Tuesday, December 10, 2013
Monday, December 9, 2013
MAONO YA HUDUMA YA EFATHA
![]() |
| mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Josephat Mwingira. |
Huduma ya Efatha ni maono aliyopewa Mtumishi wa Mungu, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira ambayo ndani yake kuna kusudi la Kiungu. Neno Efatha linapatikana katika kitabu cha Marko 7:34, maana yake FUNGUKA.
Ili kufanikisha kusudi hilo, MUNGU alimpa Mtume na Nabii vipengele 10 vya kutekeleza ambavyo kwa pamoja ndivyo vinavyoumba Huduma ya Efatha.
1. Kuikomboa Tanzania ili iweze kusimama mbele za kiti cha hukumu na kupokea baraka za MUNGU.
2. Kuliandaa kanisa la YESU KRISTO kwa ajili ya kunyakuliwa lisilo na mawaa wala makunyazi.
3. Kufanya Kanisa la YESU KRISTO liwe na Mamlaka.
4. Kudhihirisha uweza katika KRISTO YESU, kwa Ishara, Miujiza, Uponyaji na Ukombozi wa Roho, Nafsi na Mwili.
5. Kuwafanya watakatifu wawe na umoja.
6. Kumzalia BWANA matunda yaani kuwaleta watu kwa YESU.
7. Kupokea vipawa vya MUNGU kama mahitaji yetu, ROHO MTAKATIFU, lugha mpya na kuvigawa.
8. Kusimamia kazi ya MUNGU na kuruhusu maongozi ya ROHO MTAKATIFU yaweze kutenda kazi.
9. Kuhakikisha kuwa malango ya kuzimu yananyamazishwa.
10. Kuwa tayari wakati unaofaa na usiofaa kuhubiri NENO la MUNGU.



Thursday, December 5, 2013
UTUME, UNABII NA MIUJIZA UNAVYO LIPASUA KANISA.
Na Robert E. Maziku 0653340950
1wakorintho 12:4~6
Efeso 4:11~13
Bwana Yesu asifiwe,
Nimekuwa nikifurahishwa sana na ninapo sikia Mtumishi fulani anatumiwa na Mungu katika upande fulan ikiwa yote ni kuujenga mwili wa Kristo. Kwa mfano ni nadra kumpata mtumishi aliyekilimiwa huduma zote tano kwa maana ya Mtume, Mchungaji, Nabii, Mwinjilisti na Mwalimu.
Kumekuwa na huduma tatu ambazo mtu akisikiwa anayo wala watu hawashtuki nadhani hii inatokana na fikra kuwa hizo ni kawaida mtu kuwanayo ambazo ni UCHUNGAJI, UINJILISTI na UWALIMU. Utata huwa unaanza pale mtu anapojitambulisha ni NABII au MTUME, hii inatokana na watu au wapendwa kuzipa uadimu ndani ya kanisa.
Kabla sijaendelea hebu niweke kamsingi kadogo hapa, DHEHEBU sio WOKOVU. Dhehebu huweka mipango mbalimbali ili kumfikia Mungu yaani Mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu, wakati tunapozungumza wokovu, ni mpango wa Mungu kumtafuta Mwanadamu.
Kwa msingi huo, kanisa au dhehebu ili angalau litimize lengo la kumtafuta Mungu basi yapaswa kanisa/Dhehebu kuwa na huduma zote tano kwa wakati mmoja kwani hivi vitu vinasaidiana katika utenda kazi.
CHANZO CHA MPASUKO.
Kumekuwa na hofu ya kuibiwa washirika kutokana na uwepo wa watumishi wajiitao manabii ambao wamekuwa na mvuto kwa watu kutokana UPAKO na MIUJIZA. Mtumishi ambae si Nabii ila ni Mwalimu au Mchungaji tu wamejikuta wakianzisha siasa za dini yaani kupanga mipango ya kuwachafua hao wenye upako ili kurejesha washirika.
Nimejaribu kujiuliza hivi, kuna Mtumishi gani hapa Tanzania au nje ya Tanzania mwenye neema ya kutumiwa katika ishara na miujiza hajawahi kuchafuliwa kutokana na Huduma yake?? Jibu ni hakuna hebu angalia hii list halafu ujiulize nani hana kashfa, NABII GB MALISA, ASKOFU ZACHARY KAKOBE, MH. GEODAVY, ASKOFU DUNSTAN MABOYA, MCH. GWAJIMA, NABII TB. JOSHUA, NABII UEBERT ANGEL, MCH BULDOZER MWAMPOSA ASKOFU MWINGIRA na wengine uwajuao wewe wenye neema hiyo wote hawa wana kashfa ya uchawi sasa tatizo ni upako au uchawi?.
Kumekuwa na kamsemo cha kawaida sana siku hizi mtu asikiapo habari za matendo makuu ya Mungu utasikia ZICHUNGUZENI HIZO ROHO!!, sawa hata mimi nakubaliana na hilo neno ila tatzo huwa hawazichunguzi hizo Roho zaidi yakuishia kuhubiri ubaya wa Mtumishi. Kunasiku rafiki yangu mmoja alikuwa anajaribu kunionesha ni namna gani Mama Rwakatale na Mzee wa Upako wanatumia uchawi kwa kutoa pointi ya kitoto kabisa, anasema kwenye TV matangazo yao huwa yana EFFECT(mionzi flani ambayo huonekana mikononi ikimaanisha nguvu). Akadai utatoaje hizo nguvu Mtumishi wa Mungu kama mchawi, nikagundua hizo ndizo siasa za kanisa.
UTUME, UNABII NA MIUJIZA UNAVYO LIPASUA KANISA.
Mtazamo wa Manabii na Mitume kwa sasa hakuna na kama wapo ni wachache ndio unao sababisha haya yote. Shetani amekuwa akifurahia sana hivi vikumbo. Katika hao nilio wataja hapo juu na wale ambao sijawataja ila wapo katika njia hio ni ngumu sana kuwasikia kwenye vyombo vya habari wakiwaponda watumishi wengine zaidi sana hao walio kinyume nao kuwasikia wakiwaponda. Hivi inakuwaje mtu yuko radhi kuamini mchawi anauwezo wa kumrudisha mtu mzukule ila haamini kama Gwajima anaweza akatumiwa na Mungu kuwarudisha mizukule??, Mtu kuombewa akiwa mbali bila kuguswa akapona watu wanashangaa wanasahau kama kuna mitume waliponya kwa VIVULI vyao!! Sasa hivi kanisa limegawanyika, wapo wanao chukulia kama MIUJIZA ni mpango wa shetani kukamata watu na wapo wanao amini MIUJIZA ni mpango wa Mungu kuwa hudumia watu.
PONGEZI
Pongezi za pekee ziende kwa Mchungaji Swai wa T.A.G Mwanza kwakuwa Mtumishi asiye kuwa na udini wa Udhehebu ndani yake. Amekuwa baba wa Kiroho mzuri wa Mchungaji Gwajima pamoja na kuwa tofauti kihuduma kwa sasa ila amekuwa akimtia moyo wakati huo kuna walokole wako kidini zaidi hawawezi kumtia moyo au kumkubali mtumishi asiye katika Dhehebu lake.
Mchungaji Gwajima na Mchungaji Swai wakisaidiana kumchakaza Shetani Tanga
PONGEZI YA PILI
Nawashukuru waimbaji wainjili wamekuwa wakikwepa sana Dhambi ya ubaguzi na kutoa hukumu zisizo na uhakika kiroho. Siajabu kumuona Flora Mbasha akihudumu katika mkutano usio wa EAGT, Sio yeye bali waimbaji wengi wako hivyo najua yawezekana sababu ya ikawa ni masilahi lakini hata kama mimi huwa nasema IWE KWA HAKI AMA KWA HILA INJILI ITAHUBIRIWA(INJILI FOREVER).
Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha wakifatilia mkutano Tanga
John Lisu kama kawaida akiongoza sifa katika mkutano wa Injili chini ya kanisa la UFUFUO NA UZIMA
WITO WANGU
Naomba watu tukubali kuwa Mungu anauwezo wakufanya zaidi ya fikra zetu, Pia tuchunge sana maneno yetu kwani muda mwingi yamekuwa yakimsifia shetani badala ya Mungu. Kwa mfano unapo kubali kuwa shetani anaweza kufanya jambo fulani halafu hilohilo unakataa Mungu hawezi hapo shetani unamfurahisha sana. TUZICHUNGUZE HIZO ROHO, Hakikisha unazichunguza sio unaishia kusema halafu huchunguzi, hata mimi najua shetani anambinu nyingi za kukamata ikiwemo hizo za kutumia manabii wa wauongo kwahio tuwe makini tusimkatae Mtumishi kisa hatumiwi kama Mchungaji wako.
HII NDIO INJILI FOREVER
Tuesday, December 3, 2013
MAAJABU BINTI ASHUHUDIA KUIANGUSHA MELI YA MV SPICE MKUTANO WA GWAJIMA TANGA
Ni binti aitwae Theresia (pichani akiwa amekumbatiana na mama yake) alichukuliwa na kuwekwa bahari ya Pacific. Pamoja na mambo yote jambo lililoshangaza watu ni kudai kuwa alihusika katika kuiangusha meli ya MV Spice.
akielezea jinsi alivyofanya binti huyo alisema kuwa walitumwa kutoka baharini na kufanya kazi hiyo. Akiwa na wenzake wanne kati yao yeye akiwa Master Mind, alisema kuwa aliishusha meli hadi kwenye kina kirefu na kukusanya damu za watu.
Binti huyo ambaye alikuwa anaongea lugha ya kingereza mara kwa mara, alisema kuwa pamoja na kuangusha meli hiyo alikuwa na uwezo wa ku control fahamu za watu jambo ambalo walilifanya kwa vijana wengi.
Kilio kilitanda katika familia yake baada ya Theresia kusema kuwa hajawahi kumuona mama yake tangu 2007. Na ya kwamba mama yake alikuwa akiishi kitu kingine na sio yeye.
akielezea jinsi alivyofanya binti huyo alisema kuwa walitumwa kutoka baharini na kufanya kazi hiyo. Akiwa na wenzake wanne kati yao yeye akiwa Master Mind, alisema kuwa aliishusha meli hadi kwenye kina kirefu na kukusanya damu za watu.
Binti huyo ambaye alikuwa anaongea lugha ya kingereza mara kwa mara, alisema kuwa pamoja na kuangusha meli hiyo alikuwa na uwezo wa ku control fahamu za watu jambo ambalo walilifanya kwa vijana wengi.
Kilio kilitanda katika familia yake baada ya Theresia kusema kuwa hajawahi kumuona mama yake tangu 2007. Na ya kwamba mama yake alikuwa akiishi kitu kingine na sio yeye.
KWANINI TUNAHUBIRI INJILI?
MUNGU akubariki rafiki popote ulipo na karibu katika somo hili ambalo tunajifunza kwamba ‘’KWANINI INJILI INAHUBIRIWA?
-Injili ni habari njema za ufalme wa MUNGU ambao umeletwa kwa wanadamu na BWANA YESU KRISTO .
-Injili ni mpango wa MUNGU wa kuwaokoa wanadamu kutoka mikononi mwa shetani.
Injili ni habari za uzima wa milele ambao unapatikana katika YESU KRISTO pekee(Yohana 14:6 , Matendo 4:12).
Mwanzo wa injili ndio mwanzo wa miaka pia maana kama mwaka huu ni 2013 basi maana ni miaka 2013 tangu BWANA YESU alete habari njema za ufalme wa MUNGU yaani INJILI.
Tukizungumzia injili tunazungumzia habari njema za za pekee za kwenda uzima wa milele. Na kama tutataka tuijue injili basi inapatikana pekee makanisani au kwenye semina za kiroho na kwenye mikutano ya injili na chanzo chke ni BIBLIA TAKATIFU na sio kwingine popote. Zile injili ambazo ziko nje na BIBLIA ni injili za uongo ambazo shetani ndio alizileta kupitia WAPINGA INJILI YA KWELI yaani WAPINGA KRISTO ambao wanamtumikia shetani na hawataki kuja kwenye nuru ya ulimwengu yaani kwa BWANA YESU.
ZIFUATAZO NI SABABU 4 ZA INJILI KUHUBIRIWA KATIKA ULIMWENGU WOTE.
1; KUTII AGIZO LA BWANA YESU.
Marko 16:15-16(Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. ).
Mapenzi ya YESU ni kwamba tutoke na kuwaendea watu ili HABARI NJEMA iwafikie.
Warumi 10:13-14(kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? ).
Ndugu nimetumwa kwako na yeye na yeye anayejua maisha yako hadi mauti yako, ambaye anataka umpe yeye maisha yako ili awe BWANA na MWOKOZI wa maisha yako maana nje na yeye hakuna mwanadamu yeyote kupata uzima wa milele,(Yohana 14:6, Matendo 4:12). Hivyo kama tunataka uzima wa milele lazima tu tumfuate BWANA YESU na yeye yuko kwenye injili yake yaani kwenye BIBLIA.
2; MUNGU ANATHAMINI NAFSI YA MWANADAMU KULIKO VYOTE.
Yohana 3:16( Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. ).
Ndugu ulimwengu ni wewe hivyo MUNGU anataka uokolewe..
2 Kor 5:19 (yaani, MUNGU alikuwa ndani ya KRISTO, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. )
3; KUNA KUZIMU NA MATESO YA MILELE.
Ufunuo 20:11( Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. ).
Injili inahubiriwa ili kwamba hata kama kuna mwanadamu ataenda kuzimu basi aende kwa kutaka yeye ila maonyo kutoka kwa MUNGU kupitia neno lake ambalo injili ni sehemu yake aliyapata.
Ndugu penda injili na penda kujiunga na watu wengine kanisani ili kujifunza na kulijua kusudi la MUNGU la uzima wa milele.
4; INJILI HULETA WOKOVU.
Warumi 1:16.(Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa MUNGU uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi(wa nyumbani kwako) kwanza, na kwa Myunani(watu wa nje) pia. )
Waebrania 2:3.(sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na BWANA, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; )
-Ndugu Tafuta injili nawe utapona maana injili inaleta badiliko.
-Ingia kwa YESU na dhambi yako itakoma.
- Wokovu ni hatua ya kwanza na kuukulia wokovu ni hatua inayofuata hivyo mpendwa wangu penda kuhudhuria mafundisha kanisani.
-‘’KUMBUKA UKIPENDA IBAADA UTAKUWA UNAMPENDA MUNGU’’
MUNGU anakupenda sana ndugu ndio maana alimtuma BWANA YESU KRISTO ili wewe uwe na uzima sasa kisha uzima wa milele katika yeye.
- Ndugu injili ya kweli inaambatana na miujiza, uponyaji, kufunguliwa na kuwaweka watu huru kutoka kila pando la shetani, hivyo nenda kanisa ni utapona na pia utajifunza neno la MUNGU.
MUNGU akubariki sana na kama bado hujaokoka , ndugu chukua hatua hiyo leo na jina lako litaandikwa kwenye kitabu cha uzima, endelea na mafundisho na maombi na utamwona MUNGU kwa kila hatua ya maisha yako.
AMEN.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
Maisha ya ushindi Ministry.
Monday, December 2, 2013
MAMIA WAHUDHURIA IBADA YA SIKU YA WABABA CCC ZANZIBAR
Subscribe to:
Posts (Atom)



