SABATO KWA WALOKOLE ? NDIYO
YALIYOMO;- 1.UTANGULIZI 2.SABATO NI LAZIMA 3.HITIMISHO
LENGO LA FUNDISHO
- Kuonyesha ulazima wa sabato kwa kila mtu
anayemwamini Yesu.
ANDIKO KUU:- Waebrania 4:1 “Basi ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia
katika raha, na tuogope mmoja wenu asije akaonekana ameikosa”
1.UTANGULIZI
- Sabato ni siku ya saba, ambayo ni Jumamosi.ni siku
ya raha.
- Mungu anataka kila mwanadamu aishi sabato, ni
lazima na milele.
- Makuhani, manabii, wafalme, mitume 12 na Waizraeli
wote walishika sabato kwa uaminifu mpaka leo
- Kumekuwa na dini nyingi sana
miaka hii, makanisa mengi, huduma nyingi, Imani mbalimbali, wana-theolojia
wengi,shule za Biblia zimekuwa nyingi, makongamano, mikutano na semina nyingi sana. Lakini makundi yote
haya yanatakiwa yaingie Sabatoni, ni MUHIMU.
2.SABATO NI LAZIMA
► Sabato ni zaidi ya siku, ni zaidi ya
kupumzika nyumbani, ni zaidi ya kwenda kanisani. Sabato inamaana nyingine ya
muhimu zaidi kuliko zote. ISAYA 58:13
A) NANI MWANZILISHI WA SABATO ?
- Mungu ndiye muanzilishi wa Sabato, sio Waisraeli
wala Wasabato, Mungu anajali sabato kuliko zaka, au matoleo yoyote unayoyajua,
sabato ni sehemu 1 kati ya 7 lakini zaka ni sehemu 1 kati ya 10. Sabato ni amri
ya 4 lakini zaka na sadaka hazimo kwenye amri. KUMB TORATI 5:12
- Mambo mawili ambayo Mungu aliyafanya siku ya 7 – a) Kupumzika kuumba mambo
yanayoonekana(ulimwengu wa mwili) – MWANZO
2:1 na b) Kuanza kufanya kazi ya kuumba mambo ya rohoni(ulimwengu wa kiroho) au
Edeni – MWANZO 2:8. Yote haya yalitokea
katika siku moja,ya sabato, kupumzika na kufanya kazi tena.Iliitwa sabato ya
Bwana – TORATI 5:14, lawi 25:4
- Nakubaliana na sayansi inayosema Dunia ina umri wa
miaka bilioni 13.7, kila siku moja katika uumbaji iliwakilisha jumla ya miaka
kadhaa – ZABURI
90:4, kwa mujibu wangu, mpaka mwaka huu 2013 upo ndani ya ile siku ya 7 ya
uumbaji – MWANZO
2:2-3. Huu ni mtazamo wangu tu.
B) SABATO ILIMAANISHA NINI KABLA YA YESU ?
- Wana wa Israeli ndio warithi hasa wa kushika sabato
ambayo Mungu aliianzisha kisha akamfundisha Adamu na Eva,ingawa sabato kabla ya
Dhambi(anguko)na baada ya Dhambi kuingia Duniani ni tofauti lakini Mungu
alitaka ishikwe – KUTOKA
20:8. Kuingia sabato na kushika sabato ni tofauti, wao walishika.
► Sabato ya Adam na Eva kabla ya anguko
---- Adamu hakushika sabato, aliishi sabato, Siku zote ilikuwa ni sabato,hakuna
ibada wala siku ya ibada, hakuna hekalu, hakuna makuhani, hakuna sheria wala
torati, Mungu akaona kila kitu ni chema – MWANZO
1:31. Adam alichotakiwa ni kuitunza tu bustani – MWANZO
2:15.
► Sabato baada ya Dhambi
kuingia(anguko) ---- Sabato ikawa na dosari, badala ya kuishi kisabato
wakatakiwa kuishika sabato – TORAT
5:15e. Dhumuni likageuka badala ya kufurahia Edeni na uumbaji wote ikawa
kufanya Upatanisho – WALAWI
16:31, ikamlazimu Mungu asipumzike tena, Mungu akaweka makuhani, sheria, hekalu,
torati na kafara ambayo hayakuwa na umuhimu wowote.- WAEBRANI 8:5, 10:1, KUTOKA
25:40.
- Ukisoma vizuri kuhusu sabato utagundua kuna mambo
mawili kulwa na doto ambayo mara zote yalijitokeza wakati wa sabato, cha ajabu
haya mambo mawili yapo kinyume kabisa – WALAWI
23:32;–
1.
Kujitesa nafsi 2. Kustarehe
Mungu alitaka Waisraeli wajifunze nini ?,
1.Kujitesa nafsi -=- kwamba wajitese
nafsi zao kwasababu waliasi,wakapoteza haki zao za kumiliki bustani ya Edeni(ulimwengu
wa kiroho). Kwahiyo Mungu na Mwanadamu wote walikuwa wakiiharifu sabato – MATHAYO 12:5, ambapo sii sahihi. Hivi
unajua kuwa kusamehe dhambi na kusamehewa dhambi ni kazi kubwa ?
2.Kustarehe -=- Kwamba wajifurahishe, lakini furaha hii
haikuwa halisi ilikuwa ni kwa ajili ya kuwakumbusha mambo mawili; kuwa kabla ya
Dhambi maisha yalikuwa ya pumziko, na pia baada ya Yesu kutakuwa na pumziko – MATHAYO 11:28
- Siku ya sabato waisraeli walitakiwa kutembea
umbali wa mtupo wa jiwe, maana yake kazi wangefanya kidogo sana lakini matokeo
yangekuwa makubwa sana, ni kama teknologia
inavyofanya kazi wakati huu.
C) SABATO ILIKUWAJE WAKATI NA BAADA YA YESU ?
- Msomaji wangu naomba ujue kwamba KIPINDI cha BAADA
ya anguko na KABLA ya Yesu mambo mengi sana hayakuwa halisi, Mungu aliichagua
Israeli, makuhani,hekalu na Torati kutunza kumbukumbu, lakini hayakuwa na uhalisia(kivuli).EBRANIA
8:5
- Yesu hakuwa na tatizo na kushika sabato kwa
waisraeli, wala makuhani,wala torati, wala hekalu. Bifu la Yesu na hawa jamaa
ilikuwa ni UFAHAMU wao kuhusu sabato,ukuhani, hekalu na torati. Hawakujua
kwanini Mungu aliamua achague siku moja(Jumamosi) iwe siku ya sabato.- MATHAYO
12:1-8, 23:16-22, LUKA 6:6-11
- Hata mitume nao hawakuwa na shida juu ya siku ya
sabato, walishajua dhumuni la sabato. Ngoja nikupe huu mfano, chungu cha udongo
kina almasi zimejaa ndani, kipi cha muhimu hapo, chungu au kilichopo ndani ya
chungu ? Ndio utofauti wa Yesu na wayahudi.- MDO 13:42-44
- Yesu anapojiita Bwana wa sabato haimaanishi kuwa
yeye ndiye anayejali sana
kushika sabato, hapana, alimaanisha kuwa yeye ndiye anaeishi kisabato kwa
usahihi. Kabla ya Yesu hakuna aliyeshika sabato 100% - YOHANA 5:30, LUKA 6:12
D) SABATO IWEJE NYAKATI ZETU ?
- Ili uelewe sabato
nyakati zetu, turejee madhumuni mawili ya sabato ;- 1.Kujitesa;- Yesu ameshateswa, dhambi zote
zimefutwa – ISAYA
53:11a.
2. Kustarehe –tunatakiwa kuiishi sabato kama kabla ya anguko. Kwa kuishi kisabato tunautangazia
ulimwengu kuwa kuna sabato tutakayoiishi milele inakuja. – WAEBRANIA 4:11
- Sabato ni kutumia mambo ya kiroho kuendesha mambo
ya mwilini – 1 KORIN 2:14, sabato ni kuwa na vipawa na
karama za Roho Mtakatifu – RUMI 8:14.
Sabato ni kupumzika kutumia mwili na kuanza kutumia Roho Mt.
Sabato ni kusikiliza kila siku, kutii kila siku na kutenda kila siku- MATHAYO
7:24
E) JE, UPO TAYARI KUISHI KISABATO ?
- Sabato ni lazima hapa Duniani kwa mlokole na Mroma
na Muislamu na Wanaojiita wasabato. Kama umechoka kuonewa na kuwa omba-omba,
ingia kwenye sabato, kama unafurahia haya
maisha sabato haina hajakwako – MATHAYO
7:13
- Walokole wote ambao hawatembei katika mtembeo wa
Roho mt, namaanisha wasiokuwa na vipawa na karama za Roho mt hawapo katika
sabato, bado wanahangaika na kushika sabato. Ikumbukwe kuwa sabato ni lazima.
Kwa hali hii, ni afadhali ya msabato anayeshika siku kuliko mlokole asiyekuwa
rohoni ingawa wote wawili wameingia chaka - MATH 7:16
- Wasabato wote ambao hawana Roho Mt, na karama na
vipawa, hawapo katika sabato na hawastahili kuitwa wasabato, mbaya zaidi
wanamhuzunisha Roho Mt – EFESO
4:30. Chochote kinachofanyika kanisa lolote bila Roho Mt ni kumdharau Roho Mt.YOHANA
15:5
F) UTAMJUAJE MSABATO HALISI ?
- Kila mwanadamu anaejali maisha ni lazima awe
msabato(sio mjumamosi). Kumjua msabato halisi ni rahisi sana, anatoa unabii,
anafanya miujiza na uponyaji na ishara,anapambanua roho, anatafsiri na kunena
kwa lugha, anafichua mambo ya siri(hekima, maarifa), ana imani ya yasiyowezekana,
anaona maono, anaisikia sauti ya Mungu, anaweza kufukuza mapepo, anafufua wafu…. Nk – MDO 1:8,
10:38, 1KORIN 12:8, ISAYA 11:2-3
- Acha kutumia nguvu za kimwili, badala yake pumzika
mwilini harafu fanya kazi ya nguvu rohoni, sabato ni kupumzika mwilini na
kufanya kazi nzito rohoni – EFESO
6:12. Wafuatao ni watu ambao wamejaribu kuonyesha maisha ya kisabato ;- TB
JOSHUA, EUBERT ANGEL, PASTOR CHRISS, BENNY HINNY, IDAHOSA, MAKANDIWA, BOATENG,
KAKOBE, GWAJIMA, MALISA, KULOLA, COVENANT,KATHRINE, ORAL ROBERT, YONG CHO, OYEDEPO,
n.k. Hawa jamaa ndio wasabato na kila mkristo alitakiwa awe kama mmojawapo wa
hawa ndugu.- MDO 8:29,39, 7:55
- Kwakifupi msabato halisi ni yule anaeishi maisha
ya kiroho na kimwili kama ya Yesu au zaidi ya
Yesu. Yesu ni mfano wa mtu anayetaka kuwa Msabato. Yesu hakuna alichokuwa
anabuni katika huduma yake, mambo yote alielekezwa, naye alikuwa muaminifu
kutekeleza. Hiyo ndio sabato, alisikia , alitii, alifanya, hii ndiyo sabato.-
YOHANA 14:10b
G. ITAKUWAJE NISIPOINGIA SABATO ?
- Kabla sijajibu swali labda niseme kwamba
anayefaidika hasa na sabato ni mwanadamu, kutokuingia sabato hakutakuzuia
kwenda mbinguni, kwahiyo mbinguni utaingia hata kama
haujaingia sabato hapa Duniani.
-Usipoingia sabato utaishi maisha ya misuri, utakula
kwa jasho, ardhi itakuwa imelaaniwa kwako,utatawaliwa, tama yako itakuwa kwa
mwingine, shambani kwako miba itamea, lakini mbinguni utaingia. Uchaguzi ni
wako – MWANZO 3:16-18, utakuwa kama mwana mpotevu –LUKA 15:15-19
- Ipo sabato kuu naya milele inakuja, lakini kipindi
hiki tumeruhusiwa kuonja utamu wa sabato inayokuja ya milele – LUKA 11:2, utakuwa mjinga usipoonja,
lakini ukishindwa, subiri ile inayokuja, lakini kubali kuishi hapa Duniani kwa
Jasho. Usiwaseme vibaya walio elewa sabato – LUKA 11:20-22,
MATHAYO 6:9d, UFUNUO 21:1-2
3.HITIMISHO
- Kuwa msabato ni lazima, kama
unataka kuwa msabato tekeleza mambo haya mawili kikamili;- a) Amini Injili kwa
usahihi, b) Jazwa Roho Mt kikamilifu.
- Haya mambo mawili yamewashinda wasabato na
walokole wengi. Mpaka sasa wachawi na waganga ndio wanao furahia sabato, sio
wakristo. Mchawi kuingia rohoni ni rahisi lakini mlokole kasheshe, hii ni
kuonyesha wachawi ndio wasabato wazuri.
………..Remember…………THE BEST HAS COMES………………
MBONA HAPO KWENYE G, sehemu ya kwanza haujaweka aya umeweka maneno matupu? HAPO NAPO WEKA AYA inayo elezea hicho ulichoWEKA
ReplyDelete