Saturday, November 9, 2013

MOTO WA KIGENI



MOTO WA KIGENI.
by APOSTLE ELIYA

YALIYOMO
1. Utangulizi
2. Moto wa Kigeni
3. Hitimisho

MALENGO YA FUNDISO
-         Kuona madhara ya Moto wa Kigeni kanisani
-         Kuonyesha nini kifanyike kuondoa Moto wa Kigeni

ANDIKO KUU ;- Kutoka 30:7-8

1. UTANGULIZI
- Vitabu vitano vya Musa ni kivuri cha mambo ya Agano Jipya, katika torati, Mungu anapomuua mtu ujue kwamba hilo jambo ni siriasi hata Agano Jipya, pia Mungu anaposema ‘jambo fulani litakuwa milele’ Agano la kale, anamaanisha milele mpaka Agano Jipya isipokuwa utaratibu ndio utabadirika, lakini maana iwe ileile ya umilele.

- Moto wa Kigeni na Uvumba ni somo ambalo litakufanya upanue upeo wako kuhusu Mungu na kanisa lake la sasa, ambao ni mimi na wewe.

2. MOTO WA KIGENI
- Kwa wale wapembuzi wa Biblia hili neno sio geni kwao, andiko letu kuu linaonyesha kulikuwa na UVUMBA ambao ulipaswa uchomwe ili ulete manukato mazuri kwa Mungu, Sasa kuhani hakupaswa aweke uvumba wa kigeni, wala Moto wa kigeni

a) Taratibu za Mungu
-Mungu anapofanya jambo huwa anakuwa na taratibu zake, huwa hategemei mchango wa mawazo ya wanadamu—Kutoka 25:40, anataka watumishi wake wafanye kama Mungu anavyowaelekeza na washirika waitikie kile Mungu alichomuelekeza mtumishi wake.

- Siku ikatokea watoto wa Haruni kuhani walichukua moto wa kigeni kwa ajili ya kuchomea uvumba.Moto wa kigeni ulikwa ni moto ambao Mungu hakuwa amewaagiza wautumie, nini kilitokea ? –Walawi 10:1-2—walikufa bila huruma.

- Inamaanisha nini Mungu alipowaua wana wawili wa Haruni !!, inaonyesha hilo jambo lilikuwa siriasi(la umakini), ingekuwa Agano Jipya Mungu angefanya nini ?, angeondoa uwepo wake kati ya huyo mtu husika.

b) Agano Jipya
- Adhabu ya kifo Agano la Kale ni sawa na Mungu kuondoa Roho yake katika Agano Jipya. Moto uliokuwa ukitumika Agano la Kale ni sawa na Roho Mt katika Agano Jipya. Kila kitu tunachokifanya ibadani/kanisani sisi tulio okoka, Roho Mt anakiunguza ili kifae mbele za Mungu, Mfano;- Mahubiri, kuvuta watu,kujenga kanisa,kuwasaidia watu…nk.

- Moto wa kigeni Agano Jipya ni chochote kile ambacho mchungaji anakitumia kuleta watu kanisani nnje ya Roho Mt, Moto wa kigeni Agano Jipya ni kitu chochote ambacho kinamfanya mshirika awe kanisani nnje ya Roho Mt, kwahiyo moto wa kigeni upo wa aina mbili, ule unaotengenezwa na mchungaji ili kuongez washirika na ule mtu anaojitengenezea ili awe mshirika katika kanisa fulani. Kuwa na mipango ya kuvuna nafsi za watu kwa kutumia huduma za kawaida ni mizuri, lakini mara nafsi zikishavunwa haraka sana zikutanishwe ana kwa ana na Roho Mt. ---MDO 8:14-17

c) Moto wa kigeni wa WAUMINI ----- chochote kile ambachokinamvutia mtu kuwa mshirika katika kanisa fulani,nnje ya Roho Mt huwa ni Moto wa kigeni, mfano;- Jengo zuri, wamesoma, kuna vyombo, kuna vijana wa kutosha, watanipa mtaji, mchungaji amesoma, pako barabarani, walinisaidia sana, wana jumuia,wako wengi, kwaya yao nzuri,hawadai sadaka,matajiri wengi,wengi kabila langu,ukoo wangu wanasali hapo,nimeambiwa nisali hapo,mchungaji ni mpole,kanisa lipo karibu,wameniajiri,wamenipa uongozi,nimetoka nao mbali,walinisomesha,huwa wanakuwa na matamasha,huwa wanakuwa na makongamano,huwa wanatembeleana,wanaozesha kirahisi,wanatoa usafiri mpaka nyumbani. Hizi ni baadhi ya sababu zinazotengeneza Moto wa Kigeni katika maisha ya muumini. Sababu hizi sio mbaya,ila zinapochukua nafasi ya Roho Mt tayari umeshakuwa Moto wa Kigeni.TORATI 4:24, MATHAYO 16:26

-FAIDA ----- Utapata kanisa linaloendana na wewe unavyotaka kimwili,watakupa ada,    watakupenda, watakutembelea, watakukopesha….nk.

-HASARA ---- Utamkosa Roho Mt, zile shida zako za ndani kabisa hazitapata msaada, hautafunguliwa kwasababu huyo mtumishi uliyemfuata alikuwa amekutegeshea chambo cha Moto wa Kigeni ili akunase kwa mambo ya mwilini. –Mathayo 16:26

- USHAURI – Chochote kitakachokuvutia kusali sehemu fulani nnje ya Roho Mt kitakuwa mtego kwako, tafuta sehemu ambayo watakuwezesha kupokea Roho Mt, hili ndilo tumaini lako la pekee,hayo mengine yote ni kupoteza muda.Kama kanisa fulani wamekuvuna,haraka sana waambie wakusaidie upokee Roho Mt,sio hisia za Roho Mt.

d) Moto wa Kigeni wa WATUMISHI-------- hizi ni mbinu ambazo watumishi wa Mungu wanazitengeneza ili angalau kuwafanya watu wavutiwe ili waje katika makanisa yao, Mfano;- Tunasomesha, Tunatoa ajira, mchungaji nimesoma, usafiri upo,tujenge barabarani,nimewasaidia wengi,kuna chakula,pesa za kurekodi zipo,tunasaidia watu kuoa au kuolewa,nimeagiza seti ya vyombo, tutakupa nyumba, nitakuja chuoni kutoa semina,huwa sikasiriki,kila unachotaka nitakupa,tuimbe sana wapita njia wasikie,mimi ninamuonekano mzuri,navaa suti ili waje wenye pesa,naweka ibada ya kiingereza ili wasomi waje,fanyeni mninunulie gari ili watu waniheshimu,nirusheni kwenye mitandao,Runinga na redioni wanitafute,ninawapigia simu washirika wangu mara kwa mara,katika mahubiri nitaweka maneno ya kizungu,imbeni vizuri kama wazungu,mkiimba onyesheni kububujika,weka bango kubwa. Hii ndiyo baadhi ya Mioto iliyo katika mawazo na matendo ya watumishi wengi. Yote ni mema lakini yanapokuwa ndio kivutio bila Roho Mt yanakuwa Moto wa kigeni.

- FAIDA ---- Mtumishi atawapata wale aliowarushia chambo,watu watajaa,waimbaji watakuwa wengi,matajiri watakuja,atawatumia atakavyo, atavuna pesa…..nk.

- HASARA ----- Atakosa mtembeo wa Roho Mt, atatoa hesabu ya alivyowatumbuiza waumini, hataweza kufungua shida za ndani kabisa,watu watakuja na matatizo yao na pia watarudi nayo,washirika hawatapata msaada wa kiroho kwasababu mtumishi aliwavutia na Moto wa kigeni.

- USHAURI- Kama mtumishi anataka avune nafsi za watu kwa kupitia mambo ya kawaida sio mbaya, lakini huyo mtu anapoanza kuja kanisani haraka sana akutanishwe na Roho Mt, namaanisha awezeshwe kupokea Roho Mt kwasababu ndio tumaini pekee la mshirika. Nikisema Roho Mt namaanisha Roho Mt sio malue-lue,sio kuaminishwa tu.
MDO 19:1-6

3. HITIMISHO
- Kama washirika na watumishi wataamua waelekeze vipaumbele vyao kwa Moto sahihi Roho Mt watagundua kuwa Mungu alishawaondoa katika uwepo wake kama watoto wa Haruni waliouawa, --Mathayo 6:33

-Mungu hana mchezo, anataka kila mtumishi atembee katika wingu la kumsikia Roho Mt, vinginevyo ni kuwaumiza washirika na kuwapoteza,kwasababu hakuna kitu bora mtumishi atakachompa mshirika zaidi ya Roho Mt,hakuna…hakuna…hakuna...hakuna.
ISAYA 42:19

- Kila mtumishi alenge kuwasaidia washirika wakutane na Roho Mt na kila mshirika adhimilie kutafuta mtumishi ambaye atamuelekeza kupokea Roho Mt, vinginevyo,kwa wote wawili ni Moto wa Kigeni.

…………….……THE BEST HAS COME……………..

No comments:

Post a Comment