SOMO #4. KITABU CHA VIZAZI
Andiko Kuu-Mwanzo sura yote ya 5
UTANGULIZI
“Mwanadamu Mteule Atakufa (Na) Kuhuzunika
(Lakini) M’barikiwa Atashuka (Na) Kufundisha (Kuwa) Kifo
chake kitawaletea Wapotevu Faraja”. Sentensi hii ni ufupisho wa
ujumbe uliomo kwenye Sura ya 5 ya kitabu cha Mwanzo.
- 1. MAJINA YA VIZAZI (Kabla ya Yesu)
·
Adam(930)
- Mtu (Mwanadamu)
·
Sethi(912) - Mteule
·
Enoshi(905) – Atakufa (Na)
·
Kenani(910) – Kuhuzunika
LAKINI
·
Mahalaleli(895) – M’barikiwa
·
Yaredi(962) – Atashuka (Na)
·
Henoko(365) – Kufundisha (Kuwa)
·
Methusela(969) – Kifo chake kitawaletea
·
Lameki(777) - Wapotevu
·
Nuhu (950) - Faraja
Mungu alificha unabii wa ujio
wa mkombozi wa ulimwengu, Ishara alikuwa METHUSELA-kwamba mwaka atakaokufa
kutakuwa na Gharika, lakini kwa Rehema za Mungu ndio maana aliishi miaka mingi
kuliko wote.
Huu ni uzao wa Adam, hakuna
aliyefikisha miaka elfu moja (Isipokua Henoko alitwaliwa), hii inaonyesha
kulikua na asili ya kupungukiwa na utukufu kwasababu ya Dhambi.Pamoja na hayo
Mungu aliahidi atakuja mtu atakaeanzisha uzao mpya wa milele.
2. 2. KUZALIWA UPYA (Wakati wa Yesu)
- · Tumeona maana za majina kumi ya kizazi cha Adamu, majina yalikuwa na ujumbe wa Injili uliojificha ndani yake,kwamba ingawa mwanadamu alianguka lakini yupo atakaewafariji.
·
Jina la Mahalaleli na Yaredi yanaleta ujumbe
kuwa Yesu atashuka kutoka Mbinguni – Yohana 3:13, 6:38,10:10b
·
Kama hili andiko linavyosema- Yohana
6:42-47-wengi hawakumuamini, walijua Yesu ni Mtu wa kawaida sana, lakini Yesu
alitaka wamuamini ili awasamehe Dhambi zipate kuja nyakati za Kuburudishwa.
- · Habari njema ni kwamba wote waliompokea aliwafanya wawe watoto halali wa Mungu- Yohana 1:11-13, huku ndio kunaitwa kuzaliwa upya ua mara ya pili-Yohana 3:3
·
Vizazi vile kumi vya mwanzo viliharibika,
walikua na asili ya Adam ya uasi, lakini Mungu anataka kuanzisha uzao mpwa
wenye asili ya Yesu aliyetoka Juu.
·
Siku moja umati ulimuimbia Yesu “Hosana
M’barikiwa ajae kwa jina Bwana”-Mathayo 21:9, hii kauli ilionyesha imani yao
kwa Yesu, wale ambao waliendelea kugoma kumuamini aliwaonya-Mathayo 23:39.
- · Yesu ni Mtu pekee aliyetumwa kuwapa tuwapa tumaini jipya wanadamu baada ya kuwa wamefanya dhambi, Yesu alikuja kwa wakati mtimilifu-hakuwahi wala hakuchelewa.
3 3. UZAO MTEULE (Baada ya Yesu)
·
Mwaka huu, kwa watanzania, tunatumiaje ujumbe wa
kitabu cha vizazi vya Adamu?
·
Mtume Paulo anaona siri ya ujio wa Yesu wenye
kufariji kwa kutuondolea dhambi- Wafilip 2:6-9. Ujio wa Yesu ulimpelekea auawe
kifo cha Msalaba, kifo chake ni malipo ya utumwa wetu ndio maana ametuletea
FARAJA .
- · Mtume Paulo anatilia mkazo ujio wa Bwana Yesu – Wakolosai 1:22- Yesu alitakiwa aje AFE ili kifo chake kilete upatanisho.
·
Leo hii unaweza kupatanishwa na kuwa na Faraja,
wanadamu tupo katika hali ya jina la Enoshi, lakini Mungu anataka tuishi na
hali ya Nuhu kwa sababu ya Methusela.
·
Kila mbegu inapokufa ndipo huzaa aina nyingi ya
asili yake, sawa na Methusela-kifo cha Yesu kinawafanya wengi wawe wenye Haki
kwa kumuamini tu.
- · Mtume Petro anasema tutubu zije nyakati za kuburudishwa-Mdo 3:19. Leo hii unaweza ukaburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana Yesu, kwasababu kifo chake kimeleta Faraja.
·
Dhumuni kuu la Yesu kuja Duniani ni kuokoa wenye
dhambi – 1 Timontheo 1:15,Luka 19:10, usiogope kumkubali Yesu,dhambi zako
hazijamshangaza Mungu kwani anazijua, anakusubiri utubu akusamehe.
4 4. HITIMISHO
CHUKUA HATUA;- Mpango wote huo Mungu
alioutengeneza unaweza ukaukubali au ukaukataa, lakini LEO HII,MUDA HUU
unaosoma unaweza kuwa na Faraja la maisha yako yako hapa Duniani hata baada ya
kufa.
Warumi 10:9-10; Unaweza kumuamini
Mungu kwa alichokifanya kupitia Yesu kwa
KUAMINI MOYONI na KUKIRI KINYWANI kama maandiko yanavyosema. Kama upo tayari
kuamini fautisha sara hii ya toba; Sema
“Ee Mungu Baba, wewe ni mwenye haki,
mimi ni mkosaji, hivyo naomba unisamehe.Ninaamini moyoni kua ulimfufua Yesu
toka wafu, na ninakiri kuwa Yesu ni Bwana na kuwa ni Mwana wa Mungu”.Amen
No comments:
Post a Comment