Friday, October 25, 2013
KAFARA YA DAMU
Na: Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima
Somo: Kafara ya Damu
Lengo la somo hili ni kuwatoa wale waliopo mapangoni,mashimoni,uvunguni au waliofichwa mahala popote pale kutokana na kafara ya damu.
Mara nyingi ukisema neno “kafara” watu wanajiuliza kwamba “kwani huyu ni mganga wa kienyeji?”hii inatokana na watu kutopata mafundisho kuhusu mambo haya.
Utaona Neno kafara limeandikwa zaidi ya mara 19 kwenye biblia,na ukisoma biblia utaona kuna watu walitoa kafara za damu kwa ajili ya mafanikio fulani fulani. mfano mfalme wa Moabu ambaye alimtoa mwanae (2wafalme 3:26-27)
Damu ni nini?
Kumbukumbu la torati 12:23
Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama.
Mambo ya Walawi 17:11
Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.
Mambo ya Walawi 17:14
Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali.
Kwa nini Mungu anazuia kunywa damu?
Mungu anazuia kunywa damu kwa sababu damu ina uhai.
Mwanzo 4:10
Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
Katika andiko hili tunajifunza mambo yafuatayo;
1. Damu ina sauti
2. Damu inaweza kulia.
3. Mungu anaweza kusikia kilio cha damu
Pia damu inao uwezo wa kumfuata mtu mana kuna uhai katika damu,utaiona hii katika;
Mathayo 27:24
Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.
Matendo ya Mitume 5:28
Akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.
AINA ZA DAMU.
A. Damu inayonena mazuri(mema)
B. Damu inayonena mabaya.
A. Damu inayonena mazuri(mema).
Damu ya Yesu ndiyo unayonena mema,Damu ya Yesu inanena mafanikio,kuinuliwa,ushindi,uwezo na mambo yote mema.
Waebrania 12:24
Na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
B. Damu inayonena mabaya.
Wachawi,waganga wa kienyeji,washirikina nao wana madhabahu zao. Mfano, wachawi wakitaka kuloga huwa wanakutana mahali, na kawaida yao huwa wanakutana kwa vikundi, mfano wachawi wa kibosho,wachawi wa Marangu huwa wanakutana mahali na kumwaga damu,na mahali hapo wanapokutana ndipo madhabahu yao ambapo kuhani wao wa madhabahu ni Shetani.
Kumbuka damu huwa inamwagwa kwa ajili ya madhabahu.
Madhabahu ni nini? Madhabahu ni daraja kutoka ulimwengu wa roho kwenda ulimwengu wa mwili na kutoka ulimwengu wa mwili kwenda ulimwengu war roho.
Madhabahu huwa inaundwa na vitu vifuatavyo;
1) Madhabahu yenyewe
2) Kuhani wa madhabahu
3) Mungu wa madhabahu
4) Nguvu za madhabahu
5) Watu wa madhabahu
Mwanzo 8:20
Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Mwanzo 12:7
Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea.
Mwanzo 13:4
Napo ndipo palipokuwa na madhabahu aliyofanya hapo kwanza; naye Abramu akaliitia jina la Bwana hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment