Thursday, April 17, 2014

KATIBA MPYA

KATIBA MPYA NA INJILI FOREVER


Haleluya wapendwa katika bwana wetu Yesu kristo,

         Nianze kwa kukutoa fikra za uwepo wa udini katika mada hii kwasababu sitazungumzia dini ya Kikristo au yoyote bali nitazungumzia wokovu ambao sio dini. Kuokoka sio dini na kama kuna mtu ameokoka na anamawazo ya kuwa hio ni dini basi hajaelewa. Ukiulizwa katika taasisi yoyote kuwa dini yako ni ipi jibu Mkristo sio Mlokole utakuwa umekosa swali.

       Haya acha tuendelee na mada tajwa hapo juu, Napenda kuzungumzia uhusiano wa katiba na Injili ila sitataja maandiko wala vifungu vya maandiko ila nitaandika kirahisi sana ili kila mtu aelewe. Binafsi naona watu walio okoka (sio kila Mkristo) wakiitumia vyema nafasi yao kunauwezekano mkubwa wa kupata katiba nzuri na yenye manufaa kwa taifa miaka mingi ijayo kwa sababu zifuatazo.

       Chochote unachokiona katika hali ya macho ya nyama kilianza kutokea katika hali ya Roho, namaanisha kabla ya Yesu kuyaona mateso atakayo yapata msalabani aliyaona kwenye maombi getsemane. Ngoja niweke msisitizo hapo, kabla hauja anguka kiroho katika hali ya watu kukuona ulisha anguka rohoni. Kwa maana hio kabla haijatokea machafuko katika nchi sababu ya uwepo wa vifungu vibaya vya kikatiba basi vurugu hizo lazima mtu alieokoka na mwanamaombi aliona katika hali ya Roho.

      Nini maana yake, Nchi yoyote ile hatma yake imewekwa chini ya wanamaombi, nafikili ningekuwa mimi Rais ningekuwa na kikosi cha wanamaombi ambao wataona yajayo kabla hayajatokea. Hebu pata picha wanamaombi wanaingia katika maombi wanapata habari ya hatari ya uwepo wa vifungu vitakavyo iangamiza nchi nadhani licha ya kumshukuru Mungu pia wataenda kutoa maoni yao ili katiba iweje ili isije kupatwa na yale walio yaona.

     Cha ajabu wanamaombi wamekuwa wakijisahau kama tunaishi katika hali ya Roho na Mwili kwa wakati mmoja kitu ambacho huwafanya waishie kufanya maombi bila kutoa maoni katiba mpya iweje, au kutokupiga kura kwa kusingizia siku ya kura ni jumapili.

LENGO LANGU

    Najua muda wa kutoa maoni umeisha naomba watu walio okoka wafatilie Bunge maalum la Katiba ili kujua ni mambo gani muhimu yapo na yapi hapo kwahio ukatae au ukubali utakapofika mchakato wa kupiga kura katika kuikubali ama kuikataa katiba kuliko kungoja wanasiasa wakushawishi ambapo kunauwezekano mkubwa kukubali mawazo ya chama fulani sababu unakipenda.

    Katiba ni makubaliano kati ya watawala na watawaliwa namna ya kuishi na inapotokea umeenda kinyume na hayo inakuwa ni kosa kubwa. Kwa mfano likatoka wazo la kufutwa mikutano yote ya injili Tanzania najua wanamaombi watajifungia kwenye vyumba nakuanza kukemea huku wamesahau kuwa wao hawakutoa mawazo yao katika ukusanyaji wa maoni. Najua maombi hayaepukiki ila tuwe wazuri katika kuzitumia akili zetu pia ili isije kutimia TUNA ANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.

IMEANDIKWA NA ROBERT MAZIKU 0653340950

No comments:

Post a Comment