Thursday, November 21, 2013

FAHAMU KWA SEHEMU KUHUSU MAISHA YA BEATRICE WILLIAM WA BSS

                Beatrice akiimba baada ya kuokoka.

          Ilikuwa Ijumaa ya Tarehe 15/11/2013 nikiwa Vijibweni Soweto(Kigamboni) kwenye mkutano niliokuwa nimealikwa na rafiki yangu Peter Michael ambae ni Blogger wa Maisha ya ushindi. Muhubiri katika mkutano huo alikuwa ni Cosmas Chidumle. Akili yangu ilikuwa na shauku ya kumuona Mtumishi wa Mungu Cosmas Chidumle hasa kutokana na historia yake ya mziki hapa Tanzania.

        Nilifika mapema kabla ya mkutano kuanza pia nilimuwahi mwenyeji wangu Peter Michael, nikiwa nimekaa kwenye viti ghafla nikamuona binti ambae akili yangu ilianza kumpambanua ni nani kwasababu ilikuwa kama namfahamu vile ila ilinipa tabu kidogo kumkumbuka. Nilipo ona picha haiji nikaamua kumpotezea, mpaka muongozaji wa ibada alipo simama akasema "Namkaribisha dada Beatrice William aje aimbe nyimbo mbili" watu wakaanza kushangilia bado nikapotezea. Nikasikia "naitwa Beatrice William wengi wananijua kwa jina la Beatrice wa BSS, Sasa sisaki mahela namsaka Yesu" Akili yangu ikafunguka na mdomo wangu ukasema ANHAAA.

Beatrice William akiwa na Robert Maziku(Mwandishi wa Makala hii).

      Namshukuru Mungu nimefanikiwa kutimiza ahadi niliyowaahidi wasomaji wetu wa Blog ya Injili Forever ambapo niliwaambia nitawaletea mahojiano. Mahojiano haya yamefanywa Tar 20 na 21 mwezi wa kumi na moja 2013. 

FATILIA HAPA SASA,
Robert Maziku(RM): Bwana yesu asifiwe dada.
Beatrice William(BW): Amen Habar yako?
RM: Nzuri unaongea na Robert wa Blog.
BW: Ok. Niambie,
RM: Samahani dada, Nataka kujua baadhi ya mambo ambayo watu wakiyafaham kuhusu wewe yataleta chachu nakuwa sehemu ya Injili.
                      

                                  Beatrice kabla hajaokoka

BW: Haina shida, (kwa sauti ya kukaribisha mazungumzo).
RM: Kwanza kabisa majina yako ninani na mwenyeji wa wapi?
BW: Majina yangu ni Beatrice William, ni Mhaya ingawa nimekulia Mwanza.
RM: Unamiaka mingapi?
BW: Nilizaliwa miaka 32 iliyopita, ni mtoto wa nne kati ya watoto wanne kwahio ni mtoto wa   mwisho.
RM: Inasemekana umeolewa na unawatoto?
BW: Niliolewa miaka 13 iliyopita ila kwasasa sipo kwenye mahusiano kwa muda wa miaka minne unaelekea mwaka watano sasa. Hata wakati nashiriki Bongo star search sikutoka kwa mume. Mimi ninawatoto watatu wa kwanza anamiaka kumi na tatu(13), wapili kumi na moja(11) mdogo anamiaka nane 8.
RM: Ulianza lini kuvaa mavazi ya kiume?
BW: Nilipo maliza shule tu sketi nikaachana nazo sikupenda kabisa sketi.
RM: Kwanini ulipenda hayo mavazi?
BW: Kwakweli ilikuwa nikivaa hayo mavazi najisikia ninaujasiri wa ajabu sana.
RM: Mambo gani ambayo uliyafanya kabla ya kuokoka hautayasahau?
BW: Aisee ni mengi mno, unajua mimi nilikuwa mbabe sana nilishawahi kuchapwa viboko na sungusungu kule Mwanza kama mara mbili hadhalani sababu ya utukutu. Kwamfano nilishawahi kumchana mtu na viwembe mgongoni mpaka mgongo ukatapakaa damu, nimecheza sana kamali,           kunasiku nilikamatwa na watu wa usalama usiku saa tisa natembea kwa vile mavazi yangu yalikuwa yanaonesha ni mwanaume walinipiga sana maana nilivaa pia kofia. Wamekuja kunifunua baadae ndio wanajua alaa kumbe ni binti!!
RM: Ulishawahi kuvuta Bangi??
BW: Hapana mimi nilikuwa mlevi sana.
RM: Kwaneno moja unaweza kutuambia YESU ni nani kwako?
BW: YESU NI KILA KITU.
RM: Kwanini ni kila kitu?
BW: Kwasabau Beatrice aliyeshindwa kubadilishwa na mtu yeyote hata Sungu sungu walishindwa mpaka nikawa sieleweki kama ni mwanaume au mwanamke sasa watu wananielewa ni jinsia gani Yesu ameweza kunibadilisha kwahio ni KILA KITU.
RM:Kwanini uliokoka?
BW: Ilitokea tu, ilikuwa tar 16/03/2012 ndipo niliokoka. Kabla ya kuokoka nilikuwa nimekaa miaka  kama kumi na sita(16) bila kusali popote. Siku hiyo nilikosa amani sana nikawa natafuta msaada   kutoka kwa Mtumishi (Mchungaji) yeyote aniombee niokoke basi ndio nikafanikiwa kupata   namba ya Mama(Mchungaji Rwakatale)akaniombea.

RM: Kunautofauti gani kabla na baada ya kuokoka?
BW: Utofauti upo ikiwemo sasa naeleweka mimi ni jinsia gani, nirahisi hata kuelekeza kuwa yule ni mwanamke.
RM: Unafanya huduma gani kanisani nje ya uimbaji?
BW: Huwa nahubiri kidogo kabla ya kuimba.

Beatrice Akimuombea mtoto aliyekuwa na mapepo(Mchunguze vizuri huyo mtoto utagundua alikuwa ameanguka chini).

RM: Hausikii kama una Uinjilisti ndani yako?
BW: Hio nikweli huwa nasikia pia hata watu wananiambia kuhusu hicho naamini muda ukifika                     nitafanya kwa sasa nafanya uimbaji kwanza. Pia huwa naombea na watu
wanafunguliwa                       namshukuru Mungu.
RM: Album yako inaitwaje?
BW: WEWE SI WAKAWAIDA (Jina la Album)
RM: Kwanini sio wakawaida?
BW: Kwasababu Yesu sio wakawaida.

KAMA UNAHITAJI KUPATA ALBUM YA BEATRICE WILLIAM WASILIANA NAE KWA 0658402366 BEI NI TSH 5000 TU.


MWISHO WA MAHOJIANO.
TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO WA BEATRICE WILLIAM MUNGU AMBARIKI.

No comments:

Post a Comment