Sunday, December 22, 2013

UPATANISHO

Na:Cyrian Sallu.

Yohana 14:23,24 Makao ni sehemu au mahali palipotengenezwa ili kitu au kiumbe kiishi.,Neno la Mungu linasema kuwa sisi ni makao yake Yesu kristo.Yohana15:5nyakati hizi ambazo kibiblia zinaonekana kuwa ni za mwisho wanadamu  wameamua kumfukuza Yesu ndani yao na kuruhusu Yule  roho asi ambaye ni shetani. Yohana15;7 anasisitizia umuhimu wa sisi kuwa makao  na anaahidi kutufanyia yale yote tunayomwomba tukiamini kwa jina lake atatupa.Moja ya sababu  zinazoleta shida ndani ya mioyo ya wanadamu ni kutokuwa na Mungu ndani yetu, na hili linawapata wakristo wanaojichanganya,ambao kanisani kuingia kwao ni desturi dini wanaziheshimu wakiingia kanisani wanasifu,   sadaka na michango mbalimbali wantoa lakini bado hawaamini uweza wa kriso ndani yao,na kristo mwenyewe ndani yao hayumo.
       Kupitia neno la Kristo anasema neno lake likikaa ndani yetu na yeye atakaa ndani yetu,na kupitia neno la Mungu unamruhusu Yesu mwenyewe aje kukaa na wewe.jitahidi kila neno linapokuja kwako uliruhusu likae ili kristo akae na wewe.Yohana 6:63’’Roho ndiyo itiayo uzima mwili haufai kitu’’ Ufalme wa Mungu umeenea kila mahali na  wakristo wameukataa na kuutupilia mbali ,ndiyo maana utashuhudia maajabu mengi ya kushangaza wanayafanya wakristo na siyo wapagani.Yohana 6:64.Kuamini ni kusadiki na kusadiki ni kuwa ni mmja wa waliosikia,wakristo wengi licha ya kushuhudia na kuona mambo makuu wanayotendewa na Mungu  bado  kuamini kwao kuko mbali  kwamaana hiyo wamempa nafasi shetani  ya kukaa kwao.Na kama hulisikii neno la Mungu  juwa wazi kuwa sauti utakazozisikia ni zashetani  kwa kuwa  zipo njia zilizompa uhalali wa  yeye kukaa kwako na  Mtu anaye tumkishwa na shetani anaweza kuwa mchawi hata bila yeye kujua.
,Kutoka 22:18 ,19. Maana mchawi kila akikaa anakuwa na hamu ya kuwaua wenzake  na huyu siku zote anamuhusu shetani  na ameshampa kibali cha kukaa ndani yake.Wakristo wengi licha na kumshuhudia Kristo katika maisha yao bado wanaendelea  kutambikia na kutoa kafara mbalimbali kwa shetani na maagano haya yanawapatanisha na shetani  ndiyo yanayomfanya  ibilisi apate nafasi ya kukaa ndani yetu na kutumiliki .Kumb18:22.
  Wapo manabii na watumishi ambao shetani  ndani yao ameweka pepo saba za utambuzi na wamekuwa wakiwapotosha walio wengi wakidhani kuwa ni Mungu aliyejiinua,na ili kuziepuka  roho hizi ni kuwa mtu wa kusali na kuomba ili Mungu mwenyewe ajidhihirishe kwako.Kumb 5:7,jambo linalotupoteza wakristo wengi ni  juu ya kusikiliza mafundisho na mafunuo  ya Miungu  au ya watu ambao  wanakaa na shetani na roho hizo za uasi zinakaa ndani yao.Katika maandiko Mungu anazungumza juu ya kujua mti wa mema na mbaya  ambao ni uhalali wa  kufanya uchaguzi ,ikifika mahali  ndani yako ukaanza kusikia hali ya kuwachukia watumishi bila sababu yoyote  jua ndani yako  shetani ameshapata nafasi,na kazi kubwa ni kuondoa kuamini kile Kristo alichofanya ndani yetu,na ukiona hivyo basi omba ibada ya upatanisho na Mungu ili Kristo aweze kutukuzwa ndani yako.       
Wakolosai 1:21 Neno linasema kuwa ni Yesu awezaye  kutupatanisha  na Mungu baba kwa njia ya neno lake,Wapo wakristo wengi wanafanya dhambi kwa  siri wakiwaficha wachungaji wao,wakristo wenzao na kusahau kuwa hao ni wanadamu na hawana mbingu ya kuwapeleka,na neno linatuweka wazi kuwa  Mungu huichunguza mioyo na viuno vyake na kwake hakuna siri kwa kuwa anajua  kesho na keshokutwa ya mwanadamu.Dhambi hizi  anazofanya mwanadamu ndizo zinasababisha  asipokee baraka,(Yeremia 48:7-8 )kwa maana hiyo ukiruhusu dhambi wewe mwenyewe kwa makusudi jua wazi kuwa huwezi kumwona Mungu wala kupokea Baraka kutoka kwake.
Kwa maana hiyo muombe Roho mtakatifu akukumbushe  dhambi ulizozifanya  aidha wakati unajua au hujui,ili kwamba uweze kufanya  matengenezo ya maisha yako ili uweze kujenga mahusiano mema na Mungu baba ambaye neno linasema kuwa ni mwema wa yote lakini pia ni mwingi wa rehema,na huwanyeshea mvua walimao na wasiolima,kwa maana hiyo hana ubaguzi wa mtu, ukitubu yeye ni mwema anasamehe na kusahau kabisa.Basi msihi roho mtakatifu aliyeko ndani yako aendelee kufanya mabadiliko ndani yako na Yesu mwenyewe aweze kukaa kwako milele.


Mungu akubariki sana.
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

No comments:

Post a Comment