliyookoka haitafanya kazi itazidiwa nguvu na walokole maana wao wanauwezo zaidi ya chuma ulete,  basi nilisafiri mikoa mingi hapa nchini na hiyo chuma ulete nikiwachukulia watu fedha bila kunigundua.
 Baada ya mafanikio mganga aliniagiza niende kule kwake, Bariadi ili akanielekeze mambo muhimu wakati ule maisha yangu yalikuwa mazuri sana! kwani niliweza kuwasaidia ndugu zangu, nikiwa kwa mganga mwaka huo wa 2004 mganga akanitaka nimtoe  mwanangu wa kwanza afe (yaani nimtoe sadaka mali iweze kukaa na kutulia) baada ya kusema hivyo mganga mimi nilikataa akanifukuza na baada ya kuondoka kwa mganga huyo mali ziliteketea ikiwa pamoja na magari nyumba na mwisho nikakubali, ila wakati na mpeleka yule mtoto kwa mganga kumtoa sadaka nikakuta mganga amekufa mwaka huo ulikua mwaka 2005,  mwishoni mwaka 2006 nikiwa nimeshafilisika na wakati huo nikiwa na watoto watatu nikalukwa akili ndugu zangu wamenipeleka kwa waganga wengi bila mafanikio mwishowe ndugu wakanitelekeza bila msaada, mke wangu akaenda kwao na mali chache ndugu waliziuza ili kunitibisha kwa waganga bila mafanikio niliendelea kuteseka na nilipokutana na YESU KRISTO kwa kufanyiwa maombi hiyo ilikuwa mwaka 2008 Magomeni kanisa Anglikana,a mbapo siku ya jumanne nilifika pale nikakutana na mtumishi wa Mungu haitwae Henry Ramadhani ambaye alinifanyia maombi nikapona kabisa majini yote yakaondoka, mwaka huo huo 2008 nikabatizwa hapo magomeni Angalikana  na chini ya mchungaji Elisha Tendwa ambapo ilikuwa tarehe 11- 5 -2008 nilibatizwa mimi Hamis Juma Hamisi nakupewa jina la Cosmas Juma Hamis nilisimamiwa ubatizo na huyo mzee Henry Ramadhani ambaye aliniombea nakupona nilibatizwa mimi na wanangu siku hiyo hiyo ambao mmoja anaitwa Suzana Cosmas Juma mwingine Martin Cosmas Juma na yule ambaye alitaka mganga amchukue kichawi ili niendelee kumiliki mali alibatizwa Zanzibar kwa jina la Marrygoreth Cosmas Juma.
 Baada ya ubatizo niliendelea na mafundisho juu ya imani mpya ya kristo nikapata kipaimara kanisa la Angalikani mbezi lous chini ya mchumngaji Paul Mtweve na baada ya kipa imara mzee Ramadhani aliongea na wachungaji ambapo nilipelekwa kwenda kusomea kozi ya utumishi wakanisani chuo cha Anglikana morogoro kiitwacho kwa jina la MOROGORO BIBLE COLLEGE nilisoma mpaka mwaka 2010 baaada ya kumaliza masomo nikaludi Dar, nikiwa Dar nilipangiwa kituo cha kazi kama mwijilisti kanisani, kanisa la Anglikana na Roho Mtakatifu chini ya mchungaji Johnson Lameck ambapo mwaka mmoja nilipata pigo kubwa sana kifamilia la kufiwa nikarudi Tabora, nikiwa Tabora niliendelea kumtumikia mungu ambapo pamoja na ndugu kuwa waislam na, mimi ni Mkristo nimeona njia ya mimi kwenda mbinguni nikimfuata Yesu Kristo yeye ndiye njia, kwa sasa napatikana katika kanisa la Anglikana Kakola Kahama dayosisi ya Tabora nikiwa ndie Mwinjilisti wa kanisa hilo lakini pia ni mwenyekiti wa Kamati ya uinjilisti chini ya mchungaji Israel Baada, lengo langu ni kuendelea na masomo zaidi kwani namshukuru mungu kwa kuisoma elimu ya kiislam kwa miaka 25 hivyo naelewa dini hiyo vilivyo kwanza nikiwa nimeisoma na pia kukulia katika familia ya kisomi ya dini hiyo na wenye kufuata maadili yote kiislam, kiu yangu kwa sasa pamoja nakutumika kwenye makanisa mengi nikifundisha semina mbalimbali, endapo na nitapata mfadhili wa kuniendeleza kimasomo zaidi kwa upande Ukristo nitafurahi zaidi na muda huu ambao niko Kahama Shinyanga nimeendelea kutumika nikiwa na mwinjilisti wa kanisa la Angalikana katika parishi ya Kakola, natumika katika kutoa ushuhuda namna nilivyo zama katika uchawi wa kimajini baada ya kukaa nayo na jinsi ambavyo Babu yangu alivyonilisisha uchawi na namna nilivyo achana na hayo yote na kumupokea yesu kristo, endapo mtu au kanisa au kikundi chochote cha kikristo kikinihitaji kwa ajili ya ushuhuda wa nguvu za Yesu zilizo niokoa mimi na wanangu napatikana kwa

No:-  0789 351 590 ,0714 351 590
au Barua pepe
amostelesphory@gmail.com
Asante Mungu Awabariki sana
Mimi Ev Cosmas Juma
Mwislam niliyeokoka.

CHANZO: MAISHA YA USHINDI BLOG

 

Saturday, January 18, 2014

HUYO NDIYE MUIGIZAJI BRIAN DEACON ALIYEIGIZA KAMA "YESU" NA ANACHOKIFANYA KWA SASA KATIKA MAISHA..!!




                                                                John Honore's photo.  John Honore's photo.
                                     

Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji 


huyo ambaye ni



 mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko 


Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia 


yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni


 nesi. Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo


 alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa


 yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo


 mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.



Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS'' Aliigiza filamu ya


 Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama


 akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa


 waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano


 huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba 


wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael


 walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo 


New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za 


majukwaani na uigizaji. Brian Deacon miaka iliyofuatia baada 


ya kuigiza kama Yesu.Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani


 wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake 


aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama 


yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema


 alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka 


kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza 


jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo


 mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na 


maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla 


hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka 


mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa


 kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake 


kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na


 kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina


 gani.watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian 


Deacon ni mwigizaji mkuu.Katika miezi saba waliyochukua 


kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa 


masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa


 siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake 


kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba


 angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa 


anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na


 kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa


 mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu 


mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati


 anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja


 alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea


 na mapepo yalimtoka mwanamama huyo. Siku nyingine


waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12


 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma


 kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian


 anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze 


nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni


 Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36


 walikubali kurudi kuendelea na kaziAmesema mtihani 


mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 


usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya


 mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau 


kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri


 hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda


 mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema 


usiku.Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom


 Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa


 umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa


 muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo


 lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio


 maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu


 hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya 


kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa


 kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya 


kwanza akaona ni 


kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo


 ya watu. Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza


 majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 


30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na 


watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za


 mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha


 maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo


 ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao


 kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo


 chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari 


imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200


 zikiwa njiani kutafsiriwa. Brian anawaambia watu kwamba


 yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na


 kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema


 ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na


 kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu


 hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya 


filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao


 Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo 


imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya


 watu. kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed &


 Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya 


mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa


 mwaka 1978.