Monday, November 25, 2013

HATIMAYE FAMILIA YA DONNIE McCLURKIN YAMPUMZISHA BABA YAO

Donnie McClurkin mkono wa kuume akiwa na marehemu baba yake katikati pamoja na ndugu yao wakifurahia jambo.

Hatimaye familia ya gwiji la muziki wa injili Donnie McClurkin wamepumzisha mwili wa baba yao siku ya jumamosi katika mazishi ambayo yalihudhuriwa na familia pamoja na watu wa karibu wa familia hiyo, mazishi hayo yamefanyika huko Manhattan jijini New York ambapo awali yalitanguliwa na ibada ambayo pia ilishirikisha ndugu hao na marafiki zao wa karibu.


Donnie akiwa na watoto wake wawili Michelle na Matthew pamoja na ndugu wa familia hiyo ambao baada ya mazishi walikwenda kwenye moja ya mgahawa na kupata chakula pamoja ikiwa pamoja na kumaliza siku nzima wakiwa pamoja kama familia. Ni takribani miezi 10 sasa tangu mwanamziki huyo kufiwa na mama yake ambapo wiki moja iliyopita ndipo alipokufa baba yake mzazi ambaye katika maelezo yake Donnie amesema alikuwa mtu wake wa karibu sana na rafiki kipenzi.


Baba na watoto wake mara baada ya ibada ya mazishi.

Baba mdogo na shangazi zake Donnie wakiwa katika picha ya pamoja.

Michelle na Matthew watoto wa Donnie wakiwa katika picha ya pamoja.


Dada yake na Donnie mchungaji Andrea akiwa amembeba mmoja wa watoto kutoka familia yao baada ya ibada ya mazishi.

Familia picha za pamoja.

Picha inayoonyesha jeneza na Donnie akiwa mbele wakati wa mazishi, familia haijaachilia picha kamili za makaburini.

Familia ya McClurkin wakipata chakula cha pamoja baada ya mazishi.SOURCE: GOSPEL KITAA BLOG

Sunday, November 24, 2013

MATUKIO YA MKESHA WA MAOMBI LANDMARK HOTEL

NABII COVENANT AKITOA UNABII KATIKA MKESHA WA IJUMAA 22/11/2013

 Upako ukifanya kazi
 Ahsante Yesu nimefunguliwa
 Miriam Kusula akiongoza sifa
 Niraha iliyoje kugundua Mungu anakufamu vilivyo. Mtu huyu alikuwa anafurahia unabii
Mama huyu alimshukuru Mungu kwa unabii ambao aliambiwa atapata mtoto mwaka uliopita.

MUNGU AKUBARIKI NABII COVENANT NA AZIDI KUKUTUMIA

Saturday, November 23, 2013

USHITAKI WA SHETANI (PART TWO)

Na Fredrick Mulinda

..........Mtu awaye yote asifikiri kwamba jambo hili la mashitaka linafanyika huko juu, angani! Si kwamba shetani amesimama akiwa amevalia suti yake nyekundu mbele ya sofa kubwa jeupe halisi liitwalo kiti cha enzi na kutushitaki. Badala yake anazurura kwenye uharibifu na kutokuamini vilivyo katika nia zetu za mwili, katika sauti zisizokoma za dhamiri zetu zilizoharibika, katika fikra zilizopotoka na fahamu za kipuuzi juu ya Mungu.......... Endelea sasa

Sababu inayowafanya watakatifu wengi washindwe katika majaribu na mashitaka ya mwovu ni kwa sababu hawataki kumpinga shetani. Kwa miaka mingi tumekuwa tukifundishwa kumkimbia shetani, kujinasua katika miego yake, na tumekuwa tukifanya hivyo. Lakini katika siku hii ya kutiwa nuru ya kweli, wote walioangaziwa wamegundua kwamba ni joka yule yule, yule joka mkubwa, ambaye amekuwa akitutishia tumkimbie na kumwogopa badala ya kumpinga, na kwa sababu tumekuwa tukikimbia, amefanikiwa kwa kiasi kikubwa “kuponda visigino vyetu”; na la kusikitisha zaidi ni kwamba tumekuwa tukifanyiwa hivyo tukiwa ndani ya nyumba yetu! Pia ni joka yule yule ambaye amekuwa akitushitaki mchana na usiku mbele za Mungu katika hekalu lake ambalo ni wewe na mimi, na mbele za kiti cha enzi cha Mungu ambacho kiko ndani ya roho zetu!
Unaona! Maono ya joka aliyoyaona Yohana yanafunua asili/tabia ya joka la kiroho, lakini shetani haji katika mwili kama jitu lenye pembe, mkia na sura ya kutisha. Huja katika tamaa zako mwenyewe. Husema katika mawazo yako mwenyewe. Hukutesa kupitia hisia zako mwenyewe. Vita hufanyika katika mawazo yako mwenyewe akinena maneno ya mashitaka ndani yako mwenyewe. Huandaa kesi yako na kuisoma katika roho yako mwenyewe. Kadhalika Mungu naye yuko huko huko. Roho wa Mungu anayekaa ndani yako naye hunena kutokea huko huko ndani yako, katika nia yako ya roho, katika patakatifu pa patakatifu pa roho yako, akinena maneno ya faraja, tumaini, ushindi, neema nk.
Sauti ya Baba hutupa uhakika na neema kuu. Twamsikia akisema, “Nakupenda mwanangu; mimi nimekuzaa, na nitakuwa baba kwako; Nitakutia nguvu, nitakushika kwa mkono wangu wenye nguvu, maana mimi ni mwaminifu nami nitaitimiliza kazi niliyoianza ndani yako na kukuleta katika utukufu bila kunyanzi wala waa.”
Na hapo hapo, mbele za Mungu, katika hekalu lake—ndani—huibuka sauti ya upinzani, sauti ya nia ya mwili, nia ya kidini—mshitaki! Ni huko huko katika fikra, katika mbingu za ulimwengu huo ambao ni wewe, ambako shetani anatakiwa atolewe na kuangushwa, yeye pamoja na kila kitu kilichoinuka kijiinuayo juu ya elimu ya Mungu aliye ndani yako!
Kweli shetani anaweza kutushitaki, lakini Mungu hatatuhukumu. Shetani ni mshitaki/mwenye kuhukumu. Sasa, kama Mungu atatuhukumu basi atakuwa akifanya shughuli moja na shetani—watakuwa wabia! Lakini je, Mungu yuko upande wetu au kinyume chetu? Rumi 8:31-34 inaweza kutupa majibu. Lakini tunajua kwamba huyu baba yetu wa ajabu, Huyu mkombozi wetu, mwenye upendo kuliko viumbe vyote, ndiye aliyegeuza mioyo ya baadhi yetu na kuielekeza kwake. Mungu baba alimtuma Yesu afe msalabani ili atukomboe. Lakini bado dini inatuambia kwamba sharti Yesu atulize hasira zake kwanza. Lakini ukweli ni kwamba Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee, Yesu. Hatukumchagua sisi bali yeye ndiye alituchagua. Tunampenda kwa sababu alitangulia kutupenda. Sasa ni nani mwenye kuhukumu? Hakika si Mungu! Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu kwao walio katika Kristo Yesu. Nini kitatutenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu? Jibu lake ni la hakika. Hakuna kiumbe chochote katika ulimwengu wote kinachoweza kututenganisha na upendo wa Mungu.
MAOMBEZI YA YESU
Ina maana gani hasa kusema kusema kwamba Yesu anatuombea/anatutetea?Ah! Kila nikisoma neno la Mungu na kujifunza kwa roho wake wa kweli mambo mengi yanakuwa wazi, na mojawapo ni kwamba, ijapokuwa maombezi ya Kristo kwetu yanamwelekea Mungu, maandiko yanadhihirisha kwamba “msukumo” wa kwanza wa maombezi hayo SI kumwelekea Mungu, bali kumwelekea mwanadamu, kuelekea upande wetu, kutusogeza kwa Mungu, kutuvuta kuelekea kwa Baba, kutenda kazi kwa nguvu ndani yetu, ili tuweze kujiachia kwake, kuuishi ufunuo wa roho yake katika maisha yetu.
Ni kweli Yesu ni mpatanishi wetu, mwombezi, mwanasheria (advocate), anasimama kati yetu na Mungu. Lakini nini hasa afanyacho? Je, ni kweli kwamba anatuombea kwa Baba ili aturehemu? Hapana! Hakuna kitu kama hicho! Neno la kiyunani litumikalo ni “entuchano” likiwa na maana ya “kukutana na, kuzungumza na, kusihi.” Sasa swali libaki kuwa hili: Ni yupi huyo ambaye Yesu anakutana naye, anazungumza naye au anamsihi? Ni Mungu au ni mwanadamu? Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee kwa ajili yetu. Je, ndiye huyu huyu tena anayehitaji mtu akutane naye, azungumze naye au amsihi??? Je ni huyu Baba aliyeupenda ulimwengu anayehitaji mtu amsihi ili awe mwenye rehema na neema kwetu? Sikiliza! “yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho”
Kwa hiyo tunaona kwamba maombezi ya Yesu ni kutuelekea sisi (to us-ward), kukutana na sisi, kuzungumza na sisi, kutusihi sisi, kutupatanisha sisi, kuufunua moyo wa Baba kwetu, kuturejesha kwa Baba ili kwamba tupatanishwe nay eye! Shughuli yote ya maombezi ya Kristo imetuelekea sisi na si Mungu. Mungu hahitaji kupatanishwa na sisi. Ni huyo huyo Mungu asiyeonekana, asiyejulikana, aliyemtuma Kristo kwetu, kukutana nasi, kuzungumza nasi, kutuvuta sisi ili kwamba sisi na Baba tuwe umoja tena. Si jambo la kubariki moyo hilo?
Ni wakati wa kunasuka katika mitego ya huyu mwovu ambayo kwa hiyo wengi wametegwa (2Tim 2:26). Ni mashitaka makubwa kama nini na hukumu isiyotamkika ambavyo huyu joka ajifanyaye malaika wa nuru amekuwa akiwarushia ndugu zetu katika Kristo. Kati ya udanganyifu wake mkubwa uletao utumwa ni pamoja na kuwafunga watu katika kweli nusu—kuwaachia kweli inayotosha tu kuwaweka utumwani badala ya kweli yote inayoweka huru. Kuharibu kweli kwa kiwango ambacho wasikiaji hupata majibu yasiyo sahihi na kubaki na maswali yasiyojibiwa, na wakati mwingine kuogopa hata kujiuliza maswai hayo! Kila wiki Cathedro zinajaa wafungwa wa mshitaki wa ndugu zetu, na bado hawaielewi kweli ijapokuwa sauti za “manabii” zinapaa juu kama sauti ya tarumbeta huku maandiko mengi yakisomwa mbele zao kila sabato (Acts 13:27).
Ni ufunuo kamili tu unaoweza kufukuza uongo wa mshitaki wetu, na kadri tunavyoifahamu kweli ndivyo uwezekano wa kudanganywa unavyopungua. Tumepewa Roho Mtakatifu atuongoze katika kweli, si nusu, bali yote.
Mara zote ibilisi asipofanikisha kutudanganya kwa njia ya vitisho hujaribu njia hii ya mashitaka. Njia hizi mbili zinatoka ndani na nje. “Shetani wa dini zetu” hutuhukumu/hutushitaki kutokea kwenye fikra zetu wenyewe kutokana na kweli nusu nusu za kidini tulizomeza. Njia nyingine ya kutushitaki ni kuendelea kutuhubiria habari za dhambi zetu na upungufu wetu na kushindwa kwetu. Jambo hili lazima limfanye mtu ajihukumu, na kama tukiweza kujihukumu, hakutakuwa na hitaji la mwingine kutuhukumu; kwa maana mshitaki atakuwa amefanikisha utume wake.
Kadri unavyozidi kumfahamu Mungu, kujisogeza kwake, kufahamu kweli yake na kuisema bila hofu ndivyo mashitaka yanavyozidi kuwa mengi. Mojawapo ya sababu ya mashitaka kwa ndugu waliopiga hatua ya ukuaji ni kule kunasuka kwao katika kongwa la dini. Maneno ya watu walio huru huonekana kama vile yanatishia mamlaka za wakuu wa dini, yanatishia mfumo wa kanisa la kitaasisi, na hasahasa na vyanzo vya mapato na utajiri wa taasisi hizo. Ukisema kinyume na hayo ndipo utakapojua kwamba sehemu kubwa ya utendaji kazi wa shetani si katika baa, si katika danguro, si katika vijiwe vya bangi, au katika ulimwengu wa misukule—ni katika dini! Utashitakiwa kwamba tumepotoka kiimani, kwamba una mafundisho potofu, kwamba unakufuru na mengine mengi. Wakuu wa dini wataonesha kwa uwazi kabisa kwamba kama tusipoungana nao na kusema yale wanayosema siku zote, utakuwa umejitenga nao, umekataa kutii mamlaka iliyowekwa, na kwa sababu watakufukuza au wewe mwenyewe utaona mazingira yao hayakufai tena, basi utashutumiwa kwamba “umeacha kukusanyika kama ilivyo desturi ya wengine” (hahahaha!), umepoteza mwavuli wao, na bila wao huwezi kupata njia nyingine ya kuijua kweli!!!

 

Friday, November 22, 2013

UKWELI KUHUSU USHTAKI WA SHETANI (PART 1)

VIDEO YA “MSHITAKI WA NDUGU ZETU”

Na Fredrick Mulinda

“Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana AMETUPWA CHINI MSHITAKI WA NDUGU ZETU, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku” (Ufu. 12:10).



Kuna jambo la muhimu ningependa tujifunze katika sehemu ndogo tu ya mstari huu. Ni kuhusu mshitaki wa ndugu zetu anayesemwa hapa--lile joka kubwa jekundu liitwalo ibilisi (Ufu 12:9), “diabolos” kwa kiyunani, maana yake “mshitaki” au “mwovu.” Sitaweza kuongelea habari za kuangushwa kwake kwa sasa, bali kazi yake kama mshitaki, pamoja na kuonesha kile ninachokiita “ukweli uliofichika” katika kazi yake hiyo. Mimi ni kati ya watu ambao huamini kwamba uelewa usio sahihi hupelekea kuwa na imani isiyo sahihi, na kama kuna uongo niliowahi kuusikia ukihubiriwa ni pamoja na kazi za huyu mdudu aitwaye shetani.



HAYA TUANZE


Ukitulia kidogo na kutafakari mstari huu nilionukuu, unaweza kuona kwamba maneno haya yanatufundisha kitu kikumbwa; Kwamba “mashtaka” asili yake ni uovu—ni ya kishetani! Sina shaka kwamba kila mmoja wetu amekuwa akikutana na matukio ya kushitakiwa mbele za Mungu. Usiniambie kwamba wewe umekuwa ukiishi katika mbingu za juu sana kiasi kwamba hujapata kushitakiwa na ibilisi!


Huyu mwovu hunena kupitia nia ya mwili na kutushitaki. Kadhalika kazi hii pia hufanywa na watumishi wake. Mojawapo ya ushindi ambao wana wa Mungu wanautazamia ni pamoja na kumshinda huyu “mshitaki.” Asifiwe Mungu kwa sababu maandiko yanaonesha kwa uwazi kwamba wakati ibilisi anafanya kazi ya kupeleka “mashitaka” kinyume na sisi, Mwokozi wetu Kristo Yesu anafanya kazi ya “maombezi” kwa ajili yetu.


Hata hivyo, ninafahamu kwamba ukweli mkuu unaohusu maombezi ya Kristo kwetu umefunikwa na theolojia ya wanadamu iliyochakachuliwa vibaya. Nina hakika ndugu yangu kwamba hata wewe umesikia kama mimi wahubiri wakijaribu kueleza huduma ya Yesu ya maobezi kwa watakatifu inavyofanywa, pamoja na mashitaka ya ibilisi kwetu. Melezo yao mengi ukiyasikiliza yanavunja moyo. Karibu wote (au wengi) maelezo yao yanafana na haya yafuatayo:


Shetani ni adui na mshitaki wa ndugu zetu, husimama mbele za Mungu Baba huko mbinguni na kupeleka mashitaka ya wakristo mchana na usiku. Shetani humwambia Mungu madhaifu yetu yote, kushindwa kwetu kwote, huorodhesha dhambi zetu zote tuzifanyazo kwa mawazo, maneno na matendo na kumpelekea Mungu baba. Hutushitakia udhaifu wetu huo bila kusita, bila kukoma na bila huruma mbele za Baba.


Kwa upande wa Baba, yeye hudhihirishwa kama mwenye kukwazwa na kuchukizwa sana na dhambi zetu, na kwamba ana hasira na wale watendao dhambi; kwamba yeye yuko tayari kutoa adhabu kwa kusudi la kutuliza hasira zake. Hulazimishwa kufanya hivyo na asili yake ya utakatifu na haki ambavyo humfanya asipuuzie hata kijikosa kidogo bali kila kosa alipatie adhabu inayostahili.


Kutokana na upotofu huu wazazi wengi kwa kutojua wamepofusha mioyo na akili za watoto wao kwa vitisho hivi kwamba Mungu atawaadhibu vikali wakikosea na kwamba kila sekunde anawatazama ili wakikosea waadhibiwe ipasavyo. Hata mambo magumu zaidi wanaambiwa watoto wadogo kuhusu “ukatili” wa Mungu wao. Hili linamfanya Mungu aonekane kama mzee mkali, katili, mwenye kutoa adhabu kwa kusudi la kutuliza hasira zake, mwenye macho kama x-ray ambayo yanaweza kupenya sehemu yoyote hadi ndani ya mioyo ya wanadamu, na katika giza nene la usiku, huku akiwa ameshikilia bakora ya kutisha na kuwatazama kwa uso wa ukali!


Kuhusu Yesu, wahubiri wetu katika “video” hii humwonyesha kama mtu anayesimama mbele za Baba mwenye hasira kali, na kuomba kwa kubembeleza sana ili kutuliza hasira zake asiwapatilize wanadamu maovu yao kwa sababu ya hasira yake kubwa dhidi ya dhambi. Wanadai kwamba hasira ya Baba inaweza kutulizwa na kuridhishwa, na adhabu kuondolewa kama kaka yetu mpendwa, Bwana na Mwokozi wetu, Mwana wa Mungu wa kwanza, Yesu Kristo, mtetezi wetu, mwanasheria (advocate), atasimama kinyume na shetani mbele ya kiti cha hukumu cha Baba, na kumsihi Baba kwa niaba yetu, kwamba atusamehe kwa ajili yake tu, na kutuondolea adhabu kwa msingi kwamba yeye alikwishalipa gharama kwa ajili ya msamaha wetu. Kwa mujibu wa dhana hii hasira ya Mungu inaweza kutulizwa tu kama akikumbuka jasho la damu, mateso ya kikatili na kifo cha aibu alivyopata mwanae wa kwanza, Yesu.


Kwa maelezo hayo mafupi ndugu yangu, nashindwa kujizuia, na kwa hiyo sisiti hata kidogo kukuambia kwamba mafundisho ya jinsi hiyo si tu kwamba ni uongo uliopitiliza, bali pia ni upuuzi, ni takataka! Chimbuko lake ni kwenye mapokeo ya kirumi yanayomfananisha Mungu kama mtawala wa kiimla (dictator) katili, mwenye kuogofya, aliyekwazika, anayeridhishwa na kumwagika kwa damu za wale waliomkosea; na hili linamfanya Kristo awe kama mtetezi wa mtuhumiwa hadi kiongozi katili (Mungu) anaporidhika na hasira zake kutulizwa.


Si hivyo tu, bali pia inamaanisha kwamba kama asingekuwapo mtetezi wetu Yesu, Mungu angemsikiliza shetani katika yale mashitaka yake na bila kusita atuangamize au kutuadhibu vikali. Kwamba tungeweza hata kupoteza wokovu wetu na kutupwa jehanamu ya moto kwa sababu ya mashitaka ya shetani, kama mtetezi wetu mwenye rehema, Yesu, asingeingilia kati kila mara kumzuia Mungu, huku akimshawishi kwa kumwonyesha damu iliyomwagika kwa niaba yetu.


Huo ni uharibifu mkubwa wa kweli iliyo katika maandiko. Zaidi ya hayo, ni upuuzi wa kipumbavu na makufuru yasiyotamkika! Bwana asifiwe kwa sababu Roho wa kweli anazidi kuifunua kweli katika viwango vinavyoongezeka kila siku, na kwa njia hiyo tunauona utukufu wa Mungu ukizidi kuongezeka na asili yake ya upendo na rehema, hekima na nguvu, wema na fadhili ikizidi kufunuliwa, pamoja na kupata picha kubwa ya kusudi lake la vizazi na vizazi alilonalo kwa wanadamu.


Ninashawishika kupita mashaka ya kibinadamu kwamba hata shetani mwenyewe si mpumbavu kiasi cha kuamini kwamba angeweza kumkaribia Baba yetu kwa mashitaka dhidi yetu tulio watoto wake na kufanikiwa kumshawishi atuhukumu kwa sababu ya kushindwa kwetu!


Napenda kila anayesoma hapa afahamu kwamba hakuna sehemu yoyote katika maandiko inayosema kwamba shetani huwashitaki watakatifu KWA Mungu! Yasemavyo maandiko ni hivi: “ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye M-B-E-L-E za Mungu wetu, mchana na usiku.” Ni jambo moja kushitakiwa mbele za Mungu, na ni jambo jingine kabisa kushitakiwa kwa Mungu. Linatakiwa lieleweke vema kabisa kwamba SHETANI HAWEZI KUTUSHITAKI KWA MUNGU. Yeye hutushitaki mbele za Mungu. Ndugu yangu, SI Mungu Baba, Mwenyezi, ambaye shetani anatafuta kumshawishi juu ya udhaifu wako na kutokustahili kwako! Ni wewe mwenyewe!!!


Shetani hana tatizo katika kuelewa mipaka ya uwezo wake katika suala zima la kumshawishi Mungu mweza yote, ajuaye yote, mwenye hekima yote nk, juu ya udhaifu wako na kutokustahili kwako. Lakini kama akiweza kukufanya uamini hivyo, kwamba wewe umeshindwa, huna tumaini, kwamba haiwezekani wewe kuufikia mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu, kwamba ni jambo lisilowezekana kwako kugeuzwa na kuichukua sura ya Mwana wa Mungu, au kuufikia uzima usio na kikomo katika Kristo; kwamba wewe ni mwenye dhambi, kwamba Mungu hakupendi; kisha akafanikiwa kukuacha katika hali ya kuhukumiwa na kukosa tumaini, basi mashitaka yake yatakuwa yametimiliza kusudi lake la kukuibia tumaini lote, imani, ujasiri, amani, furaha na ushindi! Kwa njia hii Kristo hawezi kuumbika ndani yako.


Mtu awaye yote asifikiri kwamba jambo hili la mashitaka linafanyika huko juu, angani! Si kwamba shetani amesimama akiwa amevalia suti yake nyekundu mbele ya sofa kubwa jeupe halisi liitwalo kiti cha enzi na kutushitaki. Badala yake anazurura kwenye uharibifu na kutokuamini vilivyo katika nia zetu za mwili, katika sauti zisizokoma za dhamiri zetu zilizoharibika, katika fikra zilizopotoka na fahamu za kipuuzi juu ya Mungu..........SOMO LITAENDELEA HAPA HAPA KAARIBU............

Thursday, November 21, 2013

FAHAMU KWA SEHEMU KUHUSU MAISHA YA BEATRICE WILLIAM WA BSS

                Beatrice akiimba baada ya kuokoka.

          Ilikuwa Ijumaa ya Tarehe 15/11/2013 nikiwa Vijibweni Soweto(Kigamboni) kwenye mkutano niliokuwa nimealikwa na rafiki yangu Peter Michael ambae ni Blogger wa Maisha ya ushindi. Muhubiri katika mkutano huo alikuwa ni Cosmas Chidumle. Akili yangu ilikuwa na shauku ya kumuona Mtumishi wa Mungu Cosmas Chidumle hasa kutokana na historia yake ya mziki hapa Tanzania.

        Nilifika mapema kabla ya mkutano kuanza pia nilimuwahi mwenyeji wangu Peter Michael, nikiwa nimekaa kwenye viti ghafla nikamuona binti ambae akili yangu ilianza kumpambanua ni nani kwasababu ilikuwa kama namfahamu vile ila ilinipa tabu kidogo kumkumbuka. Nilipo ona picha haiji nikaamua kumpotezea, mpaka muongozaji wa ibada alipo simama akasema "Namkaribisha dada Beatrice William aje aimbe nyimbo mbili" watu wakaanza kushangilia bado nikapotezea. Nikasikia "naitwa Beatrice William wengi wananijua kwa jina la Beatrice wa BSS, Sasa sisaki mahela namsaka Yesu" Akili yangu ikafunguka na mdomo wangu ukasema ANHAAA.

Beatrice William akiwa na Robert Maziku(Mwandishi wa Makala hii).

      Namshukuru Mungu nimefanikiwa kutimiza ahadi niliyowaahidi wasomaji wetu wa Blog ya Injili Forever ambapo niliwaambia nitawaletea mahojiano. Mahojiano haya yamefanywa Tar 20 na 21 mwezi wa kumi na moja 2013. 

FATILIA HAPA SASA,
Robert Maziku(RM): Bwana yesu asifiwe dada.
Beatrice William(BW): Amen Habar yako?
RM: Nzuri unaongea na Robert wa Blog.
BW: Ok. Niambie,
RM: Samahani dada, Nataka kujua baadhi ya mambo ambayo watu wakiyafaham kuhusu wewe yataleta chachu nakuwa sehemu ya Injili.
                      

                                  Beatrice kabla hajaokoka

BW: Haina shida, (kwa sauti ya kukaribisha mazungumzo).
RM: Kwanza kabisa majina yako ninani na mwenyeji wa wapi?
BW: Majina yangu ni Beatrice William, ni Mhaya ingawa nimekulia Mwanza.
RM: Unamiaka mingapi?
BW: Nilizaliwa miaka 32 iliyopita, ni mtoto wa nne kati ya watoto wanne kwahio ni mtoto wa   mwisho.
RM: Inasemekana umeolewa na unawatoto?
BW: Niliolewa miaka 13 iliyopita ila kwasasa sipo kwenye mahusiano kwa muda wa miaka minne unaelekea mwaka watano sasa. Hata wakati nashiriki Bongo star search sikutoka kwa mume. Mimi ninawatoto watatu wa kwanza anamiaka kumi na tatu(13), wapili kumi na moja(11) mdogo anamiaka nane 8.
RM: Ulianza lini kuvaa mavazi ya kiume?
BW: Nilipo maliza shule tu sketi nikaachana nazo sikupenda kabisa sketi.
RM: Kwanini ulipenda hayo mavazi?
BW: Kwakweli ilikuwa nikivaa hayo mavazi najisikia ninaujasiri wa ajabu sana.
RM: Mambo gani ambayo uliyafanya kabla ya kuokoka hautayasahau?
BW: Aisee ni mengi mno, unajua mimi nilikuwa mbabe sana nilishawahi kuchapwa viboko na sungusungu kule Mwanza kama mara mbili hadhalani sababu ya utukutu. Kwamfano nilishawahi kumchana mtu na viwembe mgongoni mpaka mgongo ukatapakaa damu, nimecheza sana kamali,           kunasiku nilikamatwa na watu wa usalama usiku saa tisa natembea kwa vile mavazi yangu yalikuwa yanaonesha ni mwanaume walinipiga sana maana nilivaa pia kofia. Wamekuja kunifunua baadae ndio wanajua alaa kumbe ni binti!!
RM: Ulishawahi kuvuta Bangi??
BW: Hapana mimi nilikuwa mlevi sana.
RM: Kwaneno moja unaweza kutuambia YESU ni nani kwako?
BW: YESU NI KILA KITU.
RM: Kwanini ni kila kitu?
BW: Kwasabau Beatrice aliyeshindwa kubadilishwa na mtu yeyote hata Sungu sungu walishindwa mpaka nikawa sieleweki kama ni mwanaume au mwanamke sasa watu wananielewa ni jinsia gani Yesu ameweza kunibadilisha kwahio ni KILA KITU.
RM:Kwanini uliokoka?
BW: Ilitokea tu, ilikuwa tar 16/03/2012 ndipo niliokoka. Kabla ya kuokoka nilikuwa nimekaa miaka  kama kumi na sita(16) bila kusali popote. Siku hiyo nilikosa amani sana nikawa natafuta msaada   kutoka kwa Mtumishi (Mchungaji) yeyote aniombee niokoke basi ndio nikafanikiwa kupata   namba ya Mama(Mchungaji Rwakatale)akaniombea.

RM: Kunautofauti gani kabla na baada ya kuokoka?
BW: Utofauti upo ikiwemo sasa naeleweka mimi ni jinsia gani, nirahisi hata kuelekeza kuwa yule ni mwanamke.
RM: Unafanya huduma gani kanisani nje ya uimbaji?
BW: Huwa nahubiri kidogo kabla ya kuimba.

Beatrice Akimuombea mtoto aliyekuwa na mapepo(Mchunguze vizuri huyo mtoto utagundua alikuwa ameanguka chini).

RM: Hausikii kama una Uinjilisti ndani yako?
BW: Hio nikweli huwa nasikia pia hata watu wananiambia kuhusu hicho naamini muda ukifika                     nitafanya kwa sasa nafanya uimbaji kwanza. Pia huwa naombea na watu
wanafunguliwa                       namshukuru Mungu.
RM: Album yako inaitwaje?
BW: WEWE SI WAKAWAIDA (Jina la Album)
RM: Kwanini sio wakawaida?
BW: Kwasababu Yesu sio wakawaida.

KAMA UNAHITAJI KUPATA ALBUM YA BEATRICE WILLIAM WASILIANA NAE KWA 0658402366 BEI NI TSH 5000 TU.


MWISHO WA MAHOJIANO.
TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO WA BEATRICE WILLIAM MUNGU AMBARIKI.

Tuesday, November 19, 2013

SABATO KWA WALOKOLE ? NDIYO

By Apostle Eliya -0759 166 934


SABATO KWA WALOKOLE ? NDIYO

YALIYOMO;- 1.UTANGULIZI  2.SABATO NI LAZIMA  3.HITIMISHO

LENGO LA FUNDISHO
- Kuonyesha ulazima wa sabato kwa kila mtu anayemwamini Yesu.

ANDIKO KUU:- Waebrania 4:1 Basi ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha, na tuogope mmoja wenu asije akaonekana ameikosa

1.UTANGULIZI

- Sabato ni siku ya saba, ambayo ni Jumamosi.ni siku ya raha.
- Mungu anataka kila mwanadamu aishi sabato, ni lazima na milele.
- Makuhani, manabii, wafalme, mitume 12 na Waizraeli wote walishika sabato kwa uaminifu mpaka leo

- Kumekuwa na dini nyingi sana miaka hii, makanisa mengi, huduma nyingi, Imani mbalimbali, wana-theolojia wengi,shule za Biblia zimekuwa nyingi, makongamano, mikutano na semina nyingi sana. Lakini makundi yote haya yanatakiwa yaingie Sabatoni, ni MUHIMU.

2.SABATO NI LAZIMA
Sabato ni zaidi ya siku, ni zaidi ya kupumzika nyumbani, ni zaidi ya kwenda kanisani. Sabato inamaana nyingine ya muhimu zaidi kuliko zote. ISAYA 58:13

A) NANI MWANZILISHI WA SABATO ?

- Mungu ndiye muanzilishi wa Sabato, sio Waisraeli wala Wasabato, Mungu anajali sabato kuliko zaka, au matoleo yoyote unayoyajua, sabato ni sehemu 1 kati ya 7 lakini zaka ni sehemu 1 kati ya 10. Sabato ni amri ya 4 lakini zaka na sadaka hazimo kwenye amri. KUMB TORATI 5:12

- Mambo mawili ambayo Mungu aliyafanya siku ya 7 a) Kupumzika kuumba mambo yanayoonekana(ulimwengu wa mwili) MWANZO 2:1 na b) Kuanza kufanya kazi ya kuumba mambo ya rohoni(ulimwengu wa kiroho) au Edeni MWANZO 2:8. Yote haya yalitokea katika siku moja,ya sabato, kupumzika na kufanya kazi tena.Iliitwa sabato ya Bwana TORATI 5:14, lawi 25:4

- Nakubaliana na sayansi inayosema Dunia ina umri wa miaka bilioni 13.7, kila siku moja katika uumbaji iliwakilisha jumla ya miaka kadhaa ZABURI 90:4, kwa mujibu wangu, mpaka mwaka huu 2013 upo ndani ya ile siku ya 7 ya uumbaji MWANZO 2:2-3. Huu ni mtazamo wangu tu.

B) SABATO ILIMAANISHA NINI KABLA YA YESU ?

- Wana wa Israeli ndio warithi hasa wa kushika sabato ambayo Mungu aliianzisha kisha akamfundisha Adamu na Eva,ingawa sabato kabla ya Dhambi(anguko)na baada ya Dhambi kuingia Duniani ni tofauti lakini Mungu alitaka ishikwe KUTOKA 20:8. Kuingia sabato na kushika sabato ni tofauti, wao walishika.

Sabato ya Adam na Eva kabla ya anguko ---- Adamu hakushika sabato, aliishi sabato, Siku zote ilikuwa ni sabato,hakuna ibada wala siku ya ibada, hakuna hekalu, hakuna makuhani, hakuna sheria wala torati, Mungu akaona kila kitu ni chema MWANZO 1:31. Adam alichotakiwa ni kuitunza tu bustani MWANZO 2:15.

Sabato baada ya Dhambi kuingia(anguko) ---- Sabato ikawa na dosari, badala ya kuishi kisabato wakatakiwa kuishika sabato TORAT 5:15e. Dhumuni likageuka badala ya kufurahia Edeni na uumbaji wote ikawa kufanya Upatanisho WALAWI 16:31, ikamlazimu Mungu asipumzike tena, Mungu akaweka makuhani, sheria, hekalu, torati na kafara ambayo hayakuwa na umuhimu wowote.- WAEBRANI 8:5, 10:1, KUTOKA 25:40.

- Ukisoma vizuri kuhusu sabato utagundua kuna mambo mawili kulwa na doto ambayo mara zote yalijitokeza wakati wa sabato, cha ajabu haya mambo mawili yapo kinyume kabisa WALAWI 23:32;
     1. Kujitesa nafsi  2. Kustarehe

Mungu alitaka Waisraeli wajifunze nini ?,
1.Kujitesa nafsi -=- kwamba wajitese nafsi zao kwasababu waliasi,wakapoteza haki zao za kumiliki bustani ya Edeni(ulimwengu wa kiroho). Kwahiyo Mungu na Mwanadamu wote walikuwa wakiiharifu sabato MATHAYO 12:5, ambapo sii sahihi. Hivi unajua kuwa kusamehe dhambi na kusamehewa dhambi ni kazi kubwa ?
2.Kustarehe -=-  Kwamba wajifurahishe, lakini furaha hii haikuwa halisi ilikuwa ni kwa ajili ya kuwakumbusha mambo mawili; kuwa kabla ya Dhambi maisha yalikuwa ya pumziko, na pia baada ya Yesu kutakuwa na pumziko MATHAYO 11:28

- Siku ya sabato waisraeli walitakiwa kutembea umbali wa mtupo wa jiwe, maana yake kazi wangefanya kidogo sana lakini matokeo yangekuwa makubwa sana, ni kama teknologia inavyofanya kazi wakati huu.

C) SABATO ILIKUWAJE WAKATI NA BAADA YA YESU ?

- Msomaji wangu naomba ujue kwamba KIPINDI cha BAADA ya anguko na KABLA ya Yesu mambo mengi sana hayakuwa halisi, Mungu aliichagua Israeli, makuhani,hekalu na Torati kutunza kumbukumbu, lakini hayakuwa na uhalisia(kivuli).EBRANIA 8:5

- Yesu hakuwa na tatizo na kushika sabato kwa waisraeli, wala makuhani,wala torati, wala hekalu. Bifu la Yesu na hawa jamaa ilikuwa ni UFAHAMU wao kuhusu sabato,ukuhani, hekalu na torati. Hawakujua kwanini Mungu aliamua achague siku moja(Jumamosi) iwe siku ya sabato.- MATHAYO 12:1-8, 23:16-22, LUKA 6:6-11

- Hata mitume nao hawakuwa na shida juu ya siku ya sabato, walishajua dhumuni la sabato. Ngoja nikupe huu mfano, chungu cha udongo kina almasi zimejaa ndani, kipi cha muhimu hapo, chungu au kilichopo ndani ya chungu ? Ndio utofauti wa Yesu na wayahudi.- MDO 13:42-44

- Yesu anapojiita Bwana wa sabato haimaanishi kuwa yeye ndiye anayejali sana kushika sabato, hapana, alimaanisha kuwa yeye ndiye anaeishi kisabato kwa usahihi. Kabla ya Yesu hakuna aliyeshika sabato 100% - YOHANA 5:30, LUKA 6:12

D) SABATO IWEJE NYAKATI ZETU ?

- Ili uelewe sabato nyakati zetu, turejee madhumuni mawili ya sabato ;-   1.Kujitesa;- Yesu ameshateswa, dhambi zote zimefutwa ISAYA 53:11a.
 2. Kustarehe tunatakiwa kuiishi sabato kama kabla ya anguko. Kwa kuishi kisabato tunautangazia ulimwengu kuwa kuna sabato tutakayoiishi milele inakuja. WAEBRANIA 4:11

- Sabato ni kutumia mambo ya kiroho kuendesha mambo ya mwilini       1 KORIN 2:14, sabato ni kuwa na vipawa na karama za Roho Mtakatifu RUMI 8:14. Sabato ni kupumzika kutumia mwili na kuanza kutumia Roho Mt. Sabato ni kusikiliza kila siku, kutii kila siku na kutenda kila siku- MATHAYO 7:24

E) JE, UPO TAYARI KUISHI KISABATO ?

- Sabato ni lazima hapa Duniani kwa mlokole na Mroma na Muislamu na Wanaojiita wasabato. Kama umechoka kuonewa na kuwa omba-omba, ingia kwenye sabato, kama unafurahia haya maisha sabato haina hajakwako MATHAYO 7:13

- Walokole wote ambao hawatembei katika mtembeo wa Roho mt, namaanisha wasiokuwa na vipawa na karama za Roho mt hawapo katika sabato, bado wanahangaika na kushika sabato. Ikumbukwe kuwa sabato ni lazima. Kwa hali hii, ni afadhali ya msabato anayeshika siku kuliko mlokole asiyekuwa rohoni ingawa wote wawili wameingia chaka - MATH 7:16

- Wasabato wote ambao hawana Roho Mt, na karama na vipawa, hawapo katika sabato na hawastahili kuitwa wasabato, mbaya zaidi wanamhuzunisha Roho Mt EFESO 4:30. Chochote kinachofanyika kanisa lolote bila Roho Mt ni kumdharau Roho Mt.YOHANA 15:5

F) UTAMJUAJE MSABATO HALISI ?

- Kila mwanadamu anaejali maisha ni lazima awe msabato(sio mjumamosi). Kumjua msabato halisi ni rahisi sana, anatoa unabii, anafanya miujiza na uponyaji na ishara,anapambanua roho, anatafsiri na kunena kwa lugha, anafichua mambo ya siri(hekima, maarifa), ana imani ya yasiyowezekana, anaona maono, anaisikia sauti ya Mungu, anaweza kufukuza mapepo, anafufua wafu. Nk MDO 1:8, 10:38, 1KORIN 12:8, ISAYA 11:2-3

- Acha kutumia nguvu za kimwili, badala yake pumzika mwilini harafu fanya kazi ya nguvu rohoni, sabato ni kupumzika mwilini na kufanya kazi nzito rohoni EFESO 6:12. Wafuatao ni watu ambao wamejaribu kuonyesha maisha ya kisabato ;- TB JOSHUA, EUBERT ANGEL, PASTOR CHRISS, BENNY HINNY, IDAHOSA, MAKANDIWA, BOATENG, KAKOBE, GWAJIMA, MALISA, KULOLA, COVENANT,KATHRINE, ORAL ROBERT, YONG CHO, OYEDEPO, n.k. Hawa jamaa ndio wasabato na kila mkristo alitakiwa awe kama mmojawapo wa hawa ndugu.- MDO 8:29,39, 7:55

- Kwakifupi msabato halisi ni yule anaeishi maisha ya kiroho na kimwili kama ya Yesu au zaidi ya Yesu. Yesu ni mfano wa mtu anayetaka kuwa Msabato. Yesu hakuna alichokuwa anabuni katika huduma yake, mambo yote alielekezwa, naye alikuwa muaminifu kutekeleza. Hiyo ndio sabato, alisikia , alitii, alifanya, hii ndiyo sabato.- YOHANA 14:10b

G. ITAKUWAJE NISIPOINGIA SABATO ?

- Kabla sijajibu swali labda niseme kwamba anayefaidika hasa na sabato ni mwanadamu, kutokuingia sabato hakutakuzuia kwenda mbinguni, kwahiyo mbinguni utaingia hata kama haujaingia sabato hapa Duniani.

-Usipoingia sabato utaishi maisha ya misuri, utakula kwa jasho, ardhi itakuwa imelaaniwa kwako,utatawaliwa, tama yako itakuwa kwa mwingine, shambani kwako miba itamea, lakini mbinguni utaingia. Uchaguzi ni wako MWANZO 3:16-18, utakuwa kama mwana mpotevu LUKA 15:15-19

- Ipo sabato kuu naya milele inakuja, lakini kipindi hiki tumeruhusiwa kuonja utamu wa sabato inayokuja ya milele LUKA 11:2, utakuwa mjinga usipoonja, lakini ukishindwa, subiri ile inayokuja, lakini kubali kuishi hapa Duniani kwa Jasho. Usiwaseme vibaya walio elewa sabato LUKA 11:20-22, MATHAYO 6:9d, UFUNUO 21:1-2


3.HITIMISHO

- Kuwa msabato ni lazima, kama unataka kuwa msabato tekeleza mambo haya mawili kikamili;- a) Amini Injili kwa usahihi, b) Jazwa Roho Mt kikamilifu.

- Haya mambo mawili yamewashinda wasabato na walokole wengi. Mpaka sasa wachawi na waganga ndio wanao furahia sabato, sio wakristo. Mchawi kuingia rohoni ni rahisi lakini mlokole kasheshe, hii ni kuonyesha wachawi ndio wasabato wazuri.

………..Remember…………THE BEST HAS COMES………………