Wednesday, March 5, 2014

IDUMU INJILI MTAANI, DODOMA KITAELEWEKA TU


Sanamu ya kumuenzo baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwenye eneo la Nyerere Square ikionekana kwa mbali, ambapo Oscar Mwanyanje akipita mbele yake kwa nje na megaphone yake akihubiri injili mitaani.
Mara zote inaia moyo kuona kwamba bado kuna hudma ya Injili mtaani, na kwamba wako wenye kuitwa kwa namna hiyo wapate kupanda mbegu na kisha kusubiria mavuno. Hali ndivyo ilivyo kwa Bwana Oscar Mwanyanje, mhitimu wa shahada ya uhasibu kutoka chuo cha biashara (CBE) Dodoma.

GK ilipomtia machoni, ilipata shauku ya kujua kunani, ili basi nawe upate kujuzwa mwanzo wa jambo hili ukoje. Kwa maelezo ya Bwana Mwanyanje, anasema kuwa ameitiwa kwa hili jambo, na punde tu alipohitimu masomo mwaka jana, basi sauti ya kuhubiri Injili mtaani ilimjia.

Hakuna kulala hadi kieleweke, wiki ya pili ya injili inasonga.
Licha ya kwamba alijua kwamba ndani yake jambo hili limekuwepo kwa muda mrefu, aliufanya moyo kuwa mgumu kutii, jambo ambalo anasema lilimletea matatizo makubwa hata kiasi cha kukaribia kufa.
Muuzaji wa Biblia pamoja na wapita njia wengine wakimshangaa Oscar Mwanyanje wakati akihubiri maeneo ya uhindini, Dodoma.

Kwa elimu yake, na kwa baadhi ya kazi ambazo aliwahi kuomba, anaeleza kwamba zingine zilikuwa rahisi, na hata 'interview' kuwa rahisi, lakini kuna siku alipotoka kwenye 'interview', sauti ikamjia ikimwambia kuwa hatopata kazi hadi afanye kwanza kile ambacho Mungu amemuagiza.

Halikadhalika, Bwana Mwanyanje ametoa rai kwa wajumbe wa bunge maalumu la katiba kumtafuta Mungu kwanza, kwani kutokana na ukinzani wa mawazo kutoka makundi mbalimbali ya wajumbe hao bungeni, hawatoweza kufikia muafaka kwa maslahi ya taifa, basi ni vema wakatambua kwamba Bunge linamhitaji Mungu.

CHANZO: GOSPEL KITAA BLOG

No comments:

Post a Comment