Saturday, April 19, 2014

Je unamfahamu mwenyekiti wa waislamu waliookoka, Afrika Mashariki na Kati!


Mtume Peter Rashid Abubakar

Alitokea kwenye familia ya kichawi, mama yake alijiita ni mungu na kufanya miujiza mbalimbali ikiwemo ya kunyesha mvua. Sheikh Alhaji Rashid Tatashajara Abubakar, aliwahi kufanya shughuli za kisheikh katika msikiti wa Ilala mtaa wa Mwanza ambapo pia alikua mwanafunzi wa sheikh Yahaya Hussein ambaye ni marehemu kwa sasa.

Alianza kujifunza madrasa, akapanda vyeo na kusomea vyuo vya kichawi baada ya kuhitimu majaribio mbalimbali ikiwemo kufukua makaburi, kunywa damu za watu, kuhamisha nyota za watu, na kumeza majini 360 na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mkuu wa wachawi Afrika mashariki na kati!

Anasema katika mambo hayo yote, alikua akitumwa kushambulia watumishi wa Mungu mbalimbali, aliwahi kujaribu kwa Moses Kulola, Emmanuel Lazaro na Askofu Mwanisongole. Lakini alishindwa na kupata mieleka iliyompelekea kuumwa sana.

Akielezea ushuhuda wake kwa ufupi, Jinsi alivyompokea Bwana Yesu, ilikuwa sababu ya mke wake wa pili kupita kwenye mkutano wa Injili na kuponywa tumbo lililomsumbua kwa muda mrefu bila mafanikio ya kupona “mke wangu alikuwa akirudi nyumbani na kuimba nyimbo za makafiri, baadaye anaenda kanisani, sasa adhabu ya mtu anayekiuka sheria ni viboko 40, nilipotaka kumchapa mkono ukaganda, ndio mke wangu akasema piga magoti chini, akaniombea na mkono ukarudi mahala pake, baada ya hapo mengi yalitokea kukatisha story Mungu alianza kunifundisha na kunitumia”

“Siku Moja mtaa wa Salender Bridge kama mliwahi kusikia kisa cha dada aliyeota manyoya, alifikishwa kwangu nikamuombea kwa Jina la Yesu naye akapokea uponyaji. Kwa sasa yuko Marekani! nimemuona Mungu kwa jinsi ya tofauti kule nilikotoka nilikua namtumikia shetani, kwa sasa namtumikia Bwana Yesu, na kila ulimi utakiri kwamba Yesu ndiye Mungu”

Alhaji Rashid Abubakary kwa sasa ni mwenyekiti wa waislamu waliookoka Afrika mashariki na kati. Mungu amekua akimtumia kwa jinsi ya tofauti na amealikwa makanisa mbalimbali na kueleza shuhuda nyingi ambazo Bwana Yesu amefanya na kufanya kwenye maisha ya watu wengine. 

Mtume Peter Rashid Abubakar
Kanisani kwake.

Huu ni ushuhuda kwa ufupi tu kumhusu Mtumishi wa MUNGU Peter Rashid Abubakar pia kumbuka kuwa
YESU akiwa kazini kuwafungua watu kanisani kwa Mtume Peter Rashid Abubakar

Mtume Peter Rashid Abubakar ndiye mwanzilishi wa huduma ya Glory to God Miracle Center(House of Prayer For All Nations) Tanzania jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment