Saturday, April 26, 2014

KILA KITABU KATIKA BIBLIA KINAMZUNGUMZIA YESU KRISTO.

BWANA YESU asifiwe.
Ubarikiwe sana ndugu popote ulipo na ubariki sana kwa kufatilia habari na mafundisho kupitia Maisha ya ushindi blog na page yetu katika facebook.


Karibu tujifunze mambo haya muhimu kwa kila mtu.

Hapa leo nazungumzia VITABU VYA BIBLIA TAKATIFU NA MAANA ZAKE na JINSI KILA KITABU KINAVYOMZUNGUMZIA BWANA YESU.



1:  MWANZO- Ni kitabu kinachozungumzia uumbaji wa KRISTO. Mwanzo sura nzima ya kwanza inazungumzia uumbaji alioufanya BWANA YESU na kwa kuthibitisha hilo angalia Yohana 1:1-3( Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa MUNGU, naye Neno alikuwa MUNGU.  Huyo mwanzo alikuwako kwa MUNGU. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. ). 
 Bila ya uumbaji wa KRISTO hakuna ambacho kingeumbwa. YESU KRISTO ni MUNGU muumbaji, tusome tena Waebrania 1:2 (mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. ).

Kitabu cha Mwanzo kinazungumzia uumbaji wa KRISTO ambaye vitu vyote aliviumba yeye.

-Tunafahamu kwamba vitu vyote viliumbwa kwa Neno na Neno ni YESU KRISTO. Hivyo YESU KRISTO ni MUNGU muumbaji wetu.



2: KUTOKA-Ni kitabu kinachomwelezea BWANA YESU kama mwanakondoo wa Pasaka. Kumbuka pasipo kumwaga damu hakuna ukombozi.


-Bila sadaka ya mwanakondoo wana wa Israeli wasingetoka utumwani Misri, na ukisoma Biblia tukio la mwisho kabla hawajatoka Misri walichinja kondoo na kupaka damu ya kondoo hao katika miimo ya milango ya nyumba zao, likatokea pigo kwa wazaliwa wa kwanza wa wamisri wote hivyo waisrael wakatoka (Kutoka 12:21-36) na hata sisi bila BWANA YESU kujitoa sadaka msalabani tusingepata wokovu.Waebrania 11:23-29



3: MAMBO YA WALAWI-Kitabu hiki kinamzungumzia YESU KRISTO kama sadaka yetu kwa ajili ya dhambi zetu. Walawi 16:30-34.( Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za BWANA. Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele. Na kuhani atakayetiwa mafuta na kuwekwa wakfu badala ya baba yake, ataufanya huo upatanisho, naye atayavaa mavazi ya kitani, yaani, yale mavazi matakatifu.
Naye atafanya upatanisho kwa ajili ya patakatifu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya hema ya kukutania, na kwa ajili ya madhabahu; naye atafanya upatanisho kwa ajili ya makuhani, na kwa ajili ya watu wote wa kusanyiko. Na amri hii itakuwa amri ya milele kwenu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kila mwaka. Naye akafanya vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa. ).


-Kumbuka kwamba yale ambayo yalitokea katika agano jipya kumhusu BWANA YESU ni yale yale ambayo yeye mwenywe alikishwa yasema katika agano la kale kupitia watumishi wake.



4:HESABU-Kitabu hiki kinamwelezea BWANA YESU kama Mwokozi aliyeinuliwa juu ili kutukomboa Hesabu 33:1-4( Hizi ndizo safari za wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa jeshi zao chini ya mkono wa Musa na Haruni.  Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya BWANA; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa.  Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa mkono wa nguvu mbele ya macho ya Wamisri wote, hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, BWANA aliokuwa amewapiga kati yao; BWANA akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo. ).

YESU ni Pasaka yetu.



5:KUMBUKUMBU LA TORATI-Kitabu hiki kinamwelezea BWANA YESU kuwa nabii wetu mkuu wa kweli Kumbukumbu 18:18( Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. )



6:YOSHUA-Kitabu hiki kinamwelezea BWANA YESU kama Jemedari wetu wa Wokovu wetu.

-Yoshua mwenyewe ni mfano wa KRISTO aliye jemedari wetu wa wokovu.Yoshua 1:1-11.

-Na hata maana ya Yoshua ni Mwokozi, na MWOKOZI wa kweli ni BWANA YESU KRISTO pekee.



7: WAAMUZI-Ni kitabu kinachomwelezea BWANA YESU kama mwamuzi wetu, Ndugu na mwamuzi wetu.

-Katika kitabu cha waamuzi, kulikuwa na waamuzi 15 na 1 wa 16 ambaye yeye alijipa uamuzi yaani Abimeleki.


Waamuzi hao 15 ni Othnieli,Ehudi,Shamgari,Debora,Baraka, Gideoni,Tola,Yairi,Yeftha,Ibzani,Eloni,Abdoni,Samsoni,Eli na Samweli.

-Waamuzi walikuwa katika makundi matatu.



A. Waamuzi wa kivita mfano Samson na Gideoni.


B. Kundi la makuhani. Mfano Eli.


C. Kundi la manabii. Mfano Samweli.


-Makundi haya matatu  ya waamuzi yako ndani ya kila aliyeokoka.

-Sisi sasa ni askari wa BWANA kwa ajili ya vita, sisi sasa ni manabii wa BWANA YESU na sasa sisi ni makuhani wa MUNGU.



8: RUTHI-ni sawasawa na waamuzi kinazungumzia habari moja , pamoja na agano ambalo BWANA YESU atalifanya. Na agano la BWANA YESU ni kweli daima.



9: SAMWELI WA 1 – Kinamwelezea BWANA YESU kama mfalme wetu, aliyetawala na atakayetawala milele.



10: SAMWELI WA 2 –Kinamwelezea YESU kama mtawala  na anaendelea kutawala , mfano licha ya Sauli kutawala lakini BWANA YESU aliendelea kutawala kupitia Daudi.

11: WAFALME NA MAMBO YA NYAKATI- Vitabu hivi pia vinaendelea kumzungumzia BWANA YESU kama mfalme anayetawala.



11: EZRA NA NEHEMIA-Vitabu hivi vinamwonyesha BWANA YESU kama mrudushaji wetu, ametukusanya tena  na pia amerudisha yaliyokuwa yamechukuliwa na adui.

Vitabu hivi mwanzo vilikuwa kitabu kimoja na vinamzungumzia BWANA katika hali sawa.



MUNGU akubariki sana.

Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

                       MUNGU akubariki sana .

                        Ni mimi ndugu yako

                          Peter M Mabula

                    Maisha ya Ushindi Ministry.

                         0714252292

No comments:

Post a Comment