Saturday, October 26, 2013

UKWELI KUHUSU ZAKA

ZAKA AGANO JIPYA?

By Apostle Eliya-0756 166 934

YALIYOMO
1.Utangulizi
2.Nani ni Nani
3.Zaka Agano Jipya ?
4.Zaidi Ya Zaka
5.Hitimisho

LENGO LA SOMO
- Kuonyesha nani anayestahili kupokea Zaka
- Kuonyesha uhalali wa Zaka nyakati zetu

ANDIKO KUU ;- MWANZO 14:18-20

1. UTANGULIZI
- Utakumbuka Zaka imezungumziwa sana Agano la Kale,kwahiyo nitakuchukua nikupeleke kwa makuhani na walawi na wana wa Israeli. Ukweli utakaougundua utakushtua, huwezi kuamini.

2. NANI NI NANI
- Nani ni nani maana yake ni nani anapaswa atoe zaka, na nani anapaswa apokee zaka. Kwamujibu wa Mungu, mtu ambaye hana dhambi ndiye aliyestahili kupokea zaka, na mtu yeyote mwenye dhambi alitakiwa atoe zaka, kwa lazima ili uwepo wa Mungu uwe juu yake.

- Mchakato wa zaka ulianza rasmi wakati wa ukuhani, kulikwa na makabila 12, makabila 11 yalipaswa yatoe kwa kabila moja la walawi, na katika kabila la walawi kulikuwa na kundi la makuhani, na katika kundi la makuhani kulikuwa na familia ya kuhani mkuu, na mwisho kuhani mkuu ambaye alikuwa Haruni.TORATI 18:5

►Huduma ya Ondoleo la Dhambi ;- Watu au mtu anayefanya huduma ya Ondoleo la Dhambi ndiye aliyestahili kupokea zaka. Ndiyo maana nikasema asiyekuwa na dhambi ndiye aliyestahili ili awafanyie upatanisho wengine, hivyo ilim’bidi Haruni atoe Ng’ombe peke yake ili angalau awe mtakatifu na wapatanishe wengine. – Walawi 16:11

b) Majukumu ya kuhani
Haya ndio yaliyokuwa majukumu ya kuhani,- Waebrania 8:3
1)kutoa dhabihu (2)kutoa vipawa (zawadi)
-Utagundua utoaji wa zaka unahusiana moja kwa moja na ondoleo la dhambi na kupokea vipawa, mtu mwenye dhambi hakuluhusiwa kupokea zaka wala kutoa vipawa (zawadi). Ni laana kumpa zaka mwenye dhambi.

►Kutoa Dhabihu – Kuhani alikuwa akichukua matoleo kutoka kwa wana wa Israeli na kuyagawanya katika taratibu zake, matoleo mengine yalikuwa yakichomwa, mengine yakitikiswa,mengine yakichinjwa. Lakini kati ya matoleo yote haya, matoleo mengi yalikuwa yakichomwa na yaliyobaki yalikuwa mali ya makuhani, hii desturi ilikuwa ni kila siku asubuhi na jioni, lakini sadaka zilikuwa zikichomwa usiku kucha, moto ulikuwa hauzimiki kwa ajili ya sadaka ya dhambi.WALAWI 6:13

► Kutoa Vipawa – Hii huduma ni muitikio wa Mungu kwa wana wa Israeli,Mungu alikuwa anawapa zawadi kwa kuwa wamejitakasa na wameondolewa dhambi kwa yale matoleo waliyoyatoa.Ndio maana akawaahidi kuwabariki na kuwalinda na alae. MALAKI 3:11

d) Majukumu ya wana wa Israeli
(1) Kutoa zaka zote na kamili sehemu sahihi. MALAKI 3:10
►Sababu za kutoa zaka (1) Wasamehewe dhambi (2) Wapate vipawa (baraka)

-Katika sababu zote mbili utagundua zaka za Israeli ilikuwa ni kwa ajili yao wenyewe. Makuhani wale, washibe ili wawahudumie katik ondoleo la dhambi. Kwakufanya hivyo Mungu akasamehe dhambi na kuwalinda.

3. ZAKA AGANO JIPYA ?
-► Kuhani mkuu Agano jipya ni Yesu, na wana wa Israeli ni kanisa.

a) Majukumu ya kuhani Yesu
1. Kufanya upatanisho na (2. Kutoa Vipawa(zawadi)- Yohan 14:16-17
Majukumu makuu ya ukuhani yesu alishayatimiza yote, alifanya upatanisho—Ebrania 9:12, alishatoa vipawa,zawadi,karama na huduma – Efeso 4:11, katika Agano Jipya, Roho Mt ni zawadi pekee ambayo kuhani anapaswa atoe kwa watu wanaomtolea zaka,— Mathayo 20:22

b) Majukumu ya Kanisa (ktk zaka) ---
(1) Kutoa nafsi kamili – Mathayo 16:26 – Mungu anaithamini nafsi sana.
(2)Kutoa matoleo sehemu sahihi – LUKA 5:14

►Sababu za kutoa zaka
(1) Kupeleka injili. RUMI 10:15
(2) Kumuwezesha Mtumishi aliyepigwa muhuri na Roho Mt.FILP 4:15

Yesu hahitaji kuwezeshwa na zaka zetu na pia Yesu hahitaji zaka zetu ili akampatie Mungu, au ili aendelee kutupatanisha kila mwaka.

4. ZAIDI YA ZAKA
-► Kuhani mkuu Yesu, ametutolea zaka bora kwa Mungu akapaa kwenda mbinguni, majukumu ya kikuhani ambayo Yesu ameliachia kanisa ni mawili; - (1) Kusambaza injili na (2) kuwawezesha watu kupata Roho Mt.
Mtumishi sahihi lazima ajilengesha katika haya majukumu mawili.

a)Kwanini Utoe Zaka ?. Kwaupatanisho alioufanya Yesu unatubidiisha zaidi ya kutoa, Mungu haitaji zaka, anatuhitaji sisi kama tulivyo, anahitaji toleo zaidi ya zaka, ndio maana Mitume walitoa vitu vyote shirika, walijua Mungu anataka miili yao, nafsi,roho na mali zao zote – MATENDO 2:44-47
-Unatakiwa utoe zaka kwasababu umeshindwa kutoa mali zako zote na moyo wako, kwasababu Mungu hataki zaka, anataka kila kitu chako. Kwahiyo Agano Jipya tunatoa zaka kwasababu tumeshindwa kutoa mali zetu zote ukilinganisha na kazi ya upatanisho ya Yesu na kipawa alichotupa cha Roho Mt.

- Kama kutoa zaka ni muhimu, Swali linalokuja, zaka apewe nani ? kwasababu mpokea zaka angestahili kuwa Yesu sasa hayupo !! Wengi wamejifanya watumishi ili wapokee zaka. Toa zaka kwa mtumishi aliye sahihi, utamjuaje mtumishi sahihi ?

b) Wapi utoe zaka ? – mimi nakushauri toa zaka sehemu ambayo wanafanya kazi ya kikuhani aliyoiacha Yesu --- kutoa vipawa (zawadi), ninamaanisha hivi, katoe zaka ulipo pokea Roho Mtakatifu. Dalili ya kujua mtumishi anastahili kupokea zaka ni kuwezesha watu wapokee Roho Mt, hapa haijalishi wito wa mtumishi. Kila mtumishi wa kweli nilazime awe amepigwa muhuri na Roho Mt ili awawezeshe wengine kupokea Roho Mt.

- Wewe kama ni mtumishi usiniambie kwamba huna wito wa kuwa na Roho Mt, anayetofautisha wito ni Roho Mt, hivyo kila mpokea zaka anatakiwa awe na Roho Mt na awezeshe wengine kupokea, yaani huu ndio msingi wa mpokea zaka halali.

► Naomba watu wafundishwe hivi;- Badala ya kuwafundisha kutoa zaka ni Amri, waambiwe kile Yesu alichofanya kuondoa dhambi ili watu watoe zaka kwa moyo wa kuelewa, kwamba wanachokitoa hakiendani na walichofanyiwa.Kwahiyo zaka iwe pale pale ila mtazamo na msukumo ubadirike, wajue bila Yesu, chochote wanachokitoa kisingewakomboa.GALATIA 5:18

5. HITIMISHO
- Tafadhali Wachungaji – kama hujawawezesha washirika wako kupokea ahadi kuu ya Mungu, Roho Mt, hiyo zaka haupokei kihalali, hebu uwe na huruma, wamekuwezesha wewe tu lakini wewe hujawawezesha.

-Tafadhali Waumini – Zaka unayotoa, kama ungempa anayewezesha watu kupokea ahadi kuu ya Mungu, Roho Mt, usingeibiwa, na Mungu angekulinda na alae.

- Soma KUMB TORATI 18:1-5, Kama Mungu amemuita kweli mtumishi, Mungu atakutoshereza, usiwatishie washirika kuwa wasipotoa zaka watakufa, au Mungu atawalaani, sio kweli.

...................................................................THE BEST HAS COM................................................

No comments:

Post a Comment