Monday, May 5, 2014

UJUMBE WA UNABII WA MUNGU KWA WANANCHI WA TANZANIA




MATENDO YA MITUME SURA YA 17 MSTALI WA 26

SAUTI YA MUNGU KWA WANANCHI WA TANZANIA
Mungu amenituma kuwaambia watanzania wa makundi yote yakwamba Kusudi lake la Kuanzisha Taifa letu ni ili wananchi wote wa Tanzania tuishi maisha ya ;-----....
1.     Kuwaziana mawazo mema ya kizalendo.
2.     Kutazamiana kwa mtazamo wa kizalendo.
3.     Kuneneana maneno mema ya amani .
4.     Kutendeana matendo mema ya upendo.
5.     Kuonana kwa jicho jema la upendo.
6.     Kuhusiana kwa uhusiano mwema wa upendo.
7.     Kufanyiana maamuzi mema ya haki.
8.     Kusimamiana kwa misimamo mema ya haki.
SASA NI WAKATI WAKUTOKA MISRI ASEMA BWANA MUNGU WA MILELE
Mungu amenituma niwaambie wananchi wa Tanzania mtoke katika maisha ya maadili mabaya mnayoyaishi hivi sasa , Anasema mtoke katika maisha ya;-----
1.     Kuwaziana mawazo mabaya kwasababu ya tofauti mlizonazo.
2.     Kutazamiana mtazamo mbaya kwasababu ya tofauti mlizonazo.
3.     Kuneneana maneno mabaya yasiyo ya amani kwasababu ya tofauti mlizonazo.
4.     Kutendeana matendo mabaya ya uovu kwasababu ya tofauti mlizonazo.
5.     Kuonana kwa jicho baya la uovu kwasababu ya tofauti mlizonazo.
6.     Kuhusiana kwa uhusiano mbaya kwasababu ya tofauti mlizonazo.
7.     Kufanyiana maamuzi mbaya yasiyo ya haki kwasababu ya tofauti mlizonazo.
8.     Kusimamiana kwa misimamo mibaya isiyo ya haki kwasababu ya tofauti mlizonazo.

SASA NI WAKATI WA KUINGIA KAANANI KATIKA NCHI YA USTAWI NA MAENDELEO ENDELEVU
Mungu amenituma niwaambie watanzania waingie katika maisha yatakayoleta ustawi na maendeleo endelevu kwa Taifa lenu, Mungu amesema niwaambie waingie katika maisha ya maadili mema maisha ya ;------
1.     Kuwaziana mawazo mema ya amani ya upendo na ya haki ambayo ndio mawazo ya uzalendo.
2.     Kutazamiana kwa mtazamo mwema, mtazamo wa amani wa upendo na wa haki ambao ndio mtazamo wa kizalendo.
3.     Kuneneana maneno mema ya amani ambao ndio ya kuliunganisha Taifa letu na kulifanya kuwa na amani na utulivu.
4.     Kutendeana matendo mema ya upendo ambayo ndio yanayoimalisha umoja na mshikamano ndani ya Taifa letu.
5.     Kuonana kwa jicho jema la upendo ambako ndio kunakoimalisha umoja na mshikamano ndani ya Taifa letu.
6.     Kuhusiana kwa uhusiano mwema wa upendo ambako ndio kunaimalisha Umoja na mshikamano ndani ya Taifa letu.
7.     Kufanyiana maamuzi mema ya haki ambayo ndio yanayojenga mawasiliano ya haki ya kuaminiana ndani ya Taifa letu.
8.     Kusimamiana kwa misimamo ya haki ambako ndio kunajenga mawasiliano ya haki ya kuaminiana ndani ya Taifa letu.
MUAFAKA WA UJENZI WA MAADILI YA TAIFA LETU NDIO UHAI WA TAIFA
Mungu ameniambia niwaambie wananchi wa Tanzania wa makundi yote mfikie muafaka wa ujenzi wa maadili ya Taifa lenu, anataka mkubaliane mambo mawili;----
1.     Mungu anataka mkubaliane maadili mema ya ujenzi wa maisha ya Taifa kuwa ndio msingi pekee wa ujenzi wa maisha ya Taifa lenu.
2.     Mungu anataka mkubaliane sasa kuacha kutumikia maadili mabaya katika ujenzi wa maisha ya Taifa lenu na kuingia katika kujenga maisha ya Taifa lenu kwa kufuata maadili mema



FAIDA ZA KUKUBALI MATAKWA YA MUNGU KWA TAIFA LETU
Mungu amesema namimi kuwa kama wananchi wa Tanzania tutakubali kufikia muafaka wa ujenzi wa maisha ya Taifa letu kama nilivyoainisha hapo juu ndipo tutafanikiwa kujenga Taifa lenye
A.    Wananchi wenye Sauti moja ya kuisikiliza
B.     Wananchi wenye mwelekeo mmoja wa kuufuata
C.     Wananchi wenye amani na utulivu (Muafaka wa kitaifa)
Katika hili Mungu amenithibitishia wazi kuwa kama tutakubali mpango wake ataponya kila eneo la maisha ya watanzania,ataponya maisha ya roho za watanzania,ataponya maisha ya miili ya watanzania hawatakufa kabla ya wakati,ataponya ndoa za watanzania,ataponya familia za watanzania,ataponya koo za watanzania,ataponya makabila ya watanzania,ataponya vyama vya siasa vya watanzania,ataponya huduma za watanzania,ataponya makampuni ya watanzania,ataponya taasisi za watanzania,ataponya mashirika ya watanzania,ataponya jumuia za watanzania,ataponya miradi ya watanzania,ataponya vikundi vya watanzania,ataponya madhehebu ya watanzania na ataponya dini za watanzania
D.    Wananchi wenye nguvu moja ya kuinyenyekea (Umoja wa kupendana)
Katika hili Mungu amesema nami na kunithibitishia wazi kuwa kama tutakubali mpango wake ataimalisha ushirikiano wa upendo katika ndoa katika familia katika koo katika makabila katika vyama vya siasa katika huduma katika vikundi katika taasisi katika mashirika katika makampuni katika jumuia katika miradi katika madhehebu na katika dini mbalimbali
E.     Wananchi wenye mamlaka moja ya haki (Mawasiliano ya kuaminiana)
Katika hili Mungu amesema name na kunithibitishia wazi kuwa kama tutakubali mpango wake atajenga mawasiliano ya haki ya kuaminiana ndani ya ndoa zetu ndani ya familia zetu ndani ya koo zetu ndani ya makabila yetu ndani ya vyama vyetu vya siasa ndani ya huduma zetu ndani ya taasisi zetu ndani ya mashirika yetu ndani ya makampuni yetu ndani ya jumuia zetu ndani ya miradi yetu ndani ya madhehebu yetu na ndani ya dini zetu


HASARA ZA KUPUUZIA MATAKWA YA MUNGU KWA TAIFA LETU
Mungu amenituma niwaambie watanzania wenzangu kuwa madhala ya kukataa maagizo yake ni makubwa sana, baadhi ya madhala ambayo yataonekana kwa Taifa letu ni pamoja na ;------
A.    Watanzania kupoteza sauti moja ya kuisikiliza, ndani ya Taifa letu kutainuka sauti nyingi ambazo zote zitataka kusikilizwa na wananchi wa Tanzania na madhala yake ni watanzania kushindwa kujua ni sauti ipi haswa ya kuisikiliza ndipo wananchi wengi wataanza kuzisikiliza sauti za makundi wanayotoka hapo ndipo Taifa letu litakabiliwa na kukua na kupanuka kwa migawanyiko kwa misingi ya tofauti za wananchi wake.
B.     Watanzania kupoteza mwelekeo mmoja wa kuufuata, ndani ya Taifa letu kutainuka mielekeo mingi ambayo yote itataka kufuatwa na wananchi wa Tanzania na madhala yake ni watanzania kushindwa kujua ni mwelekeo upi haswa waufuate ndipo wananchi wengi wataanza kufuata mielekeo ya makundi wanayotoka hapo ndipo Taifa letu litakabiliwa na kukua na kupanuka kwa mielekeo mingi inayoligawa Taifa letu
C.     Watanzania kugawanyika kwa misingi ya tofauti zao , ndani ya Taifa letu kutapanuka na kukua kwa kasi migawanyiko kwa misingi yatofauti zetu za dini, makabila, rangi,asili,matabaka,rika, jinsia,vyama vya siasa,maeneo wanakotoka,koo,familia, kazi,ajira,aina za maisha,taasisi,mashirika,vikundi,jumuia,madhehebu,ndoa,huduma,makampuni,Miradi, hali hii itaua uzalendo wa wananchi wetu na kutufanya wananchi wa Tanzania kupoteza amani na utulivu kabisa
Sambamba na hilo kukataa muafaka wa ujenzi wa maadili mema ndani ya Taifa letu utapelekea watanzania wengi sana kuanzia sasa kufa kwa namna za ajabu bila sababu za msingi hali hii itashtua taifa zima, pia ajali hazitakua na ufumbuzi kwani mara dufu ajali na vifo vitatokea, tena Mungu akaniambia kutatokea kusambaratika kwa kutisha kwa ndoa za watanzania, kusambaratika kwa familia, koo, makabila,vyama vya siasa, huduma, makampuni,taasisi,mashirika,miradi,vikundi,jumuia,madhehebu, dini, serikali nk

D.    Watanzania kupoteza Nguvu moja ya kuinyenyekea kama Taifa, ndani ya Taifa letu kutaangamia kabisa umoja wa kitaifa, wananchi wataanza kuimalisha umoja wa kupendana kwa misingi ya tofauti zao, watanzania tutaanza kupendana kujaliana na kuthaminiana kwasababu ya kutoka dini moja,kutoka kabila moja,kutoka ukoo mmoja,kutoka eneo moja,kutoka rika moja, kutoka jinsia moja, kutoka tabaka moja, kutoka kundi moja ndani ya Taifa hili, hali ya upendano ,kujaliana na kuthaminiana kwa kutanguliza utaifa wetu itakufa kabisa
E.     Watanzania kupoteza mamlaka moja ya kuitii, ndani ya Taifa letu kutabomoka kabisa mawasiliano ya kitaifa,wananchi wataanza kujenga mawasiliano ya kuaminiana kwa misingi ya tofauti zao,watanzania tutaanza kuaminiana kwasababu ya kutoka dini moja, kutoka kabila moja,ukoo mmoja,kutoka eneo moja,kutoka jinsia moja, kutoka rika moja,kutoka tabaka moja kutoka kundi moja ndani ya Taifa hili,hali ya kuaminiana kwa kutanguliza utaifa wetu itakufa kabisa
Maneno haya niamini na kweli, Mungu ameyaweka ndani ya moyo wangu namimi nimeona vema niyaweke wazi kwa Taifa zima, Taifa linao uchaguzi wakuyakubali au kuyakataa, lakini imani yangu ni kwamba Mungu atafanya upesi kuyathitisha maneno haya kuwa yanatokana na kisima cha hekima yake iliyo tukufu sana
Nawashukuru watanzania wenzangu kwa kunisikiliza

Mtume Joseph Goliama

1 comment:

  1. Mungu awabariki na awalinde,Mungu ni upendo,na anataka nasi binadamu tumufanane,alituumba kwa sura yake mwenyewe,alakini kwa kupungukiwa na imani ikatufanya kuwa watumwa wa dhambi,na njoo inatuma binadamu uteseka,lakini upendo wake ni mkuu,anaendelea kututafuta,kumbe tutii sauti yake.

    ReplyDelete