Friday, March 21, 2014

MWIGIZAJI WA HOLLYWOOD AMPATIA RIHANNA UJUMBE KUTOKA KWA ROHO MTAKATIFU

Rihanna akijipiga picha ya mchoro(tattoo) wa msalaba aliyojichora hivi karibuni.
Mwigizaji nyota wa nchini Marekani Stephen Baldwin amemtumia ujumbe maalumu kutoka kwa Roho mtakatifu mwimbaji maarufu wa muziki wa nje ya kanisa Rihanna kutokana na wimbo wake uitwao "What Now" ambao unapatikana katika album yake iitwayo 'Unapologetic' aliyoitoa mwaka juzi.

Kupitia anuani yake ya twitter jumanne hii mwigizaji huyo aliandika kwamba huwa hana kawaida ya kufanya kile ambacho anakifanya(kuandika ujumbe) huo, lakini ameiona video ya wimbo wa 'what now' ya mwimbaji Rihanna ambayo mwishoni kuna mwanga umepita ukionyesha msalaba, huku
Stephen Baldwin.
mwimbaji huyo akimalizia kwakusema …hajui aende wapi" na kwamba Roho mtakatifu anajibu kwamba "ni kweli unajua, umenifahamu mimi kitambo sasa toka ulipokuwa mtoto, unakumbuka jina la Yesu, ni nuru ya uso wako, ni furaha ya moyo wako, rudi kwa Yesu" ndivyo alivyoandika mwigizaji huyo huku chanzo cha habari hii kikisema hapana shaka ujumbe huu ulikuwa mahususi kwa mwanadada huyo ambaye jina lake la kuzaliwa ni Robyn Rihanna Fenty.

Baldwin ameongeza kwamba "pia kama ukipata nafasi ikiwa ni dakika ya 3:29 katika video iliyopo YouTube, najisikia Roho mtakatifu ananiambia kitabu cha Yohana 3:29……

Mwigizaji huyo ambaye alimkabidhi Yesu maisha yake baada ya tukio la kigaidi la septemba 11 mwaka 2001 huko nchini Marekani, alitoa ujumbe huu kwa wafuasi wake 35,000 katika anuani yake ya twitter akiwataka kuusoma ujumbe huo huku pia ikiwa haijulikani kama moja ya lengo la mwigizaji huyo ni kukutana na Rihanna kisiri ili kumuhubiria injili ya Yesu. Rihanna ambaye amekulia katika mazingira ya Kikristo katika visiwa vya Barbados inasemekana hataki kuweka bayana imani yake mbele za watu kwakuogopa kupoteza mashabiki ambao wamejigawa katika makundi mbalimbali yakiwepo ya wasiomwamini Mungu, wanaomwamini na wale wa imani nyingine.

Ujumbe wa Stephen kutoka katika anuani yake ya twitter.

1 comment:

  1. hiyo ni neema ya Bwana ambayo Rihana ameipata kwa kupitia huyo mwigizaji, sasa kinachotakiwa tuu hapo ni Rihanna kumkiri Yesu Kristo maishani mwake na achane na ya ulimwengu,

    Maana Bwana mwenywe alisema katika 1 John 2:15 Je, si upendo wa dunia au mambo katika dunia. Mtu anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwamo ndani yake.

    Na pia huyo mwigizaji pia anatakiwa aachane na hiyo kazi maana pia kwenye huo mstari wa Biblia nao pia unamuhusu, Bwana anataka wote tumtukie yeye na tuachane na ya ulimwengu.

    ReplyDelete