Friday, June 27, 2014

Mahakama nchini Sudan yamuachia huru Mwanamke aliyetakiwa Kunyongwa kwa kosa la Kubadili Dini.


Wakili wake Elshareef Ali, ameambia BBC kuwa mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kuolewa na mwanamume mkristo aliachiliwa huru Jumatatu.
Meriam na mumewe Daniel siku ya harusi yao.
Meriam ameolewa na mwanamume mkristo na alihukumiwa kifo na mahakama ya kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada ya kukata kukana kuwa yeye ni mkristo.

Hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama ya rufaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna.

Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.

'Hamu kumuona mkewe'
Mumewe Meriam Daniel Wani, alisema kuwa ana hamu sana kumuona mkewe kwani taarifa hiyo ilitolewa bila yeye mwenyewe kuitarajia.

Ameambia BBC kuwa anataka familia yake kuondoka nchini Sudan haraka iwezekanavyo.
Mume wa Meriam Daniel Wani akiwa amewapakata watoto wake, mdogo kushoto alizaliwa gerezani hivi karibuni.
Wanandoa hao walioana kanisani baada ya kukutana mwaka 2011.
Hukumu ya kifo dhidi ya Meriam Yahia Ibrahim Ishag, ambaye alijifungulia gerezani, ilisababisha gadhabu sana hadi katika ulingo wa kimataifa.

"Tuna furaha sana kuhusu hatua hii ya serikalli na tunaelekea sasa kumchukua,'' alisema wakili wa Bi Meriam Elshareef Ali.
Bwana Ali alisema kuwa Bi Meriam alionyesha ujasiri mkubwa sana wakati huu wa masaibu yaliyomkumba.

''Ni ushindi kwa uhuru wa dini na imani, tunaamini kuwa katika siku za usoni hakuna mtu atakayelazimika kupitia masaibu kama yaliyomkumba Meriam,'' alisema wakili wake.

Babake Meriam alikuwa muisilamu ingawa mamake alikuwa mkristo na Meriam akaamua kuolewa na mwanamume mkristo.
Amekuwa gerezani tangu mwezi Februari pamoja na mwanawe mdogo.

Hata hivyo bwana Ali alisema kuwa hajaona hukumu ya mahakama ya rufaa na kwamba alipokea taarifa hizo kupitia kwa vyombo vya habari. BBC Swahili imeripoti.

ROSE MUHANDO KUZINDUA ALBAMU YAKE YA FACEBOOK AUGUST 3/2014 JIJINI DAR.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLVwiVzZK8sRYGobNzbXyWGg6qeZLT3nNvG287nVZXxh-2bPyrrskMamzOYMmTT1oc2j1hjtlNdEY5DWspmYtCG0Vc_Wvg5r4prmtRhcJyoQ0CgDSHayypBxfpIey9Mu1jCRxorSpoYXo/s640/ROSE.jpg
Rose Muhando ndani ya Wololo ambao pia ni wimbo mpya.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee leo wakati alipokua akitangaza Uzinduzi mkubwa wa Albam ya Shikilia Pindo maarufu ka FACEBOOK ya mwimbaji wa muziki wa injili anayevuma, Rose Muhando utakaofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Agosti 3 /2014 jijini Dar es salaam, ambapo amesema baadhi ya mapato yatakwenda kuviwezesha mitaji zaidi ya vituo 10 vya watoto yatima jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua zaidi kwa Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi huo unaoatarajiwa kuwa mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa waimbaji wa muziki wa injili.

Monday, June 23, 2014

SONG: Mateso Sita


TAMASHA LA UIMBAJI NDANI YA FPCT MOROGORO LA FANA

Ilikuwa ni jumapili ya Tarehe 22 mwez wa 6 katika ukumbi wa kanisa la FPCT Morogoro ambapo tamasha kubwa la uimbaji lilifanyika likishirikisha kwaya na vikundi binafsi vya uimbaji.

Habari njema katika tamasha hilo ilikuwa taarifa rasmi ya uwepo wa tamasha kubwa mwezi wa nane litakalo ongozwa na waimbaji wakubwa Afrika Mashariki akiwemo Sarah K na Solomon Mkubwa.

Baadhi ya picha za Tamasha ni hizi zifuatazo,




 Mtumishi wa Mungu Mwita akitawala jukwaa
 Kwaya ya KKKT Majengo (Kihonda)
Chotlda Mathias akimuimbia Mungu ndani ya ukumbi wa FPCT Morogoro

BEN PAUL AKILI YESU NDIO MPENZI WAKE WA KARIBU WAKIFANYA USHIRIKIANO PACHA NA PAUL CLEMENT


Hii ilikuwa katika tamasha kubwa la LIVE RECORDING iliyo fanywa katika kanisa la VCCT. Kama hukuhudhulia na ulishawahi kuzisikia sauti za hawa watu katika kazi tofauti tofauti basi utakuwa umepata picha japo kidogo. NANI AJUAE PENGINE HII NI MBEGU SAFI ILIYO PANDWA NA PAUL CLEMENT KWA BEN PAUL,



MUNGU YU MWEMA, HONGERA PAUL CLEMENT

Saturday, June 21, 2014

KUPANDISHA MAPEPO KWA MFANYA HAFSA KAZINJA KUBADILI DINI.

Hafsa Kazinja anayetamba na Wimbo wa Mlala Nje huku video yake ikiwa tayari, ameamua kuikacha dini yake ya Kiislam na kuhamia kwenye Ukristo.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Hafsa alisema alifikia uamuzi huo baada ya kusumbuliwa na maruhani ambayo yalimfanya arukwe na akili.


Mwanamuziki Hafsa Kazinja.

“Niliumwa sana hadi ikaonekana nimerukwa na akili, maruhani ndiyo yaliyokuwa yananisumbua. Kuna kipindi yalikuwa yakiniambia nisile samaki wala dagaa, mara yakaniambia natakiwa kuwa mganga.

“Njia zote ziligonga mwamba, nikaambiwa nisali na nimuachie Mungu, nikawa nikisali sauti zinanijia nimtukane Mungu tena matusi makubwa, nimeenda hadi kwa waganga, mashehe na walokole wakaniombea na nikapoteza pesa nyingi hadi nikauza nyumba yangu na magari lakini wapi. Nimekwenda Kanisa la Zoe ndiyo nimepona, namshukuru Mungu.
“Sasa nimeamua kuwa Mkristo, yaani nimebadili dini kwa kumaanisha, nampenda Mungu katika roho na kweli. Sijabatizwa hivyo bado sijabadili jina ila nasali Kanisa la Zoe lililopo Segerea jijini Dar.”