ndugu nimesoma lakini napenda utambue
kuwa katika BIBLIA MUNGU amefanya maagano makuu mawili na wanadamu la
kwanza MUNGU alifanya agano na wana wa Israel kupitia Musa KUTOKA 24:4-8
{........... Musa akatwaa nusu ya ile
damu ..... kisha akakitwaa KITABU cha agano akakisoma masikioni mwa watu
.......Musa AKAITWAA ILE DAMU AKAWANYUNYUZIA WATU AKASEMA HII NDIO DAMU
YA AGANO ALILOFANYA BWANA PAMOJA NANYI KATIKA MAMBO HAYA YOTE} tunaposema
agano maana yake ni mapatano kwa hiyo mmoja kati ya walioweka agano
akilivunja kuna kuwa na maamuzi mengine, hawa wana wa Israel walivunja
agano WAAMUZI 2:11,20 [Wana wa israel walifanya yaliyokuwa maovu machoni mwa BWANA nao wakawatumikia mabaali] katika mstari wa 20 MUNGU mwenyewe anatangaza kuvunjika kwa agano {Basi
hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israel naye akasema kwa kuwa taifa hili
wamelihalifu agano langu nililowaamuru baba zao wala hawakuisikiliza
sauti yangu} kumbuka katika agano hili la MUNGU na wana wa
Israel MUNGU aliwapa Amri 613 na Amri 10 za msingi ili waenende na
kuishi kwa hizo lakini wakavunja na baada ya hapo MUNGU kupitia manabii
akasema atafanya agano jingine au agano jipya tusome katika YEREMIA
31:31-33 {Angalia siku zinakuja asema BWANA nitakapofanya AGANO JIPYA
na nyumba ya Israel na nyumba ya yuda si kwa mfano wa agano lile
nililofanya na baba zao katika siku ile nilipowashika mkono ili kuwatoa
katika nchi ya misri AMBALO AGANO LANGU HILO WALILIFUNJA ingawa
nalikuwa mme kwao asema BWANA .....................} Pia MUNGU akasema kupitia EZEKIELI
36:26-27 {Nami nitawapa ninyi moyo mpya nami nitatia roho mpya ndani
yenu nami nitatoa roho ya jiwe iliyokua ndani yenu........] ndugu kumbuka kile kitendo alichofanya Musa katika KUTOKA 24:8 na linganisha alivyofanya BWANA YESU katika MATHAYO 26:28 {Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ongoleo la dhambi}
pia soma ZAKARIA 9:11 hivyo ndugu hapo nilikua nakutofautisha kati ya
agano la kwanza na la pili na kila agano lilikua na taratibu zake
ikiwemo hiyo ya sabato yaani siku ya jumamosi na tukiangalia vitu vingi
tu vimebadirika mfano sadaka za kuteketezwa na mengine mengi na ukisoma WAEBRANIA 7:22{Basi kwa kadri hii YESU amekua mdhamini wa agano lililo bora zaidi}
Pia soma WAEBRANIA 12:24 . ndugu mpendwa kiukweli kuabudu siku yeyote
ni sawa pia wengine hutumia kigezo kwamba YESU aliabudu siku ya sabato
hiyo ni kweli kwa sababu alizaliwa chini ya sheria WAGALATIA4:4{Hata ulipowadia utimilifu wa wakati MUNGU alimtuma mwanae ambaye amezaliwa na mwanamke, AMEZALIWA CHINI YA SHERIA}
pia kumbuka kuwa Agano jipya lilianzia Golgota pale msalabani YESU
aliposema IMEKWISHA ila kumbuka jambo moja usije ukasahau kwa maana
watu wengine kwa kuielewa vibaya BIBLIA wanadhani agano la kale yaani
maandiko ya agano la kale hayatakiwi kutumika kwani lilifutwa lakini si
kweli kilichobadilika hapo ni mapatano kati ya MUNGU na wanadamu na
kumbuka popote pale kwenye maelezo haya nilipotumia neno AGANO LA KALE
au AGANO JIPYA simaanishi vile vitabu 39 vya agano la kale au vile
vitabu 27 vya agano jipya bali mapatano kati ya MUNGU na waisrael
kupitia Musa na mapatano mapya ya MUNGU kwa wanadamu kupiti BWANA YESU
Hivyo vitabu vyote vya Biblia bado vinatumika na vitatumika siku zote
hadi kurudi kwa YESU. Nikirudi kwenye swali lako la kuhusu siku ya
kuabudu tambua ya kwamba unaruhusiwa kuabudu siku yeyote ndio maana kuna
makanisa wana ibada jumapili wengine jumatano jioni na kwa wiki nzima
ibada zinaendelea kwani jumatatu inaweza kuwa siku ya wamama hivyo kuna
kuwa na ibada ya wamama ,jumanne siku ya vijana hivyo kuna kuwa na ibada
ya vijana hivyo siku zote ni sahihi kabisa kuabudu ndio maana katika WAKOLOSAI 2:16-17 Biblia inasema mtu asiwahukumu ninyi kwa sababu ya sabato.pia
soma WAGALATIA 4:9-11. MUNGU BABA akubariki sana na umeuliza swali
zuri sana ili pia ujumbe huu uwasaidie na wengine ambao watausoma na
kujifunza kitu.Amen {haya yalikuwa ni
sehemu ya majibu kwa ndugu Danald kazole kutoka maisha ya ushindi alipo
uliza shwari la kwanini baadhi ya Wakristo hawafuati sabato?} hata wewe
unaruhusiwa kuuliza swari au kutoa maoni ya kibiblia kuhusu shwari hili
katika blog hii au katika www.facebook.com/MaishaYaUshindi.
No comments:
Post a Comment