MUNGU MWINGI WA VINGI
YALIYOMO
1.UTANGULIZI,
2.MUNGU
WA MILIONI,BILIONI NA TRILIONI
3.HITIMISHO
DHUMUNI
LA SOMO
- Kuonyesha nguvu na hekima
ya Mungu
ANDIKO
KUU -- ISAYA 55:9-‘Kwa maana kama vile mbingu
zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia
zangu zi juu sana
kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu’
1.UTANGULIZI
-
Ninawashukuru wana sayansi kwa kujaribu kuonyesha ukuu wa Mungu kwa ushahidi,
mimi ni mmoja wa wakristo wengi ambao tunaamini ukuu wa Mungu bila ushahidi, utakaposoma
huu ujumbe mtazamo wako kwa Mungu utabadirika.
-Mungu
wa Milioni, Bilioni na trilioni ni kuonyesha vipimo na uwingi na utajiri Mungu
anaofanya nao kazi, Mungu hazuiliwi na muda na nafasi, ni mwingi wa vingi.
2.MUNGU
WA MILIONI, BILIONI NA TRILIONI
-Mungu
niwa ajabu sana
kuliko tunavyodhani, nitajaribu kukugusia kidogo tu kuhusu nguvu na hekima ya
Mungu.
A
) RADI (Thunderstorm)
-
Radi ni muungulumo tunaousikia wakati wa masika, wakati mwingine radi
huambatana na umeme wake.
-Kila
Radi inapopiga, inatoa galoni karibia milioni 100 za maji
-
Radi inatoa nguvu(electric energy) ya umeme zaidi ya milioni 10 kWh
-
Kila mwaka hutoakea Radi zaidi ya milioni 16
=Mwanga
wa Radi(Lighting)
-
Mwanga wa Radi unatoa Volts za umeme zaidi ya milioni 100
-Joto
lake ni 50 000 ºF
-
Urefu wa Mwanga ni maili 5
-
Kwa makadilio, kila sekunde kunakuwa na mwako mara 100 Duniani kote.
B
) JUA (Sun) –Isaya 40:26
-
Jua lina Joto la zaidi ya milioni 27 ºF
-
Jua lipo umbali wa maili bilioni 93 toka hapa Duniani
-
Nguvu ya mada (mass energy) itokayo katika jua ni tani milioni 5 kwa kila
sekunde moja
C)
DUNIA
-Hii
Dunia tunayoishi ina umri wa miaka Bilioni 13.7
-
Jua 1 linajaa Dunia zaidi ya milioni 100
-
Sayari 1 ya Oktola inajaa Jua kadhaa na mamilioni ya Dunia
-
Sayari ya Oktola ipo umbali wa maili Trilioni 200, Oktola inang’aa mara 100
zaidi ya Jua, Oktola ina kipenyo kikubwa mara 20 zaidi ya Jua.
-
Sayari ya Betajuzi 1 inajaa ma-trilioni ya Dunia, Betajuzi ni kubwa kuliko
Oktola, Betajuzi ina kipenyo mara 600 zaidi ya Jua, Betajuzi ina ng’aa mara
6000 zaidi ya Jua
-
Pamoja na hayo,kuna sayari kubwa zaidi ya Betajuzi.
►Yote
haya Mungu ameyafanya ili tumtafute,tumjue, tumpende ,tumtumikie na kumwabudu
D)
NYOTA NA GALAKSI(Galaxy) – ZABURI 147:4-5
-
Huu ulimwengu tunaouishi una galaksi zaidi ya Bilioni 100
-
Kila Galaksi moja, ndani yake kuna nyota zaidi ya Bilioni 100
-
Kila Galaksi inakipenyo chenye urefu wa zaidi ya maili Trilioni kwa mapana yake
-
Kwahiyo kwa ujamla, kuna nyota zaidi ya Ma-trilioni katika huu ulimwengu.
-
Pamoja na uwingi wote huu Mungu anajua namba na jina la kila nyota
=►Ulimwengu (universe) –
zaburi 19:1
-
Kupita
katika kipenyo cha ulimwengu kwa mwendokasi wa mwanga (186,000) maili kwa
sekunde ni sawa na kuzunguka Dunia mara 7 kwa sekunde
-
Inachukua
miaka Bilioni 28 kupita katika kipenyo cha ulimwengu kwa mwendokasi wa mwanga
(186,000 X 186,000) m/s
E)
MADA (Matter) – Ayubu 37:14
Mwanasayansi
Albert Einstain aligundua hii fomula ; E = M x C x C
Ambapo
E- Nguvu ya Mada(energy), M- uzito wa mada (Mass enegy) na C- Mwendokasi wa
Mwanga.
-
Kama ingewezekana kubadiri ujito (mass) wa mti wa kawaida kama mpera kwenda
Nguvu ya umeme (electric energy), umeme ambao ungezalishwa ni Trilioni 45 kWh,
ili uelewe vizuri, bara la marekani linafua umeme wa kWh trilioni 4 kwa mwaka,
kwahiyo kwa mti mmoja ungeweza kuzalisha umeme kwa bara la marekani kwa muda wa
miaka 10 bila kukatika. kijiwe kimoja cha chumvi ya mezani, kinaweza kutoa
umeme ambao ungetumika kwa muda wa zaidi ya mwezi katika nyumba za kawaida za
kitanzania.
=►Hakika Mungu ana nguvu
kupita maelezo
F)
THELUJI(Snow) --- Zaburi 147:16, Ayubu 38:22
-
Theluji inatokana na kuganda kwa mvuke wa maji angani, kuganda kwa maji
kunatengeneza vichembe vya barafu vidogo ambavyo vinashikiliwa na chaji za
umeme (pole) za Hydrogen, na hapo ndo
tunapata theluji. Ikiwa angani kwa ule uzito wake inaanza kuanguka katika uso
wa nchi
-
kwa msaada wa mashine ya kuonea na kukuzia (microscope) kuna maajabu kwenye
kila kichembe cha theluji
-
Kila siku Trilioni za vichembe vya theluji vinaanguka katika uso wan chi, cha
ajabu kila kichembe kimoja kamwe hakifanani na kingine kwa uzuri,rangi na umbo.
Kwakweli vinarangi yakuvutia mno.
G)
VINASABA (DNA) ---ZABURI 104:24
Ni
ghara ya habari za siri (information storage)
-Habari
za vizazi na vizazi zinatunzwa katika vinasaba, kwahiyo ndani ya vinasaba(DNA)
kuna habari za toka Adamu mpaka wewe umayesoma hapa
-Kila
mwanadamu alinza akiwa seli moja, baada ya hapo kunakuwa na maelezo ambayo seli
moja inapokea toka kwa DNA namna mwanadamu anvyotakiwa kuwa
-
Toka seli(cell) moja mwanadamu anakuwa na seli zisizopungua trilioni 100, na
katika mgawanyiko wa ke katika kutengeneza tishu seli zinakaa katika
maelfu-elfu, na kila tishu moja inafanya kazi tofauti na tishu nyingine.
-
Ncha ya sindano ikiwekwa DNA, habari iliyomo ndani ya hiyo DNA nisawa na
kuandika vitabu vingi ambavyo ukivipanga vinafika mwezini(moon) na kupita
►
Hekima ya Mungu yapita fahamu zetu
G)
JICHO LA MWANADAMU
-
Kila siku jicho linajongea zaidi ya mara 100 000
-
Macho yanauwezo wa kuelewa jumbe milioni 1.5 kwa pamoja
-
Jicho linaweza kutofautisha rangi zaidi ya milioni
-
Jicho linauwezo wa kujisafisha, kujiponya ,kutanuka na kusinyaa na likajipanya
lenyewe.
-Mwacho
ya mtu mmoja kamwe hayafanani nay a mtu mwingine
Macho
yanakwenda pamoja kuhakikisha ufanisi.
3.HITIMISHO
-Sio
sahihi kujua uweza wa Mungu kwa nadharia, unapojua kweli kadhaa kwa uhalisia
ndipo unapojua Nguvu na Hekima Mungu
-
Haya niliyoandika ni machache mno ukilinganisha na ukuu wa Mungu, sijaelezea
kuhusu SAMAKI, NDEGE,MAUA,WADUDU,MBEGU,UPEPO,WANYAMA,MIMEA, MADINI, HEWA NK.
-
Kwakweli Mungu ni wa ajabu sana,
ni Mungu wa Ma-milioni, Ma-bilioni na Ma-trilioni
………..Remember…………………….THE
BEST HAS COMES………
No comments:
Post a Comment