Thursday, October 31, 2013

SIRI



HII NI SIRI
By Apostle Eliya


YALIYOMO

1. UTANGULIZI

2. SIRI

3. HITIMISHO



LENGO LA SOMO

- Kufunua Siri iliyofichika

-Kuonyesha umuhimu wa kubadili vipaumbele vyetu





ANDIKO KUU ;- KOLOSAI 1:26 “Siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote,bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake”



1.UTANGULIZI


-Ninapoangalia mimea, wanyama, sayari, mazingira na ulimwengu kwaujumla ninagundua kwa hakika kuna kitu kinapungua, kuna siri imejificha.



-Hapa ninapoandika haya mafundisho kuna siri nyingi zimenizunguka, hata hapo unaposoma haya mafundisho ya Apostle Eliya, kuna siri nyingi zimekuzunguka. Hapo ulipo unaweza kuingia katika Bustani ya Edeni ambayo Adam na Hawa walifukuzwa miaka 6000 iliyopita. Sasa twende wote tukagundue hii siri……..



2. SIRI


- Najua watu wengi hawajui kilichotokea katika bustani ya Edeni wakati wa Adam na Hawa, wana Theolojia wamejaribu kutengenezea somo ailimradi watengeneze mtaala, lakini wameshindwa kufunua siri iliyokuwa imejificha. Hata hivyo Theolojia sii ya Muhimu sana. Asili ya Biblia ni Rohoni, ukiingia rohoni utaigundua, kwahiyo hatuwategemei wana theolojia kutuchambulia kila kitu, Hapana.—2 Petro 1:21



a).Bustani ya Edeni – NWANZO 2:8-9


- Bustani ya Edeni ni bustani ambayo ndani yake kulikuwa na bustani nyingine ndogo.



- Kinachofanya wapendwa wengi wasielewe hizi sura za mwanzo kwasababu hizi sura za mwanzo zinachanganya matukio ya kimwili na kiroho. Mungu aliumba Dunia na vitu vyote kwa siku sita, siku ya saba akapumzika, cha ajabu siku hii ya pumnziko ndo aliamua apande bustani. Hii bustani ilikuwa niya kiroho na vyote vilivyochipushwa vilikuwa ni alama za rohoni.



- Kitu cha muhimu katika hadithi ya Bustani ya Edeni ni miti iliyokuwa imepandwa, kulikuwa na miti mitatu ; 1. Mti unaotamanika kwa macho na unaofaa kuliwa, 2. Mti wa uzima na 3.Mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Miti hii mitatu pamoja na matunda yake yote niya kiroho. Mungu aliwaambie matunda ya mti wa kwanza na wapili wanaruhusiwa kula ila matunda ya mti wa tatu hawakuruhusiwa kula.



-Mti wa Kwanza ni Roho Mtakatifu, na mti wa pili ni Yesu na mti wa tatu Shetani. Hii bustani ambayo ni mbingu ya pili tulipewa wanadamu kuimiliki, kwahiyo Dunia pamoja na mbingu ya pili(ulimwengu wa kiroho) ilikuwa ni mali ya Adam na Hawa, kwa kule kuasi kwao wakapoteza haki ya kumiliki ulimwengu wa kiroho pamoja na huu ulimwengu, vyote vikawa chini ya Shetani, lakini ile bustani ndogo ndani ya Edeni haikuwa chini ya Shetani kwasababu ilifungwa, ingawa ipo ndani ya Edeni.



b).Adam na Hawa


- Waliumbwa katika ulimwengu huu wa mwili – Mwanzo 2:7

Pumnzi aliwapulizia ilikuwa ni Uhai(uwepo wa Mungu), namaanisha Roho Mt,hii Roho ilitoka baada ya uasi na ilirudi rasmi wakati wa Yesu—Yohana 20:22, ndio maana waliweza kuwekwa katika ulimwengu wa kiroho(Edeni), shetani alimuingia nyoka akamdanganya Hawa na hatimaye Adam akashawishika. Matokeo walifukuzwa nnje toka Bustani ya ndani ya Edeni, na pia walifukuzwa ndani ya Edeni, yale makalipio aliyoyatoa Mungu yalikuwa katika ulimwengu wa kimwili. Mwanzo 3:16-19



-Kwanini walifukuzwa ?

Tayari walishafanya Dhambi kilichotakiwa kufuata ni kutubu na mwisho kula matunda ya ile miti miwili, lakini hiyo toba haikutakiwa ifanyike kwa mdomo, hapana, lilitakiwa jambo lifanyike katika ulimwengu wa kimwili, lazima damu imwagike. Sasa mwanadamu hakujua kuwa amefanya kosa ambalo lina GHARAMA NYINGI na KUBWA za kulipa. Unadhani walikula vipi tunda ?



c).Kurudi Tena katika Bustani ya Edeni.


- Kikwazo cha Adam na Hawa cha kutokuruhusiwa kuingia tena katika Bustani ya Edeni ni Dhambi ambayo malipo yake hakuna mwanadamu ambaye angeweza kulipa, sasa Yesu ameshalipa, nini kilichobaki ? Kumbe hapo ulipo unaweza kuingia tena katika Bustani ya Edeni, najua huwezi kuamini lakini kile kikwazo kimeondolewa. Kuingia tena katika ulimwengu wa kiroho ni haki yako, hapo ulipo upo karibu sana na Bustani ya Edeni, tatizo ni nini ? umefumbwa macho – Efeso 1:18



d).Umuhimu wa Kuingia Bustani ya Edeni.


- Siri za kila mwanadamu unaweza ukazigundua kama utaingia bustani ya Edeni, manabii wote Mungu aliwapa neema ya kuingia katika ulimwengu wa kiroho bila wale Malaika walinzi kuwasumbua – Ezekieli 37:1-2. Henoki alitumia Muda wake mwingi kuwa katika Bustani ya Edeni ndio maana Mungu akamwambia baki hukuhuku—Mwa 5:24, vipi kuhusu Nabii Eliya Mtishibi ?—2 Wafalme 2:11, wote hawa wapo katika Edeni wanakula good-time. Mtume Paulo aliweza kuperuzi ulimwengu wa kiroho, Stefano wakati wanampiga mawe aliweza kuperuzi ulimwengu wa kiroho – Mdo 7:55, Yesu aliwaambia wananfunzi wake nilimuona shetani akianguka toka juu, wewe unadhani Yesu alimuonaje shetani pasipokuwa alikuwa katika ulimwengu wa kiroho ? Watu wengi unaowasoma katika Biblia waliweza kuingia katika ulimwengu wa kiroho na kurudi katika ulimwengu wa kimwili, nikama vile kufumba na kufumbua macho.—Marko 9:4



-  Huu ulimwengu tunaouishi, haukutengenezwa ilitujifunze mambo yaliyomo, HAPANA, tulipaswa kuwa tunajua mambo yote bila kufundishwa kwasababu siri zote zimefichwa katika Edeni. Ndiyo maana mimi nasema huu mpango wa shule sio kwa ajili yakukuelimisha, bali kukupotezea muda ili usijue unapotakiwa kuwepo. Huu ulimwengu na mambo yote yaliyomo ni rahisi kuyafahamu ukiwa rohoni, lakini ukiwa mwilini itakughalimu sana, kwasababu haukutengenezwa kwa mtu wa mwilini, ndio maana uchunguzi mmoja wa kisayansi unaweza ukachukua muda mwingi na mapesa mengi. Ngoja nikuulize, mfalme dawa ya kumtibu mfalme Hezekia, nabii Isaya aliisomea wapi ?



-Ngoja nikushitue kidogo ; Wanasayansi wanasema kipenyo cha Ulimwengu ni Maili 93 bilioni, ukipita katikati ya hiki kipenyo kwa mwendo kasi wa mwanga itakuchukua miaka 28 Bilioni kumaliza kipenyo cha ulimwengu, unajifunza nini hapa? Kama umefunguka kimawazo utagundua mambo yanayoendelea ulimwenguni ni juu ya akili za asili za mwanadamu wa kawaida. Kila mbegu unayoiona imetengenezwa kwa namna ya ajabu na huwezi kugundua kwa macho yako viwango wa kabohaidreti, protini, fati na nguvu iliyomo ndani ya kila mbegu, na kuichunguza mbegu moja inaweza ikakugharimu muda na gharama,sasa kuna mbegu mabilioni. Vipepeo unaowaona wapo aina chungu nzima, hujaingia kwenye miti na matunda pamoja na elimu ya unajimu. Ngoja nikwambie, kuna Galaksi Mabilioni katika huu ulimwengu wetu, kila galaksi ina nyota karibia Bilioni 100. Hii Dunia yetu ikiingizwa ndani ya jua, zitatakiwa Dunia karibia Milioni moja ili upate ukubwa wa Jua, umbali wa kutoka hapo ulipokaa mpaka kwenye  Jua ni mabilioni ya maili. Kwavipimo hivi, nani aliumbiwa huu ulimwengu ? hata akili zetu haziwezi kufikiri ? ndomaana nikasema kuna siri imefichika.



- Waulimwengu


Waulimwengu ni watumishi wa shetani wanaofanyakazi kwa jina la serikali, makampuni, viwanda, taasisi, mashirika. Amini au usiamini shetani anajua ule uwezo ambao Mungu alituumbia na tukaaupoteza na kisha akaturudishia tena, hataki tutambue haya mambo ndiomaana anajaribu kutupotezea muda kwa mtindo wa AJIRA, ajira ni kifungo kimojawapo kizuri sana, Mchakato wa elimu pamoja na mitaala yake pia ni kifungo. Daktari mmoja alisema alichukua miaka 40 kumchunguza nyani,hebu ona !! huku sinikupoteza muda !!, haya ndio madhara tunayoyapata kwa ile dhambi ya asili na kukataa kuingia katika bustani ya Edeni. Fanya urudi Bustanini. Ndio maana ukisoma Biblia vizuri hukuti hata sehemu moja Mungu akiwaambie Waizraeli sumbukieni maisha, anajua nini tulichokipoteza na hakirudi kwa kufanya majaribio mengi ya kisayansi, siku zote aliwaambia mkitii mtakuwa watu bora Duniani. Tatizo liko rohoni.—TORAT 7:14



e).Mapepo katika ulimwengu wa kiroho.


-Malaika walioasi wote walitupwa kuzimu, lakini muhura wao bado haujafika wa kufungwa kwahiyo wanatumia muda mwingi kuwa katika ulimwengu wetu na ule tulioupoteza wa kiroho, mipango mingi hupangwa huko, wala hatuoni ndio maana wanatutesa. Kama tungekuwa na uwezo wa kurudi Bustanini, tungeweza kufukuzana nao na kuwakamata na kuwapiga kwasababu mwendokasi wao sio mkali ukilinganisha na mwendokasi wetu wa mawazo, kama roho zetu zingeweza kuingia ulimwengu wa kiroho tungeweza kutoka sayari moja na kwenda nyingine kwa sekunde, kama Pepo limejificha nyuma ya sayari ya Pluto ningeweza kwenda mara moja na kumkamata na kumtupa kuzimu tena. Kumbuka Edeni alipewa Mwanadamu sio Shetani.



-Kwakweli tulipoteza kitu cha muhimu sana, macho yetu ya kiroho yalifungwa. Mpaka muda huu ninaoongea wanadamu hawajui umuhimu wa kurudi tena katika Bustani ya Edeni, tumeshazoelea shida, ndio maana hatuogopi kufanya dhambi, kumbe kila dhambi tunayoifanya inatufumba macho ya kiroho, watoto wadogo wanahuo uwezo kuingia katika Bustani nzuri ya Edeni lakini anapokuwa na kuanza kufanya dhambi macho yake yanafumbwa, maana yake anafukuzwa katika bustani,sasa kurudi tena nikasheshe.



3.HITIMISHO


-Kama hujakubaliana na mimi, fanya uchunguzi wa kila kitu duniani, kama utashindwa haimaanishi wewe huna akili au muda wako wa maisha ni mafupi, HAPANA, badala yak e nikwamba ulimwengu huu wa mwili uliumbwa kwa ajili ya mtu wa kiroho. Ugumu upo kwasababu tunataka tuugundue kwa namna ya kimwili.



-Vitabu vya siri za huu ulimwengu viliachwa katika bustani ya Edeni, tafadhari turudi tukasome tufurahie maisha. Lakini, tutaingiaje Bustanini wakati kuna Malaika walinzi ?—Mwanzo 3:24.





……………….….THE BEST HAS COME…………………

No comments:

Post a Comment