Na Joseph Goliama
HATUA
YA SITA YA USHUHUDA HUU NI HII HAPA
Kila
mwanadamu anapaswa kujua kuwa Mungu ni msingi wa kila kitu kinachoonekana na
kisichoonekana, Ninaposema Mungu ni Msingi wa kiila kitu namaanisha kuwa Mungu
ni chanzo cha kila kitu yeye ni asili ya kila kitu na yeye ni mwanzo wa kila kitu
yaani Mungu ni kiini cha kila kitu hapa nataka ujue wazi kuwa ninaposema Mungu
ni msingi, kiini, asili, mwanzo na chanzo cha kila kitu namaanisha kwamba
Uzima, upendo na haki ndio msingi, asili, kiini,mwanzo na chanzo cha uumbaji
wote wa Mungu, ninapata matumaini sana pale ninapojua kwa hakika kuwa Mungu
niye chanzo cha maisha yangu ya hapa duniani ufahamu huu umenifanya nifanye
kila niwezalo kurudi kwenye msingi wangu, kurudi kwenye kiini changu, kurudi
kwenye asili yangu, kurudi kwenye mwanzo wangu, kurudi kwenye chanzo changu kwa
hakika kurudi kwenye chanzo,asili,kiini,mwanzo na msingi wangu ni kurudi katika
maisha ya Uzima maisha ya upendo maisha ya haki na kwa hakika mtu yule ambaye
amerudi katika chanzo chake milele Uzima, upendo na haki havitakuwa adimu
katika maisha yake kwakuwa ameunganishwa na majibu ya uhitaji wake
Nataka wanadamu wenzangu ambao wanatafuta Uzima wanaotafuta Upendo na
wanaotafuta haki wajue wazi kuwa wanamtafuta Mungu na yakwamba naweza kwa neema
ya Mungu kuwasaidia kukutana naye kwasababu amenituma kumtambulisha kwa
wanadamu ili yeye mwenyewe Mungu akutane nao nakujhitimisha uhitaji wao katika
maisha yao
HATUA
YA SABA YA USHUHUDA HUU NI HII HAPA
Baada
ya kueleza jinsi Mungu alivyojifunua kwangu sasa nataka wanadamu wenzangu muelewe
kuwa Mungu alisema nami kuhusu miili yenu aliniambia watu wangu wanakufa kabla
ya wakati wao kwa sababu Uzima , nguvu za Uzima na mamlaka ya Uzima imeadimika
katika maisha yao, kiukweli maneno ya Mungu yalinichoma sana hasa ukizingatia
kuwa Mungu tayari alishaniambia kuwa yeye ni Uzima yeye ni nguvu za
Uzima(UPENDO) na yeye ni mamlaka ya Uzima(HAKI), hivyo aliponiambia kuwa
wanadamu wanakufa kabla ya wakati wao moja kwa moja niliangalia nakujua wazi
kuwa ni kweli hapa duniani wanadamu wengi wanahangaika sana kwa sababu miili
yao inahitaji Uzima, nguvu na mamlaka yakufanya kazi ipasavyo, miili au viungo
vya wanadamu mara nyingi vinapata magonjwa na magonjwa hayo yamekuwa sababisho
la roho za wanadamu kutoka ndani ya miili hiyo
Ukiienda mahospitalini utajua nini naongea hapa hospitali utawakuta wagonjwa
wengi sanA na wote wanahitaji Uzima, wanahitaji uzima wa kiungo chao kimoja
baadhi kwa mujibu wa maelezo hapo nyuma nataka uelewe wazi kuwa mwanadamu
anapohitaji uzima humuitaji Mungu kwakuwa Mungu ni Uzima hapa nataka kukuuliza
wewe mwenye pumu wewe mwenye vidonda vya tumbo, wewe mwenye kisukari, wewe
mwenye ngiri, wewe mwenye kansa, wewe ,mwenye ugonjwa wa moyo ,wewe mwenye
ugonjwa wa mifupa wewe mwenye leukemia, wewe mwenye uonjwa wa kichwa, wewe
mwenye ugonjwa wa kifua, wewemwenye ugonjwa wa kiungo chochote cha mwili wako
jeeeee unajua kuwa unahitaji Uzima? najeee unajua Uzima ni Mungu?
HATUA YA NANE YA USHUHUDA HUU HII
HAPA ISOME
Baada
ya kukujulisha kuwa Mungu ni Uzima ni Upendo nani Haki, na baada ya kukujulisha
kuwa Mungu hana umbo ndio maana hata Uzima hauna umbo hata upendo hauna umbo
hata haki haina umbo na baada ya kukujulisha kuwa duniani kote wanadamu
wanahitaji Uzima, Upendo na haki nayakwamba wanadamu tunamtafuta Mungu bila
kujua kuwa tunamtafuta pale tunapotafuta Uzima, upendo na haki , na baada ya
kukusaidia kujua wazi kuwa hata Yesu mwenyewe aliishi na Mungu kwakuwa aliishi
na Uzima na Upendo na haki, na kwakuwa Yesu aliishi na Mungu ndio maana maisha
yake yote aliishi maisha ya kumfunua Mungu baba yake kwakufunua Uzima, upendo
na haki kwa wale wote waliokuwa wanatafuta Uzima, upendo na haki na kwakuwa
Yesu aliishi na kutembea na Mungu baba yake ndio maana alifunua asili ya Mungu
ya wokovu, utakatifu na ushindi. kwa ukweli huo huo nataka ujue kwa hakika kuwa
Mungu wetu yeye ni Uzima yeye ni Upendo yeye ni haki, Mungu huyu
ninayemzungumzia anataka kujifunua kwako yeye mwenyewe anataka kujifunua kwako
ili wewe ujue wazi kuwa yeye ndiye Uzima wako yeye ndiye Upendo wako yeye ndiye
haki yako, kwa hakika ili Mungu ajifunue kwako unapaswa wewe kwanza kumjua
yeye, kumjua Mungu ni kujua mawazo yake ni kujua mtazamo wake ni kujua maneno
ya kinywa chake ni kujua matendo yake ni kujua mwonekano wake ni kujua
mahusiano yake ni kujua maamuzi yake ni kujua misimamo yake, kuyajua haya ni
kujua maisha ya Mungu, maisha ya Mungu ni maisha ya Uzima ni maisha ya upendo
nani maisha ya haki, maisha ya Mungu ndio yanayomfanya tumuite Mwokozi,
mtakatifu na Mshindi, maisha ya Mungu ndio yanayotufanya wanadamu tumjuao, tuweze
kuishi maisha ya kumtegemea, kumpenda na kumuamini, maisha ya Mungu yenye
sehemu hizo nane nilizozitaja yanamfanya Mungu kuwa adui mkubwa wa shetani,
Mungu ni adui wa shetani maana yake adui wa mauti adui wa uovu ni adui wa
yasiyo ya haki. Mwanadamu anayetaka kukutana na Mungu yaani kukutana na Uzima
kukutana na Upendo na kukutana na haki lazima akubali kuyatoa maisha yake ili
ndani yake Mungu(Uzima, upendo,haki)aishi na pia akubali Mungu kuutumia mwili
wake kujifunua kwake na kwa wanadamu wengine
Jiulize maswali haya
1. Uko tayari Mungu aishi nawewe? yaana uko tayari Uzima, upendo na haki viwe
maisha yako ya kila siku kila wakati?
2. Uko tayari Mungu atumie mwili wako kujifunua kwako na pia autumie mwili wako
kujifunua kwa wengine? kwanini Mungu anataka aafikiane (akubaliane nawewe,aweke
agano nawewe, apatane nawewe) nawewe kuishi nawewe mwanadamu na kutembea nawewe
mwanadamu hapa duniani? jibu ni rahisi yeye Mungu hana Umbo yeye hana mwili
kama sisi wanadamu , hivyo ili aishi na kutembea hapa duniani ni lazima
akubaliane apatane,aweke agano afikie mapatano nawewe mwanadamu anayetaka
kuishi nawewe na kutembea nawewe, ndio maana tunasema Mungu wetu ni Mungu wa
maagano
Jee! uko tayari kukubaliana na Mungu aishi ndani yako kama alivyoishi ndani ya
Yesu Kristo? na jee! uko tayari kutembea na Mungu hapa duniani kama
alivyotembea na Yesu Kristo? kama Utakubali kuishi na kutembea na Mungu
nakuhakikishia Uzima, upendo na haki havitakuwa adimu siku zote za maisha yako
Kumbuka katika MUNGU NI MMOJA PART HII YA 8 , tumejifunza maisha ya Mungu wetu
yale maeneo nane na yakwamba Mungu anataka kuishi na kila mwanadamu na kutembea
na kila mwanadamu ili Uzima, upendo nahaki visiwe adimu hapa duniani.
HATUA YA TISA YA USHUHUDA HUU HII
HAPA ISOME
Baada
ya kujifunza katika hatua za awali za kumjua Mungu wetu kisha kuyajua maisha
anayoishi Mungu wetu sasa tujifunze ni kwa namna gani mwanadamu bila kujali
dini yake, kabila lake, rangi yake, Taifa lake, jinsia yake ,rika lake, asili
yake, ukoo wake au bila kujali chochote awezavyo kuweka makubaliano na Mungu,
mapatano na Mungu,maafikiano na Mungu,agano na Mungu la kuishi na Mungu na
Kutembea na Mungu hapa duniani na milele mbinguni
Tukumbuke kuwa Mungu hana umbo wala mwili, yeye ni Mungu wa wote wenye mwili,
yeye ni Uzima yeye ni Upendo yeye ni haki, Mungu hana mwili ndio maana
akikaribishwa na mwenye mwili kwake ni rahisi kuingia ndani ya mwenye mwili na
kufanya makao ndani yake, hufanya makao kwa kuishi ndani ya mwenye mwili na kwa
kawaida akiishi ndani ya mwanadamu humsaidia mwanadamu huyo kila anapohitaji
Uzima, upendo na haki kwakuwa yeye mwenyewe ndiye jibu la uhitaji wa mwanadamu,
huwezi ukaishi na Mungu uzima ukawa adimu au upendo ukawa adimu au haki ikawa
adimu kwako, ukiishi na Mungu unaishi na utoshelevu wako, yeye anakuwa maji kwa
kiu yako anakuwa chakula kwa njaa yako, utajiona huitaji kitu kwakuwa yeye ni
kila kitu kwako. kuishi na Mungu ni sawa na mwanamke anayeishi na mwanaume wake
mwenye kila kitu anachokihitaji hakika mwanamke huyo huishi na utoshelevu wake
wote na hujiona kila anachokihitaji ni mume wake tuu na hatahitaji mwingine
zaidi ya mume wake, hali hiyo ndio inayompata mwanadamu anayeishi na Mungu na
kutembea na Mungu hapa duniani hatahitaji chochote zaidi ya Mungu, maisha yangu
yamebadilika sana baada ya kukutana na Mungu wangu hivi sassa moyo wangu
unahitaji kuishi na Mungu na kutembea na Mungu tuu kwani najua kama ntaishi
naye na kutembea naye basi atanisaidia mimi na wanadamu wenzangu kupitia mimi
Kuingia agano na Mungu ndio njia pekee yakuingia katika maisha ya Uzima ya
upendo na ya haki yaani maisha ya Mungu ndani yetu, agano na Mungu unapaswa
kuliweka kwa kukubali yafuatayo
1. Kumkubali Mungu maishani mwako kwa kukubali Uzima, upendo na haki kuwa
maisha yako ya hapa duniani na milele mbinguni
2. Kukubali maisha ya Mungu kuwa maisha yako ya hapa duniani na milele mbinguni
3. Kukubali kuyajenga maisha yako ya hapa duniani kwa kumtumikia Mungu yaani
kutumikia Uzima,upendo na haki kwa kuyafuata maisha ya Mungu yaani kwakufuata
mawazo yake,mtazamo wake,maneno ya kinywa chake,matendo yake,mwonekani
wake,mahusiano yake,maamuzi yake na misimamo yake
Kama utaamua kukubaliana na Mungu maisha hayo kuyaishi ndipo utakuwa umefanyika
kiumbe kipya na kimsingi ndio kuzaliwa mara ya pili, ndio kuanza maisha mapya
na Mungu ndio kuingia katika ufalme wa Mungu ndipo kuanzia hapo Mungu atakuwa
mfalme wako atakuwa Mungu wako yaani atakuwa uzima wako atakuwa Upendo wako
atakuwa haki yako. nasisitiza kabisa kuingia katika agano na Mungu kunakupa
sauti ya Mungu na mwelekeo wa Mungu maishani mwako, kama hauisiki sauti ya
Mungu wala hauoni mwelekeo wa MUNGU MAISHANI MWAKO USIJIULIZE,sababu ni hii
hauna makubaliana yoyote na Mungu, hauna mapatano yoyote na Mungu hauna
maafikiano yoyote na Mungu, kama utaweka mapatano na Mungu,kama utaafikiana na
Mungu maisha yako yatapata sauti ya kuisikiliza na yatapata mwelekeo wa
kuufuata nawe utakuwa na amani na Mungu. unajua kwanini wanadamu wengi
wanaogopa kifo ?wanaogopa kifo kwasababu hawana agano na Mungu,hawana
maafikiano yoyote na Mungu na maisha yao wanaishi kama wamekuja duniani kwa
bahati mbaya. lakini nakushauri wewe mfanye Mungu kuwa maisha yako ya hapa
duniani ili ukienda mbinguni uishi naye na kutembea naye milele
Mungu ni Mungu wa agano sisi ni warithi wa agano jipya tunapaswa kuishi katika
agano letu ambalo linatutaka tuishi na Mungu na kutembea na Mungu hapa duniani
na milele mbinguni. weka agano na Mungu sasa,kubali kuishi naye na kutembea
naye hapa duniani na milele mbinguni. ukiweka agano na Mungu unakuwa
umejikabidhi maisha yako kwa Mungu naye atawajibika kukutunza,kukulinda na
kukutetea siku zote za maisha yako wewe na yeye hapa duniani mpaka atakapoamua
urudi nyumbani ukakae nae milele
HATUA YA KUMI YA USHUHUDA HUU HII
HAPA ISOME
Ikiwa
utaamua kuweka agano na Mungu ikiwa utapatana naye kuishi naye na kutembea naye
hapa duniani na milele mbinguni baada ya kifo chako cha mwili, basi unakuwa
tayari umeanza maisha mapya, maisha haya nayafananisha na maisha ya wawili
waliooana na sasa wanaanza maisha ya ndoa yao, cha kwanza kinachopaswa
kufanyika baada ya kuingia Agano na Mungu ni kujua kwa upande wako unapaswa
kuishije katika agano lako na Mungu, hapa jiulize unapaswa utumikiaje mawazo ya
Mungu?unapaswa utumikiaje mtazamo wa Mungu?unapaswa utumikiaje maneno ya kinywa
cha Mungu?unapaswa utumikiaje matendo ya Mungu?unapaswa utumikiaje mwonekano wa
Mungu?unapaswa utumikiaje mahusiano ya Mungu?unapaswa utumikiaje maamuzi ya
Mungu?unapsawa utumikiaje misimamo ya Mungu......hapa nataka ujue wazi kuwa
unakuwa wakati umewadia wa wewe kufa ili Mungu aishi ndani ya mwili wako
kupitia wewe, hapa unapaswa kufa yaani mawazo yako yanapaswa kufa,mtazamo wako
unapaswa kufa, maneno ya kinywa chako yanapaswa kufa, matendo yako yanapaswa
kufa, mwonekano wako unapaswa kufa,mahusiano yako yanapaswa kufa,maamuzi yako
yanapaswa kufa na misimamo yako inapaswa kufa na kama maisha yako hayo yakifa
yanafufuka maisha ya Mungu ndani yako, maisah ya Mungu maana yake mawazo ya
Mungu,mtazamo wa Mungu,maneno ya kinywa cha Mungu,matendo ya Mungu,mwonekano wa
Mungu,maamuzi ya Mungu na misimamo ya Mungu kwa misingi hiyo nataka ifike wazi
wewe usiiishi bali Mungu aishi ndani yako ndani ya mwili wako.
Kumruhusu Mungu aishi ndani yako ni hatua ya kwanza kabisa ya ukombozi wa mwili
wako mwanadamu, Mungu anapoishi ndani ya mwili wako anaua nafsi yako anaua self
yako anaua uwewe(your self)anaua yale maeneo yako nane niliyoyataja hapo juu,
anapoua self yako wakati huo huo yeye anachipua ndani yako,yaani maeneo yake
yale nane yanaanzan kuchipua ndani ya moyo wako
Kuishi na Mungu ni kufanya nini? kuishi na Mungu ni kwa namna gani? kuishi na
Mungu ni kwakumtafakari yeye Mungu,,kama unataka kuishi na Mungu
lazima,lazima,lazima,lazima,lazima,lazima,lazima uishi naye katika mawazo yako
kwa kumuwaza yeye wakati wote,unapomtafakari Mungu most of your time unamruhusu
aumbike ndani ya moyo wako, Mungu huumbika ndani ya moyo wa mwanadamu pale
mwanadamu anapochukua muda wake masaa yake kumtafakari, kumtafakari Mungu ni
kufanya nini? Nikuchukua muda kutafakari,kuwaza kufikiria sana 1. mawazo yake,
2. mtazamo wake, 3. maneno ya kinywa chake,4. matendo yake,5. mwonekano wake,6.
mahusiano yake,7. maamuzi yake na 8. misimamo yake kama utachukua muda kwanza
kuyajua maisha hayo ya Mungu kisha ukaamua kuchukua muda wako mwingi kama sio
wote wakukaa hapa duniani kuwaza hayo,matokeo yake utaanza kuyasahau maisha
yako ya kibinadamu na kujikuta unabadilika na watu watakaokuwa jirani nawe
wataanza kuona mabadiliko ya maisha yako sana tena sana.
Kuishi na Mungu ni ukombozi wa mwili wako unakuwa umempata wa kukusaidia dhidi
ya mauti ,nguvu zake na mamlaka zake, unakuwa umejitenga na wanadamu wanaokufa
bila Mungu kutaka, inaniuma sana kujua wazi kuwa wapo wanadamu maisha ya miili
yao yamekatiliwa na ajari, silaha,magonjwa,sumu,wanyama wakali,wanadamu wenzao,hali
za hewa,mabadiliko ya maumbile ya dunia nk inaniuma sana kuona hayo yanatokea
huku Mungu akitangazwa bila mabadiliko yoyote.
Kuishi na Mungu kunamnyima nafasi shetani kuteka nyara mawazo yako nakuishi
ndani yako, shetani ambae ndiye matatizo yetu wanadamu anapigana vita vikubwa
na Mungu wakigombea mawazo ya wanadamu , Mungu na Shetani wote wanagombea
kumiliki mawazo ya wanadamu na kuyatumia kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu.
SHETANI NA MUNGU WANAPIGANIA KILA MMOJA KUMILIKI MAWAZO YA MWANADAMU, MWANADAMU
ANAYEKUBALI MAWAZO YAKE KUTEKWA NYARA NA KUTUMIWA NA SHETANI DAIMA HATMA YA
MAISHA YAKE INAKUWA MIKONONI MWA SHETANI NA UUMBAJI WA MUNGU.
..................................................MWISHO........................................