SOMO #1. HAPO MWANZO
Andiko Kuu:- Mwanzo Sura ya 1 yote
1.
MAHUSIANO
Neno “Mungu” katika kitabu cha
Mwanzo 1:1 ni ELOHIM, ni neno lenye
uwingi katika umoja. Neno ELOHIM linabeba nafsi tatu katika umoja, hizi nafsi
tatu bila shaka ni – Mungu Baba, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu au Mungu Baba,
Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, kuwapanga huku hakumaanishi mmoja ni
mkubwa kuliko mwingine ila kwa namna walivyo jitokeza kwetu.
·
UUMBAJI- Mungu alitaka awe
na MAHUSIANO NA MWANADAMU, ila asingeweza kuendesha mahusiano bila kuwa na
MASKANI,kwahiyo andiko linaanza na kutuonyesha Mungu anavyoshughulika na
maandalizi ya Maskani. Kuanzia Mwanzo
1:1 mpaka Mwanzo 1:25-Mungu alikua akiandaa maskani ili aanze mahusiano na
mwanadamu.
·
MWANADAMU – Kilele cha
uumbaji wa Mungu ni mwanadamu, baada ya Mungu kua amemaliza kuandaa
maskani na siku ya kukutania (SABATO),
ndipo alipomuumba na Mtu ili aanze Mahusiano nae. Kama tunavyojua mwanadamu ana
asili mbili – Utu wa Ndani-Mwanzo 1:26-31 na Utu wa Nje-Mwanzo 2:7,15. Baada ya
haya yote Mungu alikua akimtembelea Adamu muda wa Jua kupunga ili awe na
mahusiano nae “awe Mungu wake na Mtu awe
Mtu wake”.
2.
DHAMBI
·
Mungu alimuumba Mwanadamu akiwa na Asili ya
Mungu, alikua Mwenye Haki, Mtakatifu amejaa Utukufu na HIYARI.Mungu alimpa
mwanadamu uhuru wa hiyari kwasababu alimuumba kwa mfano wake.Mwanadamu sio
roboti au mwanasesele, haendeshwi na mitambo bali ni lazima achague kwa hiyari
yake. Kwasababu mwanadamu ana uhuru ni lazima achague kutii na kuamini
atakacho.
·
JARIBIO LA UTII – Mungu alipenda kujua kama Adamu atamtii na Kumuamini anachosema
au laa, wakati huo Shetani ambaye ni Baba wa Uongo nae yupo kazini kuhakikisha
Mwanadamu hamtii Mungu na hivyo kuvunja
mahusiano. Mungu alitoa katazo-Mwanzo 2:17, Adamu alitii hii kauli siku
zote mpaka siku Shetani aliyofanikiwa kumuingia Mwanamke- Mwanzo 3:1-9. Hivyo Mwanadamu alifanya Dhambi
kwa kumtii na kumuamini Shetani kuliko Mungu, matokeo yake ni KUFUKUZWA-Mwanzo
3:24, mahusiano YAKAVUNJIKA, mpaka Dhambi na urejesho wa utukufu vishughulikiwe
kwanza, ndio maana Mungu akatoa Ahadi ya kuondoa Dhambi na kumrejeshea
mwanadamu utukufu.
3.
UREJESHO
a. MASIHI:-
Mungu alimpenda sana Mwanadamu, hivyo
akawa na wivu nae lakini gharama ya kumrejesha ili mahusiano yaendelee ni kubwa
mno, ikabidi Mungu awaahidi kwamba angalikuja mtu mwenye thamani atakae wafanyia
UREJESHO,mtu huyo angeliitwa MASIHI- Mwanzo 3:15. Mungu alionyesha namna huyo
masihi atavyowarejesha, kwa kuchinjwa – Mwanzo 3:21.
Kabla ya huyo masihi kuja,
mwanadamu itatakiwa atoe sadaka ya mnyama aliye safi ili Dhambi yake iendelee
kufunikwa kila mwaka, na kila asiyeua mnyama alionyesha kumtii na kumuamini
Shetani kuliko Mungu kwani njia pekee ya kumkaribia Mungu ni kumwaga Damu isiyo
na Hatia.
Mungu alionyesha NJIA YA
UPATANISHO kwa mfano kwa kumvika Adamu Koti la Ngozi, wakati huo Damu ya mnyama
ilifanya upatanisho, huu mfano ulipaswa uigwe na Wanadamu.Tatizo linakuja –
Damu za wanyama hazikufaa KUMFUTIA HATIA MWANADAMU kwani uthamani wa Mwanadamu
ni mkubwa kuliko wa mnyama, hivyo Damu ya mnyama ILIFUNIKA TU DHAMBI, na ndio
maana Mungu akaahidi MASIHI ili arejeshe Mahusiano kwa KUFUTA DHAMBI – Isaya
59:20.
b. ROHO
MTAKATIFU:- Mwanadamu alipoasi alipungukiwa na utukufu, hivyo Mtu
akishasamehewa Dhambi hupewa zawadi ya Roho Mtakatigu (Utukufu).Kama Mungu
alivyoahidi kuwapa wanadamu ZAWADI ya MASIHI ndivyo Mungu alivoahidi kuwapa
wanadamu ROHO WAKE MTAKATIFU – Isaya 44:3,kwahiyo Masihi na Roho Mtakatifu ni
ZAWADI – Luka 24:49 ambazo Mungu aliziahidi ili arejeshe MAHUSIANO yaliyokua
yamevunjika kwasababu ya Dhambi – Isaya 59:2.
Mungu alimpulizia PUMZI
mwanadamu akawa nafsi hai lakini baada ya Dhambi Mungu hakumuona tena Adamu
(alishakufa kiroho), ile pumzi ilikua imetoka, ndio maana Mungu akaahidi-
atatia Roho yake na Mtu ataishi tena – Ezekieli 37:14.
c. MAHUSIANO:-
Mungu alianzisha Mahusiano, baada ya Dhambi mahusiano yakavunjika mpaka Dhambi
ishughurikiwe na baada ya Dhambi kushughurikiwa mwanadamu anapewa utukufu tena
na hatimae MAHUSIANO YALIYOVUNJIKA yanarejeshwa.Mahusiano haya tunaonjeshwa
tukiwa hapa Duniani lakini Mahusiano kamili yatakua Mbinguni – Ufunuo 21:3-7,
iko hivyo kwasababu Mahusiano ya Mungu na Adamu yaliendeshewa kwenye MASKANI YA
EDENI, hapa Duniani hakuna Edeni, ndio maana Yesu akasema anakwenda kuandaa mahali
– Yohana 14:2-3.
Licha ya Mungu kuahidi zawadi ya
MASIHI na ROHO MT, pia aliahidi MAHUSIANO kurejeshwa, sharti likiwa ni
kusamehewa Dhambi kwanza(kwa Yesu) na kupewa nguvu (Kwa ROHO MT), baada ya hapo
Mwanadamu anaanza kuonja Mahusiano ya Mbinguni akiwa hapa Duniani – Mathayo
6:10. Mungu aliahidi kurejesha Mahusiano kwa kufanya Maskani yake kuwa katikati
ya Wanadamu – Walawi 26:12, Ezekieli 27:37 “Mungu
anakua Mungu wao na Watu wanakua watu wake”.
4.
HITIMISHO
·
Kuanzia sura ya 4 ya kitabu cha mwanzo mpaka
malaki, kumejaa ahadi za ujio wa Masihi,ujazo wa Roho
MT na urejesho wa Mahusiano, vitabu vya Injili
vinaonyesha utimilizo wa Ahadi zilivyoahidiwa na Mungu-Yohana 4:25-26, 11:27.
Nyaraka za mitume zinathibitisha utimilizo wa Ahadi – Mdo2:39, 13:23 na Efeso
2:22.Hivyo LEO hii tunaweza kudai kile kilichoahidiwa na kutimizwa na Mungu.
·
Kwanini Mungu anafanya haya yote? – Kwasababu
ANAMPENDA Mwanadamu sana.
·
Hizi Zawadi zilizoahidiwa ndio zinaitwa EPANGELIA
na ndio mpango mkuu wa Mungu.
by 0753 011 774
No comments:
Post a Comment