By Apostle eliya simon-
KUTUMIA UHURU KUWA HURU.
YALIYOMO
- Utangulizi
- Uhuru
wa Hiyari
- Madhara
ya Uhuru
- Hitimisho
ANDIKO KUU: Kumbu Torati 30:15-20
….nimekuwekea mbele
yako leo uzima na mauti, Baraka na laana….
LENGO LA SOMO:
i.Ni kuonyesha uhuru wa kuwa huru
(ii). Kufichua
kichaka cha Haki za Binadam
1.UTANGULIZI
•►Haki za binadamu,ni msemo ambao upo mdomoni mwa watu na
taasisi nyingi, umoja wa mataifa wanakazia haki za binadamu,serikali na taasisi
zake, mashirika na mtu binafsi-binafsi wamekuwa macho kwenye haki za binadamu
►Kuna nini hasa nyuma ya haki za binadamu? Kuna ajenda gani
ya siri inayoendelea?
Katika fundisho hili la haki za binadamu,utajifunza maneno
yanayoambatana na haki za binadamu,kama UHURU,
HIYARI NA MAAMUZI, pia utajifunza kutumia uhuru wako kutokuwa huru.
2.UHURU WA HIYARI
-►Linapotumika neno HAKI ZA BINADAMU, UHURU, HIYARI, maneno
haya ni kama kivuri au kichaka kinachoficha
uhalisia wa nia ya moyoni. Nia ya moyo wa mwanadamu toka enzi na enzi ni kutaka
kutumia uhuru kuwa huru, mbali na Mungu na sheria na amri zake,hitaji hili la
moyo linajificha ndani ya HAKI ZA BINADAMU na UHURU WA HIYARI.
-►Uhuru wa hiyari ndio jambo la pekee ambalo mwanadamu
amepewa na Mungu uhuru asilimia 100, Mungu hana haki ya kuvunja uhuru wa hiyari
wa mwanadamu hata nukta moja. Kwa uhuru wa hiyari alionao Mwanadamu, maamuzi
yapo mikononi mwake. Kuwa na uhuru sio dhambi,lakini kutumia uhuru ili kuwa
huru ndio dhambi.
A) UHURU WA HIYARI YA
MAAMUZI TUMEPATA WAPI?
►Tunafahamu kuwa mwanadamu wa kwanza ni Adam na Eva, kabla
ya kuasi kwao uhuru wa hiyari zao zote walimkabidhi Mungu, hivyo walitumia
uhuru wao kutokuwa huru,lakini siku walipoamua kutumia uhuru wao kuwa huru
ndipo walipoharibu.
- Mwanzo 3:1-7, Shetani kabla hajawa shetani, alikuwa
malaika, lakini baadae akatumia uhuru wake kuwa huru, awe mbali na Mungu. Eva
nae akachagua kuwa HURU mbali na Mungu na Adamu nae akawa ndani ya mstari. Toka
mwanadamu wa kwanza alipochagua kutumia uhuru wake kuwa HURU mbali na Mungu,
ndio wote tukapata uhuru wa hiyari.
B) KWANINI UHURU?
►Kuna sababu zinazomfanya mwanadamu atake kuwa huru, na hizi
sababu zimejificha nyuma ya neno HAKI ZA BINADAM na neno UHURU,toka Adamu
alipoasi kwasababu ya kutaka kuwa huru na ndio mpaka leo dhambi kubwa ya
wanadamu ni kutaka uhuru wao kuwa huru, mbali na Mungu na sheria zake na amri
zake.
► Mambo matano(5) yanayomdanganya mwanadamu kutaka kutumia
uhuru wake kuwa huru bila Mungu: Maarifa,
Pesa, Dini, Tamaduni, Serikali. Haya mambo 5 ambayo ninayaita M’BADALA
WA UFALME siyo mabaya wala sio dhambi isipokuwa namna
yanavyotafutwa kwa kudhaniwa kuwa kuna uhuru ndio tatizo.
MAARIFA
►Mwanadamu anadhani kuwa siku atakapopata maarifa ya kutosha
atakuwa huru,tena atajitoshereza mahitaji yake mbali na Mungu. Hii dhambi ndio
ya Adamu na Eva hasa, ule mti ulikuwa unafaa kwa maarifa, neno maarifa limetokana
na neno la kilatini (sciencia) likimaanisha sayansi(elimu).
► Nenda chuo chochote muulize mwanachuo mmoja kwanini
anatafuta sana
maarifa,atakupa majibu mazuri ambayo hayataonyesha waziwazi kuwa anataka kuwa
huru mbali na Mungu,ndio maana nikasema hii dhambi niya moyoni zaidi. Kwanini
elimu imepewa kipaumbele sana
kuliko ufalme wa Mungu? Tatizo nini? …. Uhuru.
PESA, DINI, TAMADUNI NA SERIKALI
► Kwakifupi,mambo yote ambayo mwanadamu anadhani kuwa niya
muhimu sana
kuliko Mungu, ni kumkataa Mungu na kutaka kuwa huru kwa jina halali la
pesa,dini,tamaduni na serikali. Kitendo cha kutafuta sana haya mambo 5 n’nje ya Mungu ni sawa na
kumwambia Mungu unataka ujiendeshe mwenyewe asikuchoshe na amri zake.
3.MADHARA YA UHURU
► Toka Adamu, moyo wa mwanadamu unamchukia Mungu, hivyo huwa
unatafuta njia m’badala wa kumtoa Mungu katika maisha ya mwanadamu,kama nilivyosema hapo juu,m’badala ambao mwanadamu
amejitafutia ni yale mambo 5 hapo juu. Haki za binadamu zinajaribu kumwambia mtu
atumie uhuru wake kuwa huru na Biblia (Mungu)
-JUHUDI ZA KUTUMIA UHURU KUWA HURU
A) ADAMU-Mwanzo
3:23-24
► Shetani alitumia uhuru wake kuwa huru mbali na
Mungu,akafukuzwa mbinguni, Adamu na Eva walitumia uhuru wao kuwa huru mbali na
Mungu,wakafukuzwa Edeni.
Haya ndio matokeo ya kutumia uhuru wa hiyari kuwa huru, kila
maamuzi anayoyafanya mwanadamu, Mungu atahakikisha mwanadamu anapata matokeo ya
maamuzi yake.
B) WANA WA ISRAELI NA
MUSA –Hesabu 14:26-28
► Moyoni mwa wana Israeli hawakumtaka Mungu wa mababa
zao,ambae Musa alimtambulisha kwao, sasa ili wawe huru na miungu yao ya Misri, wakataka
kurudi Misri kwa kisingizio cha njaa, vita , kifo na magonjwa. Baada ya Musa
kuwa mlimani kwa siku 40 ndipo wakaonyesha kilichokuwa moyoni,waliabudu sanamu.
►Utagundua dhambi ya uhuru siku zote huwa inajaribu
kujificha kwenye jambo ambalo litaonekana kuwa halali, uhalali ukishapatika
ndipo utakapogundua kilichokuwa nyuma ya uhuru. Mpaka sasa ni nani asiyejua
umuhimu wa elimu na pesa? Hizi ni sababu halali
C) ISRAELI NA
SAMWELI —1 Samweli 8:4-7
► Ile dhambi ya kutaka kuwa huru haikuishia jangwani kwa
Musa, ikaendelea mpaka wakati wa Samweli. Kutaka mfalme ilikuwa ni kisingizio
tu,lakini dhumuni hasa ilikuwa ni kuwa huru mbali na Mungu waliyedhani
anamashariti na masheria mengi. Mungu akawapa walichokitaka na matokeo ya
maamuzi yao
akawabebesha.
► Baadhi ya madhara ya maamuzi yao
mpaka leo tunayaona hata hapa Tanzania,
kodi,ushuru, ajira kuwa serikalini, maisha kuwa juu ili viongozi walipwe. Yote
haya ni matokeo ya Mwanadamu kutaka kuwa huru mbali na Mungu kwa kisingizio cha
kutaka Raisi na serikali isiyofungamana na dini yoyote. Serikali haina dini?
Kwanini?
D) WANA WA ISRAELI NA
YESU – Yohana 8:21-23
►Toka kwa Adam, wakati wa Musa,na wakati wa Samweli mpaka
nyakati za Yesu kale kamchezo ka mwanadamu kutaka kuwa huru bado kalikuwa
kanamkeleketa moyoni. Wakamkataa Yesu kwa njia halali ya Uhuru na Haki ya
mwanadamu ya kuchagua.
E) NYAKATI ZETU
►Nyakati hizi niza wasomi wengi, lakini ile dhambi ya kutaka
kutumia uhuru kuwa huru bado ipo moyoni, ingawa dhambi ni ileile lakini miaka
hii imetengenezewa mazingira na majina mazuri (Haki za Binadamu), na nyimbo
zimetungwa – Freedom Song, na filamu zimetengenezwa – Independent Day, na vyuo
vimejengwa – Liberty University, na Luninga hazipo mbali – Independence
Television(ITV), Na nyimbo za Taifa(Anthem)--♫...dumisha uhuru na umoja…♫,pia …♫.utumwa
wa nchi nyerere ameukomesha…♫
4.HITIMISHO
►Wana siasa na watu mbalimbali wanapopigania haki za
binadamu, usidhani ya kwamba wanauzalendo sana,
hapana,wana ajenda yao
ya siri,ipi hiyo? Wanataka utumie uhuru wako uwe huru katika maamuzi yako bila
kuingiliwa na misingi ya Mungu na Biblia
► Ungeniambia nikushauri, ningekushauri mambo mawili ;
i) Usitumie uhuru wako kuwa huru, na
(ii) Tumia uhuru wako
kutokuwa huru.
.......HOSE………THE BEST HAS COME………….
No comments:
Post a Comment