Tuesday, July 11, 2017

SOMO#3. KAINI, HABILI NA SETHI

SOMO#3. KAINI, HABILI NA SETHI

Andiko Kuu-Mwanzo sura yote ya  4
11.   KAINI, HABILI NA SETHI (Kabla ya Yesu)
1.       Adam na Hawa
·         Adam na Hawa walifukuzwa Bustanini (Maskani) kwasababu ya Dhambi, lakini Mungu aliwafanyia Upatanisho ingawa haukuwa mkamilifu kwasababu UTHAMANI WA MWANADAMU SIO SAWA NAWA MNYAMA, ndio maana mahusiano yao yaliendelea NJE ya Bustani (Maskani).
·         Adamu na kizazi chake chote kilishaingiwa na Kasoro, walikuwa na Sura ambili – Ya Mungu na Shetani, kwahiyo kila anaezaliwa kwa asili ni lazima afanye maamuzi ya KUCHAGUA, ama Mungu au Shetani.
2.       Kaini na Habili – Mwanzo 4:1-7
·         Adam na Hawa walipata watoto-Kaini na Habili wakiwa na Asili ya wazazi wao
·         Kaini alikuwa mtoto wa kwanza, mkulima, Mungu alimkataa yeye na Sadaka yake. Lakini Mungu alimtakabali Habili na Sadaka yake, alikuwa mtoto wa pili, mchunga kondoo. Swali- Kwanini Mungu amtakabali Habili na asimtakabali Kaini?
·         Sadaka waliyotakiwa kutoa ilikuwa ni sadaka ya UPATANISHO/KUFUNIKA DHAMBI/KUSITIRI DHAMBI, sasa sadaka yenye hii sifa ni sadaka yenye DAMU. Kaini alitoa sadaka nzuri lakini haikuwa na Damu kwani kinachofanya upatanisho ni Damu
·         Kaini alijibunia njia yake ya kufanya upatanisho kama Baba yake na Mama yake hii inaonyesha hakumuamini Mungu, lakini Habili alifuata njia ya Mungu ya KUUA KONDOO ili kufanya upatanisho, hii inaonyesha alimuamini Mungu na akahesaiwa HAKI kwa hii IMANI yake.
·         Mwanzo 4:8-18. Kaini muasi akamuua mwenye Haki Habili, akalaaniwa TENA kama wazazi wake na AKAFUKUZWA kwenye uwepo wa Bwana akaenda kuendeleza kizazi KIASI, na wakati huo hakukua NA kizazi cha haki kwani Habili alishakufa.
3.       SethiMwanzo 4:25-26
·         Vizazi viwili toka kwa Adam- cha haki kilishauawa lakini cha UASI kilizidi kuchanua, Dunia nzima ilijawa na kizazi hiki cha Kaini cha Uasi, hakukua na aliyekuwa AKIMCHA Mungu mpaka MTOTO WA KIUME alipozaliwa – SETHI.
·         Baada ya Adam kumpata Sethi akasema “ Mungu ameniwekea uzao…..’ Maneno haya yanaonyesha huyu mtoto wa kiume ni utimilizo mdogo wa ahadi aliyoitoa Mungu wakati anamlaani Hawa-Mwanzo 3:15.
·         Huyu mtoto wa kiume Sethi akaanza kutengeneza kizazi cha haki kwani walikuwa wakiliitia jina la Bwana. Adam alidhani kizazi hiki cha haki kingedumu milele, baada ya vizazi kumi vya haki, haki ikaanza kupotea kwani wengi walivutwa na kizazi cha uasi cha Kaini.
·         Unabii wa kuzaliwa mtoto wa kiume, mkombozi-Hakua Sulemani - 1Nyakati 22:9-10, bali ni Imanueli - Isaya 7:14,9:6

.   2.   AGANO JIPYA (Wakati wa Yesu)
1.       Unabii wa kuja Mtoto Yesu
·         Mungu aliwa ahidi Adam na Hawa kuhusu UZAO wa Mwanamke – kwamba Bikra angepata mtoto wa kiume ambaye ndie angelikuwa mkombozi. Hawa alipomzaa Sethi alidhani kuwa Sethi alikuwa ndio Utimilizo kamili wa ahadi ya Mungu.
·         Nabii Isaya anaona uhitaji wa mtoto wa kiume mwingine ambaye sio Sethi – Isaya 7:14-16. Sethi hakufaa kwa sababu alikuwa na asili ya uasi ndani yake ingawa kwa nje alifanya vizuri ukilinganisha na kaka yake Habili. Isaya 9:6-7.
·         Luka 2:10-14. Huu ndio utimilizo wa Ahadi aliyomuahidi Hawa, ingawa wao walidhani ni Sethi. Mtoto huyu wa Kiume Yesu ndiye MWOKOZI, mbingu zilifurahi, malaika walishuka , mji ulitaharuki lakini wakati wa Sethi hakukua na chochote.
2.       YESU
·         Kuna laana iliyotakiwa kuwapata Waisraeli kwa kumwaga Damu za Haki, lakini ili mtu AEPE hiyo laana alitakiwa kumuamini Yesu asitiriwe- Mathayo 23:34-36.
·         Yohana 3:16- Mungu alimtoa mwanawe ili aanze upya uzao wa Haki, waliokuwa wakimwamini yesu walipewa uwezo wa kuwa uzao mteule, watoto wa Mungu kwa njia ya Imani juu ya Yesu – Yohana 1:12-13,
·         1Yohana 2:22-23,3:1-2

        3. NYAKATI ZETU (Baada ya Yesu)
1.       Damu ya Yesu Yanena Mema- Ebrania 12:24-Tuliona Damu ya Habili ilikuwa ikinena mbele za Mungu, lakini haikuwa inanena mema bali mabaya, ingawa Habili alikuwa mwenye haki lakini alipouawa bila hatia alidai kisasi lakini Yesu hakufanya hivyo, alisema “Baba uwasamehe…’ Luka 23:34. Baadae tutaona mambo 7 ambayo Damu ya Yesu inayanena.
2.       Vizazi viwili – uzao mteule na Wana wa Uasi- 1Yohana 3:10-12, Yuda 1:11- wana wa ibilisi, lakini 1Petro 2:8-10 ni wana wa mungu. Wale watoto wawili wa Adamu ni Unabii mpaka nyakati hizi, kwamba kuna watu wa aina mbili tu haijalishi tunajidanganyaje – aidha ni wa Kaini au Habili ama wa Shetani au wa yesu, hakuna katikati.
3.       Imani juu ya YesuGalatia 3:26- Leo hii mimi na wewe twaweza kuwa Wana kwa kumuamini Yesu tu. Mungu atakuhesabia Haki kama Habili alivyohesabiwa haki kwa njia ya Imani tu- Waebrania 11:4

   4.     HITIMISHO
CHUKUA HATUA- Leo hii unaweza kuwa mwenye Haki kama Habili kwa njia ya Upatanisho ambayo Mungu aliianzisha kwa njia ya Damu ya Yesu, Mungu anakupenda hivyo ameamua akusitiri kwasababu anakupenda – 1Petro 4:8. Lakini pia Leo hii unaweza UKACHAGUA kuwa MUASI kama Kaini kwa kujibunia njia zako za kumpendeza Mungu bila Damu-Waebrania 9:22

BY
APOSTLE  ELIYA
THE EPANGELIA CHURCH
MAKULU-DODOMA

0753 011 774

SOMO #4. KITABU CHA VIZAZI

SOMO #4. KITABU CHA VIZAZI
Andiko Kuu-Mwanzo sura yote ya 5

UTANGULIZI
Mwanadamu Mteule Atakufa (Na) Kuhuzunika (Lakini) M’barikiwa Atashuka (Na) Kufundisha (Kuwa) Kifo chake kitawaletea Wapotevu Faraja”. Sentensi hii ni ufupisho wa ujumbe uliomo kwenye Sura ya 5 ya kitabu cha Mwanzo.

  1.   1. MAJINA YA VIZAZI (Kabla ya Yesu)

·         Adam(930)  - Mtu (Mwanadamu)
·         Sethi(912) - Mteule
·         Enoshi(905) – Atakufa  (Na)
·         Kenani(910) – Kuhuzunika

LAKINI

·         Mahalaleli(895) – M’barikiwa
·         Yaredi(962) – Atashuka (Na)
·         Henoko(365) – Kufundisha (Kuwa)
·         Methusela(969) – Kifo chake kitawaletea
·         Lameki(777) - Wapotevu
·         Nuhu (950) - Faraja

Mungu alificha unabii wa ujio wa mkombozi wa ulimwengu, Ishara alikuwa METHUSELA-kwamba mwaka atakaokufa kutakuwa na Gharika, lakini kwa Rehema za Mungu ndio maana aliishi miaka mingi kuliko wote.

Huu ni uzao wa Adam, hakuna aliyefikisha miaka elfu moja (Isipokua Henoko alitwaliwa), hii inaonyesha kulikua na asili ya kupungukiwa na utukufu kwasababu ya Dhambi.Pamoja na hayo Mungu aliahidi atakuja mtu atakaeanzisha uzao mpya wa milele.

2.   2. KUZALIWA UPYA (Wakati wa Yesu)
  • ·         Tumeona maana za majina kumi ya kizazi cha Adamu, majina yalikuwa na ujumbe wa Injili uliojificha ndani yake,kwamba ingawa mwanadamu alianguka lakini yupo atakaewafariji.

·         Jina la Mahalaleli na Yaredi yanaleta ujumbe kuwa Yesu atashuka kutoka Mbinguni – Yohana 3:13, 6:38,10:10b
·         Kama hili andiko linavyosema- Yohana 6:42-47-wengi hawakumuamini, walijua Yesu ni Mtu wa kawaida sana, lakini Yesu alitaka wamuamini ili awasamehe Dhambi zipate kuja nyakati za Kuburudishwa.
  • ·         Habari njema ni kwamba wote waliompokea aliwafanya wawe watoto halali wa Mungu- Yohana 1:11-13, huku ndio kunaitwa kuzaliwa upya ua mara ya pili-Yohana 3:3

·         Vizazi vile kumi vya mwanzo viliharibika, walikua na asili ya Adam ya uasi, lakini Mungu anataka kuanzisha uzao mpwa wenye asili ya Yesu aliyetoka Juu.
·         Siku moja umati ulimuimbia Yesu “Hosana M’barikiwa ajae kwa jina Bwana”-Mathayo 21:9, hii kauli ilionyesha imani yao kwa Yesu, wale ambao waliendelea kugoma kumuamini aliwaonya-Mathayo 23:39.
  • ·         Yesu ni Mtu pekee aliyetumwa kuwapa tuwapa tumaini jipya wanadamu baada ya kuwa wamefanya dhambi, Yesu alikuja kwa wakati mtimilifu-hakuwahi wala hakuchelewa.


3  3.   UZAO MTEULE (Baada ya Yesu)
·         Mwaka huu, kwa watanzania, tunatumiaje ujumbe wa kitabu cha vizazi vya Adamu?
·         Mtume Paulo anaona siri ya ujio wa Yesu wenye kufariji kwa kutuondolea dhambi- Wafilip 2:6-9. Ujio wa Yesu ulimpelekea auawe kifo cha Msalaba, kifo chake ni malipo ya utumwa wetu ndio maana ametuletea FARAJA .
  • ·         Mtume Paulo anatilia mkazo ujio wa Bwana Yesu – Wakolosai 1:22- Yesu alitakiwa aje AFE ili kifo chake kilete upatanisho.

·         Leo hii unaweza kupatanishwa na kuwa na Faraja, wanadamu tupo katika hali ya jina la Enoshi, lakini Mungu anataka tuishi na hali ya Nuhu kwa sababu ya Methusela.
·         Kila mbegu inapokufa ndipo huzaa aina nyingi ya asili yake, sawa na Methusela-kifo cha Yesu kinawafanya wengi wawe wenye Haki kwa kumuamini tu.
  • ·         Mtume Petro anasema tutubu zije nyakati za kuburudishwa-Mdo 3:19. Leo hii unaweza ukaburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana Yesu, kwasababu kifo chake kimeleta Faraja.

·         Dhumuni kuu la Yesu kuja Duniani ni kuokoa wenye dhambi – 1 Timontheo 1:15,Luka 19:10, usiogope kumkubali Yesu,dhambi zako hazijamshangaza Mungu kwani anazijua, anakusubiri utubu akusamehe.

4  4.    HITIMISHO
CHUKUA HATUA;- Mpango wote huo Mungu alioutengeneza unaweza ukaukubali au ukaukataa, lakini LEO HII,MUDA HUU unaosoma unaweza kuwa na Faraja la maisha yako yako hapa Duniani hata baada ya kufa.


Warumi 10:9-10; Unaweza kumuamini Mungu  kwa alichokifanya kupitia Yesu kwa KUAMINI MOYONI na KUKIRI KINYWANI kama maandiko yanavyosema. Kama upo tayari kuamini fautisha sara hii ya toba;       Sema “Ee Mungu Baba, wewe ni mwenye haki, mimi ni mkosaji, hivyo naomba unisamehe.Ninaamini moyoni kua ulimfufua Yesu toka wafu, na ninakiri kuwa Yesu ni Bwana na kuwa ni Mwana wa Mungu”.Amen

SOMO#5. SAFINA NA DHABIHU YA NUHU

SOMO#5. SAFINA NA DHABIHU YA NUHU
Andiko Kuu: Mwanzo sura yote ya 6,7,8 na 9

1.       NITAFUTILIA MBALI KILA KITU (Kabla ya Yesu)
·         Mungu alimwambia Nuhu mwisho wa kila kitu umefika, kwasababu ya Dhambi.Mungu alighairi kuwa amemuumba mtu, hakuweza kuvumilia uozo wa dhambi za mwanadamu akasema ataangamiza kila kitu ISIPOKUWA kiumbe kikamilifu, chenye haki hakitaangamia.
·         Kwasababu Mungu ni mwenye Haki anapotaka kuhukumu hua ni lazime aonye kwanza kisha kwa wanaokubali maonyo hua anawatengenezea namna  ya kua salama wakati wengine wakiadhibiwa kwa maamuzi walioamua.
  • ·         Mpango wa kuwaepusha watii na kuwaadhibu waasi ni SAFINA, wote waliokubali maonyo na kutii na kumuamini Mungu kwamba anachosema ni kweli ataadhibu dhambi akawaandalia sehemu salama ya kuwasitiri – safina.
  • ·         Nuhu alikuwa MKAMILIFU (mwenye HAKI), lakini ukamilifu wake hakuupata kwa ujanja wake bali IMANI – kwamba aliamini Mungu alichomwambia – Mwanzo 7:1
  • ·         Safina ilikuwa na sifa moja kubwa sana – iliweza kuhimili gharika yote, kikamilifu, na kuwahifadhi salama waliondani yake- mwanzo 8:13.Kama watu wangelimuamini Mungu anachosema kua ni kweli wangeingia kwenye safina  na wote wangekua salama kwani safina ilikuwa na uwezo wa kuhimili mishindo yote ya Gharika.
  • ·         Wote walioingia Safinani walitoka salama kwani safina iliwahifadhi, ikawafunika- Mwanz 8:15-19

·         Ni kitu gani kinachotuonyesha kwamba Nuhu alikuwa mwenye Haki?-soma mwanzo 8:20-21-Tabia ya Nuhu ilikuwa ni kutoa sadaka ya KUTEKETEZWA, alimwaga Damu ya wanyama, hii ilimfanya awe mwenye Haki, na Mungu aliposikia Harufu nzuri alighairi kuilaani nchi, badala yake akaibarikia.
  • ·         Inavyoonyesha njia pekee ya kupata Neema machoni pa Mungu ni kumwaga Damu ya mnyama asiye na Hatia kama alivyofanya Nuhu, na kwasababu hiyo alipata neema ya kuingia kwenye safina. Mungu alitaka kianze kizazi kipya cha Haki toka kwa Nuhu mara baada ya Gharika- Mwanzo 6:18
  • ·         Lakini huu uzao a Nuhu ambao Mungu alitegemea utakua wenye Haki, baada ya Gharika ulitenda dhambi tena- mwanzo 9:20-22, kukawa na laana tena. Huu udhaifu wa anguko unamfanya Mungu aandae njia ya kukomesha dhambi kikamilifu kwa kumtoa mtoto wake wa pekee, ambaye ni kondoo wa kweli – Isaya 43:25

2.       SAFINA NA DHABIHU (Wakati wa Yesu)
·        
  • Yesu ndie safina ya kweli, kwamba ukiwa ndani yake utakuwa salama- Yohana 15:7-8, Yesu alikuwa akizungumza na Martha maneno haya-Yohana 11:25-26, ingawa alimuuliza swali la muhimu sana – Unayasadiki hayo? Hili swali ni la muhimu sana kwani Imani ndio inayosukuma matendo. Kama Nuhu alitoa Sadaka kwasababu alimuamini Mungu.
  • ·         Katika sala ya Yesu- Yohana 17:21, Yesu alikua akiwaalika watu kwa maombi-kwamba watu wakutane na Mungu ndani ya Yesu.Njia ya kukutana na Mungu ni Yesu.

·         Yesu ni mtu pekee aliyeweza kuhimili adhabu/kipigo cha Mungu, ndio maana ukiwa ndani yake uko salama kwani ameweza kuhimili mapigo ya Mungu –Isaya 53:10. Adhabu kubwa ambayo Yesu alitamani aiepuke ni kule kutengana na Mungu kwasababu ya Dhambi, ndio maana akasema “ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke-Luka 22:42-44”.

  • ·         Nuhu Mwenye Haki; Nuhu alipata haki kwa kuamini njia aliyoitoa Mungu ya kumkaribia-Kumwaga Damu ya mwana kondoo asiye na Hatia.Habari njema ni kwamba Yesu alipokuja alitaka kila mmoja awe kama Nuhu kwani Yeye ndiye Kondoo wa kweli, hafuniki dhambi bali huondoa kabisa.
  • ·         Kama vile Nuhu alivyoishi wakati wa Gharika na Baada ya Gharika, ndivyo Yesu alivyowaambia watu wa kipindi kile “aniaminiye mimi ajapokufa ataishi”-Yohana 11:25, pia Yohana 5:24. Ninajua kuna watu hawakumuamini, ni sawa na wakati wa Nuhu watu hawakumuamini Mungu na Nuhu pia, kwasababu walikua hawajawahi kuona mvua, hivyo walidhani wangepata uhalali wa kufanya dhambi, eti kwa sababu hawajawahi kuoona Mvua.

·         Yesu alitofautisha makundi mawili ya watu – walioamini na wasioamini kwenye –Yohana 6:36-37, aliwahakikishia kwamba yeyote atakae mfuata hatamtupa kamwe.

3.       KIFUNIKO (Baada ya Yesu)
  • ·       Mtume Paulo: Anasema hakuna Hukumu (Gharika) kwa wanaomwamini Yesu –Rumi 8:1, kwasababu Mungu ameshaihukumu Dhambi kwenye mwili wa Yesu-Rumi 8:3.

·         Ukiwa ndani ya yesu, Mungu anakuangalia kitofauti, hata kama ulikuwa mtukanaji na mwenye jeuri Mungu atakusamehe-1 Timotheo 1:13-14 (Kwasababu umefunikwa na Yesu)
·         Kwanini Yesu ni wa muhimu sana? -1Timotheo 2:5-6, ndiye mpatanishi kati ya Mungu na Mtu, na sababu iliyomfanya awe mpatanishi ni kutoa mwili wake ambao ni mkamilifu uwe KAFARA. Kama Nuhu alivyotoa kondoo Mungu akasikia Harufu nzuri, ndivyo Mungu anavyotufurahia sisi katika Kristo Yesu -2Korintho 2:15-16.
  • ·         Safina na Dhabihu: Safina ilikuwa ni mfano wa Yesu, ukiingia ndani ya Yesu uko salama na utakutana na Mungu ndani ya Yesu kwani Mungu hukaa ndani ya Yesu-2Korintho 5:19, ukiwa ndani ya Yesu, Yesu anaweka Maneno yake ndani yako – Yohana 15:10, hivyo utatakiwa kutii.
  • ·          Kuhusu Dhabihu ya Nuhu-Leo hii hatuna dhabihu ya kumshawishi Mungu aridhike na Harufu nzuri kama wakati wa Nuhu, hata hivyo ile ulikuwa ni mfano tu-Dhabihu ya kweli ni Yesu-Waebrania 10:8-10. Wewe ulitakiwa utoe Dhabihu safi kwa Mungu lakini Mungu ameamua akutolee badala yako, wewe unachotakiwa kufanya ni  kukubali tu alichokifanya Mungu, na hapo inatakiwa IMANI-Waebrani 11:6-7, kwamba ukimwamini Yesu umefutiwa Dhambi zote.


4.      HITIMISHO
INGIA NDANI YA YESU LEO - Ingia ndani ya Yesu, Mungu anapomuadhibu Yesu uwe salama.

TOA DHABIHU KAMILIFU – Huna dhabihu kamilifu na huwezi kupata, hivyo ikubali Dhabihu aliyoitoa Mungu ili mpatane na yeye, dhabihu mkamilifu/safi ni Yesu aliyetolewa na Mungu.

Thursday, January 15, 2015

KAKOBE: UCHAGUZI USIFANYIKE JUMAPILI


  1.  
    Juzi Jumapili 11.1.2015, maelfu ya waumini wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) linaloongozwa na Askofu Mkuu Zachary Kakobe, walivaa TShirt zenye maandishi “UCHAGUZI USIFANYIKE JUMAPILI”, katika ibada maalum ya maombi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Katika maombi hayo maalum yaliyofanyika katika Kanisa hilo lililoko barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar-Es-Salaam; Askofu Kakobe aliwaongoza waumini hao kumshukuru Mungu kwa ajili ya roho ya usikivu iliyomwingia Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyetangaza katika hotuba yake ya Mwaka Mpya kwamba Kura ya Maoni kuhusu Katiba pendekezwa itafanyika ALHAMISI 30.4.2015.

    Katika maombi hayo, Askofu Kakobe alisema kwamba kwa miaka mingi, kilio cha Wakristo wengi kimekuwa kwamba siku ya kupiga kura isiwe siku ya Jumapili inayoingilia haki ya Kikatiba ya kupiga kura na uhuru wa kuabudu kwa Wakristo usiotakiwa kuingiliwa na mamlaka ya nchi, kama inavyoainishwa katika Katiba, Ibara ya 5 (1) na Ibara ya 19 (2); hivyo hawana budi kumshukuru Mungu kwa jinsi ambavyo Serikali ilivyosikia kilio chao, kwa kutangaza kwamba Kura ya maoni itafanyika Siku ya Alhamisi, badala ya siku iliyozoeleka ya Jumapili.


    Kwa msingi huohuo, waumini hao walimwomba Mungu katika maombi hayo kwamba, Serikali izidi kuwa na usikivu na hivyo kutangaza siku ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ambayo haitakuwa Jumapili, wala Jumamosi wala Ijumaa; ambazo ni siku za kuabudu kwa waumini wa madhehebu yote ya Wakristo, Wasabato na Waislamu; ili Wakristo na Watanzania wote kwa ujumla wapate kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura. Askofu Kakobe alisema kwamba imekuwa kawaida kwa wanasiasa kujiuliza kwa nini watu wengi hawajitokezi siku ya kupiga kura, bila kuwaza juu ya kujenga mazingira ya kuwawezesha watu wote kupiga kura, kwa kuifanya siku ya kura kutokuwa siku ya Ibada.


    Askofu Kakobe alitoa mifano ya nchi zinazotuzunguka ambazo hufanya Uchaguzi wao Mkuu kuwa siku ambayo siyo siku ya Ijumaa, Jumamosi au Jumapili; ili watu wengi wajitokeze kupiga kura, kwa mfano Zambia ambayo itakuwa na Uchaguzi siku ya JUMANNE 20.1.2015, baada ya Rais wao aliyechaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa JUMANNE 20.9.2011, kufariki. Vilevile alitaja siku za Uchaguzi Mkuu uliopita wa nchi nyingine kama ifuatavyo: Malawi (JUMANNE 20.5.2014); Zimbabwe (JUMATANO 31.7.2013); Kenya (JUMATATU 4.3.2013); Uganda (JUMATATU 18.2.2011); Rwanda (JUMATATU 9.8.2010); Burundi (JUMATATU 28.6.2010); na Afrika Kusini (JUMATANO 7.5.2014); na baada ya kutaja mifano hiyo, aliwaongoza waumini kumwomba Mungu ili kwamba Serikali iwe na usikivu katika jambo hili pia, na kutangaza Siku ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu wa 2015 katika nchi yetu Tanzania, kuwa siku yoyote ambayo siyo Jumapili, Jumamosi, wala Ijumaa; na kuifanya siku hiyo kuwa siku ya mapumziko maalum yenye kazi moja tu kuu, ya kupiga kura.





























    Attached Thumbnails Attached ThumbnailsClick image for larger version. 

Name: 3C9A0956.jpg 
Views: 0 
Size: 201.9 KB 
ID: 218234   Click image for larger version. 

Name: 4B7A0898.jpg 
Views: 0 
Size: 315.5 KB 
ID: 218235   Click image for larger version. 

Name: 4B7A0899.jpg 
Views: 0 
Size: 288.7 KB 
ID: 218236  Click image for larger version. 

Name: 4B7A0900.jpg 
Views: 0 
Size: 334.1 KB 
ID: 218237   Click image for larger version. 

Name: 4B7A0901.jpg 
Views: 0 
Size: 297.8 KB 
ID: 218238   Click image for larger version. 

Name: 4B7A0908.jpg 
Views: 0 
Size: 351.1 KB 
ID: 218239  Click image for larger version. 

Name: 4B7A0909.jpg 
Views: 0 
Size: 339.3 KB 
ID: 218240   Click image for larger version. 

Name: 4B7A0910.jpg 
Views: 0 
Size: 355.7 KB 
ID: 218241   Click image for larger version. 

Name: 4B7A0944.jpg 
Views: 0 
Size: 332.8 KB 
ID: 218242  Click image for larger version. 

Name: 4B7A0945.jpg 
Views: 0 
Size: 290.5 KB 
ID: 218243   Click image for larger version. 

Name: 4B7A0947.jpg 
Views: 0 
Size: 296.9 KB 
ID: 218244   Click image for larger version. 

Name: 4B7A0948.jpg 
Views: 0 
Size: 331.9 KB 
ID: 218245  Click image for larger version. 

Name: 4B7A0999.jpg 
Views: 0 
Size: 300.3 KB 
ID: 218246   Click image for larger version. 

Name: 3C9A0971.jpg 
Views: 0 
Size: 259.4 KB 
ID: 218247   Click image for larger version. 

Name: 3C9A1004.jpg 
Views: 0 
Size: 214.6 KB 
ID: 218248SOURCE: JAMII FORUM  

Wednesday, January 14, 2015

NILIMPENDA MSICHANA KUMBE NI JINI NA AMENITESA SANA

     


                Naitwa Patrick Bundala niko mailimoja Kibaha ni mwajiriwa wa serikali ni Askari ila nyumbani ni Tabora na huku niko kikazi tu, nina mke na watoto 4. Kuna kitu kibaya kilinitokea nikiwa kozi ya uongozi huko Zanzibar mwaka 2009, tukiwa kozi tulikua tunapata mapumziko siku za weekend hivyo kutumia nafasi hiyo kwenda kutembea beach na siku hiyo ya tukio baya  ilikua jumamosi ambapo tuliondoka tukiwa wengi tu kama 50 na kwenda maeneo ya kilimani karibu na migombani ambako kuna beach nzuri sana na siku ya jumamosi jioni beach huwa inajaa watu wa kila aina na siku hiyo haikua mara ya kwanza mimi kwenda huko beach kwani kila weekend lazima niende huko beach ili kuburudisha macho na kuangalia mazingira na watu maana mimi kwa Zanzibar ilikua mara ya kwanza kwenda hivyo kwa umaarufu wa Zanzibar nilitaka hadi natoka huko niwe na cha kuwasimulia huku nyumbani kumbe ilikua bahati mbaya sana kwangu siku hiyo, wakati siku hiyo tumefika beach tulitawanyika kila mtu eneo analotaka na wengine walienda kuogelea na mimi licha ya kufahamu kuogelea lakini siku hiyo sikutaka kuogelea lakini nilitaka kutafuta binti mzuri ili nimtongoze na tuwe wapenzi na nilienda pembeni kidogo eneo ambalo watu walikua wachache na kukaa mkao wa kuangalia watu na baada kama ya dakika 40 alipita dada mmoja aliyevaa ninja akiwa ni nusu mwaarabu na nusu mwafrika na nikajikuta namtamani sana alinipita kidogo na kugeuka na kuniangalia na mimi nikaona hiyo ndio nafasi ya kumwogelesha na kikamwita akaja na ajabu sikumwambia chochote lakini sijui aligundua kuwa natafuta mwanamke maana alisogea na kunisalimia na akakaa pembeni yangu na kunichangamkia sana, na kwa sababu nilitaka mpenzi nilidhani kuwa huyo ni changudoa ambaye huwa anaenda kutafuta wanaume beach, Baada ya kukaa tuliendelea na story na ajabu yule dada akaniambia mwenyewe kuwa amenipenda sana maana nimemjali na mimi nikaona kuwa  hiyo nafasi ya kumpata mrembo yule siwezi kuipoteza na muda huo huo nikaanza kumwambia mambo ya mapenzi maana nilidhani ni kahaba na nilipomwambia hivyo alicheka na kusema amekubali ila anataka ajue kwanza jina langu, kwa sababu ya kuepusha maswali ya kuulizwa zaidi na ili asije akakataa kwa sababu ya majina yangu ya kikristo japokua hata kanisani sijawahi kwenda nilimwambia kuwa mimi naitwa Saleh Juma na yeye akasema anaitwa Munira, akafurahi sana na kusema kuwa nafaa sana na amefurahi sana kukutana na mimi. Sikutaka kuopoteza nafasi hiyo nilimwambia kuwa tunaweza kuwa wote usiku ule? akasema mbona mapema sana nikasema kwa sababu amenivutia sana, akaongea kwa madaha na kusema amekubali na kwa sababu ya binti yule nilisahau yote na kumwambia tuondoke twende tukaongelee guest house akakubali na tukaondoka saa ile ilie na kupanda gari za airport na tukashukia mkunazini na kutafuta gest tulipata na nikaalipia na tukaingia chumbani na lengo langu japokua nililipia chumba hadi asubuhi lakini nilitaka tu tufanye mapenzi na niondoke kuwahi foleni ya usiku kule kozi, tukiwa chumbani tulianza michezo ya kimapenzi na akanivulisha nguo zote na mimi nikamvulisha nguo zote isipokua nguo ya ndani na baadae kidogo akashuka kitandani na kusimama huku akinitazama kwa macho makali sana nikaanza kushtuka na ghafla kibanio chake cha nywele kikaachia ghafla na tukio la ajabu sana likatokea nywele zake zikalefuka na kuongezeka zikajaa chumba chote, nikiwa nimejilaza kitandani nilikaa ghafla na baada ya muda kidogo zile nywele zilisinyaa na kuwa za kawaida na kile kibanio kijiweka mahali pake na kubana nywele, Munira akasema kuwa yeye ni jini na anataka tu damu yangu kwani ana njaa sana nilikimbilia mlangoni ghafla huku nikiwa uchi na kujaribu kufungua mlango lakini haukufunguka japokua hatukufunga, akasema siwezi kumtoroka hata siku moja na kwa sababu mimi nimempenda na yeye amependa nyama yangu na damu yangu, nilijikaza lakini nilikua hoi karibu na kuzimia na nikaona njia iliyobaki ni kupiga kele ili watu waje kunisaidia na nilipopiga kele sauti haikwenda kokote maana nilipanua mdogo kwa nguvu zangu zote lakini sauti iliyotoka ni kama namng'ong'eza mtu kiukweli nikikua kama nimechanganyikiwa na niliposhidwa zoezi hilo niliwaza kuwa njia iliyobaki ni kulibembeleza tu lile jini na nilipoliangalia nilikuta linakwato miguuni na miguu ina manyoya kama mbuzi na meno limetoa na kuwa marefu zaidi ya rula ya kupigia mistari, Hakuwa tena yule msichana mrembo munira ambaye nilimpenda sana kwa muda mfupi, Nilimwambia yule jini anibadilishie adhabu akakataa na nilijikuta naomba maombi kwa MUNGU anihurumie na ajabu kama dakika 5 zilizofuata mlango uligogwa na ghafla lile jini likawa Munira yule wa beach na kwa sababu ya mlango kuendelea kugongwa yule jini alienda kufungua na mimi muda huo nikaanza kuvaa nguo kiaskari yaani nusu dakika nimeshavaa zote, Alikua ni dada wa mapokezi akileta chakula chipsi mayai na  na soda na munira kwa ujanja akasimama katikati ya mlango na kuanza kusema sisi hatukuagiza chochote na muda huo huo nikwamwambia yule dada aingie ndani maana kuna kitu nataka kumtuma akaja na alipokaribia tu nikatoka ghafla na kumwaga kile chakula chote huku nikisema kuwa yule dada sio mtu ni jini yule dada mhudumu naye akaakimbia na sikujua kilichoendelea ila nadhani yule jini alipotea muda huohuo maana nilipofika tu nje nilimkuta akinisubiri na kuniambia sina ujanja wa kumtoroka na kwasababu ilikua ni barabarani na watu wengi wanapita nilipiga kelele na kusema jamani niokoeni na vijana fulani waliokua wanapita mmoja wao akasema wewe umekua chizi yaani unaongea peke yako niliondoka kwa kukimbia kama mita 100  na kupanda gari ambayo ilinipekeka hado kambini na nilipofika tu kambini nilimwona tena yule jini na akaniambia kuwa kuniua lazima anaiue tu tena usiku uleule nilipiga tena kele na askari wenzangu wakaanza kucheka sana wakisema nimepandisha mashetani na nikawaelezea kuwa sijapandisha chochote ila ni hali halisi na nikawasimulia mwanzo wa tukio hadi mwisho na usiku huo sikulala maana usiku wa saa 7 nilimwona tena yule munira jini na nikapiga kelele na wenzangu kwa hasira wakasema nisiwasumbue lakini mmoja wao ambaye ameokoka akaniambia namhitaji YESU ili niwe huru. Kwa sababu ya shida nilimwambia niko tayari kuokoka kuanzia sekunde ile, akasema kuwa wao wana kundi lao la maombi hapo kozi ambalo ni kundi la waliookoka kutoka makanisa mbalimbali na huwa wana ratiba ya maombi hivyo muda ukifika atanijurisha ili twende wote na muda huo akaniombea ulinzi wa MUNGU. Muda wa maombi ulipofika tulikwenda na niliombewa na wakati wa maombezi ikasikika sauti kuwa ipo siku watanipata tu. lakini namshukuru MUNGU sana maana nilipona tangu saa ile na nimeendelea na wokovu hadi leo na hakuna chochote walichofanya. Nampenda YESU na namshukuru sana kwa kuniponya na kuniokoka pia kuniepusha na mabaya yale. MUNGU akubariki sana ndugu mtumishi wa MUNGU.

SOURCE: Miasha ya Ushindi