Saturday, October 12, 2013

UKUBWA WA IMANI



Ni mimi ndugu yako Pete Michael Mabula
BWANA YESU asifiwe
Nakukaribisha mpendwa katika somo hili muhimu kwa waenda mbinguni
Soma linahusu IMANI
-kipimo cha imani ni kidogo sana lakini hukaa ndani ya mwana ma MUNGU
{Mathayo 17: 20 ''YESU akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. } pia  {mathayo 21:22 Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. } {Luka 17:5-6 ''Mitume wakamwambia BWANA, Tuongezee imani. BWANA akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. }
-Imani tuliyonayo inaweza ikafanya kazi kubwa sana ikiwa hatutakuwa na shaka aina yoyote { Mathayo 14:28-31 ''Petro akamjibu, akasema, BWANA, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea YESU. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, BWANA, niokoe. Mara YESU akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? ]
-Imani ya KIMUNGU hutaka kutoka katika hali ndogo hadi kuwa kubwa {Warumi 1:17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani. }  Pia {Marko 11:23Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. } pia {Mathayo 13:31-32 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake}

-Imani ili ikue ni lazima uwe na utii na uvumilivu

1-Utii {1 Samweli 15:22-23''Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme. }  Pia {Wafilipi 2:8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. }

2 uvumilivu {Wagalatia 5:22''Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, UVUMILIVU, utu wema, fadhili, uaminifu, }

-Uvumilivu ni namba moja,
 -kitu kidogo tu ambachokinasababisha kuondoa furaha, amani, wema fadhili, uaminifu kitu pekee ambacho ni muhimu baada ya hayo kutokea ni uvumilivu

                        MAADUI WA IMANI
A:  Hofu na kutokuamini {Warumi 8:14-15''Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU. Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. }
Pia {Luka 8:49-50Alipokuwa akinena hayo, alikuja mtu kutoka nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa; usimsumbue mwalimu. Lakini YESU aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa. }
-Hofu huvunja sana moyo hata kama kuna jambo unaliweza unashindwa

B: Kukataa tama /woga {Hesabu 13:30-33''Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi. } Pia {2Timotheo 1:7Maana MUNGU hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. }  Na pia tumalizie na {Ufunuo 21:7-8 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote,}MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka wakati wa kufanya hivyo ni sasa maana Biblia inasema wokovu ni sasa. Ndugu nakushauri umpe BWANA YESU maisha yako na MUNGU atakubariki sana pia utakuwa na uhakika wa uzima wa milele kama ukiishi katika YESU siku zote huku ukifuata neno lake.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula
       Huduma ya maisha ya ushindi.

No comments:

Post a Comment