Tuesday, January 7, 2014

MABOYA: Mwaka 2014 ni wa Kifalme, haki, kuinuliwa katika Roho Mtakatifu.




Askofu Mkuu wa kanisa la Calvary assemblies Of God Mtume na Nabii Danstan Maboya ametabiri kwa Taifa kuwa mwaka 2014 utakuwa wa kifalme,amani,furaha na haki katika msingi wa Mungu kupitia roho Mtakatifu.

Akizungumza katika kilele cha sikuu ya mwaka mpya iliyoambatana na ibada ya kufunga na kuomba kwa siku arobaini kwa kanisa la Jesus Power lililopo eneo la sombetini Jijini Arusha, Mtume Maboya ametangaza mwaka 2014 kuwa mwaka wa furaha,amani na haki.

Aidha Mtume Maboya amethibitisha tamko hilo kwa kufuata misingi ya Neno la Mungu kama ilivyo nenwa katika injili ya Mathayo 11:28~30 na Mathayo 9:27~31 ambapo amelitaka Taifa kuishi katika misingi ya neno la Mungu na kuyashika maagizo yake ililiweze kubarikiwa.

Aliongeza kwa kuamuru na kutangaza furaha kwa Taifa la Tanzania waitunze tunu ya amani iliyo letwa na Mungu kupitia waasisi wa Taifa hili akiwemo Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Hata Hivyo Mtume Maboya alitoa wito kwa viongozi wote walioshika dhamana ya kuliongoza Taifa hili kuzingatia haki,amani na upendo kamili kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu.

Kwa upande wake mchungaji wa kanisa hilo Jennifer Cormack amewataka wakristo kushiriki katika kuhudhuria ibada ya kufunga na kuomba jinsi itakavyo wezekana kwa siku 40 ili Mungu aweze kuonekana katika Taifa na kuliwezesha kuenenda katika misingi ya haki,amani na upendo.


Aliwataka watu wenye mahitaji ya maombezi kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo mateso ya nguvu za giza wawasiliane na kitengo cha huduma ya maombezi kwa namba 0768 121213 na 0687 121213.

No comments:

Post a Comment