Reuven Rivlin amechaguliwa na bunge la Israel 10.06.2014 kuwa rais mpya wa taifa hilo la kiyahudi akichukuwa mahala panapoachwa na Shimon Peres
Rais mteule wa Israel Reuven Rivlin |
Akitangaza ushindi huo wa Reuven Rivlin,spika wa bunge la Israel Yuli Edelstein amesema Rivlin amewashinda katika kinyang'anyiro hicho mpinzani wake wa mrengo wa kati Meir Sheetrit kwa kura 63 dhidi ya 53 katika zoezi la upigaji kura kwa siri katika bunge la nchi hiyo lenye viti 120.
Rais Schimon Peres na mwenzake wa Palestina Mahmoud Abbass |
Hata hivyo rais huyo mteule wa Israel mwenye umri wa miaka 74 atakuwa na kibarua kigumu kufuata nyayo za rais anayeondoka madarakani Shimon Peres ambaye haiba yake na umaarufu ulimpa nafasi ya kutumia wadhifa wake wa urais ambao hauna mamlaka makubwa katika kuueneza au kuupa nguvu ujumbe wa amani katika ngazi ya kisiasa.Wengi wa wadadisi wa mambo wanaashiria kwamba baada ya kuondoka Peres madarakani mwezi Julai huenda mwelekeo wa siasa za Israel ukajikita kutoka kwenye mrengo wa Kimataifa na kuzingatia zaidi masuala ya ndani.
Katika Duru ya mwanzo wabunge walipiga kura kuamua juu ya wagombea watano waliojitokeza kugombea nafasi hiyo akiwemo Dalia Itzik mwanamke wa kwanza kuwahi kushikilia nafasi ya spika wa bunge la Israel,Knesset,jaji msatafu wa mahakama kuu Dali Dorner na mshindi wa tuzo ya Nobel ya Kemia Dan Shechtman.
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu akiwa bungeni |
Shimon Peres rais anayestaafu |
No comments:
Post a Comment