AGANO KUU
YALIYOMO; 1).UTANGULIZI
2).AGANO KUU 3).HITIMISHO
DHUMUNI LA SOMO
- Kugundua Agano kuu kati ya sisi
na Mungu
ANDIKO KUU; Ezekieli 37:27 –
‘Tena maskani yangu itakuwa pamoja nao,nami nitakuwa
Mungu wao,nao watakuwa watu wangu.’
1. UTANGULIZI
- Kila Mwanadamu asiyesikia au kusoma
au kujua hili Agano kuu amelaaniwa, narudia tena A M E L A A N I W A ---
YEREMIA 11:3-4. Mtu yeyote asiyejua hili Agano kuu ALAANIWE, ALAANIWE, TENA
ALAANIWE kabisa
- Wengi wanajua kuna maagano mawili,
la kale (AK) na Jipya (AJ), lakini sio kweli. Agano lipo moja tu, ndio
nimeliita AGANO KUU. Kwamujibu wangu AK naliita MCHAKATO KIVULI na AJ naliita
MCHAKATO HALISI.
- Ukweli ni kwamba Mungu ameweka agano
na kila kilichoumbwa, kalini sitazungumzia haya maagano, mfano; agano la
chumvi, Agano la walawi na Yuda, agano la viumbe, agano la marafiki na agano la
Macho, badala yake nitazungumzia Agano moja tu --- Agano kuu.
2. AGANO KUU
- Nimemshangaa sana Mungu baada ya kusoma hili
andiko – TORATI
29:10-15 Mungu aliweka Agano moja(Horebu) na wanadamu wote, Kuanzia Ibrahimu
mpaka Mtanzania wa mwisho, rudia kusoma huo mstari wa 15. Bado Yesu akarudia =
YOHANA 17:20. Tofauti iliyopo ni MICHAKATO (Matengenezo) ya kufanya hilo Agano liwe halisi.
EBRANIA 9:10
A).AGANO LIPO MOJA TU
- Kama Mungu ameweka Agano na kila kiumbe, itakuwa
ni ajabu sana asipokuwa na Agano na Mwanadamu, pia itakuwa ni ajabu sana akiwa na Maagano
tofauti-tofauti na wanadamu, ndio maana nasema kuna Agano moja.
- Yeremia 11:4. Ahadi Kkuu ya Agano kuu ni Uzima wa
milele = 1YOH 2:25
- Agano Kuu Moja ni Lipi? EZEKIELI 37:27
-
Agano kuu hili hapa, Mungu anasema; “Maskani yangu itakuwa pamoja nao”, “Nitakuwa Mungu wao”, “watakuwa watu wangu”. Hili ndilo Agano Kuu, lina sentesi tatu (3) tu.
AU
-
Kwa Kiswahili kingine Mungu angesema; ‘Nitakuwa na mahusiano nae’, ‘Nami nitakuwa Mume wake’, ‘naye atakuwa mke wangu’ =ISAY
54:5-6
AU
-
Ni sawa na Mungu kusema; ‘Makao yangu pamoja nao’, ‘Nitakuwa Baba yao’, ‘Watakuwa wana wangu’. = UFUNUO 21:7
-
Sasa ili hili Agano Kuu litimie, kulikuwa na vikwazo
ambavyo vilitakiwa viondolewe kwa michakato maalum, hii michakato ndio watu
wakaiita Agano la Kale na Agano Jipya. Hii ni michakato tu na sio maagano. YEREMIA
31:33-34
- Vikwazo Vikuu cha Agano Kuu.
- Kwazo la kwanza ni Dhambi
- Dhambi ya ulimwengu – YOHANA 1:29
- Dhambi halisi – YOHANA 5:14, 8:11, 1YOH 2:2
- Kwazo la pili ni Mungu na Agano lake kueleweka
kwa wanadamu. Sio rahisi mtu amuelewe Mungu asiyeonekana na Agano lake lisiloonekana.
Ndio maana Mungu amekuwa akitumia Ahadi, angalau tu aeleweke. ISAYA
53:1
- Vichakatuo Vya Agano Kuu
- Vichatuo ni vitu ambavyo vilitakiwa
vifanywe ili Agano kuu lifanyike kisha liwe endelevu;
·
Mungu anaanzisha Agano kwa kutamka NENO – MWANZO 12:1
·
Mwanadamu anaitikia kwa kuamini— kwa hiyari- TORATI 30:14
·
Mungu anafuta Dhambi za Mwanadamu -- kwa Damu – WAEBR 9:12
·
Mungu anampongeza Mtu kwa kuamini— anampa Roho - MDO 2:28
·
Mtu anatakiwa atunze Agano -- asimhuzunishe Roho - EFE
4:30
- Vielezi vya Agano Kuu
- Ili Mungu aeleweke kwa Mwanadamu,
anaambatanisha Ahadi na viapo kwenye Agano kuu, kwasababu sentesi 3 za Agano
hazimshawishi Mwanadamu kujibidiisha kwenye Agano kuu;
·
Nchi Mpya – 17:7-8
·
Uzazi mwingi – MWANZO
28:14
·
Baraka/utajiri/kutawala – MWANZO 22:17-18
- Ishara(Viashiria) Vya Agano Kuu.
- Kama
umegundua ni kwamba Agano ni NENO tu linalotamkwa, hivyo Agano huwa
halionekani, kwasababu hiyo Mungu ameweka Ishara ili iwakumbushe wote wawili
kuwa wapo kwenye Agano Kuu;
·
Damu --- ni kwa ajili ya Mungu – KUTOKA 12:13
·
Kupigwa muhuri --- Nikwa ajili ya Mwanadamu – MWANZO 17:11
=►Malupu-lupu ya Agano Kuu ni Baraka – utajiri na kumtawala Adui.
B) MCHAKATO KIVULI NA MCHAKATO HALISI
- Hili Agano la Kale lilitoka wapi ? Hili lilikuwa
ni wazo zuri la watu(Baada ya Yesu) kuwafanya watu waelewe utofauti wa kabla na
baada ya Yesu, hivyo wakaamua nyakati za kale waziite Agano la Kale na Nyakati
za Yesu waziite Agano Jipya. Lakini kiuhalisia, sio maagano.
- Nimekwisha kueleza hapo juu kwamba Agano kuu ni
moja lakini michakato ya kufanikisha hilo Agano Kuu ni tofauti kwa uhalisia
wake, sasa angalia jedwali hapa chini uone tofauti ya mchakato kivuli na
mchakato halisi. Kumbuka Agano Kuu ni Moja
MCHAKATO
|
KIVULI
|
HALISI
|
Nchi Tarajiwa----
|
Kanaani
=LAW 25:38-------------
|
Mbingu
Mpya=UFUN 21:1
|
Makuhani---
|
Walawi =
HESABU 17:8
|
Yesu =
WAEBR 5:6
|
Wafalme-----
|
Yuda =
|
Yesu = UFUNUO
17:14
|
Kafara------
|
Wanyama
= LAWI 23:19
|
Yesu = WAEBRANIA
10:10
|
Dhambi------
|
Kusitiriwa
= ZABURI 85:2
|
Kufutwa
= EFESO 1:7
|
Viongozi----
|
Torat/makuhani=
|
Roho Mt
=RUMI 8:9
|
Msamaha-----
|
Kila
sabato= EBR 10:11
|
Mara
moja tu= EBRA 9:12
|
Sheria------
|
Zaidi ya
600
|
1 =
EFESO 4:30
|
Amri
|
10 =
KUTOKA 34:28
|
2
=MATHAYO 22:37-40
|
Dalili
za Uwepo-------
|
Sanduku
= KUTOK 29:43-46
|
Roho Mt
= EFESO 1:13-14
|
Vita na
adui
|
Mataifa
= TORAT 20:17
|
Shetani/pepo
=EFESO 6:16
|
Wahusika
wakuu-------
|
Israeli
tu =KUTOK 3:10
|
Mtu
yeyote =MARKO 16:15
|
Tohara------
|
Zunga =
MWANZO 17:11
|
Moyo
=YEREMIA 4:4
|
Makutanio----
|
Sandukuni
=KUTOK 25:22
|
Moyoni =
KOLOSAI 1:27
|
Kuhesabiwa haki---------
|
Kwa
Sheria =LUKA 1:6
|
Imani
=RUMI 1:17
|
Ghafi za
Hekalu-------
|
Jengo
=1FALME 5:18
|
Mwili =1
KORINTHO 3:16
|
Makao ya
Roho
|
Nnje,juu
= ISAYA 61:1
|
Ndani =
YOHANA 14:17
|
Thawabu------
|
Ya muda
= EBRANIA 4:8
|
Uzima
milele = MDO 13:48
|
C) MCHAKATO KIVULI
- Agano Kuu lilianzia kabla ya ulimwengu kuumbwa =
TITO 1:2, Adam na Eva, wakalivunja, Mungu akawafukuza. Toka hapo Mungu akaanza
kutafuta mtu atakayekubali kufanya nae Agano tena, lakini huyo mtu shariti
asiwe na dhambi, kwahiyo mahangaiko yoote ya watu wa kale ni kuondoa kikwazo
cha Dhambi, lakini haikuwa rahisi kuondoa dhambi kama
walivyodhani. MWANZO 3:24
- Mara zote Mungu amekuwa akimtaja Ibrahim, Isaka na
Yakobo katika Agano kuu – WAAMUZI
2:20, Kwasababu ya kutii kwao aliwapa na Ahadi—Uzao, Nchi
na Baraka = MWANZO 17:14. Pia akaweka Ishara ya Agano nao—Kutahiliwa, yote hayo hayakuwa Agano =
JOSHUA 5:2. Ninashawishika kuona kwamba Mungu anajua vizuri sana namna ya kuuza wazo lake la Agano.
- Chunguza hizi sehemu tatu 1) Misri
2)Horebu(Jangwani) na 3) Kanaani. Mungu aliwakomboa Israeli Misri ili aweke nao
Agano = KUTOKA 8:1, akaweka nao Agano Jangwani(Horebu)= TORAT 5:2, ili akaishi
nao Kanaani=WALAWI 25:38. Zoezi hili halikuwa rahisi. Mungu kupata hisia zao
aliamua atumie utumwa wao kuwatajia Nchi yenye Maziwa na Asali, jangwani
ilikuwa ni shule ya kuishi kanaani= TORATI 4:10.
- Kama wewe ni
msomaji mzuri wa Biblia utakubaliana na mimi kwamba kila kitu kilichokuwa
kikitumika kwa ajili ya Mungu wakati wa kabla ya Yesu kiliitwa -- cha Agano.
Ikumbukwe kuwa vyenyewe SIO Agano ila ni vitu vya Agano;
·
Sanduku la Agano = 2 NYAKATI 5:7
·
Torati ya Agano = 2 WAFALME 23:2-3
·
Damu ya Agano = KUTOKA 24:8, MATHAYO 26:27-28
·
Ukuhani wa Agano = MALAKI 2:4-5
·
Mbao za Agano = TORATI 9:9
·
Waisraeli-Taifa la Agano = 2 SAMWELI 7:23-24
Sina uhakika sana kama Israeli walikuwa wanajua
wanachokifanya, ni kanakwamba Mungu alikuwa anawalazimisha ingawa ni kwafaida yao wenyewe. Nina uhakika,
Zoezi la ibada, Sheria, Vita …nk
vilikuwa vinawakela sana
= 2FALME 17:15, kwasababu walikuwa hawajui dhumuni, lakini wachache walitambua.
Swali; Watu wangapi walitoka misri na wangapi
walioingia Kanaani ?
-Ndivyo Mungu alivyofanya kwetu, ametutoa mikononi
mwa 1)Shetani=KOLOSAI 1:13 ili tufanye nae Agano kwa 2) Yesu na Roho(Duniani)=ISAYA
53:11b ili tukaishi na Mungu 3) kwenye Ufalme wake = MATHAYO 8:11. Tupo hapa
Duniani kujifunza namna ya kuishi mbinguni, pia wengi wetu hawajui dhumuni,
hivyo wengi hawataingia kwenye Ufalme = MATHAYO 7:14. Lakini ashukuriwe Mungu
kwani watu wengi miaka hii wameanza kuelewa.= UFUNUO 5:9
D) MCHAKATO HALISI – YESU
- Utagundua mvunja Agano siku zote ni Mwanadamu,
labda waisraeli hawakujua umuhimu au walifanya makusudi au walijua umuhimu
lakini hawakuwezeshwa, vyovyote vile, Mungu aliamua atatue matatizo yote ya
Agano Kuu kwa kumleta Mwanawe Yesu = KOL 1:20.Kipi kilimfanya Yesu aje?
1. Dhumuni la Ujio wa Yesu;
·
Kubadiri kivuli kuwa Halisi = WAEBRANIA 8:13
·
Kusajiri watakaoingia kwenye Agano Kuu = UFUN 5:9-10
2 Yesu na Tarajio Jipya.
- Yesu alikuja kutoka mbinguni,
anapotaja ulimwengu ujao anauhakika.
·
Ufalme wa Mungu = YOHANA 14:2-3
·
Uzima wa milele = TITO 1:2
·
Kutawala milele = UFUNUO 22:5
3. Vikwazo vya Agano kuu – kwa mujibu wa Yesu.
- Kikwazo hapa sio dhambi, kikwazo
kimebadirika
·
Kutomwamini Yesu = YOHANA 8:24
·
Kumkufuru na kumhuzunisha Roho Mt = MATH 12:31,
EFESO 4:30
4. Vichakatuo vya Agano Kuu – kwa mujibu wa Yesu
- Mambo yanayowezesha kuwepo kwa Agano
Kuu kwa mchakato Halisi
·
Yesu (Injili)= 1 KORINTHO 15:1-4
·
Roho Mt = RUMI 8:14
·
Mwamini = 1 WATHESALONIKE 5:10
►Tunayapokea
Yote haya kwa kuliamini jina la Yesu = WARUMIN 10:9
5.Ishara za Agano Kuu –kwa mujibu wa Yesu
- Sifa ya Ishara au kiashiria ni
lazima kionekane, sasa utamjuaje mtu aliye ndani ya Agano Kuu ?
·
Kumwamini Yesu = YOHANA 11:25
·
Uwepo wa Roho Mt- Karama na Matunda = 1 KORINTHO
12:4-6
·
Kuwa na Nguvu- Kutoa Mapepo = LUKA 11:20, 1 KORI
4:20
=►Ahadi kuu
ya Agano kuu ni uzima wa milele = yuda 1:21
E) MUNGU KUTIMIZA AGANO LAKE KUU
- Baada ya Mambo yote, na michakato yote kutimizwa
ndio sasa Mungu anasema nitalitimiza Agano langu Kuu. Mungu atafanya makazi na
wanadamu,atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake. Itakuwaje ?
1.Kufanywa Upya—Kila kitu kitafanywa upya, huwezi amini
·
Mbingu mpya = UFUNUO 21:1
·
Nchi mpya = UFUNUO 21:1
·
Mji mpya = UFUNUO 21:2
·
Utu mpya = KOLOSAI 3:10
► Soma hapa
uone Mungu anavyosema; UFUNUO 21:7
2. Hatimaye Agano Kuu kutimia
- Yote yakisha fanywa upya, sasa ndio
Mungu atalitimiza Agano lake
Kuu rasmi. Unakumbuka
sentesi tatu(3) za Agano letu na Mungu ?
·
Maskani ya Mungu ni pamoja na Wanadamu = UFUNUO 21:3
·
Atakuwa Mungu wa Wanadamu na = YEREMIA
32:27
·
Wanadamu watakuwa watu wa Mungu = HOSEA 2:23
3. HITIMISHO
- Muda huu tunaoishi hapa Duniani ni sawa na Wana wa
Israeli walipokuwa Jangwani, usitegemee Mungu kukufanikisha yote unayoyataka
ukiwa hapa Duniani, sio kwamba hawezi au hujamuomba, la hasha, anataka utamani
kwenda kwenu. Ukitakakuelewa soma hadithi ya Israeli jangwani. =EBR 13:14
- Agano Kuu lipo moja, hakuna Agano la Kale wala
Agano Jipya, hivyo leo piga magoti umwambie Mungu kuwa unataka kuingia Agano
naye;
Awe Mungu
wako, Uwe mtu wake, na siku ya mwisho, Patakatifu pake pawe katikati yako na
watakatifu wote.
………..Remember……………THE BEST HAS COMES…………………..
Complicated Jesus did not teach complicated sermons
ReplyDeleteJesus did not teach complicated sermon every person understood him becaused He wanted everyone to understand not like this complicated.
ReplyDelete