Kwa pamoja kama kundi, vijana hawa 7 wa Kikolombia walichukuliwa na Yesu Kristo na kuonyeshwa Mbinguni na Kuzimu. Sikiliza masimulizi yao juu ya utukufu wa Mbinguni na ubaya wa Kuzimu.
(Imetafsiriwa na Mch.Peter John Mlay.)
--- (Ushuhuda wa Kwanza 1) ---
(Luke 16:19)
Akasema palikuwa na mtu mmoja tajiri, aliye vaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa hanasa na masikini mmoja jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, anavidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyo anaguka kwenye meza ya yule tajiri,hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.Ikawa yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi kule Kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa Mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia akasema Ee baba Ibrahimu, nihurumie, uumtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe una umizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa,ili wale watakao kutoka huku, kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
Bibilia,neno la Mungu lipo wazi sana juu ya somo la Mbinguni na Kuzimu. Kwenye eneo hili ambalo tumelisoma, Bwana anatuelezea juu ya maeneo mawili: Mbinguni na Kuzimu, hukumu au wokovu. Hakuna eneo nje ya haya. Hakuna Pagatori. Hakuna Limbo,eneo ambalo eti watu hufikia kwa muda halafu baadaye waende Mbinguni; Bibilia ipo wazi sana juu ya hili.
(Aprili 11 1995)
Mungu alitupa ufunuo a mbao ungebadili maisha yetu yote. Ni mara tuu tulikuwa tumeanza kufahamu juu ya Mungu na juu ya neno lake.Sisi ni vijana saba ambao Munguametupa upendeleo na jukumu kubwa la kuushirikisha ulimwengu ushuhuda huu.
Kila kitu kilianza majira kama ya saa nne asubuhi 4.00 Tulikuwa tunaomba na tulikuwa tuna jiandaa kwenda pikiniki baadaye siku ile . Ghafla majira ya saa nne 4.00 asubuhi nguvu kuu ya mwanga mweupe uliangaza kupitia dirisha mojawapo. Wakati mwanga ulipotokea, sisi sote kwa haraka tulianza kuongea kwa lugha mpya na tulibatizwa na Roho Mtakatifu .
Kwenye muda ule, sisis sote tulishangazwa na kuogopeshwa na kile tulicho kiona. Mwanga ule wa utukufu ulikuwa ukiimulika chumba chote. Mwanha huu ulikuwa na nguvu kuliko mwanga wa jua. Katikakati ya ule mwanga, tuliwaona malaika wengi wakiwa wamevaa mavazi meupe. Malaika hawa walikuwa ni wazuri sana, warefu, na wenye mvuto wa sura.
Kari kati ya Malaika wale tuliona kitu cha kutushangaza --umbo la mwanadamu. Umbo hili lilikuw ni la kiumbe maalumu sana, mtu aliye kuwa amevaa nguo nyeupe sana Nywele zake ni kama nyuzi za dhahabu. Hatukuweza kuuona uso wake kwa sababu ulikuwa unang,aa sana. Hata hivyo tuliweza kuuona mshipi wa dhahabu ukiwa matiti mwake, na maandishi ya dhahabu yaliyosema: "Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana ." Alikuwa amevaa viatu vya dhahabu halisi miguuni mwake, na uzuri wake haukuwa na mfano.Tulipo uona uwepo wa mtu huyu wote kwa pamoja tulisujudu kwa kupiga magoti.
Baadaye tulianza kuisikia sauti yake.Ilikuwa ni ya kipekee na ya ajabu sana;kila neno liliingia miyoyonimwetu kama vile upanga ukatao kuwili; kama vile ilivyo andikwa katika neno la Mungu(Waebrania 4:12). Alizungumza nasi kwa wepes lakini kwa maneno yenye nguvu sana. Tulisikia sauti yake ikisema nasi kuwa, "Watoto wangu wadogo, msiogope, mimi ni Yesu wa Nazarethi, na nimewatembelea kuwaonyesha mambo ya ajabu ili muweze kuyaonyesha na kuyaelezea kwenye, Miji, Mataifa, majiji, makanisa na kila mahali. Pale nitakapo waambia mwende, mtaenda, na pale nitakapo waambia msiende msiende."
Bibilia takatifu, neno la Mungu, linasema katika Yoeli 2:28 "Hata itakuwa baaada ya hayo ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu waume na wake watatabiri ,wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono." Huu ni wakati ambao Bwana anauandaa kwa kila mmoja.
Baadaye kitu kigeni kilitokea, mwamba ulitokea katikati ya kile chumba, na Bwana ambaye tulikuwa pamoja naye, alitufanya kuingia ndani ya ule mwamba.Mwamba ule ulikuwa na urefu wa karibu inchi saba hivi juu ya sakafu, na shimo kubwa lilitokea pale sakafuni.Lilikuwa ni kubwa,jeusi,mwanya au uwazi wa kutisha.Kwa haraka tuliweza kuwa juu ya ule mwamba na kuzama chini kupitia ule uwazi sakafuni.Ilikuwa ni giza nailituongoza hadi katikati ya dunia.
Wakati tulipo kuwa ndani ya giza lile baya, tuliogopa sana!tulitishika sana kiasi kwamba tulimwambia Bwana, "Bwana hatutaki kwenda eneo lile! Usitupeleke eneo lile Bwana! Tutoe mbali na eneo hili Bwana!" Bwana alitujibu kwa sauti nzuri na ya huruma, "Uzoefu huu ni wa muhimu sana ili muweze kuuona na kuwaelezea wengine."
Tulikuwa kwenye tanuru lenye sura kama ya pembe, na tulizubaa kwa kuangalia vivuli, mapepo na maumbo yalikuwa yakihama toka eneo moja kwenda jingine. Tuliendelea kwenda chini na chini zaidi.Ndani ya sekunde chache tulikuwa tukijisikia watupu na uoga mwingi.
Baadaye tulifika kwenye baadhi ya mapango makubwa;kwenye malango ya kutisha, kama vile njia panda. Hatukutaka kuingia mle ndani.Tuligundua harufu ya kutisha na joto lilotutetemesha.Mara tulipoingia tuliona vitu vya ajabu na maumbo ya kutisha. Eneo lote lilikuwa limezungukwa na miali ya moto;na katikati ya ile mioto, kulikuwepo miili ya watu maelfu. Walikuwa wakiteseka katika mateso makuu.Eneo lilikuwa ni la kuogopesha sana, hatukutaka kuona kile tulichokuwa tunaonyeshwa.
Eneo hili lilikuwa limegawanyika katika maeneo tofauti ya mateso na maumivu.Moja ya eneo la kwanza ambalo Bwana alituruhusu kuliona ni "Bonde la sufuria la kupikia" kama tulivyoliita. Kulikuwa na masufuria mamilioni.Masufuria haya yalikuwa yamelazwa usawa wa aridhi; kila moja lilikuwa linatokota uji wa moto.Ndani ya kila moja ilikuwepo roho ya mtu aliyekuwa amekufa na kwenda kuzimu.
Mara tuu zile roho zilipo mwona Bwana, zilianza kupiga kelele na kulalamika, "Bwana, utuhurumie! Bwana nipe nafasi ya kutoka nje ya eneo hili! Bwana, nitoe nje na nitauambia ulimwengu kwamba eneo hili ni la kwecli!" Lakini Bwana hata hakuwatazama. Walikuwepo mamilioni ya wanaume kwa wanawake na vujana eneo lile. Pia tuliwaona watu wandoa ya jinsia moja na walevi kwenye mateso.Tuliwaona watu hawa wote wakipiga makelele kwa maumivu.
Ilituogopesha kuona jinsi ambavyo miili yao ilikuwa imeharibiwa. Minyoo ilikuwa inaingia na kutoka kupitia kwenye mafuvu ya macho yao, ya midomo yao, na masikio; na ilikuwa ikijiingiza kwenye ngozi kuingia miilini mwao. Hii inatimiza neno la Mungu lililo andikwa kwenye kitabu cha Isaya 66:24 "Nao watatoka nje na kuitizama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika; nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili." Pia katika Marko 9:44,"Ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki." Tulikuwa tumeogopeshwa na kile tulicho kuwa tunakiona. Tuliona miali ya moto kama ya urefu wa inchi 9 mpaka 12 hivi. Ndani ya kila mwali wa moto kulikuwepo na roho ya mtu aliye kufa na kwenda kuzimu.
Bwana alituruhusu kumwona mtu ambaye alikuwepo ndani ya mojawapo ya masufuria yale ya moto. Alikuwa kichwa chini miguu juu na nyama za uso wake zilikuwa ziki anguka chini kwa vipande. Alibaki akimwangalia Bwana kwa makini; na baadaye alianza kupiga makelele na kuliitia jina la Yesu. Alisema, "Bwana nihurumie! Bwana nipe nafasi! Bwana nitoe nje ya eneo hili!" Lakini Bwana Yesu hakutaka kumwangalia.Yesu alimgeuzia mgongo wake. Wakati Yesu alipo fanya hivyo, mtu yule alianza kulaani na kumtukana Bwana. Mtu huyu ni John Lennon, mjumbe wa shetani wa kundi la mziki la "The Beatles." John Lennon alikuwa ni mtu aliyefanya mizaha na kumtania Bwana wakati wa maisha yake.Alisema kuwa Ukristo ungekwenda kutokomea na Yesu Kristo angesahaulika na kila mmoja.Hata hivyo leo, mtu huyu yupo kuzimu na Yesu Kristo yuu hai!! Ukristo pia hauja tokomea.
Tulipo anza kutembea kwenye ukingo wa eneo hili, roho zilikuwa zikinyoosha mikono yao kwetu na kutaka rehema.Walimwomba Yesu kuwaondoa ndani ya eneo lile, lakini Bwana hata hakuwaangalia.
Baadaye tulianza kwenda katika maeneo tofauti tofauti. Tulifika katika eneo lenye kutisha zaidi kuzimu,mahali ambapo mateso makubwa sana hufanyika; katikati ya kuzimu. Eneo lenye mchanganyiko mkubwa sana wa mateso;mateso ambayo mwanadamu yeyote hawezi kamwe kuyaelezea. Watu pekee hapa ni wale tuu ambao walimjua Yesu na neno la Mungu. Walikuwepo wachungaji,wainjilisti,wamisionari na aina zote za watu ambao waliwahi kumkubali Yesu na kuujua ukweli;lakini waliishi maisha ya pande mbili.
Walikuwepo pia wale waliorudi nyuma kiimanin; mateso yao yalikuwa ni makubwa mara elfu zaidi ya wengine. Walikuwa wakipiga makelele na kuomba rehema kwa Bwana, lakini neno la Bwana linassema katika kitabu chaWaebrania 10:26-27, "Maana kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao."
Roho zile zilikuwepo pale kwa sababu zilihubiri,zilifunga , ziliimba,na kuinua mikono yao kanisani lakini mitaani na majumbani walikuwwepo katika uasherati, uzinzi, uongo, unyanganyi. Hatuwezi kumdanganya Mungu. Bibilia inasema kwake ambaye alipewa vingi, atadaiwa vingi. (Luka 12:48)
Mungu baadaye alituruhusu kuwaona wanawake wawili ambao walikuwa ni wakristo wakiwa duniani, lakini hawakuwahi kuishi maisha ya haki mbele za Bwana Mmoja akamwambia mwenzake, "Wewe masikini mlaaniwa! ni makosa yako kwamba nipo eneo hili! hukunihubiria Injili takatifu! na kwasababu hukuniambia ukweli, nipo sasa hapa kuzimu!" Walisema maneno haya katikati ya miali ya moto, na walichukiana kwasababu hakuna upendo,rehema wala kusameheana kuzimu.
Kulikuwa na roho maelfu ya wale ambao waliwahi kulijua neno la Mungu, lakini maisha yao hayakuwa safi mbele ya uwepo mtakatifu wa Bwana. "Huwezi kucheza na Mungu wala na miali ya moto wa kuzimu!" Bwana alisema. Pia alituambia, "Wana wangu, mateso yote duniani kwa pamoja sii kitu,SII KITU, kulinganisha na mateso yale mtu hupata katika eneo lile zuri la kuzimu." Kama ni hatari kiasi hicho kwa yule anayeteseka kidogo kuzimu, ni mbaya kiasi gani basi kwa yule aliyeko katikati ya kuzimu ? ambao waliwahi kulijua neno la Bwana na kwenda mbali nalo. Baadaye Bwana alituambia kuwa wale wanao weza kucheza na moto duniani sii hivyo kuzimu hawawezi kamwe.
Tuliendelea kutembea maeneo tofauti tofauti na Bwana alituonyesha watu wa aina mbali mbali. Tuliweza kuona kuwa watu wote pale walikuwa na aina kama sita za mateso. Kulikuwepo na roho zilizo teswa na mapepo kwa aina zote za adhabu. Aina nyingine ni ufahamu wao uliosema, "Kumbuka wakati walipo kuhubiria, kumbuka wakati ulipo sikia neno la Mungu, kumbuka walipo kuambia habari za kuzimu na ulicheka juu ya hilo !" Ufahamu wao wenyewe uliwatesa; kama vile minyoo ile iliyopita juu ya miili yao, kama vile moto ule ulao ambao ni mkali mara elfu, elfu zaidi ya tunavyojua.Hii ni zawadi ambayo shetani anayo kwa wote wanao mtafuta na kumfuata.
Neno la Bwana linasema katika Ufunuo 21:8 "Bali waoga na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakao moto na kiberiti.Hii ndiyo mauti ya pili."
Baadaye Bwana alituonyesha mtu aliyeua watu sita. Watu wale sita walikuwa wamemzunguka, na walikuwa wakimpigia kelele wakisema, "Ni makosa yako kuwa tupo hapa wote, MAKOSA YAKO!" Muuaji alijitahidi kufunika masikio yake kwasababu hakutaka kuwasikiliza, lakini hakuweza kuepuka kusikia kwani kule kuzimu fahau zako zinakuwa hai zaidi.
Roho mahali pale zilikuwa zikiteseka kwa kiu ya maji isiyo vumilika na kutoshelezwa kwa njia yeyote;Kama vile kwenye Bibilia habari za Lazaro na yule tajiri. (Luka 16:19) Tajiri kule kuzimu alitaka tuu tone la maji, yangemtosha. Neno la Bwana linasema katika Isaya34:9, "Na vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, na aridhi yake itakuwa lami iwakayo."
Katika eneo lile,kila roho ilikuwa katikati ya moto. Watu huona mfano wamaji ya mto safi katikati ya moto na wanapo jaribu kuufikia, mito hiyo hugeuka kuwa moto.Huona pia miti yenye matunda ambayo hutoa maji, lakini wanapo jaribu kuchukua, huungua mikono yao na mapepo huwacheka.
Baadaye Mungu alituchukua baya zaidi ya maeneo mengine ambayo tumewahi kuyaona. Tuliona ziwa la moto na kemikali. Upande mmoja wa lile ziwa kulikuwepo na ziwa dogo zaidi. Ndani ya ziwa lile dogo, kulikuwepo naroho, milioni, milioni, zikilia na kuomba kwa Bwana kuwa rehemu. Walimwambia, "Bwana tafadhali! Tutoe nje ya eneo hili hata kwa muda kidogo! Tafadhali nipe nafsi ya kwenda nje!!!" Hatahivyo, Bwana hakuweza kufanya chochote kwa sababu hukumu yao tayri ilisha pangwa.
Kati ya roho zile milioni na milioni, Bwana alituruhusu kumwangalia mtu mmoja ambaye mwili wake nusu ulikuwa umezama katika ziwa la moto.Bwana alituruhusu kuelewa na kuyafahamu mawazo yake.Jina la mtu huyu ni Marko.Tulishangaa na yale mtu huyu aliyojisemea mwenyewe katika mawazo yake. Tulijifunza somo ndani yetu tulipo yasikia mawazo yake yafuatayo, "Ningetoa chochote kile kuwa katika nafasi yako sasa! Ningetoa kitu chochote ili kwenda duniani kwa dakika moja tuu. Singejali kama ningekuwa na hali mbaya, mgonjwa sana, ninayechukiwa sana, au mtu masikini kuliko wote duniani, ningetoa chochote kuweza kwenda duniani! kwa dakika moja tuu duniani." Bwana Yesu alikuwa ameushika mkono wangu. Yesu aliyajibu mawazo ya Mariko kwa kusema, "Mariko, kwanini ungependa kurudi duniani hata kwa dakika moja?" Kwa kulia na kwa sauti ya mateso, alimwambia Yesu, "Bwana! nitatoa kitu chochote kuweza kurudi duniani tuu kwa ajili ya kutubu na kuokoka."
Bwana aliposikia kile ambacho Mariko alisema, niliona damuikitoka katika majeraha ya Yesu na machozi yaliyajaza macho yake na alisema, "Mariko, umechelewa sana! Minyoo imewekwa iwe kitanda chako na minyoo itakufunika." (Isaya 14:11) Wakati Bwana alipo mwambia hivyo, alizama kwenye ziwa lile mojakwa moja. Ni kwa huzuni kuwa roho zile zote hazina tena tumaini. Ni sisi tuu tuliopo duniani ambao tunayo nafasi ya kutubu leo na kwenda Mbinguni na Bwana wetu Yesu Kristo.
Nina kuacha sasa na dada yangu kuendeleza ushuhuda huu, asante.
--- (Ushuhuda wa pili 2, Lupe) ---
Mungu awbariki kaka zangu wapendwa.Tusome neno la Bwana kutoka Zaburi 18:9. "Aliziinamisha mbingu akashuka, kukawa na giza kuu chini ya miguu yake" Wakati Bwana alipo ifikia mikono yangu, niliishika mikono yake tulianza kushuka chini kupitia tanuru lile.Tanuru lilikuwa linazidi kuwa giza na giza kiasi kuwa sikuweza hata kuuona mkono wangu, ambao haukuwa umeushika mkono wa Bwana
Ghafla, tulikipita kitu fulani cheusi na chenye kutoa cheche; kilikuwa kikitoa sauti.Giza lilikuwa kuu sana, mikono yako isdinge weza hata kuguza kuta za lilr tanuru.. Tulishuka kwa kasi sana, kwamba nilisika kuwa roho yangu ilikuwa ikitengwa na mwili wangu.
Mara nilihisi harufu mbaya ya kitu kilicho oza sana. Kama harufu ya miili iliyo oza. Ilikuwa ikizidi kila mara. Baadaye nilisikia sauti za mamilioni na mamilioni ya roho. Walikuwa bila kukoma wakipiga makelele, wakilia, na kuhuzunika.Ilikuwa inaogopesha sana hivyo nilimgeukia Bwana na kumuuliza, "Bwana , unatupeleka wapi? Bwana nirehemu! Tafadhali nihurumie!" Bwana alisema tuu, "Ni muhimu kwamba uone hili, ili uweze kumwaambia kila mmoja."
Tuliendelea chini kupitia tanuru hili lenye sura ya pembe hata tulipo fika eneo ambalo lilikuwa ni giza tupu. Kama vile kuondoa pazia zito machoni mwangu, baadaye niliona miali ya moto milioni nba milioni.Kwa ubaya sana nilisikia sauti zile maumivu lakini sikuweza kumwona yeyote. Niliogopa haswa. Nilimwambia Bwana, "Oh tafadhali Bwana nirehemu!Ooh tafadhali Bwana unirehemu ! Usinipeleke eneo hili! Nisamehe!" Katika muda huu, sikujua tuu kuwa mimi ni mtazamaji tuu wa kuzimu, nilifikiri ilikuwa ni siku ya mwisho. Nikiwa nimesimama mbele ya Bwana Yesu, nilikuwa nikitetemeka kwa nguvu kwa sababu nilifikiria kuwa ilikuwa ni mwisho wa maisha yangu.
Tulisogea karibu katika moto mkubwa mbele yetu; ulikuwa mkubwa na uliwaka kwa ukali. Niliendelea kwenda chini taratibu, nikiona miali ya moto mingi na kusikia sauti za mamilioni ya roho zilizo lia kwa sauti kwa pamoja.
Baadaye niliona meza ya mti ambayo haikufikiwa na moto.Kulikuwa na kitu kama chupa za bia juu yake.Zilionekana kama ni za kuburudisha lakini zilijaa moto ndani yake.Nilipo kuwa ninaangalia, mtu alitokea kw ghafla.Mwili wake ni kama ulikuwa umekwisha na kile kilichokuwa kimebaki ni vazi lililo jaa tope na moto. Alikuwa amepoteza macho yake, mdomo, na kila unywele kule motoni. Aliweza kuniona bila hata macho yake.. Nina kuambaia huyu ni mtu anaye waza , anayetafakari ,na kuona kwa kweli; sii kwa mwili wako wa asili.
Mtu huyu aliunyosha mkono wake kwa Bwana na kuanza kulia, akisema,, "Bwana nirehemu! Bwana nirehemu! Nipo kwenye maumivu! Ninaunguzwa! Tafadhali nirehemu na unitoe mahali hapa!" Bwana alimwangalia kwa huruma,na nilianza kusikia kama joto kwenye mkonom wangu.Niliangalia na kuona kuwa ni damu...damu ya Yesu! Damu ya Bwana ilitoka mkononi mwake alipo kuwa akimwangalia mtu huyu akiteseka na kuzungukwa na moto
Baadaye mtu huyu aligeuka na kuelekeza mawazo yake kwenye meza na kutembea kuelekea zile chupa.Alichukua chupa na alipo kuwa karibu ya kuinywa, moto na moshi ulitoka ndani ya ile chupa. Aligeuza kichwa chake tena na ulia kwa jinsi ambavyo sijawahi tena kusikia..Alilia kwa maumivu makuu sana na masononeko na alianza kunywa kile kilicho kuwepo ndani ya ile chupa.Lakini chupa ile ilijaa asidi\ tindikali na koo lake liliaribiwa karibu na kwisha. Ungeweza kuona tindikali ile ikipita mle tumboni na kumuumiza.
Namba ile 666 ilikuwa imechimbiwa juu ya upaji wa uso wake. Juu ya kifua chake kulikuwepo na sahani iliyo fanywa na malighafi isiyo julikana mabyo hata ule moto wala minyoo isingeweza kuiangamiza. Ilikuwa na maandishi juu yake lakini hatukuweza kuyaelewa Bwana kwa neeema yake kuu, alitupa tafsiri ya kile kilicho kuwa kimeandikwa. "Nipo hapa kwa sababu mimi ni mlevi." Alimwomba Bwana rehema,lakini neno la Mungu lipo wazi sana linaposema katika 1 Wakotintho 6:10 "Wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyanganyi, hawatauridhi ufalme wa Mungu."
Mungu alinionyesha hali ya mtu huyu muda mfupi kabla hajafaa duniani, kama vile sinema.Ilikuwa ni kama TV kubwa ikinionyesha sekunde zake za mwisho kabla hajafa.Jina lake aliitwa Luis na alikuwepo baa akinywa pombe. Niliona meza ileile na chupa ileile pale baa.Kuizunguka meza ile walikuwepo marafiki zake. (Naweza kukuambia jambo hili sasa kuwa yupo RAFIKI MMOJA TUU WA KWELI, na jina lake ni YESU KRISTO.Yeye ni rafiki mwaminifu.) Luis alikuwa akinywa na marafiki zake walikuwa tayari wamelewa. Rafiki yake mkubwa alichukua chupa na kuipasua na kuanza kumpiga nayo Luis . Alipo onma Luis amelala chini alikimbia,na Luis alitokwa na damu hadi kufa pale sakafuni. Jambo la huzuni sana ni kuwa alikufa bila Bwana Yesu.
Katikati ya mambo haya yote, kwa jinsi roho zile zote zilivyo kuwa zinalia, nilimuuliza Bwana, "Oh Bwana, tafadhali niambie je mtu huyu alijua habari zako? Alifahamu habari za wokovu wako?" Bwana kwa huzuni alijibu, "Ndiyo, Lupe, alijua habari zangu. Alinipokea kama Bwana wake, lakini hakunitumikia." Baadaye nilijisiki uwoga zaidi. Luis alilia kwa sauti na kupiga kelele"Bwana hii inaumiza!inaumiza! tafadhali nirehemu!" Aliunyoosha mkono wake tena kwa Bwana lakini Yesu aliuchukua mkono wangu na tulitembea kutoka eneo lile la moto. Moto ulio muunguza Luis ulikuwa na ukali zaidi, na alilia kwa sauti kuu zaidi, "Nirehemu! Nirehemu!!" Alitokomea baadaye kwenye ule moto.
Tuliendelea kutembea, eneo hili lilikuwa kubwa na la kuogopesha! Tuliufikia moto mwingine na nimwambia Bwana, "Bwana, hapana.! Tafadhali sitaki kuona tena haya! nakuomba unisamehe!Tafadhali nisamehe! sitaki kuona haya!" Hivyo niliyafunga macho yangu,lakini haikusaidia, kufunga au kufungua bado niliona kila kitu.Moto huu ulianza kwenda chini taratibu na baadaye nilimwona mwanamke.Alikuwa amefunikwa na tope, na tope lilijaa minyoo mingi. Alikuwa bado na nywele chache zilizo baki na alikuwa amezungukwa na minyoo pamoja na tope. Alikuwa analiwa na ile minyoo kila eneo na alilia, "Bwana nirehemu! Bwana nirehemu na unisamehe!niangalie.Hii inaumiza ! Nirehemu ! Niondolee hawa minyoo!Nitoe ndani ya mateso haya kwa sababu yananiumiza sana!" Bwana alimwangalia tuu kwa huzuni kuu . Tukiwa tumeshika mikono yake tuliweza kuhisi maumivu na huzuni ndani ya moyo wa Yesu, kwa roho zote zinazo potea na kuchomwa milele motoni kuzimu.
Mwanamke hakuwa na macho wala nyama midomoni, lakini aliweza kuona na kuhisi ; maumivu yote yalikuwa ni makuu sana. Alikuwa na chupa mkononi mwake, iliyo jaa tindikali, lakini aliamini kuwa ni manukato. Niliweza kuona kuwa ni tindikali na kila mara alipo ipulizia mwilini mwake, ilikuwa ikimuunguza. Hata hivyo aliendelea kuitumia ile tindikali tena na tena.Aliendelea kusema kuwa ile ni manukato ya dhamani sana.Aliamini pia kuwa alikuwa amevaa nguo isiyo na shingo, lakini kile nilicho kiona kiliwa ni nyoka iliyo mzingira shingoni. Aliamini kuwa alikuwa amevaa ushanga wa kupendeza sana, lakini niliona zilikuwa ni minyoo ya kweli kabisazenye urefu wa kam futi moja wakiwa na hasira na kujichimbia ndani ya mifupa yake.Alikuwa amevaa chapa ya chuma ambayo kila mmoja anayo kule kuzimu. Iliandikwa, "Nipo hapa kwa ajili ya wizi."
Mwanamke huyu hajutii dhambi zake. Bwana alimuuliza, "Magdalena, kwanini upo eneo hili,? Alijibu, "Haikunisumbua kuwaibia wengine.Kile nilicho jali ni kupata vito vya dhamani na manukato za dhamani. Sikujali ni nani niliye muibia, mradi tuu nipendeze."
Nili ushika mkono wa Kristo nilipo ona minyoo ikimwingia mwilini mwake .Magdalena aligeuka akitafuta kitu fulani. Nilimuuliza Bwana tena, "Bwana, je mtu huyu alikujua?" Na Bwana alijibu, "Ndiyo, mtu huyu alinijua."
Magdalena alianza kuangalia pembeni, akisema, "Bwana, yupo wapi mwanamke yule amliye ongea nami habari zako?Yupo wapi? Nimekuwepo hapa kuzimu kwa miaka 15 sasa." Watu wote kuzimu wanaweza kukumbuka kila kitu. Mgadalena aliendelea kusema, "Yupo wapi mwanamke huyu? Siwezi kumwona!" Nilijua kuwa mwili wake usingeweza kugeuka kwasababu nyama za ule mwili zingebaki mahali pamoja. Alijaribu kugeuka na kuangalia kwenye mioto mingine, kumtafuta yule mwanamke aliye ongea naye juu ya Mungu. Bwana alisema, "Hapana! hapana, Magdalena, hayupo hapa. Yule mwanamke aliye kuambia habari zangu yupo kwenye Ufalme wa Mbinguni pamoja nami."
Kwa kusikia hili, alijitupa wmenyewe chini ya ule moto ambao ulimuunguza zaidi. Bango lake lilikuwa likimhukumu kuwa ni mwizi. Nataka usome neno la Bwana katika Isaya 3:24. "Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizo sukwa vizuri, upaa; badala ya kisibau mavazi ya gunia, na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri."
Kwa jinsi tulivyo endelea kutembea na Bwana, niliona eneo la miraba lililojaa minyoo.Kulizunguka kulikuwepo na chuma chenye moto mwekundu.Kwenye eneo lile la miraba kulikuwepo na ubao ulio angaza kila mahali . Ubao uliandikwa,"Karibuni waongo na wasengenyaji." Mwisho wake kulikuwa na ziwa linalo tokota. Ilikuwa ni kama uji wa kikemikali unao tokota. Baadaye niliwaona watu walio uchi kabisa wakija chini eneo lile. Walipo kuwa wanateleza kuja ngozi zao zilikuwa zinabaki kwenye kile chombo.Walipo angukia kwenye ziwa lile, ndimi zao zilitanuka hadi kupasuka na minyoo ilitokea badala ya ndimi zile..Matezo yao yalianza. Neno la Mungu linasema katika Zaburi 73:18-19 "Hakika wewe huwaweka kwenye utelezi, Huwaangusha mpaka palipo haribika. Namna gani ukiwa mara! wametokomea na kutoweshwa kwa utisho."
Baada ya kuona hili, tulichukuliwa tena , nje ya kuzimu. Nina taka kukuambia kuwa Mbingu na Kuzimu ni za kweli kuzidi hata ulimwengu wetu huu tunao ujua. Ni hapa tuu unapo weza kuamua ni upande upi unao taka kwenda; kuutumia umilele na Yesu au kuunguzwa kuzimu.Bwana aliendelea kutuambia,"Pasipo utakatifu hakuna mtu atakaye niona mimi, pasipo utakatifu hakuna mtu atakaye niona mimi." (Waebrania 12:14) Hii ndiyo sababu ninakuambia kitu kile kile sasa, "Pasipo utakatifu hakuna mtu atakaye mwona Bwana."
--- (Ushuhuda wa tatu 3, Sandra) ---
Hebu twende pamoja kwenye neno la Bwana katika Mathayo 10:28 " Msiwaogope wauao mwili, wasiweze kuiua roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanum."
Wakati roho inapo fika kuzimu, mtu huyo huchukua mwili wa mauti.Bwana Yesu alinishika mkono wangu na tulianza kwenda chini kupitia tanuru lenye giza kuu linaongoza kwenda katikati ya dunia. Tulifika eneo lenye milango mingi; mmoja wao ulifunguka na tuliingia pamoja na Bwana. Sikuweza kuuachia mkono wa Bwana maana nilijua kwa kufanya hivyo ningelibakia mle kuzimu milele.
Baada ya kuingia mlango ule, niliona ukuta mkubwa sana.Kulikuwa na watu kwa maelfu waliokuwa wametundikwa vichwa vyao na komeo, na pingu zilizo wafunga mikono yao ukutani. Tuliona pia maelfu ya watu wakiwa wamesimama katikati ya mioto kila eneo.
Tulikwenda mbele ya ile mioto na mara ilianza kutulia taratibu.Mara niliweza kumwona mtu mle ndani, na alipo ongea, niliweza kujua kuwa alikuwa ni mtu.Mtu huyu alikuwa amevaa vazi la Kikuhani lililokuwa limeharibiwa kabisa .Minyoo ilikuwa ikimwingia na kutoka.Alionekana mweuusi kutokana na kuunguzwa na moto. Macho yalikuwa yamemtoka na nyama yake ilikuwa imeyeyuka na kuanguka chini. Lakini baada ya nyama yote kuanguka chini baadaye humrudia na tendo hili huanza tena.
Alipo mwona Yesu, alisema, "Bwana unirehemu,unirehemu! Tafadhali nitoe hapa hata kwa kitambo kidogo tuu! kwa dakika tuu!" Kwenye kifua chake lilikuwepo bango lilosomeka, "Nipo hapa kwa ajili ya wizi."
Wakati Yesu alipo kuja karibu, alimuuliza yule mtu,"Jina lako ni nani?" Akajibu, "Andrea, jina langu ni Andrea, Bwana." Bwana akamuuliza, "Ni kwa muda gani umekuwepo hapa?" Andrea alijibu, "Nimekuwepo hapa kwa muda mrefu sana." Mtu huyu alianza kuelezea habari za maisha yake. Alisema, alikuwa na kazi ya kukusanya fungu la kumi na kupanga jinsi ya kugawa fedha za kanisa lake la Katoliki kwa masikini.Hata hivyo,alikuwa akiiba zile fedha. Kwa macho yaliyo jaa huruma, Bwana alimuuliza, "Andrea, Uliwahi kuisikia injili ?" Andrea alijibu, "Ndio Bwana, alikuwepo mwanamke mmoja wa kikristo aliye ingia kanisani na alihubiri injili mara moja, lakini sikutaka kuipokea.Sikutaka kuiamini, lakini naiamini sasa! Sasa naamini kuwa huu ni ukweli! tafadhali Bwana nitoe mahali hapa,hata kwa kitambo tuu!"
Alipo kuwa akiongea, minyoo ilikuwa ikitambaa kwenye mafuvu ya macho yake yakitokea masikioni, na kuingia tena kupitia mdomo wake. Alijaribu kuwavuta nje kwa mikono yake lakini haikuwezekana. Alikuwa akipiga makelele kwa na kumwomba Mungu amrehemu. Aliendelea kumwomba Yesu amtoe mahali pale. Mbaya zaidi kulikuwepo na pepo linalo mtesa, muda wote yakimchoma na mikuki yao.Pepo hili lilifanana na midoli ile tuliyo nayo hapa duniani tunayo iita "Joridano". Niliiona midoli hiyo kuzimu, lakini sasa haikuwa tena ni midoli;yalikuwa hai na ni mapepo. Yalikuwa ya urefu karibu futi tatu na meno makli sana. Damu zinawatoka mdomoni na macho yao yalikuwa ni mekundu kabisa.
Yalikuwa yakimsumbua Andrea kwa nguvu zao zote, pamoja na wengine walio kuwepo eneo hili la kuzimu.. Nilipo ona hili, nilimuuliza Bwana inawezekana je midoili ya duniani, kufanana kama yale mapepo.Bwana aliniambia kuwa yale ni mapepo ya huzuni.
Tulipo endelea, tuliwaona maelfu ya watu kwenye mateso,Wakati roho inapo mwona Bwana, zilijitahidi kumfikia kwa mikono isiyo na ngozi.Nilimwona mwanamke aliye anza kupiga makelele alipo mwona Bwana Yesu. Alilia, "Bwana tafadhali nirehemu! nitoe mahali hapa!" Alikuwa akiteseka sana na aliunyoosha mkono wake kwa Bwana.Aliendelea kumwomba Bwana amtoe eneo lile hata kwa sekundr moja. Alikuwa yuu uchi kabisa na alifunikwa na tope. Nywele zake zilikuwa ni chafu na minyoo ilikuwa ikijongea mwilini mwake .Alijaribu kuiondoakwa mikono yake lakini kila alipo mwondoa mmoja mingine ilijizisha zaidi.Minyoo ilikuwa na urefu karibu inchi 6-8.Neno la Bwana linasema katika Marko 9:44, "Ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki."
Ilikuwa ni ya kutisha sana kumwona mwanamke huyu na kusikia kilio chake kwa jinsi minyoo ile kwa hasira ilivyo kuwa inaila nyama za mama huyu. Kulikuwepo na bango la chuma lililo kifuani mwake ambalo lisingeweza kuharibiwa na moto. Lilisomeka , "Nipo hapa kwa ajili ya Uzinzi." Kwa jinsi ile ile ya dhambi yake, mwanamke huyu alilazimishwa kufanya uzinzi kuzimu na nyoka wa kutisha mnene..Nyoka huyu alikuwa na miiba mikubwa kuuzunguka mwili wake, ni kama ya uerfu wa inchi 6-8 hivi.Nyoka humwingia mama hyu sehemu zake za siri na kusafiri hadi mwilini mwale hadi kwenye koromeo lake. Nyoka alipo mwingilia hivi, alianza kulia kwa makelele .
Alimwomba Bwana kwa nguvu sana amtoe eneo lile, "Bwana, nipo hapa kwa ajili ya uzinzi, nimekuwepo hapa kwa miaka 7, tangu UKIMWI ulipo niua. Nilikuwa na wapenzi sita6, na nipo hapa kwa ajili ya uzinzi." Kule kuzimu alitakiwa kuirudia dhambi yake tena na tena. Hakuna kupumzika usiku na mchana, akiteseka kwa jinsi ile ile kila mara. Alijaribu kuunyoosha mkono wake kwa Bwana, lakini Bwana alimwambi, "Blanca, kwako tayari umechelewa. Minyoo itakuwa ni kitanda chako, na minyoo itakufunika." (Isaya 14:11) Wakati Bwana alipo sema maneno hayo, blanketi la moto lilimfunika, na siku mwona tena.
Tuliendelea kutembea, tukiona maelfu na maelfu ya watu. Walikuwepo vijan, watu wazima na wazee kabisa wakiteseka kuzimu. Tulifika eneo lililo onekana kama eneo la bwawa la kuogelea la moto, likiwa na maelfu ya wanaume na wanawake ndani yake. Kila mmoja wao alikuwa na bango la chuma kifuani mwake lililosomeka: "Nipo hapa kwa kuto toa fungu la kumi na sadaka" Nilipo soma vile,nilimuuliza Bwana, "Inawezekanaje hili kuwa hivi, kwamba mtu yupo hapa kwa sababu hii??" Bwana alijibu,"Ndiyo, kwasababu watu hawa walifikiri kuwa fungu la kumi na sadaka hazikuwa ni lazima, wakati neno langu lina onyesha kuwa ni amri." Katika Malaki 3:8-9 inasema "Je! mwanadamu atamwibia Mungu? lakini ninyi mnaniibia mimi.Lakini ninyi mwasema .tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote."
Bwana aliniambia kuwa wakatim watu wake wanapo zuia fungu la kumi, inazuia kazi ya Bwana, na injili haibiriwi. Watu wa eneo hili wanateseka mara elfu zaidi ya wengine, kwa sababu, walilijua neno la Bwana na hawakulitii.
Tuliendelea kutembea na Bwana alinionyesha mtu.Niliweza kumwona kuanzia kiunoni hadi kichwani, na nilianza kuona maono ya jinsi alivyo kufa. Jina lake ni Rogelio. Alikuwa ndani ya gari lake wakati mtu alipo msogelea kumhubiria injili , na kumpa Bibilia . Lakini Rogelio alikataa maonyo ya mtu yule na aliendelea kwenye njia yake, bila ya kujua kuwa dakika chache baadaye gari lake linge pata ajali. Liliangukia kwenye korongo, na mara alikufa.
Mara tuu baada ya ajali, Bibilia ilifunguliwa katika Ufunuo 21:8, "Bali waoga, na wasioamini,na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na wahao waabuo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili." Wakati Rogelio aliposoma msitari huu, alikufa na alifika kuzimu.
Alikuwepo pale mwezi mmoja tuu na bado alikuwa na ngozi usoni mwake. Hata hivyo alikuwa akiteseka kama wengine. Mwanzo hakujua ni kwanini alikuwepo kuzimu. Nafikiri yule mkristo alipo mfikia pale kwenye gari yakr, ilikuwa ndiyo nafasi yake ya kipekee na ya mwisho ya kumkubali Bwana Yesu. Kwa jinsi ile ile ambayo wengi wamepata nafasi ya kumkubali Yesu.Leo nina kualika ufungue moyo wako kwa Yesu; Yeye tuu ndiye njia,kweli, na uzima. (Yohana 14:6) Ni kwa yeye tuu tunaweza kuokolewa kuingia ufalme wa Mbinguni (Matendo 4:12) Bwana alituambia pia kuwa tuzifuate njia zake katika utakatifu na heshima. Mungu akubarik
--- (Ushuhuda wa 4) ---
Mungu awabariki kaka zangu. Wakati Bwana alipo uchukua mkono wangu, niliweza kuona kuwa nilikuwa nimesimama kwenye mwamba, na nyuma yetu nilimwona malaika. Tulianza kwenda chini kupitia tanuru lile kwa mwendo wa kasi wa kutisha.Kwa haraka, niligeuka na kuona kuwa malaika alikuwa ameondoka, na nilijisikia hofu.Nilimuuliza Bwana, "Bwana, yupo wapi yule malaika? kwanini hayupo hapa tena?" Bwana alisema, "Hawezi kwenda pale sisi tunapo kwenda."
Tuliendelea kwenda chini naghafla tulisimama, kama kwenye lifti. Niliona matanuru kadhaa; na tuliingia mojawapo ambalo dada yangu Sandra ameshalizungumzia tayari. Pango ambalo watu walikuwa wametundikwa wakining`inia na pingu mikononi mwao. Ukuta ambao ulikuwa na watu juu yake ulikuwa ni mrefu usio na mwisho. Mamilioni ya watu walikuwa pale wakining`inia . Walikuwa na minyoo mwili mzima. Niliangalia mbele na liona kuwa kulikuwa na ukuta mwingine, kama ule mwingine. Nilimwambia Bwana, "Bwana! Kuna watu wengi sana eneo hili!" Mara, andiko liliingia akilini mwangu;ambalo silikumbuki. Bwana aliniambia, "Kuzimu na uharibifu havishibi." (Mithali 27:20)
Tulitoka pale na mara tulifika eneo linaloitwa, "Bonde la Masufuria ya moto(cauldrons)". Masufuria haya yalijaa matope yanayo tokota, na tulilisogelea moja wapo. Mtu wa kwanza ambaye nilimwona alikuwa ni mwanamke. Mwili wake ulikuwa ukipanda juu na kushuka chini katika tope lile linalo tokota la moto, lakini Bwana alipo mwangalia aliacha kwenda na alibaki akielea kuanzia kiunoni kwenda juu. Bwana alimuuliza, "Mwanamke, jina lako ni nani?" Alijibu, "Jina langu ni Rubiella."
Nywele zake zilijaa matope yanayo tokota na nyama za mwili wake zilikuwa zina ning`inia toka mifupa yake, ambayo ilikuwa mweusi kwa kuunguzwa. Minyoo ilimwingia kupitia mashimo ya macho yake, ikitoka kupitia midomo yake, ikiingia tena kupitia pua zake na kutokea masikioni. Wakati minyoo ilipo shindwa kuingia, ilifanya shimo yenyewe kupitia eneo jingine la mwili, ambayo ilisababisha maumivu yasiyo elezeka.
Alipiga makelel, "Bwana, tafadhali! Nitoe mahali hapa. Nirehemuu! siwezi kuendelea jinsi hii tena! isimamishe Bwana! siwezi kuendelea tena!tafadhali nirehemu!." Bwana alimuuliza ni kwa nini alikuwepo pale.Alisema kuwa alikuwepo pale kwa sababu ya maringo, kitu ambacho ni saw na jinsi ilivyo kuwa imeandikwa juu ya bango lake lililo kifuani mwake.Mkonoi mwake ni chupa ya kawaida, lakini kwake aliiona kama ni manukato ya dhamani kubwa. Rubiella angechukua chupa ile iliyojaa tindikali , na angejipulizia mwili wake wote. Hii ilimsababishia nyama yote iliyo puliziwa kuyeyuka kumsababishia maumivu makubwa sana.
Alipiga kelele kwa Bwana, "Bwana tafadhali, nirehemu! siwezi kuwepo tena hapa ! kwa sekunde moja tuu Bwana." Sisemi kuwa ni dhambi kutumia manukato, lakini Bwana alituambia kuwa mwanamke yule alikuwepo pale kwa ajili ya maukato yake, kama vile neno la Mungu linavyo tuambia katikaI am not saying that it is a sin to use a perfume, but the Lord told us that the woman was there because of her perfume, as the Word of the Lord tells us in Kumbukumbu la Torati 5:7 " Usiwe na miungu mingine ila mimi." Alikuwepo pale kwasababu ya uzuri wake, manukato, na maringo yalikuwa ndicho kitu cha kwanza katika maisha yake. Hata hivyo, Bwana Yesu ni mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana! Anatakiwa kuwa wa kwanza katika maisha yako; hii ndiyo maana alikuwepo pale. Kwa huzuni, Bwana alimwangalia na kusema , "Rubiella, unechelewa, minyoo itakuwa kitanda chako, na minyoo itakufunika." Wakati Bwana aliposema hivyo, blanketi la moto lilimfunika kabisa. Wakati wmili wake ukiwa umefunikwa kabisa ndani ya sufuria lile la moto, alikuwa akitesema sana.
Tulitoka pale na kwenda mbali zaidi eneo lenye milango imkubwa .Tulipokuwa tumeifikia, ilitufungukia yenyewe. Upande mwingine tuliona pango kubwa. Nilipo angalia juu niliona rangi tofauti za mwanga zikitembea kama mawingu ya moshi.Ghafla tulisikia mziki wac; salsa, ballenato, rocki, na aina tofauti ya miziki mashuhuri ambayo watu huisikiliza kwenye redio. Bwana aliuelekeza mkono wake na tuliona, mamilioni na mamilioni ya watu wakiwa wametundikwa na minyororo mikononi mwao. Walikuwa wakiruka ruka kama wanyama ndani ya moto.
Bwana alituangalia na alisema: "Angalia huu ni mshahara wa wacheza mziki." Watakuwa wakiruka kama wanyama juu na chini sawa na mapigo ya miziki. Kama ni salsa inapigwa, walitakiwa kuruka kwa mapigo yale, kama aina nyingine ya mziki ikipigwa, walitakiwa kuruka sawa na mapigo yake.Hawawezi kamwe kuacha kuruka.Lakini mbaya zaidi, viatu vyao vina misumazi ya inchi6 chini yake. Wakati wanaporuka inawangia miguuni mwao na hawatakuwa na nafasi ya kupumzika.Wakati mtu anapotaka kuacha, pepo lingekuja maramoja na kumchoma na mkuki, likiwalaani na kusema, "Msifuni yeye sasa! Huu ndio ufalme wenu sasa, msifuni Shetani! msifuni! huwezi kuacha, msifuni!ni lazima umsifu !lazima uruke! lazima ucheze!Uwezi kuacha hata kwa sekunde moja."
Ilikuwa hatari kuwa wengi wa watu wale walikuwa ni wakristo waliomjua Bwana,lakini walikuwa kwenye madisko ya usiku walipo kufa. Labda unauliza, "Wapi Bibilia inasema kwamba ni vibaya kucheza?" Katika Yakobo 4:4, Neno la Bwana linasema:: " Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui na Mungu? basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia kuwa adui wa Mungu." Pia katika 1 Yohana 2:15-17, "Msiipende dunia, wala mambo yaliyopo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake, maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.Na dunia ianpita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele." Kumbuka dunia itapita, vitu vyote hivi vitaharibika, lakini yule atendaye mapenzi ya Mungu atadumu milele.
Rafiki zangu na kaka zangu, tulipo acha eneo hili, tuliona kitu kama daraja lililo igawanya kuzimu katika maeneo tofauti ya mateso.Tuliiona roho ikipita kwa miguu juu ya daraja. Ilionekana sawa na mdoli tuliyo iona duniani; tunaiita mikokoteni ya dhamani. Ina nywele za rangi za aina mbali mbali, zina nyuso za mzee lakini mwili wa mtoto, bila maeneo ya siri. Macho yaliyo jaa uovu. Bwana alituelezea kuwa hizi ni roho za upotovu. Roho hii ilikuwa na mkuki mikononi na ilikuwa ikitembea kwa maringo katika daraja lile kama vile ni mwana wa mfalme.
Alipo kuwa anatembea, aliwachoma watu chini kwa ule mkuki wake. Alikuwa akiwalaani akisema,"Mnakumbuka siku zile mlipo kuwa nje ya makanisa ya kikristo na mlikataa kuingia ndani? Mnakumbuka siku zile walipo wahubiria na hamkutaka kusikiliza? Mnakumbuka wakati walipo wagawia vipeperushi vya injili na mkavitupa mbali?" Roho hizi zilizo potea hujitahidi kufunika maeneo yakle ambayo masikio hukaa. Huwajibu mapepo yale, "Nyamaza! Nyamaza! usiniambie tena! sitaki kujua zaidi, nyamaza!" Hata hivyo, mapepo yale hupenda kufanya vile kwakuwa huwaingizia maumivu watu wale kwenye nafsi zao.
Tuliendelea kutembea na Bwana. Kwa kule kuangalia umati wa watu, tuligundua kuwa mtu mmoja alikuwa akipiga makelele zaidi ya wengine waliokuwa wakiungua pale.Alikuwa akisema, "Baba, Baba, nirehemu!" Bwana alikuwa asisimane lakini aliposikia neno "Baba" Alisisimka na kugeuka. Yesu alimwangalia na kumuuliza,"Baba? Unaniita Baba? Hapana, mimi siyo Baba yako na wewe kamwe sio mtoto wangu. Kama ungekuwa mtoto wangu, ungekuwa sasa na mimi katika Ufalme wa Mbinguni.Ninyi ni wana wa Shetani baba yenu." Ghafla blanketi la moto lilikuja na kabisa lilimfunika mwili wake.
Bwana alituelezea habari ya maisha ya mtu yule. Mtu yule alimwita Baba kwa sababu aliwahi kumjua . Alikuwa akienda kanisani na alikuwa akilisikiliza neno la Mungu, na alikuwa amepokea ahadi nyingi za Mungu. Hivyo tuliuliza, "Nini basi kilitokea Bwana? Kwanini basi yupo hapa leo?" Bwana alitujibu, "Alikuwa akiishi maisha ya aina mbili; moja nyumbani moja kanisani. Alifikiria moyoni mwake, 'Hapana mtu anaye ishi karibu yangu, sii mchungaji, wala ndugu yeyote, hivyo naweza kufanya chochote ninacho taka. Lakini alisahau kuwa jicho la Bwana lipo juu ya njia zetu zote kwamba hakuna mtu anaye weza kumdanganya au kujificha mbele za Bwana."
Neno la Bwana linatuambia kuwa, "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; Kwakuwa chochcote apandacho mtu, ndicho atakacho vuna." (Wagalatia 6:7) Mtu huyu alikuwa akiteseka mara alfu zaidi ya wengine. Alikuwa akilipwa hukumu mara mbili: moja kwa ajili ya dhambi zake na nyingine ni kule kufikiri kuwa anaweza kumdanganmya Bwana.
Leo, watu wana jaribu kupima ukubwa wa dhambi; wanafikiri kuwa kulawitiana, kuua ni dhambi kubwa zaidi ya kusema uongo au kusengenya. Lakini mbele ya macho ya Bwana, dhambi zote hizi zina uzito mmoja na malipo sawa. Bibilia inatuiambia kuwa, "Mshahara wa dhambi ni mauti" "na roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa." (Warumi 6:23) (Ezekieli 18:20) Rafiki zangu na kaka zangu, nina waalika sasa kuukubali mwaliko wa Yesu. Yesu ameunyoosha mkono wake wa rehema kwako kama ukitubu.Neno la Bwana linatuambia kwamba yule atakaye geuza njia zake na kutubu atapokea rehema.Ni vizuri zaidi ukaamini sasa, kuliko kusubiri na kukuta njia ngumu mbeleni. Mungu akubariki.
--- (Ushuhuda wa 5) ---
Neno la Mungu linasema katika Warumi 6:23 " Kwa maaana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."
Tulipo kwenda chini mahali pale, nilisikia maumivu na uzoefu wa kifo. Nilikuwa nimeogopeshwa sana na kile nilicho kiona.Niligundua kuwa kuliwa na watu wengi, wengi sana ; wote walikuwa wakilia na kupiga makelele.Lilikuwa ni giza tupu, , lakini katika uwepo wa Bwana,giza lilitoweka.Tuliona maelfu na maelfu ya roho zote zikilia kuomba msaada na rehema.Walikuwa wakilia kwa Bwana kuwaondoa eneo lile. Tulijisikia pia maumivu kwa sababu tulijua Bwana alikuwa akiteseka sana kila alipo waona.
Wengi walilia kwa Bwana kuwaondoa mahali pale angalau kwa sekunde moja tuu. Bwana angewauliza, "Kwa nini unataka kutoka nje ya hapa?", na wangelijibu, "Kwa sababu ninataka kuokoka! Nataka kutubu na kuokoka!" Hata hivyo ilikuwa kwao tayari wamechelewa.
Wapendwa watu mnaonisikiliza sasa, sasa ndio nafasi pekee ya sisi kuchagua eneo letu la umilele. Unaweza tuu kuchagua umilele wa wokovu au wa hukumu.
Tulikwenda chini kwa zaidi. Niliona kuwa sakafu tuliyokuwa tunatembea juu yake, ilikuwa imeharibiwa na moto; na tope na moto lilikuwa linatoka ndani yake. Kulikuwepo pia na harufu ya kutisha kila mahali. Tulijisikia vibaya sana na mahangaiko kutokana na harufu na makelele ya watu wote.
Tulimwona mtu, kwa mbali ambaye alikuwa amezama chini kwenye tope la moto.Alipo toa mkono wake. nyama toka toka mifupa yake zilidondoka chini kwenye tope.Tuliweza kuona mvuke wa kikahawia ndani ya mifupa yake, hivyo tulimuuliza Bwana ninini kile. Aina hii ya mvule upo ndani ya kila mtu kuzimu.Bwana alituambia ni nafsi zao zilizokamatwa ndani ya miili yenye dhambi; Kama ilivyo andikwa katika Ufunuo 14:11 "Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, nao wamsujudia huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake."
Tulianza kuelewa vitu vingi ambavyo tulividharau duniani;Jambo la muhimu, ujumbe wa karibu zaidi ni kuwa, maisha yetu duniani yana amua ni wapi tutakapo tumikia umilele wetu baada ya kufa.
Tulipo kuwa tunatembea tukiwa tumeshikana mkono na Bwana, tuligundua kuwa kuzimu ina sehemu nyingi sana yenye mateso mbalimbali. Tulifika eneo lenye vyumba vingi na roho nyingi zinateseka huko. Roho hizi zilikuwa zinateswa na mapepo mengi ya aina nyingi. Mapepo yangeweza kuzilaani zile roho, kwa kusema, "Ninyi masikini mlio laaniwa, msifuni Shetani! Mtumikieni kama vile mlivyo fanya mlipo kuwa duniani.!" Roho zile ziliteseka sana kutokana na minyoo ile; na moto ulikuwa ni kama tindikali juu ya mwili wote.
Tuliwaona watu wawili ndani ya chumba kile cha jela, kila mmoja alikuwa ameshika kisu na anamsumbua mwenzake. Wangelisema, "Wewe masikini mlaaniwa! ni kwasababu yako ndiyo maana nipo hapa! Ulinifanya nije hapa kwasababu ulinipofusha nisujue ukweli na hukuniruhusu kumjua Bwana! Hukuniruhusu kumpokea! Mara nyingi nilipata nafasi lakini hukuniruhusu kumkubali! Ndiyo sababu nipo hapa leo, nateswa usiki na mchana!"
Kupitia maono, Bwana alituonyesha maisha yao duniani, Tuliwaona wakiwa baa ya pombe pamoja. Mazungumzo yalianza yaliyo pelekea kupigana. Walikuwa tayari walevi. Mmoja alichukua chupa iliyo vunjika na mwingine alitoa kisu. Walipigana mpaka wote wakawa wamejeruhiwa sana na wakafa.Watu hawa wawili waliwekewa kulirudia tukio hili milele.Waliteseka pia na kumbu kumbu zao kuwa walikuwa ni marafiki sana duniani, kama mtu na nduguye wakipendana.
Nataka kukuambia leo kuwa, kuna rafiki mmoja tuu wa kweli, na jiana lake ni Yesu wa Nazarethi . Yeye ni rafiki wa kweli. Ni rafiki mwaminifu, aliye pamoja nawewe katika muda wote.
Tulipo endelea kutembea tulimwona mwanamke ndani ya chumba kingine, alikuwa akinivingirisha kwenye lile tope. Nywele zake zilikuwa chafu na zenye tope. Ndani ya chumba kile alikuwepo nyoka mnene mkubwa.Alikuwa anamsogelea na kumzunguka mwili wake, na alianza kumwingilia mwilini mwake akianzia sehemu zake za siri. Alilazimishwa kufanya uzinzi na yule nyoka. Kwenye eneo hili, wanaume na wanawake waliokuwa wazinzi walilazimishwa kufanya uzinzi . Hata hivyo walilazimika kufanya hivyo na majoka yale yaliyofunikwa na vitu vikali mwili mzima kama chuma kikali cha inchi 6. Nyoka aliuharibu kabisa mwili wa mwanamke yule kila mara alipo mwingilia. Alilia sana kwa Bwana na kumwomba kusimamisha hali ile.Hakutaka kuteseka tena. "Simamisha! Sitaki kufanya tena!tafadhali simamisha hii hal!" Alimwomba Bwana amhurumie kila wakati nyoka alipo mwingilia na muuharibu mwili wake tena na tena.
Tulijitahidi kuyafunga masikio yetu tusisikie kilio chake, lakini bado tulimsikia.Tulijaribu kwa nguvu zaidi kufunga masikio yetu , lakini haikusaidia. Tulisema Bwana, "Tafadhali Bwana, hatutaki kuona na kusikia hivi tena! tafadhali!" Bwana alitujibu, "Ni muhimu muone haya, ili muwaeleze wengine. kwa sababu watu wangu wanaangamizwa, watu wangu wanaukataa wokovu halisi, njia ya kweli ya wokovu."
Tuliendelea kutembea na tuliona ziwa kubwa lenye watu maelfu na maelfu ndani yake katikati ya mioto.Walitupungia wakiomba msaada, lakini kulikuwa na mapepo mengi yakiruka juu ya eneo lile.Mapepo haya yalikuwa yanatumia mikuki yenye vichwa kama S- kuwaumiza watu wale waliokuwa wakiunguzwa katika lile ziwa. Mapepo yaliwatania na kuwalaani yakisema, "Ninyi masikini mlio laaniwa! Sasa ni lazima kumwabudu Shetani! Msifuni, msifuni kama mlivyo fanya wakati mlipo kuwa duniani!" Kulikuwepo watu maelfu kwa maelfu. Tuliogopa sana,tulihisi kama tusingeushika mkono wa Bwana tungebaki katika eneo lile la kutisha. Tuliogopeshwa na vitu tulivyo kuwa tunavihisi.
Kwa mbali tulimwona mtu aliyesimama, akiwa kwenye maumivu makubwa na huzuni. Alikuwa na mapepo mawili yakiruka juu yake yakimtesa. Yangeweza kuchimbia mikuki yao mwilini mwake na kutoa mbavu zake. Yalikuwa pia yakimtania kila mara. Zaidi ya yote Bwana alinionyesha kuwa alikuwa akiteseka kwa hofu ya kila siku juu ya familia yake aliyo iacha duniani. Mtu huyu hakutaka familia yake ije mahali pale pa mateso. Aliogopa kwa sababu hakuwahi kuwapa ujumbe wa wokovu. Aliteseka zaidi kwa kukumbuka kuwa wakati fulani walikuwa na nafas.Alikuwa mtu muhimu katika ile familia ambaye angeweza kuwapa ujumbe ule, lakini aliamua kuudharau ujumbe ule na sasa alikuwa akihofia juu ya watoto wake na mke wake.
Mateso yaliendelea pale ambapo mapepo yalipo mkata mikono yake, aliangukia kwenye matope ya moto. Kwasababu ya maumivu toka tope lile la moto, alijongea kama vile minyoo toka eneo moja hadi jingine. Nyama zilimtoka mwilini mwake sababu ya ule moto. Alianza baadaye kutambaa kama nyoka ili atoke pale. Lakini kila mara alipojaribu kwenda, mapepo yalimsukuma na kumrudisha pale na alizama zaidi kwenye lile tope.
Baadaye tuliona idadi ya mapepo eneo moja.Kitu fulani kilinivuta kuangalia, niliona kuwa mojawapo ya mapepo lilikuwa halina bawa lake moja. Nilimuuliza Bwana, "Bwana, kwanini pepo hili halina bawa moja?" Bwana alisema, "Pepo lile lilitumwa duniani kwa lengo moja, lakini halikukamilisha kazi yake, na lilikemewa na mmoja wapo wa watumishi wa Mungu na kurudishwa kuzimu. Baadaye Shetani alikuja na kuliadhibu, na kulikata moja ya mabawa yake." Ndipo tulipo gundua kuwa kama wakristo, tuna mamlaka ya kukemea mapepo yote na mamlaka zote.
Mpendwa rafiki unaye sikiliza maneno haya sasa hivi, ushuhuda huu sii kwa ajili ya kukuhukumu bali kwa wokovu; hivyo unaweza kujipima mwenyewe na kuona hali ya roho yako mbele za Bwana. Hii ndivyo ilivyo ili uweze kubadili njia zako kwa wokovu na sio kwa hukumu. Sasa hivi inua moyo wako kwa Bwana na utubu dhambi zako, ili kama Bwana akija sasa hivi uweze kwenda naye badala ya kwenda eneo lile la mateso mahali penye kilio na kusaga meno. Hapa utajua ni kwanini Yesu alilipa gharama kubwa vile pale msalabani Kalvari.
Tuliona watu wengi kuzimu ambao hawakujua ni kwa nini walikuwepo pale. Maisha yao yalijaa mambo ambayo hawakuwahi kujua kuwa ni dhambi. Mpendwa rafiki yangu, jipime mwenyewe! usifikiri kuwa kudanganya, kuiba, maringo ni vitu sahihi vya kufanya! vyote hivi ni dhambi mbe;le za macho ya Bwana! Mpendwa kaka, jeuka na acha kufanya vitu hivi!Ninakupa ujumbe huu ili uache kufanya dhambi kwa kudhamiria, na kuuangalia zaidi uso wa Bwana.
--- (Ushuhuda wa 6) ---
Zaburi 62:12 "Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana; maana ndiwe umlipaye kila mtu sawasawa na haki yake."
Asubuhi Bwana alitutembelea pale chumbani, alitushika mkono na tulianza kwenda chini.Roho yangu ilikuwa imejawa na hofu, siwezi hata kuielezea.Nilifahamu tuu kuwa siwezi kuuachia mkono wa mwokozi wangu.Nilijisikia kuwa Yesu ni maisha yangu , mwanga wangu na kila tumaini langu lilikuwa kwake; kama sivyo ningebakia mle kuzimu.Sikuwahi kuwaza kama ningewahi kwenda eneo lile.Sikuamini pia kama eneo kama hili lipo.Japo ni Mkristo nilifikiria kuwa kuna eneo linaloitwa Pagatori na labda ndilo kuzimu, lakini Mungu alinionyesha ukweli wa Kuzimu.
Tulipofika kuzimu,nilijisikia mshituko wa eneo lile.Na mapepo yote pale yalikimbia kujificha, kwasababu hakuna hata mojawapo ya pepo linalo weza kusimama mbele ya uwepo wa Yesu..Tulisikia roho zilizo kamatwa kuzimu zikipiga makelele ya nguvu, kwasababu walijua kuwa Yesu wa Nazarethi yupo pale. Walijua wote kuwa yupo mtu mmoja tuu anaye weza kuwatoa eneo lile. Walikuwa na matumaini hayo, japo ni matumaini ya uongo.
Tulitembea tukiwa tumeshikana mikono na Yesu, na tulifika eneo la uzinzi. Yesu aligeuka kumwangalia mwanamke ambaye alikuwa amefunikwa kabisa na moto. Wakati Yesu alipo mwona, alianza kutoka mle motoni taratibu, japo maumivu yake hayakusimama.Tuliweza kuona kuwa alikuwa yuu uchi kabisa na kuweza kuona mwili wake mzima. Mwili wake ulikuwa mchafu sana, na alikuwa ananuka.. Nywele zake zilikuwa zimevurugika sana na alikuwa na tope la rangi ya njano na kijani juu yake.Hakuwa na macho na midomo yake ilikuwa imechanika. Hakuwa na masikio, ni machimo tuu. Kwa mikono yake, iliyo mifupa iliyo geuka kuwa mweusi kwa moto, aliichukua ile nyama iliyo kuwa inadondoka toka usoni mwake, na kujaribu kuirudishia. Lakini jambo hili lilimpa maumivu mabaya zaidi.
Alitetemeka na kulia zaidi; kilio chake hakikukoma.Alikuwa amejaa minyoo, na alikuwepo joka kubwa lililo jivingirisha mkononi mwake. Lilikuwa ni nene sana na lenye miiba mwili mzima.Mwanamke huyu alikuwa na alama ya namba 666 iliyo chimbiwa mwilini mwake; namba ya mnyama iliyo tajwa katika kitabu cha Ufunuo. (Ufunuo 4:9-11) Alikuwa pia amevaa bango la chuma kifuani mwake, iliyo tengenezwa na madini yasiyo fahamika, haikuwa inaweza kuteketezwa na moto.. Juu ya bango lile iliandikwa jambo fulani kwa lugha ngeni, lakini tuliweza kuielewa.Ilisomeka, "Nipo hapa kwa ajili ya uzinzi."
Yesu alipo mwona alimuuliza, "Elena, kwanini upo eneo hili?" Wakati akijibu, Elena alikuwa akijipinda kutokana na maumivu yake. Alisema kuwa yupo pale kutokana na uzinzi.Alimwomba Bwana msamaha tena na tena
Baadaye tulianza kuona tukio la kifo chake.Alipo kufa alikuwa akifanya mapenzi na mmoja wa wapenzi wake, kwa sababu alifikiri kuwa mwanamke aliye kuwa anaishi naye alikuwa amesafiri.Hata hivyo mwanaume yule alirudi toka kazini na alimkuta akiwa kitandani pamoja na mwanaume mwingine,Mwanaume yule alikwenda jikoni na kuchukua kisu kikubwa na alimpiga nacho Elena nyuma mgongoni mwake.Elena alikufa na alichukuliwa kuzimu, vilevile kama alivyo kufa; bado yupo uchi kabisa.
Kule kuzimu kila kitu kinaendelea, na bado anacho kile kisu mgongoni mwake, kikimsababishia maumivu makubwa.Wakati huu alikuwa tayari yupo kuzimu kwa miaka 7 na aliweza kukumbuka kila tukio la maisha yake na kifo chake.Aliweza hata kukumbuka wakati mtu fulani alipo mhubiria habari za Yesu; kwamba ndiye pekee anaye weza kumwokoa. Lakini sasa ilikuwa tayari amechelewa sana na kwa kila aliyepo kuzimu.
Neno la Bwana linazungumza sana juu ya uzinzi, na lipo wazi sana. Uzinzi ni kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa. 1 Wakorintho 6:13 "Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula;lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili sii kwa zinaa, bali ni kwa Bwana naye Bwana ni kwa mwili." pia katika 1 Wakorintho 6:18 "FIkimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake mwewnyewe, lakini yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."
Wakati Yesu alipo maliza kuzungumza naye, alifunikwa na blanketi kubwa la moto na hatukumwona tena. Lakini tulisika sauti ya mwili wake ukiungua na makelele yale ya kutisha, siwezi hata kuyaelezea vizuri kwa maneno.
Kwa jinsi tulivyo kuwa tunaendelea kutembea na Bwana, alituonyesha watu wote pale: waabudu sanamu, wale wanao tumia na kufanya uchawi,wasio safi,washerati, waongo, na wafiraji. Tuliogopa sana, kitu pekee tulicho taka kufanya ni kuondoka pale.Lakini Yesu aliendelea kusema kuwa ni muhimu kuendelea kuangalia ili tuwaeleze wengine, ili waweze kuamini.
Tuliendelea na Yesu na tulimshika mkono wake kwa nguvu zaidi.Tlifika eneo ambalo lilinishangaza.Tulimwona kijana mdogo , wa miaka 23, akiwa ameinuliwa juu katikati ya moto. Hatukuweza kuona vizuri mateso yake ni yapi, lakini ile namba 666 ilikuwa imechimbiwa mwilini mwake. Alikuwa pia na bango lile kifuani mwake lililosomeka,"Nipo hapa kwa kuwa wa kawaida." Alipo mwona Yesu, aliunyoosha mkono wake kwa Yesu akiomba rehema. Neno la Mungu linasema katika Mithali 14:12 "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti."
Tuliposoma lile bango lililo sema, "Nipo hapa kwa kuwa wa kawaida", Tulimuuliza Bwana"Bwana, inawezekanaje!? Inawezekana mtu akaja eneo hili kwa sababu hii?" Ndipo Yesu akamuuliza, "Andrea,kwa nini upo eneo hili?" Alijibu, "Yesu, nilipo kuwepo duniani, nilifikiri kuwa , kuua, kuiba zilikuwa ndizo dhambi tuu, na ndiyo sababu sikuwahi kujaribu kuja karibu yako." KatikaZaburi 9:17 inasema "Wadhalimu watarejea kuzimu, naam mataifa yote wanao msahau Mungu."
Andrea alifanya kosa kubwa kwa kugawa dhambi, kama wengi wa watu wanavyo fanya leo.Bibilia ipo wazi sana inaposema mshahara wa dhambi ni mauti , lakini karama ya Mungu ni uzima wa milele.(Warumi 6:23) Zaidi, wakati Bibilia inapo zungumza habari za dhambi, haigawi dhambi, kwa sababu zote ni dhambi tuu. Andrea alikuwa na nafasi ya kumjua na kumpokea Yesu, lakini hakuichukua nafasi ile ambayo Mungu alikuwa amempa. Labda alikuwa na nafasi elfu kumjua Bwana, lakini hakutaka kumjua na hii ndiyo sababu alikuwa pale. Baadaye blanketi kubwa la moto lilimfunika na hatukumwona tena.
Tuliendelea kutembea na Yesu. Kwa mbali tuliona kitu fulani kikidondoka kama maumbo fulani hivi.Tulipo sogea karibu, tuliona kuwa ni watu wapya waliokuwa wakiingia kuzimu muda ule.Watu ambao ndio tuu wakekufa duniani kabla hawajampokea Yesu miyoyoni mwao, walikuwa wakiingia kuzimu.
Tulimwona kijana mmoja, mapepo mengi yalimkimbilia na kuanza kuuharibu mwili wake. Mara mwili wake ulianza kujawa na minyoo. Alipiga kelele, "Hapana! Ni nini hii? Acha! Sitaki kuwa eneo hili! Simamisha hii! Hii lazima itakuwa ni ndoto!" Hakujua kuwa amekufa, na ya kuwa amekufa bila ya Yesu moyoni mwake.Mapepo yalikuwa yakimchezea na kuuharibu mwili wake. Baadaye namba 666 ilitokea kwenye upaji wa uso wake, na bango la chuma kifuani mwake.Japo hatu kuweza kuona sababu ya yeye kuja kuzimu lakini tulijua kuwa hataweza tena kutoka mle.
Bwana alituambia kuwa , mateso ya wote walio kuzimu yatakuwa makubwa zaidi siku ya hukumu.Kama wanateseka kwa jinsi ile ya kutisha na ya kuogopesha sasa, siwezi kufikiria jinsi gani watateseka siku ile ya hukumu.
Hatukumwona mtoto yeyote pale.Tuli waona vijana maelfu kwa maelfu; wanaume kwa wanawake wa mataifa mengi. Hata hivyo kuzimu hakuna utaifa au tabaka, wote wanakuja hapa kuteswa na kuhadhibiwa. Kuna kitu kimoja ambacho kila mtu pale alikihitaji, na hicho ni nafasi tuu ya kutoka mle ndani, angalau kwa sekunde. Wanataka pia kupata angalau tone la maji kuuburudisha ndimi zao., kama vile habari ile ya tajiri kwenye Bibilia. (Luka 16:19) Lakini hii hili haliwezekani tena kwao, walikwisha chagua ni wapi watakapo kaa milele. Walichagua umilele bila ya Mungu.Mungu kamwe hampeleki mtu yeyote kuzimu, kila mmoja huenda kuzimu kutokana na matendo yake mwenyewe katika Wagalatia 6:7 "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakacho vuna."
Leo una nafasi kubwa ya kubadilisha mahali pako pa umilele.Yesu bado anapatikana sasa, na Bibilia inasema kuwa wakati tukiwa hai bado tuna matumaini.Leo una uhai, usikose nafasi hii, inaweza ikawa ni ya mwisho kwako.
Mungu akubariki.
Amen.
ReplyDelete