Thursday, November 14, 2013

  MAKANISA 7 YALIYOONYWA NA MUNGU NCHINI ISRAEL YABAKI MAGOFU

Mchungaji Florian Katunzi wa E.A.G.T City centre mmoja wa wasafiri waliorejea kutoka Israel.

Ziara ya Israeli iliyofanywa na watanzania na kurejea mwishoni mwa wiki, imekuwa ni ya kufana lakini ikiwaacha wakiwa na simanzi kubwa baada ya kushuhudia makanisa yale 7 yaliyotajwa kwenye kitabu cha ufunuo kuwa kwa sasa ni magofu kabisa.

Wakielezea licha ya safari hiyo kuwa ilikuwa nzuri na pamoja na kutembelea sehemu mbalimbali za makumbusho, lakini kilichowatia simanzi kubwa ni pale walipofika kwenye makanisa ya Efeso Laudikia, Smilna nk, na kuyakuta makanisa hayo ni magofu kabisa na hakuna mtu anayefanya ibada katika makanisa hayo ambayo Mungu aliyaonya sana.

Lakini pia walipata faraja pale walipofika kwenye kanisa ambapo panasadikiwa kuwa ndipo alipofichwa Yesu wakati Herode akitaka kuwaua watoto wote wa kiume.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa mwalimu Julias Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam, licha ya kukutana na changamato hiyo katika Imani, wamewataka watanzania na wakristo kote duniani kuacha kupuuzia mafundisho na maonyo ya Mungu ili kuepuka ghadhabu ya Mungu ambayo inaweza ikatokea muda wowote, endapo watu watakaidi kuwasikiliza watumishi wa Mungu.

Mch Frolia Josephat Katunzi, amesisitiza wakristo kuacha kudanganywa kwa vitu viharibikavyo kuwa vinaweza kuwapa uzima na matumaini katika maisha yao ya kiroho, amekemea vikali watumshi wa Mungu wanaotumia vitu mbadala ili viwe msaada kwa waumini. Amesema kuwa Neno la Mungu ndilo pekee linaweza kubadirisha maisha ya watu na kuwaponya magonjwa yao.nakuwataka watumishi hao kuhubiri Neno la Mungu lililo kweli na Hai.

 Mchungaji Katunzi akifanyiwa mahojiano na Filemoni Rupia wa WAPO Radio FM mara baada ya kuwasili kutokea nchini Israel.

 

Lakini pia katika ziara hii iliwahusisha watu wengi kutoka nje ya Tanzania, na pia kutoka mikoa mbalimbali ya hapa nchini kama vile Mza, Arusha, Mbeya Dodoma Pwani na Dar Es salaam.
Safari nyingine kama hii inaendelea kuratibiwa na itafanyika mwakani mwezi wa Machi, Mkurugenzi wa kampuni ya Gombo Tours Willy Moses Kulola amewataka watanzania wengine wengi kujitokeza na kujiandikisha mapema tayari kwa safari hiyo ya ki historia.

Mkurugenzi huyo ametoa fursa kwa watanzani ambao wanaweza kukusanya kidogo kidogo hadi kuweza kufikia kiwango kinachotakiwa katika ziara hiyo wafike ofisini kwao.
Source;-- gospel kitaa

2 comments: