Saturday, December 28, 2013

JIANDAE KUKUTANA NA MUNGU WAKO!


FALME ZA MBINGUNI NA KUZIMU, NA KURUDI KWA KRISTO
NA Angelica Zambrano

Imefasiriwa na Alpha Wilson Magubila kwa Neema aliojaliwa na Mungu

Kwa kipindi cha masaa 23, binti mdogo wa ki-Ecuado aitwaye Angelica alioneshwa falme za
Mbinguni na Kuzimu, na kurudi kwa Kristo mara ya pili. Alishuhudia Yesu akilia kwa huzuni
aonapo umati wa roho zilizopotea milele, ulimwengu uliomkataa yeye, kanisa lisilo tayari kabisa
kwa ujio wake, watu wameacha kushuhudia kwa walipotea mbali na kweli, na anasa za dunia
zimeteka hata watoto kwa shetani. Alishuhudia watu maarufu wakiteswa katika moto, waimbaji,
wanamuziki na hata Papa. Angelica alioneshwa jinsi ufalme wa Mbinguni ulivyoandaliwa kwa
uzuri na utayari, utukufu usioweza kufikirika, ambapo hakuna uovu. Japokuwa Yesu anakuja kwa
ajili ya watakatifu tu; wengi wa wana wa Mungu hawatakuwa tayari kwa siku ile, na wataachwa
nyuma katika ulimwengu utakaogawanyika vipande vipande. www.DivineUfunuo.info/23 (Mahojiano
kwa video, mwanzoni ni kwa lugha ya Kihispania, huko El Empalme, Ecuador. Sept. 29, 2009).

Maxima (Mama yake Binti):

Jina langu ni Maxima Zambrano Mora, tunasali kanisa la "Casa de Oracion" huku El Empalme.
Tulikuwa katika kufunga kwa siku 15, na kulia kwa Mungu. Binti yangu Angelica aliungana nasi
pia. Katika kipindi hicho cha siku 15 cha kufunga, niliweza kupata maono zaidi ya asili, ambayo
sijawahi kuona kabla. Tulikuwa tunaomba na kufunga katika kipindi maalumu cha kumtafuta
Bwana, tuliendelea kuomba na kulia pale nyumbani, tukisubiri Mungu aseme nasi.

Bwana alitutia matumaini makubwa sana. Kwaajili ya majaribu yetu tulikaribia kukata tamaa,
lakini Bwana alikuwa pamoja nasi kutusaidia. Alitupa neno la Yeremia 33:3 "Niite, nami
nitakuitikia, ame nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.” Binti yangu alitia
msisitizo sana katika neno hili kwa Bwana, japokuwa sikujua kwa wakati huo.
 2

Angelica (Binti Mhusika):

Jina langu ni Angelica Elizabeth Zambrano Mora. Nina umri wa miaka 18, na ninasoma chuo cha
"Colegio José María Velazco Ibarra",
hapa El Cantón, El Empalme, Ecuador. Kwanza nilimpokea Kristo nilipokuwa na umri wa miaka
12, lakini nalijiambia mwenyewe, "Hakuna hata mmoja wa rakifi zangu aliyeokoka na nikajisikia
aibu miongoni mwao", kwa hiyo nirudi nyuma mbali na Mungu na kuishi maisha mabaya. Lakini
Mungu alinivuta nitoke huko.
Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 15, nirejea tena kupatana na Bwana, lakini nia haikutulia sawa
sawa. Biblia inasema (Yakobo 1:8), "Mtu wa nia mbili husita-sita katika nia zake zote" na mimi
nilikuwa sawa na mtu huyu. Baba yangu aliwahi kusema "Hutakiwi kuwa hivyo, siyo vizuri, ni
vibaya mwanangu" lakini nalimjibu, "Hivi ndivyo nilivyo, nataka kuwa hivyo, hakuna mtu wa
kuniambia namna nitakiwavyo kuwa, wala chakufanya, wala namna ya kuvaa, au mwenendo."
Naye alijibu, "Mungu atakushughulikia na atakubadilisha wewe."

Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 17, nilimkaribia Bwana. Tarehe 28 mwezi Aprili nilimwendea
Bwana na kumwambia, "Bwana, nijisikia vibaya sana, najua kuwa mimi ni mwenye dhambi” na
nilimweleza jinsi ninavyojisikia. "Bwana, nisamehe mimi. Natamani uandike jina langu katika
kitabu cha Uzima na unipokee niwe mwanao." Nilitubu na kutoa maisha yangu kwa Bwana rasmi.
Nikasema “Bwana, naomba unibadilishe, ufanye tofauti ndani mwangu." Nililia kwa moyo wangu
wote, huku nikimwomba Bwana anibadilishe mimi. Lakini kwa kadri ya muda ulivyozidi kupita,
sikuona madiliko yoyote. Badiliko pekee nikuwa nilianza kuhudhuria kanisani, kusoma biblia na
kuomba. Hayo tu ndiyo mabadiliko katika maisha yangu.

Ilipofika mwezi Agosti, nilikaribishwa katika mfungo wa siku 15. Niliamua kushiriki, lakini kabla
ya kuanza nilisema: “Bwana, naomba unishughulikie hapa." Katika kipindi chote cha mfungo,
Bwana alikuwa anasema na karibu kila mtu, kasoro mimi tu! Ilikuwa kama vile Bwana hajaniona,
na hilo liliniumiza sana. Nikaomba, "Bwana, hutanishughulikia mimi?" Nikaomba na kulia peke
yangu na kusema tena, "Bwana, je unanipenda? Je upo hapa? Upo nami hapa? Kwanini husemi
nami kama unavyosema na kila mmoja hapa? Unasema mambo mengi kwa wenzangu, hata maneno
ya unabii, lakini siyo kwangu" Nilimwomba ishara ya kuwa yu nami, na Bwana akanipa neno la
Yeremia 33:3, "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu
usiyoyajua." Nikasema, “Bwana, je umesema nami?” Kwasababu nilisikia sauti yake na kupata
maono ya maneno yaliyoandikwa katika Yeremia 33:3.

Nikasema “Bwana, hiyo ni kwaajili yangu?” Nilitunza na kukaa nalo kimya mwenyewe wakati kila
mmoja akishuhudia waliyopewa na Bwana na kuoneshwa. Lakini mimi nilitunza siri yangu na mara
kwa mara nilijikumbusha na kutafakari maneno: " Niite" maana yake nimwombe, lakini nini maana
ya: "mambo makubwa, magumu" niliwaza, “Huenda ikamaanisha Mbinguni na Kuzimu." Kwa 3

hiyo nalimwambia “Bwana, naomba unioneshe Mbinguni tu, lakini siyo kuzimu, kwasababu
nimesikia kuzimu ni sehemu ya kutisha na mbaya sana." Lakini baadaye nikaomba kwa moyo
wangu wote, "Bwana kama ni mapenzi yako kunionesha, na iwe hivyo, lakini nibadilishe kwanza.
Naomba ufanye tofauti ndani mwangu, nataka kuwa tofauti.”

Tulipomaliza kufunga, kulikuwa na majaribu na vipindi vigumu na mara nyingine nalijisikia
kuishiwa nguvu, siwezi tena kuendelea na Bwana. Lakini alinipa nguvu. Nilianza kusikia sauti yake
na kumjua vema zaidi. Tukawa marakifi wazuri. Bwana ni rafiki yetu mwema, na Roho Mtakatifu
pia. Niliwahi mwambia, "Bwana, wewe ni rafiki yangu bora. Nataka kukujua vema," na
nilishirikiana naye katika mawazo yangu yote.

Nilimwomba kipindi chote cha mwezi Agosti hadi Novemba, na mtumishi wa Bwana akaja
nyumbani kwetu na kusema, "Bwana akubariki." Nikajibu, "Ameni." Kisha akasema, "Nimekuja
kukuletea ujumbe toka kwa Mungu…...Jiandae, kwasababu Bwana atakuonesha mambo makubwa,
magumu usiyoyajua. Atakuonesha wewe Mbinguni na kuzimu kama ulivyokuwa unamwomba
neno la Yeremia 33:3." Nikamwuliza, "Ndiyo, lakini umepataje kujua? Sijamweleza yeyote."
Akanijibu, "Mungu unayemtumikia na kumsifu, ndiye nimsifuye, alinieleza kila kitu."
Mara tukaanza kuomba. Baadhi akina dada toka kanisani kwetu na wana familia wangu
wakaungana nasi kuomba. Lakini mara tulipoanza kuomba, nilianza kuona Mbingu zikifunguka.
Mara nikasema “naona mbingu zikifunguka, na malaika wawili wanashuka kuja tulipo" Mtumishi
wa Mungu akasema “waulize kwanini wamekuja hapa”

Walikuwa warefu na wazuri wakupendeza; wana mbawa nzuri. Walikuwa wakubwa na wenye
kung’aa, na walionekana wakiangaaza, mng’ao kama wa dhahabu. Walivaa sandozi za vito vya
thamani na walivaa mavazi matakatifu. "Kwanini mko hapa?" Wakatabasamu na kusema, "Tupo
hapa kwasababu tuna kazi yakufanya….. tupo hapa kwasababu unatakiwa utembelee Mbinguni na
kuzimu na hatutaondoka mpaka yote yatakapo pita." Nikawajibu “safi sana, lakini mimi natamani
kutembelea Mbinguni tu, siyo kuzimu” Wakatabasamu na kuendelea kuwepo na hawakusema
lolote zaidi. Baada ya kumaliza maombi, niliendelea kuwaona wakiwepo.

Pia nilianza kumwona Roho Mtakatifu; ni rafiki yangu bora; ni Mtakatifu, amejaa pote na yuko kila
mahali wakati wote. Ninamwona, anaangaza na kung’aa sana, naona tabasamu lake na mtazamo
wake wa upendo! Ni vigumu sana kumwelezea, kwa sababu ni mzuri zaidi ya malaika. Malaika
wana uzuri wao lakini Roho Mtakatifu ni zaidi sana kwa yote. Naweza kuisikia sauti yake, sauti
ilijaa upendo na matulizo makuu. Siwezi kuelezea kabisa sauti yake; kama radi si radi wakati huo
huo yakuvutia. Yeye husema “Niko pamoja nawe” Kwa hiyo nalijitahidi kuendelea kutembea na
Mungu, japo majaribu yalizidi kutuzingira. Tulikuwa tunapita kipindi kigumu sana, lakini chenye
ushindi waajabu. Mie husema “Bwana, mapenzi yako yatimizwe.” Niliendelea kuwaona malaika
wale hata nikiwa shule na pia darasani. Nilikuwa mwenye furaha ajabu kwa sababu niliwaona
vema.

Mtumishi wa Bwana, aliyetutembelea, aliniambia nijiandae, kwa sababu nitakwenda kuona Mbingu
na kuzimu. Lakini pia aliniambia kitu kigumu. Alisema “Nitakufa.” Haikuwa rahisi niliposikia
neno hili.
 4

"Nitakufa namna gani? mie mdogo sana", Nilimuuliza. Akanijibu, “Usihofu juu ya lolote, Kila kitu
Mungu afanyacho hakina makosa wala mawaa, na atakurejesha duniani, ili utoe ushuhuda juu ya
Mbinguni na Kuzimu, kwakuwa hilo ndilo Bwana anataka sote tujue” Nikasema “Amen, lakini
nitagongwa na gari au nitakufaje?” Mawazo yalinisonga sana, lakini Bwana akaniambia nisihofu,
kila kitu kiko katika uwezo wake. Nikasema, “Ahsante Bwana”

Ilipofika tarehe 6 Novemba, baada ya kurejea nyumbani toka shule, malaika wale walikuwa nami,
hata nilipokuwa namsifu Bwana. Wao walikuwa hawaongei nami; bali walidumu kusema,
“Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Hallelujah," huku wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba wa
Mbinguni. Roho Mtakatifu pia alikuwa na malaika wale huku akifurahi. Watu wengi husema injili/
wokovu ni wa kuchosha/kukera, lakini huo ni uongo mkubwa toka kwa mwovu ili kuwafanya watu
wasitafute uwepo wa Mungu. Nami pia niliamini hivyo hapo kwanza, lakini baada ya kukutana na
Bwana na Roho Mtakatifu, najua injili haikeri wala kuchosha, niburudisho la ajabu hapa duniani!

Ninaweza kumwona; kucheza na kuongea naye Roho Mtakatifu. Lakini malaika walikuwa
hawaongei nami, ila walikuwa wakimsifu Bwana. Nikimwambia Roho twende nami nakufanya hili
na lile huja na kuwa nami. Ninaweza kujihisi na kumwona vema.
Japokuwa wengi hawamwoni, yeye yupo! Mahusiano haya yamendelea, hata hakuna sababu ya
kuyasimamisha, hasa baada ya kuonja radha yake na faida za Roho Mtakatifu…… hakuna njia ya
kujitenga naye jinsi alivyo mwema na wafaida, hasa nikikumbuka alikonitoa, jinsi nilivyokuwa,
ninamshukuru sana kwa rehema zake na upendo wake kwa wanadamu na kwangu mimi!

Tarehe 7, Novemba, nilipokuwa narudi nyumbani, nikasikia sauti ikisema “Jiandae, kwakuwa leo
utakufa,” Nilijua kuwa ni Roho Mtakatifu kwa vile nilimwona vema. Niliipuuza sauti yake na
kusema “Bwana, Sitaki kufa leo!” Lakini alirudia, “Jiandae, kwakuwa leo utakufa!” Mara hii sauti
ilikuwa ya juu zaidi na mkazo mkubwa. Nikajibu, “Bwana, najua ni wewe unayesema nami;
nimeuliza ili kupata uhakika tu, mapenzi yako yatendeke. Nitafanya kila utakalo niambia, najiachia
kwako Bwana, japo naogopa, najua upo nami, nawe ni wa kweli.” Niliomba, “Bwana, Yule
mtumishi wako uliyemtumia kunipa ujumbe mara ya kwanza, mlete muda huu, nimkute nyumbani,
na umpe tena neno hili aseme nami kuwa leo ndiyo siku yangu ya kufa.” Sasa mara zote Bwana
hujua ya nyuma, yaliyopo na yajayo. Alijua kuwa nitamwomba neno hili. Kwa hiyo nilipofika
nyumbani nikamkuta mtumishi wa Bwana ameishafika!.

Maxima (Mama ya Binti):
Binti yangu alipofika nyumbani, tulikuwa jikoni. Mara Angelica alipomwona mtumishi wa Bwana,
akasema, “Bwana akubariki.” Mtumishi wa Mungu akajibu, “Bwana akubariki nawe. Je uko tayari?
Kwa kuwa leo ndiyo siku Bwana atakayo kuchukua, saa kumi jioni.” Angelica alisimama na
kushikwa na mshangao kwamba Bwana amejibu ombi lake na kufanya vilevile alivyomwomba
njiani.

Angelica:
Niliposikia hayo maneno ya mtumishi, nikasema, “Ameni... lakini sitaki kufa, sitakufa! Hapana,
Bwana, naogopa, naogopa sana, ninahofu kubwa!” Mtumishi wa Bwana akasema, “Tuombe ili
hofu ikutoke sasa kwa jina la Bwana.” Nikasema, "Ameni" na tukaomba. Ghafla nikajisia hofu yote
imenitoka na furaha isiyoelezeka ikajaa ndani mwangu, nakuanza kuwaza kuwa kifo ni kitu chema
kuliko vyote nikitamanicho kinifike! Nikanza kutabasamu na kicheka wakati huo kila mmoja 5

aliyepo akinitazama. Wakaniona jinsi nilivyobadilika toka unyonge na kuwa mwenye furaha.
Nilikuwa natabasamu, narukaruka na kuimba.

Picha wakimwombea:


Maxima:
Binti yangu ghafla akawa mwenye furaha ndani ya moyo na kuanza kula. Alionja karibia kila kitu
kilichokuwepo, huku akisema, “Kama sitarudi, sawa nimeshakula na kushiba.”

Angelica:
Kila mmoja akaanza kucheka na kuuliza, “kwanini uko hivyo badala ya kuwa na huzuni, unafuraha
na mwenye raha?” nikawajibu, “Ndiyo ninafuraha: ninakwenda kumwona Bwana, nitakuwa naye,
lakini sijui kama nitarudi. Kwa hiyo nataka kugawa vitu vyangu vyote.” Wote wakastaajabu na
kuniuliza, “Unataka kugawa vitu vyako vyote?” macho ya mama yangu yalinitazama kwa
mshangao zaidi!

Maxima:
Binti yangu akaanza kugawa vitu vyake. Aligawa vyote, vyote! Ma-dada wa kanisani walikuwepo,
nao pia aliwapa baadhi ya vitu kwa kila mmoja. Nilipomuuliza nia yake, alisema, “Kama nikirudi,
watanirejeshea vyote, lakini nisiporudi, watabaki navyo.”

Angelica:
Niliwaza huzuni aliyokuwa nayo mama yangu niliposema maneno hayo. Lakini nilijisikia furaha
tupu, kwa hiyo nikaendelea kugawa vitu: nguo, kitanda, simu ya mkononi, kila kitu, lakini kwa
sharti: kama nikirudi, kila kitu kitarejeshwa kwangu. Wote wakaanza kucheka.

Maxima:
Binti yangu alikuwa na msimamo na nia ya dhati, lakini kama mama nilishikwa na huzuni sana.
Haikuwa jambo rahisi. Niliwaza, “Bwana muda huo ukiwadia, itakuwajekuwaje?” Sikuweza
kuelewa. Na walipoanza kuomba, nilikuwa napanga vitu ndani ya nyumba. Walisema, “Dada njoo
tuombe.” Lakini niliwajibu, “Nyie endeleeni, nitajiunga nanyi muda si mrefu. Ngoja nimalizie kazi
hii.”

Angelica:
Wote walikuwa wananiangalia mimi tulipokuwa tunaomba. Niliomba, “Bwana, nataka kufanya
mapenzi yako. Wewe si mwanadamu hata useme uwongo au ujute, najua wewe ni mkweli. Kama
nitakuaibisha, basi vema unichukue moja kwa moja; lakini kama nitayafanya mapenzi, basi
unirejeshe tena, lakini nisaidie kusema ukweli, niandae mimi, nisaidie kuhubiri na kuwaambia watu
kutubu.” Hiyo ndiyo ilikuwa sala yangu fupi sana. Nilimwambia mtumishi wa Bwana, 6

“Usimwambie mama yangu maneno niliyomwomba Bwana.” Naye akajibu, “sitamwambia sasa,
lakini mara Bwana atakapokutwa, nitamwambia.” Tuliendelea kuomba na kuungana katika duara.

Maxima:
Ilipofika saa 9:30 jioni, Bwana akamwambia mtumishi wake ampake mafuta binti yangu. Kwa hiyo
baadhi yetu tulikwenda chumbani na kumpaka mafuta. Alitupa dakika mbili tumpake mwili mzima,
toka kichwani hadi chini, kila mahali, mwili mzima. Akawa mwili wote amepakwa mafuta.

KIFO CHAKE
Angelica:
Mama yangu na dada mmoja, Fátima Navarrete, walinipaka mafuta. Kadri walivyokuwa
wananipaka, nilijisikia kama kuna kitu kinanifunika, kama kioo kilinizunguka mimi. Ni vigumu
kuelezea, nilijisikia kama nimezingirwa na ngao fulani, na nashindwa kuelezea nilivyokuwa
najisikia. Baada ya hapo kila walipojaribu kunigusa walishindwa!

Maxima:
Kadri tulivyokuwa tukimwombea Angelica, nilijaribu kuweka mkono juu yake, nilishindwa!
Alikuwa amezingirwa na kitu. Ilikuwa ajabu, hakuna aliyeweza kumgusa tena! Uzio huo ulianzia
kichwani hadi miguuni, karibia sentimenta 30 (Inchi 12). Hilo lilinitisha zaidi mimi. Nimewawekea
mikono wengi kabla, katika huduma ya Bwana, lakini jambo kama hili halijawahi kutokea!
Nikasema, “Oh, kuna jambo lazima linatendeka,” na nikaanza kuomba na kumshukuru Bwana.
Ghafla, nikasikia furaha kubwa sana. Huzuni iliyokuwa moyoni ikanitoka, maumivu yakakoma na
sasa nikasikia raha na furaha ajabu! Tuliendelea kuomba na ilipofika saa 10.00 jioni, binti yangu
akaanguka sakafuni.

Angelica:
Wakati wa maombi, nilisikia kuishiwa pumzi; nikashindwa kupumua. Nikasikia maumivu tumboni
na moyoni. Nilijisiki damu ikisimama, na ghafla maumivu makali mwili mzima. Nililoweza
kusema, “Bwana, nipe nguvu, nipe mimi nguvu!” kwasababu nilijisikia kushindwa kuendelea zaidi.
Sikuwa na nguvu kabisa, zote zilinitoka! Na nilipoangalia juu mbinguni, katika roho, si kwa macho
ya mwilini, niliona mbingu zikifunguka. Niliwaona malaika, siyo wawili au kumi, bali kwa
mamilioni wakiwa pamoja wamekusanyika. Katikati yao niliona mwanga, mara 10,000 zaidi ya
jua. Na nikasema, “Bwana ni wewe unayekuja!”

Maxima:
Alipoanguka chini, tulijaribu kumsimamisha, lakini hakuweza kusimama mwenyewe. Muda huu
tuliweza kumgusa. Alikuwa akisema, “Omba. Sina nguvu, mama, sina nguvu na ninasikia
maumivu.” Mwanzo alisikia maumivu tumboni, na baadaye moyoni. Tuliendelea kuomba na
kumsihi Bwana. Bwana alichukua maisha yake!
Picha Mwili wake:
 7

Sijawahi katika maisha yangu kumwona mtu akifa. Nilishuhudia binti yangu, akigugumia
maumivu! Haikuwa rahisi hata kidogo! Sikuweza kuelewa maneno yake ya mwisho, na mwisho
alitulia. Niliweka mikono yangu usoni pake, na kioo mdomoni kuona kama alikuwa anapumua.
Hakuwa na pumzi tena, alitulia kimya kabisa. Nilimshika, alikuwa angali na joto kama kawaida.
Nilichukua shuka na kumfunika na kwa muda mfupi akaanza kupoa na kuwa wa baridi sana.
Nywele zake zikalala, kama za maiti na akabadilika ubaridi wa barafu.

Angelica:
Yesu alikuwa anashuka chini, na nikajisikia mwili ukifa. Kadri Yesu na malaika walivyozidi
kukaribia, nikajisikia kuondoka, na sikuwa mimi tena. Sikuwa hai tena, nilikuwa nakufa na
kugugumia maumivu! Wakati mwili wangu ulipoanguka chini, walikuwa tayari wamefika. Nyumba
yetu ilijaa malaika, na katikati yao niliona mwanga mkali kuliko wa jua! Ilikuwa vigumu; nilisikia
maumivu makali wakati roho yangu ilipotenganishwa na mwili. Nilikuwa nalia na kupiga kelele,
kadri nilivyoona mwili wangu sakafuni. Nilimuuliza, “Bwana, nini kinachotokea? Nini
kinachotokea?” Nilijaribu kuugusa mwili wangu na kuurudia tena, lakini nilipojaribu, ilikuwa kama
kushika hewa: sikuweza kuugusa, mkono wangu ulipitiliza. Hakuna kati ya waliokuwa
wananiombea aliyenisikia! Na nikapiga kelele, “Bwana, nisaidie mimi!”

Maxima:
Mume wangu alifika tulipokuwa tunaomba, na alimkuta pale. Bwana alinipa nguvu kwa kuwa
sikujua la kufanya. Ilikuwa kama vile yuko mahututi (kwenye coma), lakini nilijua yuko salama,
kwasababu ilikuwa ni kazi ya Bwana. Kwahiyo nikasema “Bwana, mapenzi yako yafanyike.”

BWANA YESU KRISTO
Angelica:
Wakati huo nasikia sauti ya Bwana, sauti nzuri kama radi lakini ya UPENDO, “Usiogope, Binti,
kwa kuwa mimi ni Yehova, Mungu wako, na nimekuja hapa kukuonesha niliyokuahidi wewe.
Inuka, kwa kuwa mimi ni Yehova, ninayekushika mkono wako wa kuume na kukuambia,
usiogope, nitakusaidia wewe." Ghafla, nikasimama. Nilikuwa nimepiga magoti chini, ninauangalia
mwili wangu, nikitaka kuurejea bila mafanikio. Niliposikia sauti yake, woga ukanitoka, na sikuwa
na hofu tena. Nilipoanza kutembea, malaika wakaanza kufungua njia. Kulikuwa na mwanga mkali
ung’aao, na nilipouangalia nilisikia amani ya ajabu. Kadri nilivyoangalia, nilimwona mwanaume
mzuri, mrefu, aliyevaa vizuri na kuvutia sana kumwangalia, mwenye siha njema. Mwanga ulitoka
kwake. Kulikuwa na mwanga mkali kiasi cha kushindwa kumwangalia uso wake! Lakini niliweza
kuona nywele zake za dhahabu ing’aayo na vazi jeupe na mshipi kifuani pake. Ukisomeka,
“MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.”

Nilimwangalia miguuni pake, alikuwa amevaa sandozi zenye mng’ao wa dhahabu, dhahabu safi.
Alikuwa mzuri sana! Akaninyooshea mkono wake. Nilipomshika mkono wake, haikuwa kama
nilipojaribu kuugusa mwili wangu, mkono haukupitiliza. Nikauliza, “Nini kinachotokea?” naye
akasema, “Nitakuonesha wewe kuzimu ili ukirudi uwaambie wanadamu kuwa kuzimu ni halisi;
kuwa ni kweli ipo. Na pia utukufu wangu nitakuonesha wewe, ili uwaambie watu wangu
wajiaandae, kwa kuwa utukufu wangu ni halisi na mimi pia.” Akasema, "Binti, usiogope”
akarudia kusema tena na mimi nikasema, "Bwana, nataka tu kwenda Mbinguni, lakini siyo kuzimu,
kwasababu nimesikia kunatisha!” Akasema, “Binti, nitakuwa nawe. Sitakuacha huko na
nitakuonesha huko mahali kwasababu wengi wanajua kuzimu ipo lakini hawaiogopi. 8

Wanaamini ni mchezo, na kuzimu ni mzaha, na wengi hawajui lolote juu yake. Ndiyo maana
nitakuonesha wewe huko kwa sababu wanaopotea ni wengi kuliko wanaoingia katika utukufu
wangu.” Aliposema hayo, niliona machozi yakitiririka kwenye vazi lake. Nikamwuuliza, “Bwana,
kwanini unalia?” Akanijibu, “Binti, kwasababu wengi wanaangamia, na nitakuonesha hii, ili
uende na uwaambie ukweli na wewe usirudie hapo.”

KUZIMU
Ghafla, alivyokuwa anaongea, kila kitu kikaanza kutembea. Ardhi ilitikisika na kupasuka, na
nikaona shimo jeusi tii chini.

Shimo:

Tulikuwa tumesimama kama kwenye mwamba na malaika wakituzunguka. Nikasema, “Bwana,
sitaki kwenda mahali huko!” akasema, “Binti, usiogope niko pamoja nawe.” Kwa sekunde chache
tukashuka kwenye shimo jeusi. Nilijaribu kuangalia lakini kulikuwa na kiza kikuu. Niliona duara
kubwa, na kusikia mamilioni ya sauti.

Nilipata moto. Nikajisikia ngozi yangu kuungua. Nikamuuliza, “Bwana, hiki ni nini? sitaki
kwenda mahali huko!” Bwana akasema hilo ni lango tu la kwenda kuzimu. Kulikuwa kuna harufu
mbaya, yakutisha, isiyovumilika, na nikamsihi Yesu asinipeleke mimi. Naye akajibu, “Binti, ni
muhimu ufike na kujua sehemu hii.” Nikalia, “Lakini kwanini, Bwana, kwanini?” naye akasema,
“Ili ukawaambie ukweli wanadamu; wanadamu wanaangamia, wanapotea na wachache sana
wanaoingia ufalme wangu.” (Mat.7:14) Akishasema hivi, hulia sana. Maneno yake yalinitia nguvu
na kunihimiza, kwa hiyo nikaendelea kutembea.

Ziwa la Moto:

 9

Tulifika mwisho wa tanuru/lango, nilipoangalia chini niliona umati umefunikwa na miali ya moto.
Bwana akasema “Binti, nakupa hii.” Ilikuwa ni faili kubwa lenye karatasi ambazo hazijaandikwa
chochote. “Binti, chukua na kalamu hii ili uweze kuandika yote nitakayokuonesha,
utakayoyaona na kusikia. Utaandika kila kitu ukionacho na utaishi nayo.” Nikasema, “Bwana,
nitafanya, lakini nimeshaanza kuona mengi mno, Bwana. Ninaona roho zikiteswa, na kuzamishwa
kwenye moto.”

Maxima:
Muda uliendelea kupita, na binti yangu alikuwa bado kalala pale. “Bwana, nini kinachotokea?”
Machozi yalikuwa yakimtoka kwenye macho, lakini kila nilipomfuta, yalitoka tena. Nikaweka kioo
mdomoni pake kuona kama anapumua, hakukuwa na pumzi. Tuliangalia mapigo ya damu, wapi,
hakuna kitu!. Tuliweka mikono tumboni pake, wapi! Hakuna kitu. Mtumishi wa Bwana akasema,
“mahali alipo sasa, siyo mahali pa kutabasamu bali mahali pa mateso.”

Angelica:
Nikamwambia Yesu, Nitashuhudia kuwa kuzimu ni halisi, kwamba ipo, lakini nitoe hapa sasa!” na
akanijibu, “Binti, hatuja ingia bado mahali penyewe, na sijakuonesha chochote, tayari unataka
nikutoe huku?” nikasema “Bwana, tafadhari nitoe mahali hapa,” tukaendelea kushuka kwenye
korongo/shimo lakutisha! Nikaanza kulia na kupiga yowee, “Bwana, hapana, hapana, hapana,
hapana……… Sitaki kwenda!” naye hujibu, “Unatakiwa kuona haya.”

Niliona mapepo yakutisha, ya kila aina, makubwa na madogo. Yalikuwa yanakimbia sana, na
yameshika vitu mkononi. “Bwana, kwanini yanakimbia hivyo na yameshika nini?” akanijibu,
“Binti, wanakimbia hivyo kwasababu wajua muda wao karibu kwisha, kwasababu muda wa
kuwaharibu/kuwapoteza wanadamu, hususani watu wangu. Na walivyoshika mkononi ni
mishale ya kuwaharibu wanadamu, kwasababu kila pepo amepewa jina na kwa kadri ya jina
lake, ana mishale ya kumharibu mtu na kumleta huku kuzimu; malengo yao ni kumharibu mtu
na kumleta kuzimu.” Na niliendelea kuona mapepo yakikimbia na kutoka kuelekea duniani na
Bwana akaniambia; “Wanakwenda duniani ili kuleta na kuwatupa wanadamu huku." Alipokuwa
akisema hivyo, Bwana hulia, hulia sana. Kila alipolia nami nililia pia.

Maxima:
Binti yangu alikuwa amekufa kwa masaa 23, lakini sikutoa taarifa kwenye mamlaka yoyote.
Niliomba, “Bwana, nitasubiri kwa masaa 24. Kama binti yangu hatarudi ndani ya saa 24,
nitampigia simu Daktari.” Lakini, Bwana alimrejesha kabla ya saa 24 hazijatimia.

Angelica:
Bwana akaniambia, “je uko tayari kuona nitakachokuonesha wewe?” Nikasema, “Ndiyo
Bwana,”. Alinipeleka kwenye sero moja, ambapo nilimwona kijana akiwa matesoni katikati ya
miali ya moto. Nikajulishwa namba sero yake, japokuwa sikuweza kujua ile namba, ilionekana
kama imeandikwa kinyume hivi. Palikuwa na nembo kubwa mle ndani, na kijana alikuwa na
namba 666 kwenye kipaji cha uso. Pia alikuwa na aina ya kipande cha chuma imebandikwa
kwenye ngozi yake. Funza walikuwa wanamtafuna, haikuweza kuharibu kipande kile; wala moto
haukuweza kukiunguza. Akapiga kelele, “Bwana, nirehemu mimi. Nitoe mahali hapa. Nisamehe
mimi Bwana!” lakini Yesu alimjibu, “umechelewa, umechelewa sana: nilikupa fursa lakini
hutaka kutubu.” Nikamuuliza Yesu, “Bwana, kwanini huyu yuko hapa?” mara nikajulishwa. 10

Akiwa duniani, kijana huyu alijua neno la Mungu, lakini ghafla akajitenga na Bwana na kuchagua
pombe, madawa ya kulevya na kupita katika njia zisizofaa. Hakutaka kufuata njia ya Bwana. Yesu
alimwonya mara nyingi juu la litakalompata. Yesu akasema, “Binti, yuko hapa kwasababu kila
anayeyakataa maneno yangu, anaye amhukumuye: lile neno nilisema naye litamhukumu siku
ya mwisho,” (Yohana 12:48) na Yesu akalia tena.

Bwana akilia, nitofauti nasi tuliavyo na zaidi yetu. Yeye hulia na maumivu makali moyoni na
uchungu usioelezeka. Bwana akasema, "Sikutengeneza kuzimu kwaajili ya wanadamu,”
Nikamuuliza, “Sasa Bwana kwanini wanadamu wapo huku,” Akanijibu, “Binti, niliumba kwajili
ya shetani na malaika zake, ambayo ni mapepo;(Mat. 25:41) lakini, kwasababu ya dhambi na
kukosekana kwa toba, wanadamu huishia hapa, na wengi wangamiao kuliko wanaofika katika
utukufu wangu!" Akaendelea kulia na huniumiza sana nimwonapo akilia. "Binti, nalitoa maisha
kwaajili ya wanadamu, ili wasiangamie, ili wasiishie hapa [Kuzimu]. Nalitoa maisha yangu kwa
upendo na huruma, ili wanadamu waendee toba na kuingia katika ufalme wa Mbinguni.” Yesu
kwa huzuni huugua kiasi cha kushindwa kustahimili maumivu, kadri aonavyo watu pale kuzimu.

Kwa kuwa na Yesu, kulinifanya nijisikie salama. Niliwaza, “kama nikimwacha Bwana aende,
ninge-nasa kuzimu pale” Nikamuuliza, “Yesu, je nina ndugu yangu mahali hapa?” Akanitazama
kwa jinsi nilivyokuwa nalia na akasema, “Binti, niko nawe,” Kwasababu nilikuwa mwenye hofu
sana. Akanipeleke kwenye sero nyingine. Sikuwahi kuwaza kumwona ndugu yangu kwenye sero
ile. Nilimwona mwanamke akiteswa, alikuwa na funza wakimla uso wake, na mapepo yakimchoma
mikuki mwilini. Naye hupiga kelele, “Hapana, Bwana, nihurumie, nisamehe mimi, tafadhari, nitoe
mahali hapa kwa dakika moja!” (Luka 16:24)


Kuzimu, watu huteswa na kumbukumbu za waliyoyafanya duniani. Mapepo hudhihaki watu na
kuwaambia, “abudu na kusifu kwasababu huu ndiyo ufalme wenu!” na watu hupiga kelele 11

wakikumbuka kuwa walimjua Mungu, kwasababu walijua neno. Walimjua Bwana waliteswa mara
dufu ya wengine.

Bwana akasema, “Hakuna tena nafasi kwa walioko pale[kuzimu]; kungali na nafasi kwa walio
hai.” Nikamuuliza, “Bwana, kwanini bibi yangu mkubwa yupo pale? Sijui kama alikujua wewe.
Kwanini yupo kuzimu Bwana?” akanijibu, “Binti, yupo hapa kwasababu alishindwa
kusamehe….. binti, yeyote asiyesamehe, sitamsamehe huyu.”

Nikamuuliza, “Bwana, lakini wewe husamehe, na una rehema.” Naye akanijibu, “Ndiyo, binti,
lakini nilazima kusamehe, kwasababu hawajawasamehe wengi, na ndiyo maana wengi wapo
hapa, wameshindwa kusamehe…… nenda kawaambia wanadamu ni muda wa kusamehe, hasa
hasa watu wangu, kwakuwa wengi miongoni mwa watu wangu hawajasamehe. Waambie
waache malaaumu, mafundo, chuki mioyoni mwao, kwa kuwa ni muda wa kusamehe! Kama
kifo kikimsitukiza mtu aliyeshindwa kusamehe, huyo mtu atakwenda kuzimu, kwakuwa hakuna
awezaye kununua maisha.” Tulipoondoka hapo, bibi yangu mkubwa alifunikwa na moto na
akapiga makelele, "Aaaah," na akaanza kutukana jina la Mungu, na kumlaani Bwana; kila mtu
kuzimu humtukana Mungu.

Tulipoondoka eneo lile, nikaona kuwa kuzimu imejaa roho ziteswazo. Watu wengi huinua mikono
nje, wakimwomba Yesu msaada wa kuwatoa nje. Lakini Bwana hakuwa na lolote la kufanya kwao,
nao huanza kumtukana Mungu. Mara Yesu hulia sana na kusema, “Inaniumiza sana kuwasikia,
inaniumiza mimi sana wanavyofanya, kwasababu siwezi kufanya lolote kwaajili yao. Ninacho
kueleza ni hiki; nina nafasi kwa hao walioko duniani, ambao hawaajafa, walio hai, wanao muda
wa kutubu!”

Bwana akaniambia kuna watu wengi maaruku huku kuzimu, na pia wengi waliomjua Bwana.
Akasema, “Nitakuonesha upande mwingine wa tanuru.” Tukaenda mahali penye mwanamke
aliyezingirwa na miali ya moto. Alikuwa katika maumivu makubwa na kupiga makelele, akiomba
huruma kwa Bwana. Yesu akanyoosha mkono kwake na akaniambia, “Binti, Yule mwanamke
umwonaye pale, amezingirwa na miali ya moto ni Selena.” Kadri tulivyokuwa tunamkaribia,
akapiga kelele, “Bwana, nihurumie mimi, nisamehe mimi Bwana, nitoe mahali hapa!” lakini
Bwana akamtazama na kusema, "Umechelewa, umechelewa sana, huwezi kutubu sasa.”
Selena

Aliponiona mimi akasema, “Tafadhari, nakuomba wewe, waambie watu hivi, tafadhari sema na
usinyamaze; nenda waambie wasije mahali hapa; nenda waambie wasisikilize nyimbo zangu, wala
wasiimbe hizo nyimbo.”(1 Yohana 2:15) Nikamuuliza, "kwanini unataka mimi niwaambie hivyo?" 12

naye akanijibu, "Kwasababu kila wakati watu wanaposikiliza nyimbo zangu, nateswa zaidi na
zaidi, na mtu anayeimba na kusikiliza nyimbo zangu, anaelekea mahali hapa. Tafadhari, nenda
uwaambie wasije huku; nenda waambie kuzimu ni halisi, ipo kweli!”. Akapiga kelele na mapepo
humchoma mikuki na Selena kulia, “Nisaidie mimi, nihurumie mimi Bwana!” lakini kwa huzuni
Bwana alimwambia, “umechelewa sana.”

Nikaangalia pande zote za eneo lile, lilikuwa limejaa waimbaji na wasanii waliokufa. Walikuwa
wakiimba na kuimba, bila kusimama. Bwana akanifafanulia, “Binti, mtu aliyepo hapa, lazima
aendelee kufanya kile alichokuwa anafanya duniani, kama hajatubu."

Kadri nilivyokuwa naangalia eneo lile, niliona mapepo mengi yakinyunyiza vitu kama mvua.
Nilidhani ni mvua inanyesha. Lakini niliona watu kwenye miali ya moto wakikimbia mbali na ile
mvua na kupiga yowee, “Hapana, nisaidie, Bwana!..... Hapana, haiwezekani kuwa hivyo,” na
mapepo yalikuwa yanacheka na kuwaambia watu, “Sifu na kuabudu kwasababu hapa ni ufalme
wenu milele na milele!” Niliona miali ya moto ikiongezeka na funza za watu zikiongezeka zaidi!
Hayakuwa maji yale bali kiberiti cha kuongeza miali ya moto na kuongea maumivu ya kila mtu.
Nikamuuliza Yesu, “Ni nini kinachotokea?..... Bwana, ni nini hiki?” Bwana akanijibu, “Huu ni
ujira wa yeyote asiyetubu.” (Zaburi 11:6).

Bwana akanipeleka mahali alipo mtu aliyejulikana sana. Kabla ya maono haya, nilishi maisha kama
msichana wa kikristo wa nia mbili. Nilidhani kila mtu anayekufa anakwenda Mbinguni; wale
walifanyiwa ibada za mazishi watakwenda mbinguni, kumbe sikuwa sahihi, nilikosa. Alipofariki
Papa John Paul II, marafiki zangu na ndugu walisema amekwenda mbinguni. Taarifa zote kwenye
LUNINGA [TV], na vyombo mbalimbali vya habari vilisema, "Papa John Paul II amefariki,
apumzike kwa amani. Anafurahia sasa kuwa na Bwana na malaika Mbinguni" na mimi niliamini
yote kuwa ndivyo. Lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, kwasababu nimemwona
kuzimu, akiteswa kwa miali ya moto. Nilimtazama uso wake, alikuwa mwenyewe Papa John Paul
II! Bwana akaniambia, “Angalia, Binti, Yule mwanaume umwonaye pale, ni Papa John Paul II.
Yuko hapa; akiteswa kwasababu hakutubu.”
Papa John Paul II

Lakini nikamuuliza, “Bwana, kwanini yuko hapa? Alikuwa akihubiri kanisani.” Yesu akanijibu,
“Binti, hakuna mwasherati, wala muabudu sanamu, hakuna mchoyo na hakuna mwongo
atakayerithi ufalme wangu.” (Eph 5:5) Nikamjibu, “Ndiyo, najua ni kweli, lakini nataka kujua
kwanini yuko hapa, kwasababu alikuwa akiwahubiria umati wa watu!" Na Yesu akanijibu, “Ndiyo,
Binti, alisema mengi, lakini hakusema kweli kama ilivyo. Hakusema kweli na kweli aliijua na
japokuwa aliijua kweli, alipenda fedha zaidi ya kuhubiri habari za wokovu. Hakutoa uhalisia;
hakusema kuzimu ni halisi na mbinguni kupo; Binti, sasa yuko mahali hapa."
 13

Nilipomwangalia mtu huyu, alikuwa na joka kubwa lenye sindano nyingi mwilini mwake,
limemzingira shingoni, naye hujaribu kumtoa. Nalimwomba Yesu, “Bwana, msaidie!” Mwanaume
hupiga kelele, “Nisaidie mimi, Bwana nihurumie; nitoe mahali hapa; nisamehe mimi! Ninatubu
Bwana; Nataka nirudi duniani, nataka nirudi duniani nikatubu.” Bwana alimtazama na
kumwambia, “Ulijua vizuri yote haya. Ulijua vema kuwa kuzimu ni halisi, ipo……..
umechelewa; hakuna tena nafasi kwaajili yako.”

Bwana akasema, “Tazama Binti, nitakonesha maisha ya mtu huyu.” Yesu akanionesha kioo
kikubwa kama LUNINGA [TV]; nikaona alivyotoa misa mara nyingi kwa umati wa watu. Na watu
wale walivyokuwa waabudu sanamu. Yesu akasema, “Tazama, Binti, wapo waabudu sanamu
wengi hapa [Kuzimu]. Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa Binti. Ni mimi pekee niwezaye kuokoa,
na nje yangu hakuna mwingine aokoaye. Nawapenda wenye dhambi, lakini nachukia dhambi
Binti. Nenda na uwaambie wanadamu kuwa nawapenda na ninataka waje kwangu.”
Kadri Bwana alivyokuwa akisema, nilianza kuona mtu huyu akipokea makusanyo makubwa ya
sarafu na fedha; vyote alivihifadhi. Alikuwa na fedha nyingi sana. Naliona sura yake imeketi katika
mamlaka yake, lakini pia naliweza kuona zaidi. Japo ni kweli watu hawa hawaoi, ninakuhakikishia
wewe, sizushi, Bwana alinionesha mimi, wanalala na masista; na wanawake wengi!

Bwana akanionesha watu hawa wanaishi kwa uasherati, na neno linasema hakuna mwasherati
atakayerithi ufalme wake. Kadri nilivyokuwa naona, Bwana akaniambia, “Tazama, Binti, yote
ninayokuonesha, ndiyo yanayoendelea, ndivyo alivyoishi [Papa] na ndivyo yanayotokea katikati
ya watu wengi, katikati ya mapadre na mapapa waliopo.” Kisha Bwana akasema, “Binti, nenda
na uwaambie wanadamu ni muda wa kugeukia.”

Bwana akanionesha sehemu watu wengi wanavyoelekea kuzimu. Nikamuuliza, “Bwana, namna
gani wanakuja huku?” akanijibu, “Nitakuonesha.” Akanionesha lango lenye watu wengi wakipita.
Watu hawa walikuwa wamefungwa toka mikononi hadi miguuni. Walivaa mavazi meusi na kubeba
mizigo mgongoni mwao. Yesu akasema, “Binti, hao watu uwaonao hawanijui mimi bado. Mizigo
waliyobeba ni dhambi, lakini nenda waambie walete mizigo kwangu, nami nitawapumzisha; kwa
kuwa mie ndiye mwenye kusamehe dhambi zao zote…. Binti, nenda na uwaambie waje kwangu,
kwani nawasubiri na mikono yangu iko wazi kuwapokea, na uwaambie hapo wanaelekea mahali
hapa [kuzimu].”

Kadri nilivyokuwa nawatazama watu wakitembea, nikamwambia, “Bwana, Yule mtu pale ni
binamu yangu; na Yule kijana pia, Bwana, na Yule binti pale anayelekea kuzimu; oh familia yangu
inakuja huku kuzimu!” Bwana akajibu, “Binti, wanakuja huku, lakini nenda uwaeleze
wanakoelekea, nenda waeleze kuwa wanakwenda kuzimu. Nenda waeleze kuwa nimekuchagua
wewe uwe mlinzi wangu…… nimekuchagua wewe kama mlinzi, hii inamaanisha kuwa
unatakiwa uwaambie ukweli. Unatakiwa uende uwaeleze yote niliyokuonesha wewe. Kama
hutawaambia na jambo likampata mtu huyu, damu yake itakuwa juu yako, lakini ukiende na
kufanya nilivyokueleza, hapo mtu huyu nitamdai mwenyewe. Kama mtu hatatubu, hapo wajibu
ulionao utaondolewa, kwa kuwa atadaiwa mwenyewe na damu yake haitakuwa juu yako.
(Ezekia 3:18)"

Yesu akaniambia wengi wa watu maarufu wanaelekea huku [kuzimu], maarufu na watu muhimu.
Kwa mfano, Michael Jackson. Huyu alikuwa maarufu duaniani kote lakini alikuwa mjumbe wa 14

shetani. Japokuwa wengi wanaweza wasione na kuelewa hivyo, lakini huo ndiyo ukweli. Huyu
alikuwa na mkataba na shetani: alikubaliana na shetani ili awe na heshima na sifa ilikuwa vutia
wapenzi wengi.
Michael_Jackson

Hizo hatua na mitindo aliyokuwa anafanya, ndivyo nilivyoona mimi mapepo yakicheza na
kutembea yanapotesa watu kuzimu. Yalikuwa yanateleza kwa kurudi nyuma na siyo mbele, huku
yakipiga kelele; yakifurahia mateso wanayopata watu. Ngoja nikuambia wewe kuwa Michael
Jackson yuko kuzimu. Bwana alinionesha baada ya kufa Michael. Alinionesha Michael Jackson
akiteswa kwenye miali ya moto. Nikalia kwa Yesu, “Kwanini?” haikuwa rahisi kuona mtu huyu
alivyokuwa anateswa na alivyokuwa analia na kupiga mayowe. Yeyote anayesikiliza nyimbo za
Michael Jackson au kuziimba au ni mpenzi/shabiki wa Michael Jackson, ninakuonya kuwa shetani
anakutega katika mtego wake ili mwisho uishie kuzimu. Mara hii, jitoe na kumkana shetani kwa
jina Yesu! Yesu anataka kukuweka huru wewe, ili usipotee milele. Bwana akaniambia, “Binti,
kuna watu wanijuao pia wanakuja huku.” Nikamuuliza, “Bwana, inakuwa je mtu akujue harafu
aje huku?” akanijibu, “Mtu Yule aliyeacha njia zangu na mtu Yule anayeishi aina mbili za
maisha [wokovu na dhambi].” Akaanza kunionesha watu wanaoelekea kuzimu. Walikuwa
wamefungwa kamba toka mikononi hadi miguuni. Kila mmoja alivaa vazi jeupe, lakini
limetobokatoboka, lina-mabakamabaka na limekunjamana. Yesu akaniambia, “Binti, angalia watu
walioniacha mimi. Binti, nataka kukueleza, siji duniani kwaajili ya watu hawa. Nakuja kwaajili
ya watakatifu, waliotayari, wasiolaumiwa, wasio na makunyanzi na wasio na mawaa…… nenda
uwaambie warejee kwenye njia zao za zamani,” (Efeso 5:26-27) Nilianza kuwaona wengi
miongoni mwa wajomba zangu na watu wengine wengi waliorudi nyuma na kuziacha njia za
Bwana. “Nenda kawaambie ninawasubiri, walete mizigo yao nami nitawapumzisha." YESU
alikuwa analia baada ya kusema hayo, “Binti, wanakuja huku [kuzimu]. Nenda kawaambie
wajomba zako; nenda kawambie ndugu zako kuwa wakuja huku! Binti, wengi hawatakuamini,
lakini mimi ni shahidi wako mwaminifu, ni shahidi wako mwaminifu. Sitakuacha wewe. Hata
kama hawataamini, Binti, nenda na uwaambie ukweli huu, kwa kuwa nipo nawe. Pia Binti
nitakuonesha jinsi watu wanavyofika huku.”

Tulikwenda kwenye lango, ambapo tuliona umati wa watu wakiangukia ndani ya shimo kubwa.
Siyo elfu moja wala elfu mbili, bali wingi wake kama mchanga wa bahari, hawana idadi!
Walikuwa wananguka kwa kila sekunde, mfano wa mkono uliojaa mchanga umwakikapo chini.
Zile roho zilikuwa zinaanguka kwa kasi. YESU alikuwa akilia, na kusema, “Binti hivi ndivyo
wanadamu wanavyopotea; hivi ndiyo mwanadamu apoteavyo!!!..... Binti, inaniumiza sana mimi
nionavyo wanadamu wanavyoangamia.”

YESU akasema, “maapepo pia hufanya mikutano huku.” Na nikasema, “mapepo yanafanya
mikutano?” Yesu akasema, "Ndiyo, Binti, wanakutana kupanga, kupanga watavyowafanya
wanadamu. Wanakutana kila siku kwa siri.” Na kwa hilo, Yesu akanipeleka kwenye sero, 15

ambapo niliona meza ya mbao na viti vikizunguka meza. Na palikuwa na mapepo, aina zote za
mapepo. Yesu akaelezea, “Binti, wanapanga kwenda kuharibu nyumba/familia za wachungaji,
wamisionari, wainjilisti na wote wanijuao mimi. Binti wanataka kuwaharibu; wanamishale
mingi.”

Mapepo hucheka na kudhihaki, na kusema, “acha tuwaharibu wanadamu na kuwaleta huku.” Yesu
akasema, “Nenda na uwaambie nipo pamoja nao watu wangu. Waambie wasiache milango wazi,
wasimpe nafasi shetani, kwa kuwa shetani anazunguka-zunguka kama simba angurumaye,
akimtafuta wa kummeza. (1 Petro 5:8)" Lakini neno linasema, "anatembea kama", kwasababu
simba halisi, ni Simba wa Yuda, Yesu Kristo wa Nazareti (Ufunuo 5:5)! Yesu akasema, "Binti,
wanataka kuharibu/kuangamiza familia za wachungaji.” Nikamuuliza, “Kwanini wanataka
kuharibu familia za wachungaji?” na Yesu akajibu, “Kwasababu wanawajibu wa maelfu ya watu
ambao ni kondoo wa kundi; kondoo wa kundi Bwana aliowakabidhi wao. Wanataka watu hao
warudie dunia tena; waangalie nyuma na kuishia kuzimu…. Nenda kawaambie wachungaji
kusema iliyo kweli tupu. Waeleze wahubiri kweli tupu na kusema kila kitu ninachowaambia na
wasinyamaze nayo haya ninayowaambia!”
Tulipokuwa tunaondoka hapo, akaniambia, “Nataka nikuoneshe kitu kingine…. Wapo pia watoto
huku.” Na nikamjibu, “watoto huku Bwana? Kwanini wawepo watoto huku? Neno lako lasema,
'Waacheni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie: kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wao."
(Mathayo 19:14) Yesu akajibu, “Binti, ni kweli, ufalme wa mbinguni ni wao, lakini mtoto lazima
aje kwangu, kwa kuwa kila ajaye kwangu sitamtupa kamwe." (Yohana 6:37) Ghafla, Bwana
akanionesha mvulana wa miaka nane akiteswa kwenye moto. Mvulana akalia, “Bwana nihurumie
mimi, nitoe mahali hapa, sitaki kuwepo hapa!” aliendelea kupiga kulia na kelele. Nikaona mapepo
yamemzunguka mtoto huyu, yaliyofanana na cartoon. Kulikuwa na aina za Dragon, BoyZ, Ben 10,
Pokémon, Doral, na nyingine nyingi. “Bwana, kwanini mtoto huyu yuko huku?" Yesu akanionesha
picha ya mkanda wa maisha mtoto huyu. Nilimwona anavyotumia muda karibia wote kwenye
LUNINGA [TV] akiangalia cartoon.
Cartoon ya Ben 10: Pokemon:

Yesu akasema, "Binti, hayo maigizo ya cartoon, sinema zake, michezo mbalimbali ya kuigiza
inayooneshwa kila siku kwenye LUNINGA [TV] ni vyombo vya shetani atumiavyo kuwaharibu
wanadamu….. tazama, binti ilivyotokea kwa mtoto huyu." Nilimwona jinsi mtoto huyu
alivyokuwa mkaidi na asiye mtii kwa wazazi wake. Wazazi wake aliposema naye alikimbia na
kutupatupa vitu ovyo na kuto-watii. Baada ya hapo akagongwa na gari na ukawa mwisho wa
maisha yake. Yesu akasema, “Tangu hapo yupo mahali hapa.”

Nilimtazama mtoto Yule akiteswa. Yesu akasema, "Binti, nenda na uwaambie wazazi
wawaelekeze watoto wao kama ilivyo katika neno langu.”(Mithali 22:6) Neno la Mungu ni halisi, 16

linatuambia tumwonye mtoto kwa fimbo, lakini si kila wakati, pale tu mtoto anapoonyesha ukaidi
kwa wazazi. (Mithali 22:15)

Bwana akaniambia kitu cha kuhuzunisha sana na kuumiza mno. Akasema, “Binti, wapo watoto
wengi sana huku kwasababu ya cartoon, kwasababu ya ukaidi.” Nikamuuliza, “Bwana, kwanini
lawama ziwe hizi cartoon?” Naye akanieleza, “Kwasababu ni mapepo yanayobeba ukaidi, kiburi,
ukali na chuki kwa watoto, ili wasifanye vitu vizuri; na mapepo mengine huwaingia watoto ili
wasifanye mambo mazuri, bali wafanye mabaya: vile waonavyo kwenye LUNINGA [TV] watoto
hutaka kufanya vivyo hivyo.” Kuzimu ipo, kuzimu ni halisi, na watoto lazima waamue
watakwenda na nani. Nikasema, “Bwana, niambia, kwanini kuna watoto huku?” na Yesu akanijibu,
“Mara watoto wapatapo kujua kuna mbinguni na kuzimu, hapo wanayonafasi ya kuchagua.”

UFALME WA MBINGUNI
Kuna mengi ya kusema juu ya kuzimu, lakini kwasasa niwashirikishe niliyoyaona Mbinguni. Yesu
akasema, "Binti, sasa nitakuonesha nilichowaandalia watakatifu wangu.” Tuliondoka kule
kuzimu kupitia lango lake. Tulipokuwa tukisafiri kutoka nje ya kuzimu, ghafla tukatokea mahali
penye mwanga. Sikuona giza tena, mateso wala miale ya moto. Akasema, “Binti, nitakuonesha
utukufu wangu,” na tukaanza kupanda juu kwenda Ufalme wa Mbinguni! Mara tukafika kwenye
mlango wenye maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa dhahabu, yalisema: “Karibu
kwenye Ufalme wa Mbinguni.”
LANGO LA MBINGUNI


Yesu akasema, “Binti, ingia, kwa kuwa mimi ni Mlango na kila aingiaye kupitia kwangu,
ataingia na kupata marisho.”(Yohana 10:9)

Baada ya Bwana kusema maneno hayo, mlango ukafunguka na tukaingia. Niliwaona malaika
wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba Yetu wa Mbinguni! (Ufunuo 7:11-12) Kadri tulivyozidi
kutembea, tulikaribia meza niliyoweza kuona mwanzo wake laini siyo mwisho. (Ufunuo 19:9)
Niliona enzi kubwa, na enzi ndogo zimezungukwa na maelfu ya viti. Katikati ya viti niliona mavazi
na mataji. Bwana akaniambia, “Binti, taji unayoiona pale ni taji ya Uzima."(Ufunuo2:10)

Yesu akasema, “Tazama, Binti, hii ndiyo niliyowaandalia watu wangu.” Niliona ile meza
imefunikwa na vitambaa vyenye upindo wa dhahabu. Kulikuwa na sahani, glasi za dhahabu,
matunda; kila kitu kimeandaliwa. Ilikuwa nzuri ajabu. Kulikuwa na chombo kikubwa katikati ya
meza, kilichokuwa na mvinyo tayari kwa mulo. Na Yesu akasema, “Binti, kila kitu kipo tayari kwa
ujio wa kanisa langu.”
 17

MEZA YA KARAMU YA MBINGUNI

Tulikwenda mahali pengine, niliwaona watu wengi wakiwa bustanini. Kulikuwa na watu
wanaofahamika sana kwenye Biblia, lakini hawakuwa wazee, bali vijana. Palikuwa na kijana akiwa
na kitambaa mkononi, akicheza na kuzungukazunguka na kumsifu Bwana. Yesu akasema, “Binti,
Yule kijana pale ni mtumishi wangu Daudi.” Alikuwa akimpa utukufu Baba yetu. Ghafla, kijana
mwingine akapita na Yesu akaniambia, “Binti, huyu ni Joshua; Yule Musa; na Yule pale ni
Ibrahimu.” Yesu huwaita kwa majina yao. Wote walikuwa na mwonekano mmoja! Ajabu sana
Mbinguni! Yesu akasema, “Mwanamke Yule ni mtumishi wangu, Maria Magdalena; na Yule
mtumishi wangu Sara."

Lakini pia akaniambia, “Binti, huyu ni Maria. Maria, aliyemzaa Yesu Kristo, ambaye ni mimi.
Binti, nikwambie, yeye hana habari ya yanayotokea duniani. Nataka kukwambia, nenda
kawaambie wanadamu, waambie waabudu sanamu kuwa kuzimu ni halisi, na waabuduo
sanamu hawata urithi Ufalme wangu, lakini waambie kama wakitubu, wataweza kuingia makao
ya mbinguni. Nenda waambie nawapenda na pia waambie Maria hajui chochote
[kinachotendeka duniani] na pekee wanayeweza kuheshimu ni mimi, kwasababu si maria wala
mtakatifu Gregory wala mtakatifu yeyote awezaye kuokoa. Mimi ndiye niokoaye na nje yangu-
hakuna yeyote, hakuna yeyote, hakuna yeyote – aokoaye!” Alirudia mara tatu-kuwa hakuna
yeyote awezaye kuokoa; isipokuwa yeye.

Wanadamu wamedanganywa na kuamini kuwa kwa kupitia wadhaniwao ni watakatifu, sivyo
ilivyo, bali ni mapepo, yafanyayo kazi kupitia sanamu zilizofanywa kwa mikono ya watu. Lakini
ngoja nikueleze kwamba Bwana anataka kukupa kilicho bora. Anataka wewe uingie katika Ufalme
wa Mbinguni; tubu na kuacha uabudu sanamu. Kwasababu ibada ya sanamu haitakuokoa wewe.
Yesu Kristo wa Nazareti ndiye pekee aokoaye, aliyeutoa uhai wake kwaajili yako, yangu na
kwaajili ya wanadamu wote. Bwana ana ujumbe mzito kwa wanadamu. Huku akilia aliniambia,
“Tafadhari, Binti, usikae kimya; nenda na uwaambie ukweli, nenda na uwaambie
nilichokuonesha wewe.”
Sanamu za Maria na Waumini wa kisujudia

Nilimwona Maria akimwabudu Bwana, na niliwaona wanawake wakiwa na nywele ndefu nzuri.
Nikasema, “Bwana, wanapendeza sana walivyoweka nywele zao.” Akaniambia, “Binti, kile
uonacho ni utaji niliowapa wanawake.” Akaongeza, “Binti, nenda na uwaambie wanawake
watunze utaji niliowapa.” 18

Kisha akaniambia, “Nina kitu cha muhimu cha kukuonesha.” Nikatazama mbali kidogo na kuona
MJI UNG’AAO, MJI WA DHAHABU! Nikasema, “Bwana, kile ni nini? Nataka kwenda pale.”
Akanijibu, “Binti, nitakuonesha kilichopo pale. Ukionacho ni makao ya Mbinguni, majumba ya
Mbinguni yaliyotayari kwaajili ya watu wangu.”

Tulianza kutembea, hadi tukafika kwenye daraja la dhahabu. Mara tulipovuka daraja, tukafika
kwenye mitaa iliyotengenezwa kwa dhahabu safi! (Ufunuo 21:21)

Kila kitu kilikuwa kizuri sana, kuzuri sana pale, kunang’aa kama kioo, ni mahali pasipo pakawaida,
hakuelezeki! Tuliona majumba ya ki-mbinguni na pia tuliwaona, maelfu ya malaika wakijenga.
Baadhi ya malaika walikuwa wanajenga kwa haraka ya ajabu, na wengine pole pole na wengine
walikuwa wamesimama kabisa kujenga. Nikamuuliza Bwana, “Kwanini malaika wengine
wanajenga haraka haraka, wengine polepole, na wengine wamesimama?" Bwana akanieleza,
“Binti, hivyo ndivyo wafanyavyo watu wangu duniani, na malaika wanafanya kama wafanyavyo
watoto wangu duniani…. Binti, watu wangu hawahubiri neno langu. Watu wangu hawafungi
tena. Watu wangu hawaendi mtaani kusambaza ujumbe wa neno langu kwa vipeperushi
vinavyoeleza ukweli. Watu wanaona aibu kuhubiri. Nenda kawaambie watu wangu warudi
kwenye njia za zamani. Wale malaika uliowaona hawafanyi chochote ni malaika wa watu wangu
waliorudi nyuma na kuacha njia zangu… Binti, nenda waambie watu wangu warudi njia zao za
zamani,” (Yeremia 6:16) na baada ya kusema haya akaanza kulia Bwana.

Nikasikia watu wengine wakiimba, hivyo nikamuuliza, “Bwana, nataka unipeleke kule, ambako
watu wanaimba.” Yesu alikuwa akiniangalia, nakwambia jinsi alivyokuwa ananiangalia, sikuweza
kuona vema uso wake bali alikuwa akigeuza uso wake. Wakati huo machozi yalikuwa
yakimtiririkia kwenye vazi lake, nikamuuliza kwanini analia. Lakini hakuweza kunieleza.

Baadaye tulifika kwenye bustani nzuri sana. Pale katika majumba ya mbinguni, niliona maua
yalikuwa yakiyumbayumba huku na huku kama yapulizwayo na upepo. Hizi huenda ndizo sauti za
kuimba nilizozisikia. Bwana akaninyoshea kidole na kusema, “Binti, tazama, maua yananisifu
mimi; yananiabudu mimi! Watu wangu hawafanyi hivi tena kama walivyokuwa wanafanya
mwanzo. Watu wangu hawanisifu, hawaniiabudu mimi; hawanitafuti mimi kama mwanzo.
Ndiyo maana nalikwambia mwanzo, Binti, nenda na uwaambie watu wangu wanitafute, kwa
kuwa nitakwenda, nitakwenda, nitakwenda kwa wanaonitafuta kwa roho na kwa kweli, kwa
watu walio tayari, kwa watakatifu!” na huku akilia akasema, “Ninakuja, ninakuja!” hapo
nikaelewa kwanini alikuwa analia, kwasababu anakuja, lakini si kwa wasio na nia, watu wa nia
mbili [vuguvugu]. Atarudi kwa wale tu wanaomtafuta katika roho na kweli.

Ndipo Bwana akaniambia ninatakiwa kurudi duniani. Nikasema, “Bwana, Sitaki kurudi duniani!
Unamaanisha nini- duniani? Nataka kubaki na wewe Bwana. Umenileta huku na mimi siendi
kokote kwasababu niko na wewe!”
Yesu akasema, “Binti, ni muhimu urudi duniani ili ukashuhudie kwamba utukufu wangu ni
halisi, yote niliyokuonesha kuwa ni kweli; ili wanadamu waje kwangu, watubu na
wasiangamie.” Bwana akaanza kulia, nami nikaanguka miguuni pake; nikaona vidonda kwenye
miguu yake. Nikamuuliza, “Bwana, hivi ni vidonda vya nini?” akajibu, “Binti, ni vidonda ya jana,
nilipotoa maisha yangu kwaajili ya wanadamu.”
 19

MKONO WA YESU

Bwana akanionesha vidonda vyake vya mikononi, nilimuuliza, “Bwana, kwanini ungalinavyo hata
sasa?” akaniambia, “Binti, ni vidonda vilivyobaki.” Hivyo nikamuuliza, “je vitapona?” akanijibu,
“Vitapona na kufutika tu baada ya watakatifu wote kuungana hapa….. Binti, lazima
nikurudishe duniani: Familia yako na mataifa yanakusubiri wewe.”

Nilijaribu kukataa lakini akanyosha kidole chake chini duniani na kusema, “Tazama, wale watu
uwaonao chini pale ni ndugu zako; na mwili ule uuonao pale, ndiyo utakaoingia…… ni muda
wa kuondoka mahali hapa.” Baada ya hapo akaanipeleka kwenye mto mzuri mwangavu na
akasema, “Binti, ingia katika mto na jizamishe mwenyewe.” Kabla sijaingia ndani ya mto wa maji
ya uzima, nilikuwa najisikia furaha ya ajabu, lakini baada ya kujizamisha na kutoka nje, nilipata
furaha kuu. Nilidhani sitarudi tena nyumbani kwetu, lakini Bwana akaniambia, “Binti, unatakiwa
kurejea duniani….. Binti, nitakuonesha kitu: jinsi nitakavyorudi mara ya pili kwaajili ya watu
wangu watakatifu. Nitakuonesha jinsi siku ile ya kutisha itakavyokuwa.”

FURAHA NA MAOMBOLEZO
Tulitembea hadi sehemu yenye kioo kikubwa kama LUNINGA [TV], nikaona watu. Niliweza
kuona dunia yote. Ghafla nikaona maelfu ya watu wakipotea. Wanawake wenye mimba, mimba
zilipotea, na wakawa kama wamechanganyikiwa na kupiga mayowe.

Watoto walitoweka pande zote. Watu wengi walikuwa akikimbia huko na huku, wakipiga kelele,
“Haiwezekani, haiwezekani, nini hiki kitokeacho?”

Niliwaona wale waliomjua Bwana na kuachwa nyuma. (Mat.24:40-41) Walikuwa wakisema Kristo
amekuja, furaha imetimia. Walikuwa wakipiga kelele na kutafuta kujiua wenyewe lakini
hakuwezekana. Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo kifo kitawakimbia; Binti, siku hizo Roho
Mtakatifu hatakuwepo tena.” (Ufunuo 9:6) kulikuwa na ajali nyingi lakini sikuona hata mtu
mmoja aliyekufa: wote walikuwa wazima japokuwa wameumia [majeruhi].

Niliona mlolongo mrefu wa maelfu ya watu. Akaniambia, “Binti, tazama, hivi ndivyo kila kitu
kitakavyokuwa.” Kisha nikaona watu wakikimbia kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wakipiga
kelele, Kristo kaja, Kristo kaja!” wakisihi, “Bwana nisamehe mimi, nisamehe mimi, nichukue
nawe!”

 20

Baada ya Bwana kuwachukua watu wake [Unyakuo]

Lakini kwa huzuni Bwana akasema, “Watakuwa wamechelewa. Muda wa kutubu ni sasa…. Binti,
nenda kawaambia wanadamu wanitafute mimi, wakati huo hakutakuwa na nafasi. (Isaya 55:6)
Binti, watakuwa wamechelewa wote watakaobakia nyuma.” Baada ya Yesu kuona watu
wataobaki nyuma akaanza kulia na kusema, “Binti, nitakwenda duniani kama neno lisemavyo
katika 1 Thes. 4: 16-17: “Kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na
mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo
watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu,
ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa
maneno hayo.”

SIKU YA MWISHO

Lakini si kila mtu atakwenda na Bwana, wale tu wafanyao mapenzi yake (Mathayo 7:21) na aishiye
maisha matakatifu. Kwa kuwa Bwana aliniambia, “Wale tu walio watakatifu wataoingia Ufalme
wa Mbinguni, (Waebrania 12:14) Hakuna ajuaye, siku wala saa nitakayokuja kwaajili ya watu
wangu watakatifu, hata malaika hawajui.” (Mathayo 24:36)

Kwenye Kioo cha LUNINGA [TV] niliona watu wakikimbia huko na huku. Magazeti yalisema
“KRISTO AMEKUJA.” Kioo kikafungwa, na Yesu akamalizia kwa kusema, “Ninakuja kwa
watakatifu.” Hivi ndivyo alivyonionesha mimi. Baada ya hapo akanirudisha duniani hapa. Tukiwa
na kusanyiko la malaika wengi wakituzunguka, tulianza kushuka ngazi nzuri kama nini; ngazi
nyeupe na maua yakizunguka. Nilikuwa nalia njia nzima kushuka chini, nikimsihi Yesu, “Bwana
tafadhari usiniache hapa. Nichukue niwe nawe!” Alinijibu, “Binti, mataifa yanakusubiri,
familia yako wanakusubiri wewe…….. Binti, lazima urejee mwili wako. Lazima upokee uhai
wako, Binti, ili uweze kwenda kushuhudia yote uliyoyaona. Wengi hawatakuamini wewe; wengi
watakuamini, bali mimi ni shahidi wako mwaminifu. Niko pamoja nawe. Sitakuacha kamwe."




 21

KURUDI DUNIANI KWA ANGELICA
Maxima:
Binti yangu aliporudi, tulikuwa tunamsubiri pale, na alikuwa amelazwa pale pale chini sakafuni.
Nikasikia mguno, "uuhmm," bila kitu. Nikasema, “ahsante Bwana kwasababu Binti yangu
amerudi!”

Sote tulimshukuru Bwana. Mara akaanza kupumua polepole, kidogo kidogo. Baada ya muda wa
masaa matano, alikuwa na uwezo wa kufumbua macho na kusema. Mwanzo tulipata shida
kumuelewa asemacho; ilikuwa ni vigumu kumuelewa. Hakuwa na nguvu kabisa. Ilibidi tufunge
madirisha kwasababu macho yake hayakuwa na uwezo wa kuhimili mwanga.

Kwakuwa wadadisi, sote tulitaka atueleze alichoona. Lakini kwa kuwa alikuwa dhaifu, aliweza
kutueleza kidogo tu. Ilimchukua karibu wiki mbili hadi alipoweza kutushirikisha habari nzima ya
ushuhuda wake.

Mapepo yalikuja kumtesa baada ya hayo yote. Aliweza kuyaona waziwazi; yalijaribu kujificha
kwenye vivuli. Yalikuwepo hapa karibu siku tatu mfululizo tangu arudi, kabla hajaweza kutueleza.
Aliyauliza yalikuwa yanataka nini, nayo yakamjibu, “tumekuja kufanya mkataba nawe……. Ni
lazima ufunge mdomo, ni lazima usiseme lolote ya hayo uliyaona kule chini, kwasababu ukisema,
tutakuuwa.” Aliyaelezea yalivyo mapepo, yana sura mbaya, makubwa na manene yanatisha.
Alisema hakuna maneno yakuelezea jinsi yatishavyo kwa mwonekano. Alijaribu kuyakemea lakini
yalikataa kuondoka. Yakifika yalikuwa yanamrukia na kumchoma. Naye aliendelea kupambana
nayo na kuyakemea, lakini hakuweza kwasababu hakuwa na nguvu. Siku moja alipokuwa
anayakemea, mwanga mkali wa ajabu ulitokea na yakakimbia yote! Alikuwa ni Bwana.

Alichopitia Binti yangu hakikuwa rahisi. Alipewa ujumbe wenye maono ya ndani kwaajili ya
wanadamu, ili wamtafute Mungu. Wanadamu wanadhani wafanyayo ni sahihi. Vijana wamezama
kwenye madawa ya kulevya na pombe, na kuona ni sawa maisha hayo, lakini si sawa. Miongoni
mwa alioneshwa binti yangu ya kutisha ni wasanii wengi walivyojaa kuzimu, wanamuziki/wacheza
dansi na pia Papa John Paul II. Ni wakati wa kumtafuta Bwana, kutubu, na kujishusha na kujidhiri
mbele za zake. Neno la Mungu ni kweli lisemalo, “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu
hayatapita kamwe.”(Mark 13:31) Neno la Bwana litatimizwa katika muda wake. Bwana
alimwonesha tanuru ambalo watu walikuwa wanatembea kuelekea kuzimu. Na watu wengi tayari
wakiwakuzimu. Ni kweli haya, lakini hata watu wa Mungu hawaamini haya, wengi hawaamini.

Ujumbe mkuu ni kwamba tumtafute Bwana, siyo kwa kinywa/mdomoni, bali kutoka ndani ya
moyo, kwakuwa kurudi kwa Bwana ku-karibu. Yesu alisema, “Siko tena mlangoni; niko zaidi ya
mlangoni. Nakuja muda simrefu; kuja kwangu ku-karibu. Watu wangu wameniacha na
wamerejea mambo ya duaniani……… waambie watu wangu warudie njia zao za zamani.” 22

Kanisa leo linatakiwa kurudia njia zake za zamani; hapa tulipo ni wa motoni, tumtafute Bwana.
Pale parapanda ikilia tuwe tayari kukutana na Bwana, itakuwa ajabu sana!

UJUMBE WA MUHIMU WA BWANA

Angelica akiongea mbele ya haraiki:
Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo Roho Mtakatifu hatakuwepo tena duaniani. Siku hizo
hatakuwepo duniani.” (2 Thes. 2:7) Na nikaona msongamano mkubwa wa magari na ajali nyingi
sana. Watu wengi walijaribu kujiua, lakini Yesu akasema, “Watatafuta kifo, lakini kifo
kitawakimbia wanadamu. Kifo hakitakuwepo tena siku hizo.”(Ufunuo 9:6) Nikawaona watu
wakitazama LUNINGA [TV] na kusoma magazeti yakisema, “Maelfu na maelfu wamepotea.”
Wengi watajua kuwa Yesu ameshakuja kwaajili ya watu wake watakatifu. Wale waliomjua Bwana
lakini wameachwa, wakakimbia mitaani wakilia, wakijaribu kujiua wenyewe lakini hawakuweza
lolote.

Nilipokuwa mbinguni, Yesu alisema, “Nina kuja duniani kwaajili ya watu wangu watakatifu na
ninakuja mapema kwaajili ya kanisa langu.” Lakini wiki mbili zilizo pita Bwana aliniambia,
“Binti, ninafurahishwa na unavyotenda, kwa kuwa unatimiza niliyokuagiza na nakukupa, lakini
usiwaambie watu wangu kuwa nitakuja mapema, waambie ninakuja sasa hivi.” Tena Bwana
akasema, “Waambie watu wangu ninakuja sasa hivi na ninakuja kwa watu watakatifu. Waambie
watu wangu nakuja kwa watakatifu tu, nao ndio wataoniona mimi!.... tena usinyamaze: endelea
kuwashuhudia ninayokwambia.”

Angelica akiomba na haraiki:
Kila mmoja afumbe macho, na weka mkono wako wa kuume kifuani. Inua mkono wa kushoto juu,
kama unajisikia kulia[toba], lia tu. Sasa mweleze Bwana kile unachojisikia moyoni. Kwa wale
waliotayari kumpokea Bwana, wafuatiane nami ktika maneno haya:
Bwana, ninakushukuru kwa Upendo na huruma yako, ahsante Bwana kwa maneno yako
yaliyotufikia mioyoni leo. Baba, ninaomba msamaha kwako, unisamehe. Unisamehe mimi.
Unioshe kwa damu yako ya thamani. Andika jina langu katika kitabu cha uzima. Nipokee/nikubali
mimi niwe mwanao Bwana. Sasa hivi, ninamsamehe kila mtu niliyeshindwa kumsamehe. Ninakana
hali yangu ya kutosamehe. Ninayakana yote yalinizuia nisikufuate Bwana, ninaomba unibadilishe
Bwana na unijaze uwepo wako ndani yangu kila siku. Ahsante Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu,
Ameni.
 23



Angelica:
Ushuhuda huu siyo uwongo; siyo mzaha; siyo hadithi; siyo ndoto, kuzimu ni kweli ipo! Kuzimu ni
halisia! Kwa yeyote asiyeamini, nataka kukueleza kuzimu ni kweli ipo, ni kweli ni halisi. Ninakosa
maneno zaidi mazuri ya kuelezea uhalisia wa kuzimu. Natamani kama ungeshuhudia wewe
mwenyewe. Lakini tafadhari amini, tii na uonyeke kwa ushuhuda huu [ushuhuda ukuonye na
kukubadilisha] ili uepuke moto wa milele.

Angelica akiongea na Mfasiri/Muelezeaji:
Muda ukaribu sana, Mungu anaruhusu ishara kwa wanadamu zitokee ili kuwaonesha
kitakachotokea. Usibakie ukihukumiwa; ndilo shetani atakalo. Jiulize kama uko tayari ukitembea
kuelekea shimo la kuzimu? Leo ni siku ya wokovu, leo ni siku ya kumkaribisha Yesu, kuwa Bwana
na mwokozi wa maisha yako. Haya ni maneno rahisi lakini ni makubwa sana kusema: “Ninakubali
na kukupokea Yesu uwe Bwana na Mwokozi wangu. Ninakupa wewe maisha yangu na roho yangu
kwa moyo wangu wote. Natakuwa kuwa nawe kwa maisha ya milele.”

Chagua hatima yako baada ya maisha haya: Uzima au mauti, Mbinguni au kuzimu, Yesu au
shetani. Iko wazi, uko upande wa Yesu au upande wa shetani. Au unafanya yaliyo mema au
unafanya yaliyo mabaya. Chagua mwisho wako: uzima wa milele au ziwa la moto. Fikiria jambo
hili. Fanya uamuzi sasa. Yesu Kristo alikufa msalabani kwaajili yetu, kwa dhambi zetu, na akatupa
fursa ya wokovu kwa huruma yake. Mpokee Yesu Kristo kuwa mwokozi wako!

“Sasa umesikia ushuhuda huu, usiipoteze nafasi hii
ukaijutia milele na milele motoni.”
 24

Marejeo:
Ufunuo 19:9 ….Heri walioalikwa karamu ya arusi ya mwanakondoo. ……..maneno haya ni
maneno ya kweli ya Mungu.
Ufunuo 20:15 Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa
katika lile ziwa la moto.
Ufunuo 21:4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwepo tena; wala
maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza
yamekwisha kupita.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya
kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na
hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti.
Hii ndiyo mauti ya pili.

“Hakuna waabuduo sanamu wataourithi ufalme wa Mbinguni.”

Kutoka 20:4-5 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu
mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu wenye wivu……..
Ufunuo 21:21 Na milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia
ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
Ufunuo 21:27 Na ndani hakitaingia kamwe chochote kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na
uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana koondoo wa Mungu.
Ufunuo 22:7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
Ufunuo 22:11 Mwenye kudhuluma na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu;
na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
Ufunuo 22:12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi
yake ilivyo.
Ufunuo 22:13-15 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri
wazifuao nguo zao, wawe na amri ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango
yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila
mtu apendaye uongo na kuufanya.

Ndugu aliyefasiri ufunuo huu ni Alpha Wilson Magubila ni Mwana UWATA (Uamusho Wa Wakristo Tanzania); Jumuiya
iliyosajiriwa na Yenye Msingi wa Kutubu Dhambi na kuziacha (Mithali 28:13). Waebrania 6:4-6, 2Petro 2:20-22.
Anuani ya Posta: 80405, Dar es Salaam Tanzania, East Africa,
Simu ya Mkononi: +255-754-644559, +255-715-644559.
Barua Pepe: alphawilsonm@hotmail.com.

No comments:

Post a Comment