Tuesday, October 22, 2013

YESU NI MBUZI??




YESU NI MBUZI??

YALIYOMO
1. Utangulizi    2.  Gundua Siri    3. Ongeza Mtazamo     4. Hitimisho

DHUMUNI
-Kuvumbua Nusu nyingine ya Wokovu
-Kuongeza ufahamu juu ya Wokovu.

ANDIKO KUU; Yohana 19:34 ‘ lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki, na  mara ikatoka Damu na Maji ’

1. UTANGULIZI
- Watu wengi wanaamini kwamba DHAMBI ZAO ZILIHUKUMIWA msalabani, kwahiyo kitovu cha wakovu ni MSALABA, nakubaliana nahii Imani, lakini kuamini huku ni nusu ya picha nzima ya wokovu (Msamaha wa Dhambi)

-Kwenye hili fundisho nitaelezea Nusu ya fundisho ambalo wapendwa wengi wamelipuuzia ili kukamilisha picha kamili ya wokovu. Twende pamoja sasa;

2. GUNDUA SIRI
- Ni vyema sana ukijua mambo yote kuhusu MASAMAHA ya DHAMBI zako, lakini wapendwa wengi wanajua NUSU ya masamaha ya Dhambi zao, sasa gundua siri.

- Biblia inasema Yesu ALICHUKUA dhambi zetu, kivipi ? Isaya 53:4a,6b,11d, kwasababu Mungu alizihukumu dhambi zetu msalabani kwa njia ya Yesu, lakini Yesu alikabidhiwa wapi, na nani hizo dhambi zetu ambapo zikampelekea kusulubiwa ?

a) Kuhani na Mbuzi Wawili
- Soma kwa umakini sana MAMBO YA WALAWI 16:5,7-10,15-16,20-22, ukiweza soma sura nzima zaidi ya mara moja.
- Utaratibu huu wa Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya, sasa wana wa Israeli walitakiwa watoe Mbuzi wawili, mbuzi mmoja ni kwa ajili ya Mungu (Sadaka ya Dhambi) na mbuzi wa pili niwa Azazeli (Mbuzi wa Upatanisho).

Mbuzi wa Mungu
-Ni mbuzi kwa ajili ya sadaka ya Dhambi, huyu mbuzi alikuwa anachinjwa na damu yake ilitumiwa kunyunyiziwa kwenye kiti cha Rehema. Kiswahili kingine tungesema ndiye mbuzi aliyekuwa anabeba hukumu ya dhambi za wana wa Israeli

Mbuzi wa Azazeli
-Ni mbuzi wa UPATANISHO, huyu alikuwa akichukua dhambi za Israeli na kizipeleka jangwani bila kuchinjwa. Kuhani alitakiwa kumuwekea mikono huyu mbuzi na KUUNGAMA dhambi zote za Israeli huku mikono yake ikiwa juu ya kichwa cha Mbuzi wa Azazeli

Mbuzi hawa wawili kwa pamoja walikuwa na kazi moja-Ondoleo la Dhambi, au tungesema zoezi la kufutwa kwa Dhambi zote lilikuwa likifanywa na mbuzi wawili.

b) Agano Jipya
- Najua wengi wanaamini kwamba Yesu ndiye badala ya Mbuzi wale wawili, lakini kuna kitu cha kujifunza hapa. Aliye fungua Agano jipya ni Yohana M’batizaji,sijajua wangapi wanafahamu umuhimu wake katika zoezi la Mwanadamu kusamehewa dhambi zake (Dhambi za Ulimwengu). Nimegundua wapendwa wengi wameshindwa kumuelewa Yohana.

YOHANA- Alitabiriwa na Nabii Malaki, kuwa atakuja kwa Roho ya Eliya- Malaki 4:5-6, dhumuni lake ni upatanisho kati ya Baba na Watoto wake.
-Ujio wa Yohana haukuwa wa kawaida – Luka 1:5, 3- 17, 80, Yohana 1:6-8, 23,
-Huduma ya Yohana ilikuwa ni TOBA la Ondoleo la Dhambi (Ubatizo) Luka 3:2-6
- Watu wote waliofuata ubatizo wa Yohana iliwapasa WAUNGAME dhambi zao – Marko 1:4-6
-Ndiye anayetenganisha hasa kati ya Agano Jipya na lakale – Mathayo 11:11-14.

YESU – Yesu na Yohana walifuatana katika ujio wao hapa Duniani na katika utendaji kazi – Mathayo 11:18-19, Luka 1:36
- Yohana anaanza huduma yake kwa kubatiza, na Yesu anaanza huduma yake kwa kubatizwa, wote wawili walikuwa na ujumbe mmoja, TUBUNI, Mathayo 3:1-2, 4:17
-Yesu anaonyesha ushirikiano wa wajibu, Mathayo 3:15

 Mbuzi wa Azazeli na Yohana
- Nataka hapa uangalie mfanano na mtofautiano, Mbuzi hakuchinjwa, alikaa jangwani,kuhani alimpa maungamo. Ni sawa na Yohana, alikaa jangwani, hakuangikwa na pia watu wote walimuungamia – Mathayo 3:5-6

 Mbuzi wa sadaka ya Dhambi na Yesu
- Mbuzi alichinjwa,damu yake alinyunyiziwa, pia Yesu aliteswa na kuuawa, alimwaga Damu yake –Waebrania 9:12

c) Zoezi la KUHAMISHA Dhambi
- Dhambi ilikuwa ikihama kwa kuweka mikono juu ya kichwa, Kuhani aliweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha Mbuzi wa Azazeli (Walawi 16: 21-22), sasa wakati wa yohana watu wote walikuwa wakiungama dhambi zao na kuingia ndani ya maji (Ubatizo), kwahiyo dhambi zilikuwa zikiingia ndani ya maji. Yesu hakuwa na Dhambi, ndio ikam’bidi Yohana aweke mikono yake juu ya Yesu ili apitishe Dhambi zote za Ulimwengu kwa Yesu, na pia Yesu alivyozamishwa ndani ya maji ndo alichukua uchafu wote wa wanadamu ambao walitubu kwa Yohana

-Ubatizo wa Yesu ni tofauti kidogo na ubatizo wa wengine, sababu wengine walienda kuungama na kuoshwa dhambi zao, lakini Yesu alikwenda kukabidhiwa rasmi madhambi ya Ulimwengu na dhambi walizotubu kupindi hicho. Ndio maana wakati wa ubatizo Yohana anazungumza haya maneno---YOHANA 1:29-34

-Naomba niseme kwamba Yohana ndiye aliyekuwa muwakilishi wa wanadamu katika kumkabidhi Yesu dhambi za Ulimwengu na zawakati huo na huu, tendo zima la makabidhiano ya dhambi linawakilishwa na neno moja ---MAJI.Kwahiyo Biblia inapozungumza maji inataka kila mwanadamu ajue kwamba dhambi zake alimkabithi Yesu kwa njia ya Maji (Ubatizo), Yohana 19:34
Kuzaliwa Kwa Maji na Roho Mtakatifu
Yohana 3:5, Tito 3:5, Ebrania 10:22, 1 Yohana 5:6,9, Mdo 10:44-48, Hapa ndipo penye siri yote, wengi wanasema tumeshabatizwa kwahiyo hakuna jipya, soma MDO 8:12-17 utawaona wenzako walivyopungukiwa na kitu cha muhimu-----ROHO MT………..….
………………………………..ITAENDELEA……………………………….

No comments:

Post a Comment