SOMO#5. SAFINA NA DHABIHU YA NUHU
Andiko Kuu: Mwanzo sura yote ya 6,7,8 na 9
1.
NITAFUTILIA MBALI KILA KITU (Kabla ya Yesu)
·
Mungu alimwambia Nuhu mwisho wa kila kitu
umefika, kwasababu ya Dhambi.Mungu alighairi kuwa amemuumba mtu, hakuweza
kuvumilia uozo wa dhambi za mwanadamu akasema ataangamiza kila kitu ISIPOKUWA
kiumbe kikamilifu, chenye haki hakitaangamia.
·
Kwasababu Mungu ni mwenye Haki anapotaka
kuhukumu hua ni lazime aonye kwanza kisha kwa wanaokubali maonyo hua
anawatengenezea namna ya kua salama
wakati wengine wakiadhibiwa kwa maamuzi walioamua.
- · Mpango wa kuwaepusha watii na kuwaadhibu waasi ni SAFINA, wote waliokubali maonyo na kutii na kumuamini Mungu kwamba anachosema ni kweli ataadhibu dhambi akawaandalia sehemu salama ya kuwasitiri – safina.
- · Nuhu alikuwa MKAMILIFU (mwenye HAKI), lakini ukamilifu wake hakuupata kwa ujanja wake bali IMANI – kwamba aliamini Mungu alichomwambia – Mwanzo 7:1
- · Safina ilikuwa na sifa moja kubwa sana – iliweza kuhimili gharika yote, kikamilifu, na kuwahifadhi salama waliondani yake- mwanzo 8:13.Kama watu wangelimuamini Mungu anachosema kua ni kweli wangeingia kwenye safina na wote wangekua salama kwani safina ilikuwa na uwezo wa kuhimili mishindo yote ya Gharika.
- · Wote walioingia Safinani walitoka salama kwani safina iliwahifadhi, ikawafunika- Mwanz 8:15-19
·
Ni kitu gani kinachotuonyesha kwamba Nuhu
alikuwa mwenye Haki?-soma mwanzo 8:20-21-Tabia ya Nuhu ilikuwa ni kutoa sadaka
ya KUTEKETEZWA, alimwaga Damu ya wanyama, hii ilimfanya awe mwenye Haki, na
Mungu aliposikia Harufu nzuri alighairi kuilaani nchi, badala yake akaibarikia.
- · Inavyoonyesha njia pekee ya kupata Neema machoni pa Mungu ni kumwaga Damu ya mnyama asiye na Hatia kama alivyofanya Nuhu, na kwasababu hiyo alipata neema ya kuingia kwenye safina. Mungu alitaka kianze kizazi kipya cha Haki toka kwa Nuhu mara baada ya Gharika- Mwanzo 6:18
- · Lakini huu uzao a Nuhu ambao Mungu alitegemea utakua wenye Haki, baada ya Gharika ulitenda dhambi tena- mwanzo 9:20-22, kukawa na laana tena. Huu udhaifu wa anguko unamfanya Mungu aandae njia ya kukomesha dhambi kikamilifu kwa kumtoa mtoto wake wa pekee, ambaye ni kondoo wa kweli – Isaya 43:25
2.
SAFINA NA DHABIHU (Wakati wa Yesu)
·
- Yesu ndie safina ya kweli, kwamba ukiwa ndani yake utakuwa salama- Yohana 15:7-8, Yesu alikuwa akizungumza na Martha maneno haya-Yohana 11:25-26, ingawa alimuuliza swali la muhimu sana – Unayasadiki hayo? Hili swali ni la muhimu sana kwani Imani ndio inayosukuma matendo. Kama Nuhu alitoa Sadaka kwasababu alimuamini Mungu.
- · Katika sala ya Yesu- Yohana 17:21, Yesu alikua akiwaalika watu kwa maombi-kwamba watu wakutane na Mungu ndani ya Yesu.Njia ya kukutana na Mungu ni Yesu.
·
Yesu ni mtu pekee aliyeweza kuhimili
adhabu/kipigo cha Mungu, ndio maana ukiwa ndani yake uko salama kwani ameweza
kuhimili mapigo ya Mungu –Isaya 53:10. Adhabu kubwa ambayo Yesu alitamani
aiepuke ni kule kutengana na Mungu kwasababu ya Dhambi, ndio maana akasema
“ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke-Luka 22:42-44”.
- · Nuhu Mwenye Haki; Nuhu alipata haki kwa kuamini njia aliyoitoa Mungu ya kumkaribia-Kumwaga Damu ya mwana kondoo asiye na Hatia.Habari njema ni kwamba Yesu alipokuja alitaka kila mmoja awe kama Nuhu kwani Yeye ndiye Kondoo wa kweli, hafuniki dhambi bali huondoa kabisa.
- · Kama vile Nuhu alivyoishi wakati wa Gharika na Baada ya Gharika, ndivyo Yesu alivyowaambia watu wa kipindi kile “aniaminiye mimi ajapokufa ataishi”-Yohana 11:25, pia Yohana 5:24. Ninajua kuna watu hawakumuamini, ni sawa na wakati wa Nuhu watu hawakumuamini Mungu na Nuhu pia, kwasababu walikua hawajawahi kuona mvua, hivyo walidhani wangepata uhalali wa kufanya dhambi, eti kwa sababu hawajawahi kuoona Mvua.
·
Yesu alitofautisha makundi mawili ya watu –
walioamini na wasioamini kwenye –Yohana 6:36-37, aliwahakikishia kwamba yeyote
atakae mfuata hatamtupa kamwe.
3.
KIFUNIKO (Baada
ya Yesu)
- · Mtume Paulo: Anasema hakuna Hukumu (Gharika) kwa wanaomwamini Yesu –Rumi 8:1, kwasababu Mungu ameshaihukumu Dhambi kwenye mwili wa Yesu-Rumi 8:3.
·
Ukiwa ndani ya yesu, Mungu anakuangalia
kitofauti, hata kama ulikuwa mtukanaji na mwenye jeuri Mungu atakusamehe-1
Timotheo 1:13-14 (Kwasababu umefunikwa na Yesu)
·
Kwanini Yesu ni wa muhimu sana? -1Timotheo
2:5-6, ndiye mpatanishi kati ya Mungu na Mtu, na sababu iliyomfanya awe
mpatanishi ni kutoa mwili wake ambao ni mkamilifu uwe KAFARA. Kama Nuhu
alivyotoa kondoo Mungu akasikia Harufu nzuri, ndivyo Mungu anavyotufurahia sisi
katika Kristo Yesu -2Korintho 2:15-16.
- · Safina na Dhabihu: Safina ilikuwa ni mfano wa Yesu, ukiingia ndani ya Yesu uko salama na utakutana na Mungu ndani ya Yesu kwani Mungu hukaa ndani ya Yesu-2Korintho 5:19, ukiwa ndani ya Yesu, Yesu anaweka Maneno yake ndani yako – Yohana 15:10, hivyo utatakiwa kutii.
- · Kuhusu Dhabihu ya Nuhu-Leo hii hatuna dhabihu ya kumshawishi Mungu aridhike na Harufu nzuri kama wakati wa Nuhu, hata hivyo ile ulikuwa ni mfano tu-Dhabihu ya kweli ni Yesu-Waebrania 10:8-10. Wewe ulitakiwa utoe Dhabihu safi kwa Mungu lakini Mungu ameamua akutolee badala yako, wewe unachotakiwa kufanya ni kukubali tu alichokifanya Mungu, na hapo inatakiwa IMANI-Waebrani 11:6-7, kwamba ukimwamini Yesu umefutiwa Dhambi zote.
4.
HITIMISHO
INGIA NDANI YA YESU LEO - Ingia
ndani ya Yesu, Mungu anapomuadhibu Yesu uwe salama.
TOA DHABIHU KAMILIFU – Huna dhabihu
kamilifu na huwezi kupata, hivyo ikubali Dhabihu aliyoitoa Mungu ili mpatane na
yeye, dhabihu mkamilifu/safi ni Yesu aliyetolewa na Mungu.
No comments:
Post a Comment