Wednesday, March 5, 2014

Dini Mpya inayopinga swala la Elimu yaibuka Kakonko mkoani Kigoma.










Robert E. Maziku

Dini mpya ijulikanayo kama Sabato Matengenezo iliyo anzishwa kutokana na kumeguka kwa makanisa mawili la Anglikana na Sabato kisha kuungana. 


Mwanafunzi Annastazia ambae alifanikiwa kukwepa mtego huo na kurudi shule

Dini hio imekuwa ikiwakataza wanafunzi kuendelea kusoma na kuwasafirisha mikoani kwa kufanya kazi mbalimbali kwa mujibu wa dini hio ya Sabato Matengenezo inawazuia wanafunzi kusoma kwani shule zinawafundisha mambo yasiyofaa kinyume kabisa na msimamo wa dini hio. Pia imekuwa ikiwakataza waumini wake kutibiwa baadhi ya magonjwa.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma

Mkuu wa mkoa wa Kigoma (Issa Machibya) na Afisa Elimu (Salvatory Shauri)  wamekemea kikundi hicho cha dini kuendelea kuwazuia wanafunzi kuendelea na masomo mashuleni hasa sekondari kitendo kilichofanya wanafunzi wengi kutojiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wa 2014.


No comments:

Post a Comment